Rasimu ya mabadiliko hayo, niliyaona kwenye kikao fulani cha nchi wafadhili, nikiamini yangewekwa hadharani ili yajadiliwe na Wanzazibari kabla ya kufikishwa Barazani.
Maana ni kuwa Bara iko very much aware kila kinachoendelea Zanzibar, kwanza waliomba bendera, halafu wakaomba wimbo wa taifa, sasa hawajaomba mipaka, bali wametangaza mipaka ili Zanzibar iwe nchi in terms of defined teritory ila usiwe na shaka, hiyo ni mipaka jina tuu, kama ulivyo wimbo wao wa taifa ni wimbo tuu, na bendera yao nayo ni bendera tuu.
Kama wewe nyumbani kwako unaitwa Baba, mwanao akalipenda sana jina la baba, ukakubali naye aitwe baba, akiitwa baba anafurahi, hivi wewe sasa ndio hautakuwa baba?. Wewe utabaki baba wa ukweli na yeye baba jina.
Hivi ndivyo ilivyo status ya Zanzibar, ni nchi jina tuu ila sio dola kwa sababu bado haina vyombo vya ulinzi, vyombo vya dola, Jeshi, Polisi, TISS etc, unless KMKM ndio polisi wao na JKU ndio jeshi lao, them huu utakuwa uhaini 100%.