Zanzibar Kuwa Nchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zanzibar Kuwa Nchi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by X-PASTER, Aug 9, 2010.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  Aug 9, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Zanzibar Kuwa Nchi

  Na Hassan Shaaban, Zanzibar

  SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) inafanya marekebisho ya katiba ya mwaka 1984, ambayo yanaipa Zanzibar hadhi kamili kama nchi ndani ya Jamhuri ya Muungano.

  Marekebisho hayo ya katiba yanatarajiwa kuwasilishwa katika kikao cha Baraza la Wawakilishi kinachoanza leo Zanzibar, ambapo pia yataruhusu kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa baada ya uchaguzi wa Oktoba mwaka huu.

  Kwa mujibu wa rasimu ya marekebisho ya katiba hiyo, sura ya kwanza ibara ya kwanza iliyokuwa ikisomeka, Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imefutwa chini ya marekebisho hayo.

  Rasimu hiyo ambayo itawasilishwa na Mwanasheria Mkuu, Idd Pandu Hassan, inapendekeza kifungu hicho sasa kisomeke ‘Zanzibar ni nchi ambayo eneo la mipaka yake ni eneo lote la visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na visiwa vidogo vilivyoizunguuka na bahari yake, ambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar iliitwa Jamhuri ya watu wa Zanzibar’.

  Aidha, marekebisho hayo ya katiba yamegusa kifungu cha pili na kueleza kuwa Zanzibar ni miongoni mwa nchi mbili zinazounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Marekebisho hayo pia yamegusa mamlaka ya rais katika kuigawa Zanzibar katika mikoa, wilaya na maeneo mengineyo kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi.

  Kabla ya marekebisho hayo kifungu cha pili cha Katiba ya Zanzibar kilikuwa kikisomeka ‘kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za serikali, Rais wa Jamhuri ya Muungano akishauriana na rais anaweza kuigawa Zanzibar katika mikoa, wilaya na maeneo mengineyo kwa kufuata utaratibu uliowekwa’.

  Marekebisho hayo pia yamempa uwezo Rais wa Zanzibar kuteua wakuu wa mikoa bila ya kushauriana na Rais wa Jamhuri ya Muungano, kama ilivyokuwa kabla ya marekebisho hayo.

  Marekebisho hayo ya 10 ya Katiba ya Zanzibar iwapo yatapitishwa na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi yatamaliza msuguano uliokuwa umejitokeza kuhusu nafasi ya Zanzibar katika Jamhuri ya Muungano, baada ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda, kudai kuwa “Zanzibar si nchi”.

  Hata hivyo, baadaye Rais Jakaya Kikwete akitoa ufafanuzi wa suala hilo alisema Zanzibar ni nchi ndani ya Jamhuri ya Muungano, lakini “Zanzibar si nchi nje ya Jamhuri ya Muungano kama ilivyo kwa Tanganyika. ”

  Aidha, marekebisho hayo ya katiba yanampa uwezo Rais wa Zanzibar kuteua makamu wawili wa rais, akiwamo makamu wa kwanza ambaye atateuliwa baada ya rais kushauriana na chama kilichoshika nafasi ya pili katika kura za rais kwenye Uchaguzi Mkuu.

  Rais pia atamteua makamu wa pili wa rais ambaye atakuwa ndiye mtendaji mkuu wa shughuli za serikali ndani ya Baraza la Wawakilishi
  Wakati wajumbe wa Baraza la Mawaziri watateuliwa kwa uwiano wa viti vya wajumbe ndani ya Baraza la Wawakilishi.

  Pia mswada huo unafuta wadhifa wa Katibu Mkuu Baraza la Mapinduzi na kuweka Katibu Mkuu Kiongozi, ambapo pia kutakuwa na makatibu wakuu wa ofisi ya makamu wa kwanza wa rais na katibu mkuu ofisi ya makamu wa pili wa rais.  Tanzania daima
   
 2. P

  Pokola JF-Expert Member

  #2
  Aug 9, 2010
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Suala la kuwa Z'bar ni nchi au kinyume chake liliwahi kuzungumziwa na mahkama ya Rufaa katika kesi ya Jamhuri dhidi ya Said Machano na Wengine 14, [1994] na iliamuliwa kuwa ZANZIBAR SI NCHI. Kesi hii ilikuwa inahusisha jamaa walioripotiwa kujaribu bila mafanikio kupindua serikali (felonious treason). Kuna mambo ambayo ni lazima yawepo ili treason itokee, ikiwa ni pamoja na serikali inayohusishwa kuwa na mamlaka ya kuendesha NCHI. Kwa kuwa Zanzibar haikuwa na hadhi ya nchi, jamaa waliachiwa huru.

  Mimi nimekuwa mdau wa karibu sana wa siasa za Zanzibar, na kwa bahati nzuri naishi huku. Hisia za wenzetu wazanzibari ni kuwa wabara wamewakandamiza na kuwa ni wanyonyaji, walanguzi na ambao wanawaamulia wazanzibari viongozi. Eg. Shein si chaguo la wazanzibari. Ni Bilal. Sasa wamechoka, kwa kuwa wanaona muungano huu ni kandamizi.

  Niliwaona wakiimba katika kampeni za kuhamasisha kura ya maoni,..
  :playball:...sasa seif na karume shikaneni mikono, muende dukani...,
  eeee, mkamnunulie MLANGUZI kanzu.. ee, avae ajionee aibu...:playball:
   
 3. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #3
  Aug 9, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Kuna sehemu ya marekebisho hayo ambayo inasomeka hivi: Kutakuwa na Rais wa Zanzibar ambaye atakuwa mkuu wa nchi ya Zanzibar...
   
 4. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #4
  Aug 9, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Whatever the wording, ilimradi Hati za Muungano ziko palepale na zinafuatwa, does it really matter? Kama Zanzibar ni nchi kamili inajulikana Umoja wa Mataifa? Na umewahi kuona nchi gani iko ndani ya nchi nyingine? Na kama iko ndani ya nchi nyingine itakuwaje na international legal personality? Na kama haina international legal personality basi hiyo SI NCHI!
   
 5. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #5
  Aug 9, 2010
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Hizo ni ndoto mambo vilevile, Zanzibar ni Tanzania na kama hawapendi waende comoros.
   
 6. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #6
  Aug 9, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Hizi zote ni "calculated movements" za CUF ambazo ni anti-Muungano!
   
 7. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #7
  Aug 9, 2010
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Yetu macho!
   
 8. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #8
  Aug 9, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Nakumbia cha ajabu hao CUF wakishika madaraka ndo utashangaa watavyopigania kuimarisha muungano kisiri siri. CCM zanziba ndo inaweza kuvunja muungano na sio CUF am telling you.
   
 9. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #9
  Aug 9, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,324
  Likes Received: 1,791
  Trophy Points: 280
  Pamoja na kelele zote zile za kuukebehi muungano mwisho wa siku mechi imeisha bila kupata ushindi.Sidhani kama kuna lolote la maana linaloendelea zaidi ya kujazana maneno tu halafu ikifika jioni twaishia kwenda kulala tumechosha koo zetu na kupoteza muda kwa kutotumia akili zetu kujiletea maendeleo. Jamani, tupunguze sound tuanze kuchapa kazi.Tumezidi kipimo cha kawaida na hizi sound tunazopiga, lol.
  Muungano huu naona kama ni ngumu sana kuuvunja kwa sound hizi tunazopiga piga.
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Aug 9, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Huu ni uhaini; na Kikwete akiruhusu mabadiliko hayo atashtakiwa kwa kuvunja Jamhuri yetu. As simple as that.
   
 11. W

  WaMzizima Senior Member

  #11
  Aug 9, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 154
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Jamani mnasahau kuwa tunaishi kwenye Jamhuri ya muungano, yaani NCHI mbili ziliungana Tanganyika na Zanzibar...Sasa suala la wazanzibari kuendeleza uzalendo wao mio sio kama ni tatizo kwenye muungano, suala hapa ni jee waTanganyika wao uzalendo uko wapi? Kuna nchi au tuseme dola nyingi tu ambazo ni muungano wa nchi kadha nyingine zimedumu (kama hapa kwetu) nyingine zimeshindwa (USSR, Yugoslavia, Somalia). Lakini hata uingereza ni muungano wa nchi nne, ambazo zina mabunge yao na mawaziri viongozi, ingawa mkuu wao ni Malkia. Hapa kwetu tunae Rais wa Jamhuri wa muungano lakini hiyo haizui Zanzibar kuwa na rais, bunge, bendera, wimbo wao wa taifa na hata timu yao ya mpira kama wakitaka, hivyo ndivyo ilivyo UK ambapo Scotland, Wales, Northern Ireland wote wana waziri kiongozi, nyimbo za taifa, bunge, bendera na hata timu tofauti za football ilhali England ni kama Tanganyika yaani haina bunge inatumia bunge la muungano.

  Swala ni jee tunahitaji serikali ya Tanganyika au la? mi binafsi sioni umuhimu wake...sababu ku ni kuwa hii itadhoofisha muungano ambao naamini kuwa bado ni mzuri na najua wazanzibari wengi na watu wa bara wanauunga mkono.
   
 12. W

  WaMzizima Senior Member

  #12
  Aug 9, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 154
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Upi sasa yaani katika hayo mabadiliko lipi hasa limekugusa?

  Na swala la msingi iwapo Wazanzibari au tuseme Watanganyika wakiamua kwa kura za maoni kuvunja muungano itakuwaje?

  Swala mi nadhani ni kuruhusu uhuru wa kutoa mawazo kuhusu mapungufu kadhaa ya huu muungano wetu, kama huu muafaka umeweza kuzungumzia baadhi ya hizo kero basi ni well and good, naimani kuwa viongozi wengi tu na wanchi kwa ujumla pande zote mbili bado wana imani na muungano swala ni fine tuning ili uweze kudumu zaidi, ukumbuke kuwa nchi zote ambazo zina muungano wa kudumu hufanya mabadiliko mara kwa mara mfano marekani
   
 13. takashi

  takashi JF-Expert Member

  #13
  Aug 10, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 909
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nyinyi mlivyoiuwa Tanganyika mlitegemea na waZanzibari watafuata ...ZANZIBAR ipo pale pale na hiyo Tanganyika mtairushida tena kama zamani muda sio mrefu sana...acheni kupoteza muda wenu kuishikilia Zanzibar... kuna mikoa mingi hapa Tanganyika inahitaji kuangaliwa...
   
 14. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #14
  Aug 10, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Sidhani kama uongozi wa serikali hii upo tayari kuuvunja muungano.
   
 15. takashi

  takashi JF-Expert Member

  #15
  Aug 10, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 909
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  nenda ukalime wewe kabwela... tarehe ya muungano inajulikana na kwahiyo sio kitu cha ajabu kama tu waTanganyika wakisema nawao basi muungano huu inawezekana kuvunjwa... ninacho amini mimi ni kuwa waZanzibari wamechoka kuburuzwa... this is the beginning of the end...
   
 16. takashi

  takashi JF-Expert Member

  #16
  Aug 10, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 909
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hata kama CUF wanataka kuvunja muungano ni haki yao ya kikatiba ya kuwa na mawazo tofauti... muungano utakufa katika uhai wako( utashuhudia kuvunjika kwake) nchi ngapi ziliungana na kuvunja muungano ? kwanini isiwezekane Tanganyika na kuwa kama zamani? kuna mtu mmoja alisema hapa kuwa tatizo sio kuvunjika muungano bali waTanganyika hawapendelei kulitumia tena hili jina lao...inawezekana ikawa ni kweli...
   
 17. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #17
  Aug 10, 2010
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,342
  Trophy Points: 280
  Sina tatizo na wao ''kuvunja'' muungano! wameanza muda mrefu. Ningependa kuona haya yanafuatia.
  1. Serikali ya Tanganyika, kama alivyoshauri Jumbe, Jaji Kisanga etc.
  2. Bunge letu lisiwe na wazanzibar 80 ambao wanaamua hatima ya nchi yetu hali wana ya kwao.
  3. Serikali ya Tanganyika iwe na wizara na waajiriwa watanganyika, wazanzibar wawe kama wa nchi za EA.
  4. Suala la kodi, biashara, maliasili ikiwa ni pamoja na ardhi zishughulikiwe na kila serikali, ya Tanganyika na Zanzibar bila kuingiliana kama ilivyo kwa EA.
  5. Tuwaulize wazanzibar je wangependa kuwa na federation? kura ya maoni iwe kwa wazanzibar
   
 18. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #18
  Aug 10, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  JK ndiye aliyedai kuwa Zanzibar ni nchi ndani ya Muungano, sasa unategemea atakosoa nini hapa kama si kujitakia matatizo?
   
 19. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #19
  Aug 10, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Tanganyika ya zamani za mjerumani ilikuwa na Rwanda na Burundi, kwa hiyo unataka turudi huko, maana tunapenda mipaka iliyowekwa na wakoloni kuliko tuliyojiwekea sisi wenyewe!
   
 20. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #20
  Aug 10, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Hiyo Serikali ya Tanganyika itatusaidiaje kuondoa umaskini? Tunashabikia vitu ambavyo mwisho wa siku tutajikuta tunarudi nyuma badala ya kusonga mbele! Zenj wanataka kujikabidhi OIC ili wapewe misaada na Waarabu, Wakoloni wao wa zamani, ndio hiyo move ya kujiita nchi ndani ya nchi!
   
Loading...