#COVID19 Zanzibar: Kila Mzanzibar anayetaka Chanjo ya COVID-19 atapata, hakuna mgeni ataingia bila cheti cha Vipimo vya Corona

Hii ndio Taarifa iliyotolewa na Waziri wa Afya wa serikali ya Mapinduzi , Mh Nassoro Mazrui , lengo ni kudhibiti maambukizi ya wimbi la tatu

Bado haijafahamika kama wageni kutoka Tanganyika nao watahusishwa au la .

Chanzo : ITV

View attachment 1827101
Wageni ni wageni ,Watanganyika Kwa Zanzibar pia ni wageni,

Aisee yesu njoo katiba ije, alisikika bibi mmoja Arusha, tuna muungano wa ajabu mno, katiba ,katiba
 
Sidhani kama kuna haja hiyo, kama Katiba ya Jamuhuri haitambui Zanzibar kama nchi bali ni sehemu ya muungano hiyo inatosha.
Yani ni kama vile tuseme Palestina ijiite nchi huru yenye mipaka, rais na bendera yake na huku UN haiitambui Palestina kama nchi, basi ujue Palestine sio nchi.

Hivyo basi katiba ya Zanzibar ata iandike Mara 100 kuwa Zanzibar ni nchi huku katiba ya Jamuuri ya muungano haitambui hilo basi ujue Zanzibar sio nchi.
Bora Zanzibar ipo na ina serikali, wewe TANGANYIKA ya kwako iko wapi ? Ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sio nje ,TANGANYIKA ni koloni la Zanzibar,

Kwamba Zanzibar ananguvu , kawatia Watanganyika kitanzi,wapi waishi, wapi waajiriwe, wapi wapate ardhi ,wapi wasafiri KWA passport, ila wao hakuna limit Tanganyika na Zanzibar ni yao na ruksa popote pale

Alafu utawasikia kuandika barua UN kutaka mamlaka kamili, huku wakijua ndani ya Muungano walishaimeza TANGANYIKA ,KWA kweli Kama watataka mamlaka kamili kwanza warudishe Tanganyika yetu,
 
Hii haijakaa vizuri, ninavyofahamu mimi Zanzibar ni sehemu ya Jamuhuri ya Tanzania hivyo anayepaswa kutoa kauli hiyo ni Serikali ya Jamuhuri ya Muungano.

Ila kwa kuwa humu Jf tunawanasheria wazuri, nina imani tutapata elimu juu ya hili
Afya sio ishu ya Muungano. Hebu rudi darasani kidogo utambue mambo gani ya ni ya Muungano na mengine si ya Muungano...

Maana usipoyajua iko siku utauliza kwanini mama Samia hajamtumbua mkuu wa mkoa wa Unguja Kaskazini...
 
Sidhani kama kuna haja hiyo, kama Katiba ya Jamuhuri haitambui Zanzibar kama nchi bali ni sehemu ya muungano hiyo inatosha.
Yani ni kama vile tuseme Palestina ijiite nchi huru yenye mipaka, rais na bendera yake na huku UN haiitambui Palestina kama nchi, basi ujue Palestine sio nchi.

Hivyo basi katiba ya Zanzibar ata iandike Mara 100 kuwa Zanzibar ni nchi huku katiba ya Jamuuri ya muungano haitambui hilo basi ujue Zanzibar sio nchi.
Katiba haipo sahihi.
Zanzibar huchukuliwa Kama sehemu ya muungano katika Mambo yale tu yaliyo ya muungano.
Katika Mambo yasiyo ya muungano Zanzibar ni nchi yenye maamuzi na madaraka kamili .
 
Hii ndio Taarifa iliyotolewa na Waziri wa Afya wa serikali ya Mapinduzi , Mh Nassoro Mazrui , lengo ni kudhibiti maambukizi ya wimbi la tatu

Bado haijafahamika kama wageni kutoka Tanganyika nao watahusishwa au la...
Duh hayo nayo Mambo...nadhani ni sawa ili kureduce the outbreak
 
Afya sio ishu ya Muungano. Hebu rudi darasani kidogo utambue mambo gani ya ni ya Muungano na mengine si ya Muungano...

Maana usipoyajua iko siku utauliza kwanini mama Samia hajamtumbua mkuu wa mkoa wa Unguja Kaskazini...

Hapo hapo masuala ya Uhamiaji ni mambo ya Muungano.
 
Katika huu muungano kuna mambo ya muungano na yasiyo ya muungano. Masuala ya afya si Jambo la muungano.

Kuna haja mashuleni kuanzia shule ya msingi kuwepo mada rasmi juu ya huu muungano.

Na masuala ya Uhamiaji ni ya Muungano.
 
Nyie kaeni na ujinga wenu! Msisahau rais wa Znz ni medical doc hivyo anatenda yapasayo. Safi Znz, zuia hao bara wasiwaletee makorona kwa ujinga wao!
Nyie endeleeni kuimba mapambio ya mwenda zake mkaendelee kupukutika!
 
Sidhani kama kuna haja hiyo, kama Katiba ya Jamuhuri haitambui Zanzibar kama nchi bali ni sehemu ya muungano hiyo inatosha.
Yani ni kama vile tuseme Palestina ijiite nchi huru yenye mipaka, rais na bendera yake na huku UN haiitambui Palestina kama nchi, basi ujue Palestine sio nchi.

Hivyo basi katiba ya Zanzibar ata iandike Mara 100 kuwa Zanzibar ni nchi huku katiba ya Jamuuri ya muungano haitambui hilo basi ujue Zanzibar sio nchi.
Huu nao ni ujinga mwingine; kwani sherehe zile zinazofanyika siku nchi ya Zanzibar ilikua huru inafanyika kama nini? Au Rais Mwinyi anaongoza wilaya kama siyo Taifa?
 
Afya sio ishu ya Muungano. Hebu rudi darasani kidogo utambue mambo gani ya ni ya Muungano na mengine si ya Muungano...

Maana usipoyajua iko siku utauliza kwanini mama Samia hajamtumbua mkuu wa mkoa wa Unguja Kaskazini...
kama anapanga nani akawe rais zanzibar,kutumbua ni kazi ndogo sana kwake.
 
Hii haijakaa vizuri, ninavyofahamu mimi Zanzibar ni sehemu ya Jamuhuri ya Tanzania hivyo anayepaswa kutoa kauli hiyo ni Serikali ya Jamuhuri ya Muungano.

Ila kwa kuwa humu Jf tunawanasheria wazuri, nina imani tutapata elimu juu ya hili
Kuna mambo ya muungano na yasiyokuwa ya muungano.

au unadhani kila jambo ni la muungano?
 
Hii ndio Taarifa iliyotolewa na Waziri wa Afya wa serikali ya Mapinduzi , Mh Nassoro Mazrui , lengo ni kudhibiti maambukizi ya wimbi la tatu

Bado haijafahamika kama wageni kutoka Tanganyika nao watahusishwa au la .

Chanzo : ITV

View attachment 1827101

====

WANAOINGIA ZANZIBAR SHURTI CHETI CHANJO YA COVID-19

SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imeanza kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa Covid-19 awamu ya tatu na kutangaza wageni wote watakaoingia nchini kuhakikisha wanakuwa na vyeti vya chanjo vya ugonjwa huo.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Watoto, Nassor Ahmed Mazrui wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tahadhari ya ugonjwa huo kutokana na taarifa za kuingia kwa wimbi la tatu.

Mazrui alisema zipo baadhi ya nchi jirani zenye mahusiano makubwa na Tanzania ikiwemo Uganda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo(DRC) pamoja na Rwanda tayari wimbi la tatu la ugonjwa wa Covid-19 limeingia na serikali za nchi hizo zimetangaza karantini kudhibiti athari zaidi.

Aidha alisema kwa upande wa wizara tayari imejipanga kukabiliana na janga hilo kwa kutoa elimu kwa wananchi kuhusu dalili za ugonjwa huo huku vituo vyote vya afya vikiwekwa tahadhari za ziada.

‘’Wizara ya Afya inatoa tahadhari kwa wananchi kuhusu ugonjwa wa Covid-19 awamu ya tatu ambapo baadhi ya nchi za Ulaya na Asia umeanza kusababisha maafa makubwa na nchi jirani ya Tanzania...kuanzia sasa wageni wote watakaoingia nchini watalazimika kuonesha cheti cha chanjo kwa ugonjwa huo,’’alisema.

Aidha aliitaja mikakati mingine inayotarajiwa kuchukuliwa kukabiliana na janga hilo ikiwemo wananchi kuvaa barakoa pamoja na kuepuka mikusanyiko ya watu wengi isiyokuwa na sababu za lazima.

Kuhusu suala la chanjo ya corona kwa wananchi wa Zanzibar, alisema suala hilo linasubiri tangazo rasmi la Rais Samia Suluhu Hassan ambaye ndiye mwenye uamuzi wa mwisho.

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Mnazi mmoja Dk Abdallah Suleiman alisema wamejipanga kuhakikisha wafanyakazi wote kuanzia vituo vya afya hadi hospitali kuu wapo tayari kutoa huduma za dharura kwa wagonjwa watakaojitokeza wa Covid-19.

Alisema hadi sasa hakuna mgonjwa aliyetambuliwa kuambukizwa na ugonjwa huo huku akisisitiza hakuna taarifa za kuficha matukio ya ugonjwa huo.
View attachment 1827415
View attachment 1827414View attachment 1827416

Kichwa cha habari hii kimekaa vizuri sana:

"Kila Mzanzibari anayetaka chanjo atapata. Hakuna mgeni atakaye ingia bila cheti cha kupimwa .."

Zanzibar wamedhamiria. Tunasubiria kwa hamu watuambukize mema haya.
 
Fungia kote kabisa. Na bara pia. Siyo ulaya tu.
 
Hii picha ya mwisho ya huyo wazir imenifanya nimkumbuke yule Ustaadh CAG
 
Wameshajiridhisha na madhara ya muda mfupi na mrefu, spike proteins na lipid nanoparticles kwenye ovary na bone marrow.......thrombocytopaenia, effects za autoimmunity ambazo zinaweza kuchukua miaka kuanza kuonekana, uwezekano wa leukaemias na lymphomas, au wameamua kudemka tu kwamba wanachanja kila mzanziberi.....
 
Back
Top Bottom