Zanzibar Kuwa Nchi

Wazanzibari wanapokuja Bara ni kwa ajili ya kutafuta maisha tu na hawajiingizi katika siasa na hata akitaka kufanya hivyo hatoruhusiwa kutokana na mtandao ulowekwa wa kuwapiga vita.Ukimuona Mzanzibari yumo katika siasa za Tanganyika ni katika ngazi ya Kitaifa kwa kupitia katika MUUNGANO.

Yako mengi yanayotukera kwa mfano utasikia nchi ya watu milioni 40 yenye eneo kubwa haiwezi kuilinganisha na watu milioni moja na yenye eneo dogo lakin munasahau kuwa hata inagalikuwa nii mtu mmoja na yenye ukubwa wa maili moja lakini ilikuwa na hadhi ya nchi na tulipoungana hatukukubali kuuza utu wetu kwenu.Sisi Wazanzibari tunaamini tuna haki sawa katika Muungano huu iwe katika kuchangia katika gharama za kuuendesha na katika faida yake.
.

Tuambie katika bajeti ya ZNZ Billion 500, pungufu kuliko bajeti ya waizara ya Elimu Tanganyika, Zanzibar inaweza au inachangia kiasi gani!!!
Hivi unakumbuka bara walipotaka kuwe na visa kama zenj, nini kilitokea? Waznz walijua kuwa watakuwa loser! By any account ni wabara wangapi wanategemea Znz as compared to Waznz wanaotegemea 40 milion population Buisness and Market. Viongozi wanawadanganya in the end mwananchi wakawaida ataathirka. Hawataki muungano waznz tuvunje tu we have nothing to lose!
NAIPENDA TANGANYIKA, kama alivyoshauri RedDevil [kama sijakosea], I'm proud to be TANGANYIKA. TANGANYIKA FOR EVER
 
Kamakabuzi,
Nimekusikia. Kama wewe ni msomi wa historia utagundua kwamba tukishakubali kuvunja huu mwungano wa sasa itakuwa vigumu kuunda mwungano mwingine. Kwa sababu huo mwungano mwingine utaundwa kwa misingi ipi? Unadhani kweli maalim Seif anaweza kutuletea mwungano wa manufaa wakati yeye ana mawazo mgando ya enzi za Usultani na kudai himaya ya Mombasa? Kama mwungano wa sasa haukidhi basi ni heri kila mmoja aende lwake. Sisi mainland hatutakosa usingizi, hata siku moja.
 
Bikirembwe acha kutoa lawama ambazo hazina msingi, matatizo ya kisiasa Zanzibar yanatokana chuki zenu binafsi za upemba na uunguja, hayo yote yanajulikana waunguja mlidai kwa miaka mingi sana mpemba hawi mwenyekiti wa baraza la mapinduzi sasa kiko wapi? Mwaka huu CCM imewaweza wagombea wote wapemba kazi kwenu kunyoa ama kusuka.Pia kumbuka amani iliyopo Zanzibar ni matokeo ya muungano vinginevyo visiwa hivyo vingegeuka Somalia. Siku nyingine kabla hujatoa maoni muulize babu yako ili upate maana kamili ya muungano. Zanzibar ndiyo inayonufaika na muungano huu, gharama kubwa za kuendesha muungano zinabebwa na Tanganyika, kama hujui ulizia deni la Tanesco.
 
Watu wengine ni kama walevi vile, eti unaenda kulala Mtanzania ukiamka Mtanganyika au Mzanzibar na nchi iliyojulikana kama Tanzania haipo tena katika ramani ya dunia. Hilo ndugu zangu lawezekana tu katika ndoto yaani kama vile katoto kanalala kanaota kameokota hela halafu kanamka mikono mitupu ! Mliona wapi nchi ikisambaratika kirahisi hivyo, watu wanakaa kwenye kamkao kama ka kahawa wakitoka humo oh, sisi sasa ni nchi kamili na si sehemu ya iliyojulikana kama Jamhuri ya Tanzania. Ninavyofahamu mimi baraza la wawakilishi Zanzibar haliwezi kupitisha katiba inayopingana na katiba ya Tanzania, na kufanya hivyo ni sawa na kutangaza vita dhidi ya taifa la Tanzania - ni uhaini per se ! Anayetaka nchi ya Zanzibar ajitokeze waziwazi na kama ana ubavu atamke anauvunja Muungano huu - it simple ama ni muungano au ni nchi mbilii, vyote viwili haviwezekani, period.
 
Kinachoniishangaza kwa wale wanaoona kuwa Zanzibar inataka kujitutumua kutoka katika katika makucha ya Watanganyika - kutoa hoja zisizo msingi, kwa mfano kusema wazanzibari wanalishwa na kusomeshwa na Tanganyika ni hoja ya kitoto kwani yale ni mashirikiano ambayo yanafanywa na nchi mbali mbali. Ni watanganyika wangapi wamesomeshwa bure na Warusi na Wachina?. Au kuzungumzia wazanzibari kuwepo Tanganyika mbona Watanganyika wako sehemu nyingi tu duniani ikiwemo hapa Zanzibar? Linalotuudhi wazanzibari ni tabia ya Watanganyika kuja Zanzibar na kufanya chokochoko za kisiasa kwa kushirikisha katika matawi ya CCM na baadae kufanya maamuzi kwa maslahi ya Tanganika.Ni kawaida kuona Mbara alofika Zanzibar kwa kipindi cha miezi sita tu kuwa katibu wa Tawi la CCM au Sheha wa shehia fulanii na baada ya hapo anakaribisha wenzake ili wawe na sauti katika masuala yanayowahusu Wazanzibari. Munadhani hizi maskani zinazoleta chuki visiwani kama vile Kisonge washika dau wakubwa ni kina nani?

Wazanzibari wanapokuja Bara ni kwa ajili ya kutafuta maisha tu na hawajiingizi katika siasa na hata akitaka kufanya hivyo hatoruhusiwa kutokana na mtandao ulowekwa wa kuwapiga vita.Ukimuona Mzanzibari yumo katika siasa za Tanganyika ni katika ngazi ya Kitaifa kwa kupitia katika MUUNGANO.

Yako mengi yanayotukera kwa mfano utasikia nchi ya watu milioni 40 yenye eneo kubwa haiwezi kuilinganisha na watu milioni moja na yenye eneo dogo lakin munasahau kuwa hata inagalikuwa nii mtu mmoja na yenye ukubwa wa maili moja lakini ilikuwa na hadhi ya nchi na tulipoungana hatukukubali kuuza utu wetu kwenu.Sisi Wazanzibari tunaamini tuna haki sawa katika Muungano huu iwe katika kuchangia katika gharama za kuuendesha na katika faida yake.

Kama munaona munaonewa na hamna maslahi na MUUNGANO huu kwa nini hamtoi maoni ya kuurekebisha na kama haiwezekani kuuvunja tu moja kwa moja na mutafute koloni jengine la kutawala.


Hapo palipo na rangi.
Binafsi nafikiri unawakosea wabara, hizo siasa za chokochoko ni asili ya local people. Hii si kwa sababu ndo ilivyokuwa toka awali bali imetokana na utawala wa kiarabu.

Kwa ka takwimu kifupi kabisa KOMORO na ZANZIBAR ni kama maji na samaki sasa ni nani anayetia chokochoko kule ama nini utofauti wao na ZANZIBAR? kama hiyo haitoshi kaangalia Somalia, Sudan djibuti ni hasa nani mwenye influensi nchi zile.

As per uhuru, nafikiri acha wazanzibar wandanganywe na OMAN pamoja na SAUDIA. Juzi OMAN imerudisha wasomali 2000 bila kujali wapi wanakwenda na huko wanakopelekwa, paka umoja wa mataifa umekuja juu, lakini Oman hawasikilizi LAZIMA kelebu arudi kwao.

Above all, Yemen ina border na Saudia, but Yemen ni moja ya poorest country.
 
Whatever the wording, ilimradi Hati za Muungano ziko palepale na zinafuatwa, does it really matter? Kama Zanzibar ni nchi kamili inajulikana Umoja wa Mataifa? Na umewahi kuona nchi gani iko ndani ya nchi nyingine? Na kama iko ndani ya nchi nyingine itakuwaje na international legal personality? Na kama haina international legal personality basi hiyo SI NCHI!

Ni sawa na mtu anayeishi katika nyumba ambayo hajarithishwa bado. Hati za nyumba ni za babake ambaye bado yuko hai, na hakuna inayoonesha kuwa kamrithisha huyo mwanae nyumba hiyo. Katika kujifurahisha tu, mtoto anabandika bango mlangoni lenye jina lake linalosema 'HII NI NYUMBA YANGU'. Sidhani kama bango hilo litammilikisha hiyo nyumba.

Hivi kwa mfano Zanzibar wakisema kwenye katiba yao kuwa Rais wa Zanzibar atateua mabalozi wa kuiwakilisha Zanzibar nchi za nje, kwamba ataunda wizara mpya zikiwamo za Ulinzi, Mambo ya Nje nk (zile ambazo sasa ni za muungano), kwamba Zanzibar itajiunga UN, kwamba Rais wa Zanzibar ni Amiri Jeshi mkuu wa majeshi nk, je itakuwa hivyo kweli kwa kuwa katiba yao imesema? Au pengine kuna flaws kwenye katiba zote mbili (ya Zanzibar na ya Muungano) zinazoruhusu mkanganyiko huo wa kisheria?
 
Hiyo Serikali ya Tanganyika itatusaidiaje kuondoa umaskini? Tunashabikia vitu ambavyo mwisho wa siku tutajikuta tunarudi nyuma badala ya kusonga mbele! Zenj wanataka kujikabidhi OIC ili wapewe misaada na Waarabu, Wakoloni wao wa zamani, ndio hiyo move ya kujiita nchi ndani ya nchi!
whatever the case, let them decide on there own... 99.9% or Zanzibaris are moslems, what is wrong for them having close relation with other moslem nations... Hizi kasumba zimeshapitwa na wakati... Hebu tuangalieni jamani hapa Tangayika serekali imefanya nini...TABORA ,ARUSHA ,SONGEA, MWANZA,MARA,MTWARA,TANGA,PWANİ na mikoa mengine kuna maendeleo gani yakujivunia...Tusipachikwe kasumba ambazo hazina mpango...Tanzania ilitumia rasilimali zake na watu wake eti kusaidia harakati za ukombozi wa bara la Africa... Sasa hao tuliowasaidia wemesonga mbele sisi bado tumebakia na kasumba. Kwanini hatudai huduma bora za jamii kama vile maji ,umeme, hospitali za kisasa na elimu...Bado tumekwamishwa eti Zanzibar wanataka kuvunja muungano eti muungano usivunjike, bull shit. Kabla hujaangalia Zanzibar angalia maisha yako ya kila siku unapata huduma zote za kijamii? Nchi za nje mikoa inashindana kimaendeleo, sisi bado tumebakia na kasumba na walio wajanja wanakula nchi kidogo kidogo.
 
Tutake au mtake, tusitake au msitake, kwa marekebisho hayo Zanzibar imeshajitoa katika muungano.
Niliwahi kuandika humu kuwa wazanzibar walianza zamani kudai kidogokidogo na kila walivyodai na kukataliwa walitishia kuvunja muungano; kauli hii ikawa silaha yao kubwa ya kupata kila walichohitaji. Katika mambo aliyokuwa anadai Abdu Jumbe, wamebakiza moja tu la sarafu. Nilieleza wazi kuwa sarafu bila kuwa na uchumi imara haisaidii.
Lazima tukae tuzungumze, muungano katika hali ya sasa ni usanii - irudi nchi ya tanganyika.
Kutumia nguvu kulazimisha muungano uendelee katika hali ya sasa is unsustainable.
Nyerere alisema zitafutwe sababu za sasa za kuwa na muungano huu - ikiashiria kuwa zile za zamani zimepitwa na wakati!
Zanzibar siyo watoto wa kushindwa kujua athari na faida za kuvunja/kijuitoa katika muungano - wasing'ang'aniwe vinginevyo itaionekana madai yao kuwa wananyanyaswa ni ya kweli!

Muungano: Haupo maana wana nchi yao,bunge lao,katiba yao,wimbo wa taifa,bendera yao,mipaka yao. Huu tunaoita muungano ni Tanganyika,ndio maana kuna kuna kamati ya kurekebisha kero kati ya SMZ na Tanzania!!! kituko.
Kidogokidogo: Chama cha mpira, Bendera,wimbo wa taifa, sasa 'wamevunja' rasmi muungano
Tanganyika : Irudi hata leo, tena tuanze kutumia Tanganyika hapa JF effectively kwasababu Znz ''wameshajitoa'
Kutumia nguvu: hatuna sababu kwa vile we are not the loser in any way
Sasa tuangalie ajira, wabara warudi bara, wazenji waondoke bara huko katika ofisi za mawizara. Kama una nyumba au biashara Mznz awe kama nchi nyingine EA.
Hakuna muungano katika ardhi! period. Anzisheni sarafu yenu hata leo.
 
Muungano: Haupo maana wana nchi yao,bunge lao,katiba yao,wimbo wa taifa,bendera yao,mipaka yao. Huu tunaoita muungano ni Tanganyika,ndio maana kuna kuna kamati ya kurekebisha kero kati ya SMZ na Tanzania!!! kituko.
Kidogokidogo: Chama cha mpira, Bendera,wimbo wa taifa, sasa 'wamevunja' rasmi muungano
Tanganyika : Irudi hata leo, tena tuanze kutumia Tanganyika hapa JF effectively kwasababu Znz ''wameshajitoa'
Kutumia nguvu: hatuna sababu kwa vile we are not the loser in any way
Sasa tuangalie ajira, wabara warudi bara, wazenji waondoke bara huko katika ofisi za mawizara. Kama una nyumba au biashara Mznz awe kama nchi nyingine EA.
Hakuna muungano katika ardhi! period. Anzisheni sarafu yenu hata leo.
kinachoshangaza kwanini waTanganyika wana hofia sana kuvunjika kwa muungano?
 
AFTER ZANZIBAR REFERENDUM COMES: Constitution dilemma Send to a friend Tuesday, 10 August 2010 22:23 0diggsdigg

sengomvungi.jpg

By Bernard James and Beatus Kagashe

The constitutional amendments in Zanzibar on Monday evening, which redefined its territory as a sovereign state within the United Republic of Tanzania, have reignited the controversy over the future of the Union.

Constitutional experts faulted the changes endorsed by the House of Representatives, which they charged, were "meant to neutralise the Union, if not to kill it systematically".

With the Constitution of the United Republic proclaiming Tanzania to be a country resulting from the merger of Tanganyika and Zanzibar, as the one and only sovereign state, the experts were of the opinion that the recognition of Zanzibar as a state would "steal Tanzania's statehood". And they warned that this could herald the break-up of the United Republic of Tanzania.

An extraordinary session of the House of Representatives on Monday evening overwhelmingly passed 10 amendments, which also paved the way for the formation of a government of national unity in Zanzibar after October 31 General Election.

According to the amendments, Sections 1 and 2 of the Zanzibar Constitution, which previously identified Zanzibar as part of the United Republic of Tanzania, have been deleted.

The changes redefine Zanzibar is a state formerly known as the ‘People's Republic of Zanzibar' with its territory composed of Unguja, Pemba and all the small surrounding islands, as it was before the 1964 merger with Tanganyika.

Moving the Constitutional Amendment Bill, the State Minister (Constitution and Good Governance), Mr Ramadhani Abdallah Shaaban, said: "The new clause stipulates that Zanzibar is among the two countries that form the United Republic of Tanzania."

But a senior law lecturer at the University of Dar es Salaam, Dr Sengondo Mvungi, described the amendment as the biggest threat ever to the existence of the United Republic of Tanzania. He explained that the House of Representatives had disregarded the laid-down procedure by altering constitutional provisions touching on the Articles of the Union.

Dr Mvungi cited Article 98 (b) of the Union Constitution. Under the article, any Bill for an Act to alter any provisions of the Constitution or any provision of any law relating to any of the matters specified in List Two of the second schedule to the Constitution shall be passed only if it is supported by the votes of not less than two-thirds of all Members of Parliament from Tanzania Mainland and not less than two-thirds of all MPs from Tanzania Zanzibar.

And the matters specified in List Two, which require to be supported by two-thirds of all MPs from Mainland Tanzania and two-thirds of all MPs from Zanzibar, include the existence of the United Republic of Tanzania.

"This article of the Constitution cannot be altered by the Zanzibar House of Representatives alone. They have totally no mandate or authority on this issue," Dr Mvungi said.
He also pointed out that the fact that President Jakaya Kikwete had already dissolved Parliament in readiness for this year's elections, meant there was no room to initiate such changes.

Contacted for comment last evening, State Minister Shaaban strongly defended the amendments, saying they were meant to emphasize Zanzibar's position as a partner state in the United Republic and not a part of the Union Government.

"The United Republic is nation. The amendment means that Zanzibar is a second country forming the union between Tanganyika and Zanzibar. What we have done is to confirm our state boundaries," he said.
For his part, Dr Mvungi said that declaring Zanzibar one of the two countries that form the United Republic of Tanzania was to change the structure of the Union to form a confederal authority between the people to Zanzibar and Tanganyika.

"This means that Tanganyika retains its sovereignty and statehood and so does Zanzibar. So you form a confederation. The statehood automatically moves out of that the United Republic of Tanzania and goes to Zanzibar and Tanganyika," he explained.

"If the amendments are implemented there is not going to be a united republic of Tanzania. The nation has broken up," he said in a conversation with The Citizen on Monday before the Zanzibar approved.

Zanzibar's Attorney General could not be reached for comment yesterday, but a senior official in his Chambers said the amendments were the 10th on the Zanzibar Constitution. The changes, he clarified, only affected the Zanzibar Constitution and had nothing to do with the Union.

When The Citizen pointed out that the amendment of Union matters needed approval by two-thirds of the MPs from both Tanzania Zanzibar and Mainland Tanzania, Mr Saleh Mbarouk, said: "The interpretation of the changes will be given by the Attorney General. What I know is that members of the House of Representatives are not forbidden to pass such amendments."

But the Union Government's Deputy Attorney General, Mr George Masaju, contacted in Dar es Salaam to comment on the developments, said he had not seen the final draft of the Bill passed in Zanzibar on Monday.

"I'm hesitant to address this matter, as I have not seen the final draft. Give me time to find out what exactly has been passed by the House of Representatives in order to comment on the issue," he said.

Another lawyer, who asked not to be named because of the sensitivity of the matter, said the changes had violated the Constitution. He said Article 98 (b) of the Union Constitution stipulated the procedure for effecting amendments touching on the existence of the United Republic.

"Strictly speaking, such changes do not any value in the eyes of the law. They actually do not exist. They are unconstitutional," he said.

The president of the Tanganyika Law Society (TLS), Mr Felix Kibodya, speaking in his personal capacity, said although he strongly supported the reconciliation process that had culminated in the constitutional changes, the declaration that "Zanzibar is a state has gone beyond the aim of bringing Zanzibaris together".

He said that for the changes to have any legal authority, they must be endorsed by the Parliament of the United Republic of Tanzania, as specified in Article 98 (b).

"My understanding is that for the amendments making Zanzibar a state to have legal effect, they must have the blessings of parliamentarians from both sides through a procedure stipulated in our constitution," he said.

He added: "How can Zanzibar be a state without a commander-in-chief of the armed forces? How can it be a country without defence minister, Inspector General of Police or a foreign minister?"

He said though it was crucial to bring about peace and unity in the Isles, this should not come at the expense of the Union. "Zanzibar is a part of the United Republic of Tanzania," he insisted.

Under the newly amended Zanzibar Constitution, the Isles' President has been given powers to mark the territory's borders without consulting the Union Government.

According to the laws enacted by the House of Representatives, for effective implementation of government responsibilities, the Zanzibar leader is also empowered to divide the Isles into regions, districts and other areas.

Additional reporting by Salma Said, Zanzibar
Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
 
Hakuna Mzanzibari aliyeburuzwa, acha kupandikiza mawazo ya chuki kwa hasara ya nchi yetu!
hapa hapana mawazo ya chuki...hapa pana mawazo ya kusema ukweli tu... Watu bado mnakasumba eti muungano utavunjika ,eti CUF bla bla mimi nataka kama wewe mTanganyika kweli tueleze nini kikubwa chakujivunia? kwanini tutumie muda wetu au serekali kushikilia Zanzibar? kwanini tusiumize vichwa kuangalia Tabora, Mtwara,Shinyanga na mikoa mengine kuna nini kikubwa cha kujivunia? Hii tabia ya kutaka kuwaamulia watu wengine maisha yao sisi inatunufaisha nini? :confused2:
 
Mkuu Watanganyika hawa hofii kuvunjika kwa Muungano, isipokuwa Wazanzibar wanashindwa kusema mazi kwamba wanataka kuuvunja Muungano isipokuwa wanadai madaraka zaidi na zaidi pasipo kutaka kuuvunja Muungano.
Wee nambie kiongozi hata mmoja wa Visiwani aliyewahi kusema wazi tuuvunje Muuungano.
 
Mkuu Watanganyika hawa hofii kuvunjika kwa Muungano, isipokuwa Wazanzibar wanashindwa kusema mazi kwamba wanataka kuuvunja Muungano isipokuwa wanadai madaraka zaidi na zaidi pasipo kutaka kuuvunja Muungano.
Wee nambie kiongozi hata mmoja wa Visiwani aliyewahi kusema wazi tuuvunje Muuungano.
Mkuu uwoga na undumila kuwili umewashika.
 
Something like this could only happen under the watch of a leader of the calibre of Kikwete - weak, apprehensive and incompetent. Hata kamba hukatikia pabovu na haya yote ni matokeo ya kuparamia uongozi bila uwezo, ujasiri wala upeo wa kuona mbali. Nakumbuka na Pemba nao waliwahi kutoa madai ya kutaka wajitenge na kutoa sababu zinazofanana na hizi hizi na hawa walevi - ndio nawaita walevi kwani sidhani mtu mzima na akili zake timamu aweza kukurupuka kama hawa wapuuzi. Wangekuwa si watu wapuuzi wangetumia kikao chao hicho kuutangazia ulimwengu kuwa Zanzibar sasa ni nchi kamili na tokea sasa inataka itambuliwe hivyo. Hivyo ndivyo wanaume wanavyofanya na kamwe hawajipitishipitishi kwa kudai kwamba pamoja na kuwa nchi kamili bado wamo kwenye muungano - kwani bado wana hamu ya kupakatwa ? Kikwete hakika ataingia kwenye historia kama kiongozi aliyesimamia taifa la Tanzania likivunjika vipande vipande huku akiwachekeachekea wahaini waliopaswa kuswekwa lupango kama anavyowachekeaga wahalifu wote wale.
 
Something like this could only happen under the watch of a leader of the calibre of Kikwete - weak, apprehensive and incompetent.

Exactly, and you know what him could b thinking this is democracy!!!!!!!!
 
URUSI lilivunjika, sasa kwa nini isiwe Tanzania!! Kuna faida gani kati ya Zenj na Tanzania bara kuungana? Hata hii EAC ya sasa itavunjika tu! Labda tuangalie Miungano ambayo haijavunjika mpaka sasa kama ile ya USA na UK, je ni kwa nini? Je, mifumo au vigezo vya Muungano ni wazi na mizuri na inafaidisha kila aliyejiunga?

JK lazima atoe tamko kwenye hili na ajiandae kuyumbishwa na Nuclear scientist kama atashinda uchaguzi mkuu!!!!!!!!!
 
Tuambie katika bajeti ya ZNZ Billion 500, pungufu kuliko bajeti ya waizara ya Elimu Tanganyika, Zanzibar inaweza au inachangia kiasi gani!!!
Hivi unakumbuka bara walipotaka kuwe na visa kama zenj, nini kilitokea? Waznz walijua kuwa watakuwa loser! By any account ni wabara wangapi wanategemea Znz as compared to Waznz wanaotegemea 40 milion population Buisness and Market. Viongozi wanawadanganya in the end mwananchi wakawaida ataathirka. Hawataki muungano waznz tuvunje tu we have nothing to lose!
NAIPENDA TANGANYIKA, kama alivyoshauri RedDevil [kama sijakosea], I'm proud to be TANGANYIKA. TANGANYIKA FOR EVER

Kama ulisoma maelezo yangu ni kuwa biashara sio lazima kuwa na muungano ni nchi ngapi zinafanya biashara na hazikuungana na hata nyengine si marafiki kwa mfano Marekani na China. Kumbuka kuwa ikiwa nchi ina utaratibu mzuri inaweza kufaidika zaidi na wafanyabiashara walioko nchini kwao na huwasajiisha kuwepo.

Na kuhusu kuchangia watachangia kutokana na faida wanayoipata, kwa mawazo yangu ni kuwa Muungano huu ni wa nchi mbili zilizoungana bila kujali wingi wa watu na eneo la ardhi - kwa hivyo mgawanyo ni uwe asilimia 50 kwa 50 kwa faida na mchango wa kuendesha shughuli za Muungano ama palee upande mmoja unapokuwa hauwezi kufanya hivyo ( uwezekano mkubwa ni Zanzibar) basi upande mwengine unaweza kuzipa pengo hilo na kuchukua faida pia kwa asilimia ile ile iliyochangia uendeshaji.

Hayo yanawezekana tu ikiwa pana nia njema na sio kama sasa hivi ambapo mafuta yanaambiwa ni mali ya Muungano lakini rasilimali nyengine hata zinakaribiana na mafuta kama gesi zinaambiwa ni za Tanganyika tu.
 
Hapo palipo na rangi.
Binafsi nafikiri unawakosea wabara, hizo siasa za chokochoko ni asili ya local people. Hii si kwa sababu ndo ilivyokuwa toka awali bali imetokana na utawala wa kiarabu.

Kwa ka takwimu kifupi kabisa KOMORO na ZANZIBAR ni kama maji na samaki sasa ni nani anayetia chokochoko kule ama nini utofauti wao na ZANZIBAR? kama hiyo haitoshi kaangalia Somalia, Sudan djibuti ni hasa nani mwenye influensi nchi zile.

As per uhuru, nafikiri acha wazanzibar wandanganywe na OMAN pamoja na SAUDIA. Juzi OMAN imerudisha wasomali 2000 bila kujali wapi wanakwenda na huko wanakopelekwa, paka umoja wa mataifa umekuja juu, lakini Oman hawasikilizi LAZIMA kelebu arudi kwao.

Above all, Yemen ina border na Saudia, but Yemen ni moja ya poorest country.

Kama nimewakosea nawaomba radhi lakini msimamo wangu uko pale pale na nakusikitia sana Mkuu kama bado una mawazo kuwa Wazanzibari hawajui kuwaza wenyewe na kujua lipi zuri na baya bila ya kuwashirikisha waarabu. Kwa taarifa yako waarabu waliondoka Zanzibar baada ya Mapinduzi matukufu ya 1964 wakiwa hawana kitu( bila kupora utajiri ulokuwepo Zanzibar) ninalotaka kukufahamisha ni kuwa walipotawala Zanzibar hawakuhamisha chochote na kukipeleka kwao na ndio maana hadi mwishoni mwa miaka ya sabini Oman ilikuwa ni moja ya nci masikini duniani na walokuweko huko walikimbilia huku, ila baada ya mabadiliko yaliyotokea huko nchi yao ilinyanyuka kiuchumi na hakuna muarabu alo na ndoto ya kurudi kuja kutawala Zanzibar ila ni watanzania kutoka Zanzibar, Kigoma,Tabora, Shinyanga nk ndio wanaokimbilia huko.

Hii nyimbo ya Waarabu ndio kati ya hizo chokochoko munazotia kuwatisha watu wagawane ili Zanzibar iwe chini ya makucha ya Tanganyika.
 
nenda ukalime wewe kabwela... tarehe ya muungano inajulikana na kwahiyo sio kitu cha ajabu kama tu waTanganyika wakisema nawao basi muungano huu inawezekana kuvunjwa... ninacho amini mimi ni kuwa waZanzibari wamechoka kuburuzwa ....this is the beginning of the end...

Hivi Wazanzibari wanaburuzwa nini jamani. Elimu wengi wameipatia bara UDSM, SUA n.k. hivyo kuwatoa tongo tongo nakuanza sasa kuzungumza. Chakula kwa kiasi kikubwa kinatoka bara (mchele, mahindi, maharage kutoka mikoa ya Mbeya, Morogoro, Shinyanga n.k.). Sasa badala ya kutushukuru kwa kuwasomesha na kuwalisha wao wanajitia ujuaji usio na mantiki.
hiyo unayosema wewe ni biashara ,mteja hana ulazima wa kumshukuru muuzaji kwani ameshalipa fidia ya alicho nunua....kabla ya muungano Zanzibar wilikua wakiagiza vitu vingi kutoka bara Asia, na sehemu nyengine....Zanzibar ipo kwa miaka isiyopungua mia tano...muungano upo kwa miaka 46 tu... Zanzibar wanaweza kuishi bila ya muungano...haina maana kama hawata nunua mahindi ,mtama ,viazi na karanga kutoka Tangayika...Kwani hao wanaolima wanahitaji wanunuzi... Kwanini Tanganyika ilazimishe muungano kama kweli wao ndio wanao beba mzigo mkubwa...DOES N'T MAKE SENSE !:confused2:
 
Back
Top Bottom