Zanzibar | Special Thread

dos.2020

JF-Expert Member
Feb 17, 2009
9,144
7,455
Nimehisi nijaribu kuanzisha huu uzi kwa ajili ya kupeana support ya baadhi ya changamoto. Kwa wale wote wanaoishi Zanzibar au wanaopanga kwenda kuishi Zanzibar, Au kwa wale wanaotaka kwenda kwa ajili ya matembezi na menginayo.

Hii thread tutasaidiana kwa ajili kuelekezana mambo tofauti ikiwemo michongo ya ajira, masuala ya ununuzi wa bidhaa, mazingira ya kibiashara, masuala ya makaazi, guest houses na mikahawa kwa wanaokwenda kimatembezi pamoja na changamoto nyingengine nyingi za kimaisha, Na pia kuwasaidia muongoza kwa wale wanaohamia sasa au wanaokwenda kutembea ambao hawana wenyeji.

Natarajia watajitokeza wengi wenye uzoefu zaidi kuchangia mada hii.
 
Viwanja vya makazi vinapatikana huko Zanzibar? Na bei ni shilingi ngapi kama vipo?
 
Afadhali umefikilia kuweka mada ya wazenjibar, japo wenyewe wamelala maana walikuwa hawana sehemu maalum iliyopo ndani ya jukwaa as muungano.

Naendelea na hili hapa...
👉🏾Kwanza guest houses kwa unguja ni shida sana kupata kulingana na eneo unalotaka kustay, itakulazimu upate chumba (mfano) darajani alafu shuhuli zako ziwe Tunguu au Kivungwe huko.

👉🏾Wenyeji hawapendi Mtanganyika apange kwenye nyumba zao tena akiwa jinsia ya kiume bora wa kike anafikiliwa.

👉🏾 Ubinafsi ni mkubwa sana, ukifahamika umetoka bara, labda utoe product bora/nzuri kuliko wao ila unapigwa juju mapema asubuhi!.

👉🏾Pia mpaka kesho najiuliza, sababu ya gharama ya usafiri wa boat how ni kubwa sana kulinganisha na distance?.

👉🏾Na ...
 
Vinapatikana. Maeneo mengi kwa sasa kwenye viwanja ni kuanzia mitondooni, kisauni, maungani, kombeni na kwenda mbele huko.

Bei jipange walau kuanzia m25
Na taratibu zake za kumiliki ardhi zikoje kwa sisi ambao siyo Wazanzibari Wakaazi?

Natambua kwa upande wa Bara, ni pesa yako tu. Hakuna ubaguzi wowote ule kwa Watanzania wa pande zote za Muungano.
 
Afadhali umefikilia kuweka mada ya wazenjibar, japo wenyewe wamelala maana walikuwa hawana sehemu maalum iliyopo ndani ya jukwaa as muungano.

Naendelea na hili hapa...
Kwanza guest houses kwa unguja ni shida sana kupata kulingana na eneo unalotaka kustay, itakulazimu upate chumba (mfano) darajani alafu shuhuli zako ziwe ZU.

Wenyeji hawapendi Mtanganyika apange kwenye nyumba zao tena akiwa jisnia ya kiume bora wa kike anafikiliwa.

Ubinafsi ni mkubwa sana, ukifahamika umetoka bara, labda utoe product bora/nzuri kuliko ila unapigwa juju mapema asubuhi!.

Pia mpaka kesho najiuliza, sababu ya gharama ya usafiri kwa boat how ni kubwa sana kulinganisha na distance?.

Na ...
Kiongozi siku hizi guest bubu zipo kibao tu pale kisauni kuna wachaga wamefungua guest zipo kama tatu karibu karibu na bei ni nafuu sana mpaka elfu 5 kwa short time.
 
18 Reactions
Reply
Back
Top Bottom