Zanzibar | Special Thread

Mara nyingi nikiendaga huko nafikia lodge yangu moja iko Fuoni na inaitwa Fuoni Lodge iko poa sana na upande wake wa pili kuna bar kubwa sana vinywaji vyote vipo na kuna watoto wazuri sana ingawa ni mbali kutokea mjini huwa napumzika vizuri mno.Ipo mwisho zinapogeuzia daladala za Fuoni
 
Afadhali umefikilia kuweka mada ya wazenjibar, japo wenyewe wamelala maana walikuwa hawana sehemu maalum iliyopo ndani ya jukwaa as muungano.

Naendelea na hili hapa...
Kwanza guest houses kwa unguja ni shida sana kupata kulingana na eneo unalotaka kustay, itakulazimu upate chumba (mfano) darajani alafu shuhuli zako ziwe ZU.

Wenyeji hawapendi Mtanganyika apange kwenye nyumba zao tena akiwa jisnia ya kiume bora wa kike anafikiliwa.

Ubinafsi ni mkubwa sana, ukifahamika umetoka bara, labda utoe product bora/nzuri kuliko ila unapigwa juju mapema asubuhi!.

Pia mpaka kesho najiuliza, sababu ya gharama ya usafiri kwa boat how ni kubwa sana kulinganisha na distance?.

Na ...
Mara ya mwisho kufika zanzibar ni mwaka gani mkuu?

Zanzibar ya sasa ina mchanganyiko mkubwa wa watu. Tena sana.

Wazanzibari wengi wapo nje. Tuliobaki wengi ni wakuja lkn ndio tushakua wenyeji
 
Mara ya mwisho kufika zanzibar ni mwaka gani mkuu?

Zanzibar ya sasa ina mchanganyiko mkubwa wa watu. Tena sana.

Wazanzibari wengi wapo nje. Tuliobaki wengi ni wakuja lkn ndio tushakua wenyeji
Hata wewe ukifika Mtwara mtaa wa Magomeni utatueleza habari ya mtaani hapo kisa uliwahi kufika kwenye kimtaa kimoja tu.
 
Mara nyingi nikiendaga huko nafikia lodge yangu moja iko Fuoni na inaitwa Fuoni Lodge iko poa sana na upande wake wa pili kuna bar kubwa sana vinywaji vyote vipo na kuna watoto wazuri sana ingawa ni mbali kutokea mjini huwa napumzika vizuri mno.Ipo mwisho zinapogeuzia daladala za Fuoni

Mkuu bei zikoje Hapo Fuoni Lodge?
 
👉🏾Kwanza guest houses kwa unguja ni shida sana kupata kulingana na eneo unalotaka kustay, itakulazimu upate chumba (mfano) darajani alafu shuhuli zako ziwe ZU.
Zanziba imekalia kiutalii zaidi, yaani main target ni foreigners nje ya Tanzania. Stone town kuna guest houses za kumwaga.

Wenyeji hawapendi Mtanganyika apange kwenye nyumba zao tena akiwa jisnia ya kiume bora wa kike anafikiliwa.
Kwanini hawapendi mtanganyika apange kwenye nyumba yao? Kama wakikataa mtanganyika watampata nani? Wazanzibari hawana utamaduni wa kukodi nyumba wakiwa kwao. Huku mtu kakodi nyumba/chumba ikiwa anasoma chuo mfano. Venginevyo mtu hana pakukaa basi anakaa kwao tu

Ubinafsi ni mkubwa sana, ukifahamika umetoka bara, labda utoe product bora/nzuri kuliko ila unapigwa juju mapema asubuhi!
hizi ni fikra zako tu kwa vile ni muoga, kupigwa juju haitaki uwe mbara au mkenya, kama kupigwa juju na mshindano wako utapigwa tu. Sasa wamachinga wote waliopo Zanzibar mbona hawakupigwa juju na product zao ni za ovyo tu? Wewe kaa tu wakati kuna wabongo wenzako wanapiga mawe maisha yanasonga mbele hawatamani ata kurudi kwao :D

Pia mpaka kesho najiuliza, sababu ya gharama ya usafiri kwa boat how ni kubwa sana kulinganisha na distance?
Ushawahi kulinganisha operating costs za boti na za bus linalokwenda Tanga kutoka dar 250+ kms?
 
Back
Top Bottom