Zanzibar tushakuwa tayari kujitenga

Zanzibar tushakuwa tayari kujitenga

Mwiba

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2007
Posts
7,607
Reaction score
1,760
Takribani maoni ya Wazanzibari walio wengi mtandaoni na hapa nyumbani basi huhubiri Zanzibar kujitoa ndani ya Muungano.Suali hili kwa sasa limekuwa ndio uradi wa Wazalendo walio wengi. Kwa ufupi wanataka Zanzibar isimame kama Zanzibar na sio Sehemu au hata tuite nchi iliyo chini ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
takribani maoni ya wazanzibari walio wengi mtandaoni na hapa nyumbani basi huhubiri zanzibar kujitoa ndani ya muungano.suali hili kwa sasa limekuwa ndio uradi wa wazalendo walio wengi. Kwa ufupi wanataka zanzibar isimame kama zanzibar na sio sehemu au hata tuite nchi iliyo chini ya jamhuri ya muungano wa tanzania.

اذهبي بسلام
Go in Peace. Kama mlilazimishwa kuingia bado mna haki ya kuamua kutoka.

Pigeni kura kama nchi ya kimaamuzi, then tambaeni
 
Hili wala si tatizo; kwa vile tunaenda kuzungumzia Katiba Mpya ni vizuri Zanzibar waje na hoja ya kupiga kura ya maoni kama wanataka kubakia kwenye Muungano au watoke. Asilimia 60 ya Wazanzibari wakikubali kutoka basi tunawashika mkono wa kheri na tutawasaidia kulipa madeni yenu na kuwapiga jeki kidogo ili muanzie pazuri.
 
Ndio uzuri wa kuwa na wazee humu JF, yaani umemaliza kazi na umenifilisi hoja. kwa sababu thanks unazo nyingi, mimi nakugongea ya hapahapa kavukavu THANKS
 
zanzibari ijitenge mara ngapi toka zamani ilisha jitenga lakini umbuke kama mutachimba mafuta basi itakuwa ya mungano
 
Pigeni kura kama Wasudan na wekeni hoja yenu kwenye Katiba yenu mpya. Uhuru wa fikra na mwili ni jambo jema sana. Wazanzibari, mna haki ya kuwa huru.
 
Kuvuja kwa pakacha ... nafuu ya mchukuzi..... heri na fanaka ZNZ
 
Hata ile gharama ya kuhudumia wabunge toka Znz, Umeme nk itakuwa nafuu kubwa kwa Tanganyika mpya. Kila lakheri wazo hili.
 
the earlier the better-mi nataka kwenye hotuba yao ya kesho waliseme hili-NITASHUKURU SANA WAKIJITOA
 
Nyie Wazanzibar asili yenu wote bara sasa mnajitenga na nani? na babu zenu walioko huko bara siyo?

Acheni mawazo finyu na wazo la kujitenga hilo msahau kabisaaaa vizazi na vizazi haitkaa kamwe itokee.:smile-big:
 
By the way, sababu za msingi zilizoasilisha muungano kama hazipo tena. Siamini kuwa mwaweza tena kutawaliwa na Sultani, hivyo tafuteni forum ya kupigia kura kuihuisha Zanzibar yenu! Mnaweza pia kupata kasi ya maendelea kama msipokuwa na ubinafsi
 
Takribani maoni ya Wazanzibari walio wengi mtandaoni na hapa nyumbani basi huhubiri Zanzibar kujitoa ndani ya Muungano.Suali hili kwa sasa limekuwa ndio uradi wa Wazalendo walio wengi. Kwa ufupi wanataka Zanzibar isimame kama Zanzibar na sio Sehemu au hata tuite nchi iliyo chini ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Maswali ambayo nimekuwa nauliza na hakuna Mzanzibar aliyewahi kunijibu ni kuwa
1. Tanganyika itapoteza nini kwa Zanzibar kujitenga?
2. Kwanini Wazanzibar wasiondoke kwanza bara wakadai nchi yao wakiwa kwao?
3. Wazanzibar 400,000 wanafanya nini bara Vs Wabara 1000 walioko visiwani
4. Wazanzibar zaidi ya 50 wanafanya nini latika bunge la bara? mbona hawasusii bunge na kurudi kwenye baraza lao la uwakilishi.
5. Kwa uchumi wa bilioni 500, wabara wanafaidika nini kutoka Zanzibar? Hii ni sawa na bajeti ya wizara ya akina mama na watoto au mapato ya soko la kariakoo.
6. Zanzibar inachangia kiasi gani kuendesha serikali ya muungano.

Tujadiliane kwa haya
 
tumechoka we na tumeshindwa twamuomba mungu atusaidie kuondokana na koloni la tanganyika
 
Maswali ambayo nimekuwa nauliza na hakuna Mzanzibar aliyewahi kunijibu ni kuwa
1. Tanganyika itapoteza nini kwa Zanzibar kujitenga?
2. Kwanini Wazanzibar wasiondoke kwanza bara wakadai nchi yao wakiwa kwao?
3. Wazanzibar 400,000 wanafanya nini bara Vs Wabara 1000 walioko visiwani
4. Wazanzibar zaidi ya 50 wanafanya nini latika bunge la bara? mbona hawasusii bunge na kurudi kwenye baraza lao la uwakilishi.
5. Kwa uchumi wa bilioni 500, wabara wanafaidika nini kutoka Zanzibar? Hii ni sawa na bajeti ya wizara ya akina mama na watoto au mapato ya soko la kariakoo.
6. Zanzibar inachangia kiasi gani kuendesha serikali ya muungano.

Tujadiliane kwa haya

waulize .C.C.M watakijibu
 
Back
Top Bottom