Zanzibar tushakuwa tayari kujitenga

5. Kwa uchumi wa bilioni 500, wabara wanafaidika nini kutoka Zanzibar? Hii ni sawa na bajeti ya wizara ya akina mama na watoto au mapato ya soko la kariakoo.

Nothing to say...serikali ya Zanzibar kama soko la Kariakoo!! hahahahaaa

Wazanzibari haya ni matusi na nawaomba yawachochee kujitenga upesi sana. Yani mnalingana na kariakoo?
 
Hili wala si tatizo; kwa vile tunaenda kuzungumzia Katiba Mpya ni vizuri Zanzibar waje na hoja ya kupiga kura ya maoni kama wanataka kubakia kwenye Muungano au watoke. Asilimia 60 ya Wazanzibari wakikubali kutoka basi tunawashika mkono wa kheri na tutawasaidia kulipa madeni yenu na kuwapiga jeki kidogo ili muanzie pazuri.

Kwa tunaoamini katika demokrasia..nothing can top what you have said.
 
Ha! ondokeni hata kesho, kwani nani kawakataza? mimi kama raia wa kawaida sipati faida yoyote ya uwepo wenu,sana sana hasara kwa sababu mnanizibia nafasi yangu mjengoni!
 
Hakuna rais yeyote wa CCM atakayethubutu kuuvunja muungano, awe wa Bara au Zanzibar.
 
Hakuna rais yeyote wa CCM atakayethubutu kuuvunja muungano, awe wa Bara au Zanzibar.

Ndiba unachosema ni kweli kabisa mkuu. Nadhani iko agenda iliyojificha maana ukiangalia the way issue ya muungano inavyobebwa mara nyingi unashindwa kuelewa kuna nini nyuma ya pazia.

Ni kweli wazanzibar wamekuwa kama ndugu zetu na kwa kweli wakati wote tumejisikia hivyo. Lakini kama wao wanaona ni wakati muafaka kujiweka pembeni na kujitenga na bara hili ni jambo jema na haki yao ya msingi. Zanzibar ilikuwepo muda mwingi nje ya muungano na sasa kama wanaona mahitaji waliyonayo ni kukaa nje ya Muungano that is fine also

Kwangu mimi nawaona kama mtoto wa kiume anaejiona mbele ya wazazi ya kuwa amekuwa na sasa anaweza kujitegemea.

Kwa uamuzi kama huu, kama wanzibar wenyewe watajitokeza na kutaka kuwa pembeni ya Muungano inawezekana pia maana hata Katiba yao naamini sio jambo lililokuwa lenye kupendwa machoni mwa watawala wa CCM. Ila hatimaye maamuzi yao yalilazimisha

So wakiamua na kupaza sauti hakuna mtu ndani ya CCM au popote anaeweza kuwazuia.

Hatima iko mikononi mwenu wazanzibar, ule wakati wa kulalamika kunyonywa na bara huku bado mmeng'ang'ania ndoa inayowanyonya umepita, kama mnaona vema kujitenga na bara, okay
 
kujitenga ni sawa lakini ukumbuke mafuta tuta gawana chocote nikachotoka visiwani ni vyetu sote , na vya bara ni yaa bara tu
 
Zanzibar ni moja ya sababu ya Watanganyika kulipa bei kubwa za Umeme
 
mtoke mapema maana mkiingizwa shirikisho la afrika mashariki kwisha habari yenu hamtaweza tena kujitoa. Na mkijitoa mjue mtawekewa vikwazo na mainland af c nasikia huko hamna jeshi?
 
waulize .C.C.M watakijibu

Tatizo la Wazanzibar wengi wanaimba wimbo wasioujua, nimeweka hoja naomba nijibiwe hoja. Kuna mmoja amewahi kuniambia kwa ''hoja yake makini sana'' tutapata misaada ya kutosha kwani nchi yao ni ndogo. Nikamuuliza Haiti vipi? hakuwa na jibu.
Nina maswali 1-6 nijibiwe kwa hoja tafadhali, ili tukienda kuandika katiba tujue wenzetu wanataka nini na kwanini. Kujitenga hakuna shida yoyote. Hoja hujibiwa kwa hoja.
 
nani atawalilia? Wengi wao wana nyumba dar! ... Ahmad Rashid- Mikocheni, Mwakanjuki- Mbezi/Tegeta, Kina AH Mwinyi? Kariakoo, Tandika? .....Shauri lao!
 
tumechoka we na tumeshindwa twamuomba mungu atusaidie kuondokana na koloni la tanganyika

Nacheka sana nikiangalia Ilala, Magomeni, Kariakoo,tandika, kitope,fuoni, tomondo,bububu! Ntacheka sana nikiangalia namna wabara watakavyofanya kule kariakoo, ntacheka sana namna itapofika zamu ya kuchagua uraia kwa cc twenye baba zenj,mama singida-maisha dar-maziko mchangani! Spati picha kwa walioajiriwa bara kujenga zenj, Spati picha kwa jinsi vyeti vya kuzaliwa vitakavyochakachuliwa kulinda viwanja vyao zenj na pia kutetea ukuu wa wilaya-Duh spati picha japo move naihisi, haya bibi yangu turudi zetu kwetu biashara ishachacha! Nataka zenj tujitoe utumwani bt (frankly) we gonna suffer mostly than wadanganyika.
 
baada ya marekebisho ya katiba ya mwaka jana yaliyofanyika tayari mlishajitenga kasoro jina ndio limebaki kuonyesha kuwa kuna muungano ila mmeng'ang'ania nafasi nyingi za ajira bara za kisiasa na za serikalini mmepora ardhi nyingi bara hata mashamba ya mipunga kyela kwa kuwapa hela kiduchu wakulima mmetengeneza uchochoro mkubwa wa bidhaa feki zilizopo bara na ndio chanzo cha ukosefu wa mapato bara ya TRA mmekuwa wasafirishaji wa mazao ya misitu kutoka bara kupitia bandari bubu kwa kweli hata sisi tunaona huu muungano ni biashara kichaa tumieni mwanya wa marekebisho ya katiba kubadilisha jina ili muitwe jamhuri ya zanzibar tuachane kabisa
 
Tafakari nzuri sana....pokea thanks yangu Great Thinker.
 
wanaJF,

Mbali na michango mizuri munayoitoa na pia changamoto munazozionesha. Kwa wale watakaopata muda pitieni chapicho hili.
http://www.kituochakatiba.org/index2.php?option=com_docman&task=doc_view&gid=1208&Itemid=27

Kuna mambo mengi ya msingi kuhusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambayo yamefichikana kwa raia wengi. Pengine baada ya kumaliza kulisoma chapisho unaweza kuwa umejiongezea maarifa zaidi juu ya Muungano wa TZ na pia michango yetu inaweza kuwa ya hoja zaidi kuliko hamasa au kuonesha dharau.

mfano wa dondoo moja katika chapisho hilo ni.....
……Kushindwa kutatua matatizo kunasababishwa pia na mambo ya Muungano kutokuwa wazi kuanzia mwanzo. Mambo hayajadiliwi, si kwa pamoja wala si kwa wanachama wawili wa Muungano peke yao. Hili linaongezeka kwa tuhuma za kuwepo vitisho. Ilielezwa kuwa uongozi wa Tanzania haufurahi kila unaposikia Muungano
ukijadiliwa. Badala yake kunakuwa na mkono mzito katika kuyashughulikia mambo hayo ili Muungano uendelee kuwa pamoja; matumizi ya mabavu au njia nyingine zisizo za moja kwa moja. Imeelezewa kuwa, mpaka ulipofika urais wa rais Mkapa ilikuwa ni mwiko kuuzungumza Muungano. Matokeo yake ni kwamba watu wa
kawaida hawana habari za kutosha juu ya taratibu za Muungano.pg 55
 
Hili wala si tatizo; kwa vile tunaenda kuzungumzia Katiba Mpya ni vizuri Zanzibar waje na hoja ya kupiga kura ya maoni kama wanataka kubakia kwenye Muungano au watoke. Asilimia 60 ya Wazanzibari wakikubali kutoka basi tunawashika mkono wa kheri na tutawasaidia kulipa madeni yenu na kuwapiga jeki kidogo ili muanzie pazuri.

dah! Mkuu leo mkuu leo unaongea maneo haya! Ushazisoma alama za nyakati enh? Kweli umekomaa.
 
baada ya marekebisho ya katiba ya mwaka jana yaliyofanyika tayari mlishajitenga kasoro jina ndio limebaki kuonyesha kuwa kuna muungano ila mmeng'ang'ania nafasi nyingi za ajira bara za kisiasa na za serikalini mmepora ardhi nyingi bara hata mashamba ya mipunga kyela kwa kuwapa hela kiduchu wakulima mmetengeneza uchochoro mkubwa wa bidhaa feki zilizopo bara na ndio chanzo cha ukosefu wa mapato bara ya TRA mmekuwa wasafirishaji wa mazao ya misitu kutoka bara kupitia bandari bubu kwa kweli hata sisi tunaona huu muungano ni biashara kichaa tumieni mwanya wa marekebisho ya katiba kubadilisha jina ili muitwe jamhuri ya zanzibar tuachane kabisa

Mmeikoloni kwa muda mrefu Zanzibar sasa ni zamu yenu. Wazej wamo kwenye SMT lakini wa Tanganyika hammo kwenye SMZ, Kibao kimewageukia.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom