Zanzibar tushakuwa tayari kujitenga

Zanzibar tushakuwa tayari kujitenga

Maswali ambayo nimekuwa nauliza na hakuna Mzanzibar aliyewahi kunijibu ni kuwa
1. Tanganyika itapoteza nini kwa Zanzibar kujitenga?
2. Kwanini Wazanzibar wasiondoke kwanza bara wakadai nchi yao wakiwa kwao?
3. Wazanzibar 400,000 wanafanya nini bara Vs Wabara 1000 walioko visiwani
4. Wazanzibar zaidi ya 50 wanafanya nini latika bunge la bara? mbona hawasusii bunge na kurudi kwenye baraza lao la uwakilishi.
5. Kwa uchumi wa bilioni 500, wabara wanafaidika nini kutoka Zanzibar? Hii ni sawa na bajeti ya wizara ya akina mama na watoto au mapato ya soko la kariakoo.
6. Zanzibar inachangia kiasi gani kuendesha serikali ya muungano.

Tujadiliane kwa haya
Mkuu,

Kwa vile hao wazanzibari hawakujibu, basi itakubidi ujitafutie majibu mwenyewe.
Mimi ninachoweza kukuambia ni kuwa ukisoma kwenye hii link ninayoiweka hapa basi utapata baadhi ya majibu ya masuali yako. bofya
http://www.kituochakatiba.org/index2.php?option=com_docman&task=doc_view&gid=1208&Itemid=27

mkuu, suali la kwanza tutajuwa nini tunapoteza siku ikitokea wakijitenga. kwa sasa hivi wazenj kwetu sisi ni "common perceived threat/enemy" siku wakiwa hawapo inakula kwetu.
 
Mdondoaji said:
Fanya utafiti kidogo utaona, Wazanzibari ndio wafanya biashara wakubwa Tanganyika, Bakhressa, Zakaria, SSB wote hawa ni either wapemba au waunguja na ni walipa kodi wakubwa TRA sasa wakisema wanaondoka sijui hiyo Tanzania tunayojisifu nayo itatoka wapi. Pili tuje katika utendaji tuna mawaziri wengi wazanzibari na pia kumbuka zanzibar bado inatudai deni la fedha iliyotukopesha wakati tunaunda muungano kutokana na mauzo yake ya karafuu. Hata bado kuna mashamba na biashara mikoani zinaendeshwa na wazanzibar, property nyingi Dar, Arusha, Kilimanjaro na Mbeya wazanzibari wanamiliki imagine the spillover effect yake katika uchumi wa nchi hii?? Nyerere aliyumba tulivyo nationalize our economy sasa sijui sasa hivi akija JK atayumba vp ndio maana nasema tutawalilia

Mdondoaji,

..what makes you think kwamba Muungano ukivunjwa basi wafanyabiashara wenye asili ya Zanzibar watalazimika kufunga biashara zao zilizoko Tanganyika?

..kama wafanyabiashara hao, kwa mfano Bakhresa, wameweza kufanya biashara Malawi na Msumbiji, nchi zisizokuwa na muungano na Zanzibar, basi sioni tatizo la wao kufanya biashara ktk Tanganyika isiyo na muungano na Zanzibar.

..ikumbukwe pia wafanyabiashara wenye asili ya Zanzibar wanafaidika na soko la Tanganyika. hawapo hapa kufanya hisani, au kusaidia "yala maskini". serikali inafaidika kutokana na kodi wanazolipa, na wananchi wanafaidika kutokana na ajira na bidhaa zinazozalishwa. kwa msingi huo basi kunahitajika umakini ktk kuzitenganisha Tanganyika na Zanzibar.

..mijadala ya muungano inaharibiwa sana na hoja za "nani zaidi."
 
Takribani maoni ya Wazanzibari walio wengi mtandaoni na hapa nyumbani basi huhubiri Zanzibar kujitoa ndani ya Muungano.Suali hili kwa sasa limekuwa ndio uradi wa Wazalendo walio wengi. Kwa ufupi wanataka Zanzibar isimame kama Zanzibar na sio Sehemu au hata tuite nchi iliyo chini ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Yakhe, Zanzibar mjitenge mara ngapi, mbona mmeshajitenga, ushanfahamu sio?
 
Zomba said:
Sio mimi nikajifunze historia ya Zanzibar, wewe ukajifunze historia au hukubali kuwa Zanzibar ndio Taifa lililokuwa linatawala hii himaya yote ya pwani ya Afrika Mashariki mpaka Kongo? Au huamini kuwa machafuko Zanzibar yalianzishwa na Nyerere? Au huamini kuwa Tanganyika ndio iliomezwa na Zanzibar? Niambie ni nini katika hivyo huamini nikupe ushahidi wa kitaalam kabisa nawe utowe wako halafu tuendelee, nakuhakikishia huna.

Zomba,

..Zanzibar ilianza kudhoofika muda mrefu kabla ya muungano.

..kama ulivyoelekeza Zanzibar iliwahi kutawala eneo zima la pwani ya Afrika Mashariki.

..jinsi muda ulivyozidi kusonga mbele Zanzibar ililazimika kuyaachia maeneo hayo kwa dola[Mjerumani,Muingereza,..] zilizokuwa na nguvu zaidi yake.

..Zanzibar iliendelea kudhoofika mpaka kuwa chini ya MUINGEREZA. kumbuka ule "uhuru" wa 1963 ulitolewa na Muingereza na kupewa Sultani.
 
Ndugu zangu Mnazungumzia Zanzibar na Pemba au Zanzibar tuu??

Sidhani kama watu wa Pemba watapenda kwenda na Wazanzibar --- hii itakuwa tamu sana!!!
 
Je wazanzibari walioko bara ambao ni 10 % ya wazanzibari wote jee hawa watapewa dual citizen ship au vipi au wabebe magorofa yao kurudi nayo visiwani like wale southern sudan fellow.

Je Mwana kijiji utakua na nia njema kweli kuwapa ahueni ya kuwasamehe madeni yoteWazanzibari kwa vile bajeti yao ni sawa na soko la kariakoo ?

Sual i langu la Mwisho vipi chama chako cha CCM kinachoongoza kuiba kura Tanzania kitaendelea kuwa chama tawala kwa mtutu wa Bunduki uko tayari ndugu zako kina Mapuri na Mwakanjuki , Sepetu , Augustino Rmadhan , kisasi and others Zanzibara royal family kuwapa ardhi huko Tegeta wapate pa kufikia kwani visiwani ardhi haitoshi tena visiwa ni vidogo ?
Najua 10 % ya Wazanzibari walioko Bara wakirudi visiwani na rasilimali zao wata create economic boom kwani wako prosperous ila hawa 90 % ya wazanzibari waliko visiwani ndio wa pay price ya hawa 10% kwa tishio watawafukuza hawa kwa hiyo tuulinde muungano huu bandia what is the point ?
If many small Islands can run them self how dare you guys worried about Zanzibar if it seperate ?Mutakosa nini Watanganyika kurudisha nchi yenu ya zamani Tanganyika iliokua na jina zuri tu isio na mdoa machafu kama hii muanyoipenda Tanzania iliojaa makovu ya unynyasaji soma article hii ya MO Ibrahim kweney citizen ya jana utajua why Zanzibari hate the union what is the legality of this union Bunge lipi la Zanzibar lilipitisha huu Muuungano munaoulilia hauna uhalali zanzibar kila mmoja anajua hata mwanakijiji atupe legality ya union ? Wolfgang Dourado the former attorney general of Zanzibar bado yuko hai hakujua wala hakujuylishwa juu ya Muungano huu vipi leo kiinimchao hichi munachokililia kisochokuepo?
soma hii iko siku utafunuka macho muungano huu ni wa wanasiasa wachahche wanaokula na watanganyika majority ya Wazanzibari hawautambui and sad part kuna mawazir iwa CCM zanzibar wanasema wazi wazi tumechoka na hii kitu muungano sikuambii CUF wao wako mrengo mwengine.
Malizeni na jengeni nchi yenu Tanganyika waachieni Wazanzibari waishi kwa peace kama munataka kisiwa chukueni Comoro koloni lenu jipya Kikwete amewe ka pupet wake huko

Sudan is a warning to all of Africa Send to a friend
Tuesday, 11 January 2011 21:50
digg
One evening, some 40 years ago, a progressive north Sudanese was giving a lecture in Khartoum. He was talking about the problems posed by the chronic underdevelopment of south Sudan, and the need to entrench brotherhood and unity among all Sudanese if we were to develop as a nation.

A southern man stood up and brought the audience back to earth. “That is all fine, sir,” he said to the speaker. “But will you allow me to marry your sister?”
The prejudice to which he alluded has remained sadly relevant up to today, when the south of my country is preparing to vote in a referendum on independence.

Late last year, my foundation held its annual forum in Mauritius, a beautiful country which has led our Index of African Governance for the past four years. Some 300 African opinion leaders came together to discuss the economic integration of the continent. The debate was not about whether we need integration: African markets, as well as African voices, are too fragmented to compete globally. Rather, the debate was about why we are moving towards closer political and economic co-operation so slowly.

In the evening, as everyone danced joyfully to the music of Youssou N’Dour and Angelique Kidjo, there was a cloud hanging over the Sudanese guests among us. A woman was crying as her colleagues tried to calm her. While other Africans were celebrating their coming together, we knew that in a few weeks our country would start to break apart.

Later that night I joined my Sudanese friends from all corners of the country, the north, the south and Darfur. The meeting was reflective, sad and awkward. Looking at my friends, I wondered how each would have responded to that 40-year-old question.
Sudan has been an experiment that resonated across Africa: if we, the largest country on the continent, reaching from the Sahara to the Congo, bridging religions, cultures and a multitude of ethnicities, were able to construct a prosperous and peaceful state from our diverse citizenry, so too could the rest of Africa.

That we have failed should sound a warning to all Africans. Sudan, at one million square miles, is the continent’s largest country, sharing borders with nine other states. The fault lines that have divided us as a people extend from Eritrea to Nigeria. If Sudan starts to crumble, the shock waves will spread.

Khartoum today projects a sense of normality, modernity and relative affluence. This is in sharp contrast to the rest of the country. Lack of investment, underdevelopment and the exclusion of populations on the periphery from the political process has resulted in alienation. It has strengthened local identities.

We have not nurtured that sense of brotherhood and unity. Rather, since independence the way Sudan has been governed has undermined any potential for a common Sudanese purpose.

President Omar al-Bashir’s regime has aggravated the problem by seeking absolute power and repressing dissent. The result has been the civil wars in the south, the east and in Darfur to the west. Our country has torn itself apart.
The separation of the south following the referendum on January 9 is inevitable. The least we can do now is to separate peacefully and amicably.

I do not believe that either the ruling National Congress Party (NCP) in Khartoum or the Sudan People’s Liberation Movement (SPLM), which governs the south, want to fight. War would almost certainly bring an end to NCP rule in the north and devastate an already impoverished south. Leaders on both sides are smart enough to know that.

The north must now focus on finding a peaceful solution to the separate conflict in Darfur, and the leaders of the three main rebel movements there must come together around a coherent agenda to achieve this.

The government in Khartoum feels isolated and under siege, facing criticism from within its own ranks, the population at large and even its Arab neighbours, who are usually tolerant of each others’ misdeeds.
It needs to reflect on the outcomes of 21 years of absolute rule – and address its legacy, to which partition will now be added. If you are in a hole, stop digging.

But decent governments need decent opposition. The crumbling old opposition parties in Khartoum, led by the same grand old men who were there when I was at school, lack vision or even coherence.

The south faces its own enormous task of nation-building. Civil war and underdevelopment have left the region with little infrastructure and few institutions. Moreover, the south is not as homogenous as often portrayed: there too a national identity must be constructed, representative of the diversity of its people.

At our meeting in Mauritius we all agreed that Africa’s future is in its own hands. Freedom of movement of people, goods and capital is essential for the development of our sub-scale economies and for maximising the potential of our immense resources. Regional economic communities across Africa, the African Union and the African Development Bank are all focusing on this as a top priority.

Sudan cannot afford to be on the wrong side of history. The north and south will have to work together, but will they? Less than two decades before the independence of India and the creation of Pakistan, Winston Churchill claimed: “India is a geographic term. India is no more a country than the equator is a country.” It is with great sadness that we Sudanese must recognise that the same rings true for us.

The writer is chairman of the Mo Ibrahim Foundation and founder of the telecoms group Celtel
 
Kitu cha kushangaza ni swali aliloweka mtoa mada, la Zanzibar kujitenga, cha kujiuliza ni kujitenga na nini? Nadhani cha msingi, ambacho wengi wetu tunakisahau ni kuwa, Muungano ulijumuisha nchi mbili, Tanganyika na Zanzibar. Leo, hakuna Tanganyika kuna Zanzibar na Tanzania, Tanzania ni tunda la Muungano na si Tanganyika, Tanganyika na Tanzania ni vitu viwili Tofauti. Sasa hii Tanganyika iko wapi?

Kwa kuwa Tanzania ni tunda la Muungano wa nchi mbili na moja ya hizi nchi zilizoungana ipo, na ina Rais wake, Bendera yake, Bunge lake ambalo linaitwa Baraza la wa Wakilishi, sheria na kanuni zake na, na, na...na kwa kuwa Zanzibar ipo basi hii ndio iliyoimeza Tanganyika na kuwa haipo.

Cha msingi sio Zanzibar wajitenge, cha msingi ni waTanganyika kuanza kuomba uhuru wetu kutoka Zanzibar.
Bila Zanzibar kukubali kutupa Uhuru wetu, tutabaki hivi hivi, waondoke, waende, na kadhalika. Waondoke kutoka wapi? Kama ni Tanganyika haipo, kama ni Tanzania, huwezi kuwafukuza watu kwenye Muungano halafu wewe ubaki unajiita Tanzania. Huwezi, simpo. Uwe kwanza na nchi yako hapo ndio utaweza kusema ondoka, upo kwangu. Sasa wewe kwako huna na mna kwenu, kama ni kwenu ni nani wa kufukuzwa? Hakuna.

Waombeni taratibu wa Zanzibari watupe Uhuru wetu.
 
mzee kifimbo alikosea angetakiwa wakati anafanya muungano angesema kuwa zenji iwe mkoa na hivyo karume kuwa mkuu wa mkoa wa zenji na baada ya mwaka anamuamishia hata kigoma na kule anapelekwa mkuu wa mkoa mpya mbona mambo yasingekuwa complicated.
 
tumechoka we na tumeshindwa twamuomba mungu atusaidie kuondokana na koloni la tanganyika

Kwa taarifa yako, Yule jamaa aliyekuwa kiongozi wa kambi ya upinzani hawezi kukubali. Unajua Zanzibar Mishahara ya watumishi wa serikali ni kiduchu sana hata baraza la wawakilishi nadhani malipo ya vikao hayalingani na yale bunge la muungano, Hivyo Zanzibar kujitenga Si rahisi.
 
Fanya utafiti kidogo utaona, Wazanzibari ndio wafanya biashara wakubwa Tanganyika, Bakhressa, Zakaria, SSB wote hawa ni either wapemba au waunguja na ni walipa kodi wakubwa TRA sasa wakisema wanaondoka sijui hiyo Tanzania tunayojisifu nayo itatoka wapi.

Hiyo kodi wanayolipa TRA ni sehemu tu ya faida wanayoipata kwa kufanya biashara na si vinginevyo. Wanafanya biashara kwa kuwa kuna demand na population kubwa ya kununua bidhaa wanazotengeneza. Bakhresa akiondoka kesho au hata akifilisika bado uhitaji wa maji,ngano,ice cream n.k utabaki pale pale, na tena itakuwa fursa kwa wajasiliamali wengine watanganyika kuanzisha biashara hiyo kuziba pengo na kukidhi hilo hitaji na TRA itapata kodi vilevile. Kwahiyo kumbe ni hao akina Bakhresa wanufaikao zaidi na Tanganyika!!
 
Maswali ambayo nimekuwa nauliza na hakuna Mzanzibar aliyewahi kunijibu ni kuwa
1. Tanganyika itapoteza nini kwa Zanzibar kujitenga?
2. Kwanini Wazanzibar wasiondoke kwanza bara wakadai nchi yao wakiwa kwao?
3. Wazanzibar 400,000 wanafanya nini bara Vs Wabara 1000 walioko visiwani
4. Wazanzibar zaidi ya 50 wanafanya nini latika bunge la bara? mbona hawasusii bunge na kurudi kwenye baraza lao la uwakilishi.
5. Kwa uchumi wa bilioni 500, wabara wanafaidika nini kutoka Zanzibar? Hii ni sawa na bajeti ya wizara ya akina mama na watoto au mapato ya soko la kariakoo.
6. Zanzibar inachangia kiasi gani kuendesha serikali ya muungano.

Tujadiliane kwa haya

Na waanze kwa hao wapemba waliojazana kariakoo kuondoka tena waanze kesho. na wasirudi tena huku.
 
Wafanyabiashara wakubwa na soko lao kubwa wanalo kwao enh!?! waende wakitaka kwanza mzigo, wabunge wao wanawakilisha majimbo ya wapiga kura 1500 na wa bara wanawakilisha wapiga kura laki tatu 300,000 jimbo moja! halafu wanadai tugawane sawa sawa nafasi za uongozi!
 
mzee kifimbo alikosea angetakiwa wakati anafanya muungano angesema kuwa zenji iwe mkoa na hivyo karume kuwa mkuu wa mkoa wa zenji na baada ya mwaka anamuamishia hata kigoma na kule anapelekwa mkuu wa mkoa mpya mbona mambo yasingekuwa complicated.

Kabisa mzee(R.I.P) alikosea huwezi kuunganisha Madagascar na Sychelles au South Africa na Swaziland au na Lesotho au Congo na Burundi then wawe na haki sawa katika kuongoza na kuwakilisha,wangejumuishwa katika Tanganyika, ilitakiwa kuwa mkoa tu,muungano nchi zikaribiane ukubwa au population! muungano ungekuwa wa tanganyika na mfano Kenya au Uganda au Mozambique au Zambia, Zanzibar wangejumuishwa tu na kuwa mkoa
 
Dah mzee mwanakijiji hata wewe umebariki hili!!????.
Kweli mnataka tuanze kuitana wazanzibar, wachaga, wanyakyusa, wasukuma n.k ndani ya nchi ambayo baba wa taifa alitumia nguvu na upeo wa juu kutuunganisha na mpaka leo hatujawahi kua na vita au dharau za kikabila!!!???

Acha zako hizo zimepitwa na wakati zidumu fikra sahihi ujamaa ni imani ukiona kundi la siasa nyerere yupo mwenge tunaukimbiza mbio mbio kaburu matata azimio la arusha kilimo cha kufa na kupona,,,,,,,!; zote hizo ni kero kama muungano wa kukoroga udongo wa nchi mbili kwenye vibuyu na kuweka kwenye kikapo yote hiyo ni kero Hiki ni kizazi kingine sio kila kitu ndio mzee!
Karibu tena!
 
mzee kifimbo alikosea angetakiwa wakati anafanya muungano angesema kuwa zenji iwe mkoa na hivyo karume kuwa mkuu wa mkoa wa zenji na baada ya mwaka anamuamishia hata kigoma na kule anapelekwa mkuu wa mkoa mpya mbona mambo yasingekuwa complicated.

Mkuu,
jisomee historia ya Indonesia na East Temor.
pengine utapata mawazo mengine.
 
Ndugu zangu Mnazungumzia Zanzibar na Pemba au Zanzibar tuu??

Sidhani kama watu wa Pemba watapenda kwenda na Wazanzibar --- hii itakuwa tamu sana!!!

Mkuu,
Cha kuogopa zaidi ni huku Tanganyika (bara) ,huku utakuja ukabila na udini, vyote ni hatari tupu!
Wao watajuana wenyewe. Wenyewe husema,"waarabu wa pemba hujuana kwa vilemba". Watajuana wenyewe ,hatuna haja ya kujifanya tunawaonea huruma. Hizi comments tunazotoa humu JF ni kiashiria kuwa tunawaona wao kuwa ni kero kwetu.
 
Hii ni kama Southern Sudan. Tutakuwa huru zaidi na maamuzi na mustakhabali wa nchi yetu. Bara wana-dilute maendeleo yetu. Kwanza wanaong'ang'ania ni bara. Watuache tumekuwa sasa. Utengano ni Uimarifu kwa mdogo.
 
Mdondoaji,

..what makes you think kwamba Muungano ukivunjwa basi wafanyabiashara wenye asili ya Zanzibar watalazimika kufunga biashara zao zilizoko Tanganyika?

..kama wafanyabiashara hao, kwa mfano Bakhresa, wameweza kufanya biashara Malawi na Msumbiji, nchi zisizokuwa na muungano na Zanzibar, basi sioni tatizo la wao kufanya biashara ktk Tanganyika isiyo na muungano na Zanzibar.

..ikumbukwe pia wafanyabiashara wenye asili ya Zanzibar wanafaidika na soko la Tanganyika. hawapo hapa kufanya hisani, au kusaidia "yala maskini". serikali inafaidika kutokana na kodi wanazolipa, na wananchi wanafaidika kutokana na ajira na bidhaa zinazozalishwa. kwa msingi huo basi kunahitajika umakini ktk kuzitenganisha Tanganyika na Zanzibar.

..mijadala ya muungano inaharibiwa sana na hoja za "nani zaidi."

Joka kuu,

Ni kweli kama ulivyosema kuwa mijadala ya Muungano hutawaliwa zaidi, pia umesahau kebehi ambazo baadhi ya watanganyika wenzangu mnazo dhidi ya wazanzibari. Hicho ndio kinachofanya mjadala huu kuwa hivyo.

Kama unavyosema akina Bakhressa na wenzie wamewekeza Malawi, Zambia lakini ukija Tanganyika kuna watu wanafikiri jamaa wamewanyonya wakati ukweli ni wawekezaji. Hivyo kodi zao ndio zinalisha serikali yetu na majadiliano yafanyike kama tunauvunja muungano kuhusu wawekezaji hawa watabakiaje Tanganyika. Kumbuka kuna watanzania wenzetu wameajiriwa pia na mkiwafukuza kama baadhi yetu tunavyoona basi hawa jamaa kazi ndio watakuwa hawana. Sasa tufikirie mara mbili kauli zetu hawa jamaa wamejiestablish vizuri sana.

Pia tujiulize serikali yetu iko makini kihivyo mkae mkifahamu Tanganyika haiko stable kama mnavyotaka watu wengi wafahamu, kuna ufisadi unaoitafuna serikali, rasilimali zinachimbwa lakini mtanzania wa kawaida haina faida yeyote, udini uliotapakaa, na mengineyo mengi ambayo nasikitika kusema kwamba yakibezwa uchumi wa Tanzania utakuwa mbovu kupindukia miaka ijayo. Nitakupa mfano ufisadi pekee tukichukua Dowans 185, EPA, 155, Twin tower 200 Billions jumla ni 540 bil gawanya kwa budget ya serikali ya Tanzania kwa mwaka huu ni 11.1 Trilioni unakuta 5% ya budget yetu inaliwa kwa ufisadi. Pia ukicompare na GDP ambayo imesimama around 31.3 Trillion unakuta 2% ya GDP inaliwa na mafisadi .

Sasa tukae tukitafakari hilo na wazanzibari wamekuwa kitu kimoja na angalau wenzetu ufisadi upo lakini sio wa kutisha kama huku Tanganyika na hivyo basi nakuhakikishia wakijitenga tutaenda kugonga mlango tuwaombe kazi maana viongozi wetu huku Tanganyika wanafikiria kwanza jinsi wao na familia zao watakavyofaidika na uongozi.
 
Back
Top Bottom