gombesugu,JokaKuu,
Nimekusoma,khabar za siku tele ndugu yangu.
Binafsi nisingalipenda kuchambua kwa kina hapa,maana ni kweli usemavyo yakuwa haya majambo yameshajadaliwa mno humu Jf,tena kwa nyakati mbalimbali bila ya kupata usuluhishi/ufumbuzi!?
Hata hivyo nimependa yakuwa kama dasturi yako,unajitahidi mno kutumia lugha ya kiungwana.
Kuhusu huo mfano wako kiduchu ulotoa hapo mwisho wa hiyo bayana yako;ati Zanzibar imejifaragua kuongeza majimbo ya uchaguzi ili "ifanane" na Tanganyika/Bara!? Yaani imenilazim kucheka kiduchu....
Kwani hiyo population ya Zanzibar kwa sehemu mbalimbali visiwani mle ndo ile ile tangia ile 1964!?...haijawahi kuongezeka japo kiduchu!?
Sasa kama kuna mabadiliko/ongezeke la population kwenye maeneo/majimbo mbalimbali visiwani humo,sasa huoni yakuwa hali hiyo ndo ilofanza wao kukidhi haja ya kuongezeka kwa majimbo ya uchaguzi,badala tu ya kudai ati wamefanza/wanafanza hivyo kwa kutaka "kujifananisha" na hiyo Tanganyika!?
Nimefurahika tumezungumza japo kiduchu,nami tajitahidi kufuatilia huu mnakasha kwa utuvu.
Ahsanta.
He he hee! Misaada!
Barubaru,labda nikuulize Je huo mvungano wenu mtachangia kwa ratio ya watu, eneo au madaraka.
Je kwa Uoni wako Znz wanaweza shindwa wapi kama itaachwa huru kiuchumi na maamuzi?
Kumbuka kuwa Mvungano ni kama KOTI. kama utaona linakubana au kukutia joto si unalivua tu. Je kuna ubaya hapo?
sasa Povu zote za nini kuleta mitazamo ya kisiasa katika mambo ya kiuchumi hususan kwa Znz?
Pole sana
Si kweli, hakuna mzanzibar anayethubutu kudai nchi yake.
Wote wanaongea chumbani na uvunguni mwa vitanda, tena wanabweka wakiwa na wamefunga taulo mbela ya ahali zao. Wakitoka nje kimyaa! nitakueleza
1. Tuliwaambia kura ya maoni kuhusu mustakabali wa znz, mkagoma na kujiminya minya
2. Tukaawambia acheni msishiriki tume ya Warioba, mkudai wajumbe sawa hata kama hamjui wanalipwa na nani
3. Tukawaambia nyote mkatae serikali 1.2.3 kilichofuata ni muungano wa mkataba.
Mkagoma kuchomoa mnataka kujificha na kusetiri dhiki zenu kwa mgongo wa mkataba
4. Tukawaambia msichague wajumbe wa bunge la katiba, akili zenu zikwatuma mdai wajumbe zaidi
5. Juzi Wajumbe wa BLW walikuwa Dodoma wanakula msasa na posho, hawakugoma kuja.
Hakuna mzanzibar mwenye nyodo ya kukataa muungano. Tumeshathibitisha na tunasema wazi hakuna!
Ninyi mkae kimya tu mpate mafaio ya sasa na uzeeni. Mnapata mafao kuanzia mnasoma bura hadi kazi na uzeeni. Hakuna anayedai nchi, ni wapiga kelele tu wamejaa
Barubaru,
..muungano kati ya Tgk na Znz ni impossible kutokana na tofauti ya ukubwa wa eneo na idadi ya watu baina ya mataifa yetu.
..tofauti baina ya Tgk na Znz ni kubwa mno kiasi kwamba siku zote kutakuwa na malalamiko baina yetu.
..Znz ikitumia vizuri rasilimali zake, pamoja na kuwa na mahusiano mazuri ya kiuchumi na majirani zake, inaweza kabisa kusimama yenyewe nje ya muungano.
Tumewaambia katika midahalo makaongamano n.k. Hata maneno ya mwenyekiti wa kamati ya fedha yametoka maeneo kama JF, unajua amebeba kila kitu tulichosema. Unataka tuvute uzi kwa ushahidi?Nguruvi3.
Hapo ndio ninapoona mnajidanganya.
Ni wapi na lini mliwaambia wazanzibar hayo unayonena. Mliwaambia katika chombo gani rasmi cha habari au ndani ya Bunge au mdaharo gani wa wazi au hata katika Gazeti gani? naomba utufafanulie hapo.
Lakin pia kumbuka nchi yenu badi ni tegemezi na mara nyingi sana kunakuwa na njaa maeneo mbalimbali mpaka kufikia watu kula mizizi na hata wanyama kufa kwa njaa na ukame. Je umewahi kusikia Znz watu wanakufa njaa? Kwanini msiwatosheleze watu wenu kabla kuwapa jirani zenu Znz? Je ni akili hiyo?
Lakin kwanini muwaambie Znz wafanye na NYINYI MNAOGOPA NINI KUFANYA? Au ndo mnaogopa vivuli vyenu na fadhwila mnazopata kutokana na kuidhulumu Znz?
Lakin kwa kudhibitisha kuwa mna walakin. hebu fikiria Tanganyika ni ji nchi likuuumba kwenda kuungana na Znz yenye ukubwa wa idadi ya watu sawa na wilaya ya Ilala , tena muungano wa pasu kwa pasu. Je ni akili hiyo?
Mimi naona ni dhambi tu ya kunung'unika inawasumbua wakti wanzenu Znz wanalalamika mchana kweupeeee bila kumwogopa mtu wala nini.Poleni sana .
Wenzako walikuwa Dodoma juzi hawakusema hayo, walichukua posho wakapanda meli.Joka Kuu.
Mimi kama mtaalamu wa uchumi nasema Znz nje ya Muungano uchumi wake utakuwa kwa kasi sana na haya nilipambanua vizuri sana katika Uzi wa NINI FAIDA YA MUUNGANO KWA ZNZ.
Na kwa mtu yoyote mwenye akili timamu kabisa hawezi kukubali nchi yenye watu zaidi ya 45 Milioni ikaungane PASU KWA PASU na nchi yenye watu Milioni moja na nusu. Je inaingia akilini kweli?
Tena kwa muungano ambao ni HARAMU usiofata sharia za kimataifa ya kuunganisha nchi huru mbili huku nchi kubwa ikilazimisha huo Muungano. Je huoni kama Tanganyika kuna vitu wananufaika hapo? na manufaiko hayo kwa kutumia hiyo nchi ndogo yanafikiwa mpaka kuvimbiwa na kutaka kuifanya kama koloni lao.
ndio hao wanaoleta propaganda za kisiasa kusema Znz haiwezi simama pekee yake bila kutoa sababu za kiuchumi bali kuleta porojo za uzandiki pasi na kujua kuwa UCHUMI sio porojo ni taaluma inayojitosheleza
Free Znz.
Tumewaambia katika midahalo makaongamano n.k. Hata maneno ya mwenyekiti wa kamati ya fedha yametoka maeneo kama JF, unajua amebeba kila kitu tulichosema. Unataka tuvute uzi kwa ushahidi?
Kuhusu njaa, ndugu yangu nenda Pemba na Unguja uone. Lakini hilo si muhimu sana kwasababu njaa ipo kila mahali duniani.
Hakuna pasi pasu kaika muungano uliopo. Kilichpo ni sisi kubeba watu milioni 1. Labda unifahamishe hiyo pasu pasu ni kwa jambo gani. Hakuna kitu kama hicho, kilichopo ni kubebwa mgongoni hata mwenyekiti wa kamati ya fedha amesema.
Hivi unawezaje kuwa na pasu pasu ukiwa na mshirika asiyeweza hata kupia umeme.
Mwenyekiti wa kamati ya fedha kasema hamjawahi kutoa chochote kwa miaka 50 kwasababu ya uchumi. Kasema mwenyekiti wa kamati ya fedha ya BLW wakiwemo waliberali. Sasa kuna pasu pasu gani.
Tume ya warioba hamjui inagharamiwa na nani, pasu ipo wapi. Gharama za bunge la katiba ni zaidi ya bilioni 200. Pasu itoke wapi
Tunasema hivi kama mkija katika bunge la katiba mkubali yaishe.Kaa kimya hakuna kelele
BLW wakiwemo waliberali juzi walikuwa Dodoma raha mstarehe, hakuna aliyesimama na kudai znz! wamechukua posho wanaishia! wakiwa baharini wakali kweli kweli wakishatua Tanganyika kimyaa. Jusa alikuwepo pia.
Barubaru,Joka Kuu.
Mimi kama mtaalamu wa uchumi nasema Znz nje ya Muungano uchumi wake utakuwa kwa kasi sana na haya nilipambanua vizuri sana katika Uzi wa NINI FAIDA YA MUUNGANO KWA ZNZ.
Na kwa mtu yoyote mwenye akili timamu kabisa hawezi kukubali nchi yenye watu zaidi ya 45 Milioni ikaungane PASU KWA PASU na nchi yenye watu Milioni moja na nusu. Je inaingia akilini kweli?
Tena kwa muungano ambao ni HARAMU usiofata sharia za kimataifa ya kuunganisha nchi huru mbili huku nchi kubwa ikilazimisha huo Muungano. Je huoni kama Tanganyika kuna vitu wananufaika hapo? na manufaiko hayo kwa kutumia hiyo nchi ndogo yanafikiwa mpaka kuvimbiwa na kutaka kuifanya kama koloni lao.
ndio hao wanaoleta propaganda za kisiasa kusema Znz haiwezi simama pekee yake bila kutoa sababu za kiuchumi bali kuleta porojo za uzandiki pasi na kujua kuwa UCHUMI sio porojo ni taaluma inayojitosheleza
Free Znz.
wa mapato ya bilioni 240! kidogo kuliko ya manispaa ya Ilala.Yana nikhusu sana kumbuka Kitovu changu nilipozaliwa kilizikwa kule Kyanga, Mwera.
Itakuuma sana lakin ukweli laazima tutasema. Na waZnz wamestuka huo unyonyaji wanaofanyiwa na majirani zao.
Pole sana
Wenzako walikuwa Dodoma juzi hawakusema hayo, walichukua posho wakapanda meli.
Tunataka mpate znz yenye neema ili muendelee zaidi ndio maana tunasema susieni bunge la katiba ili mambo yaishe.
Mkija tu mumekubali kila kitu.
Nendenei mkajenge Dubai yenu hakuna wa kuwazuia tena tunawatakiwa heri muwe kama Luxenbourd au Emirate.
Hakuna anayewakatalia hilo, lakini basi onyesheni nia. Siyo kelele na posho.
Kung'ang'ania vyeo na ajira bila kujua zinatengenezwaje ni ukupe.
Miaka 50 mgongoni tumechoka, tuacheni tupumue
Na sisi tunasema tunawatakia heri wakapae na uchumi wao.Barubaru,
..nakubaliana na wewe 100% kwamba uchumi wa Znz unaweza kupaa.
..lakini hilo litategemea kama mtajipanga vyema na kutumia rasilimali zenu vizuri.
..pamoja nasimama ktk hoja yangu kwamba muungano hauwezekani kutokana na tofauti kubwa ya kieneo na population baina ya Tanganyika na Zanzibar.
NB:
..Mwakilishi hajasema kwamba Znz haiwezi kusimama peke yake na kupaa kiuchumi, bali amesema Znz haina uwezo wa kuchangia 50/50 masuala ya muungano. He also defended his views with data.
cc gombesugu, Nguruvi3
wa mapato ya bilioni 240! kidogo kuliko ya manispaa ya Ilala.
Kusomeshwa watoto bure ndio kunyonywa. Kulala usingizi na kuwasha taa hadi asubuhi bila bili ndio unnyonyaji
Kusubiri mishahara ya hazina ndio unyonyaji
Kwa bilioni 240 nani akanyonye. Hata TBL wana mapato makubwa zaidi ya hayo nani akanyonye ndama
Inaweza kabisa kusimama hakuna shaka. Ni nchi iliyokuwepo hakuna shaka juu ya hilo.Barubaru,
..muungano kati ya Tgk na Znz ni impossible kutokana na tofauti ya ukubwa wa eneo na idadi ya watu baina ya mataifa yetu.
..tofauti baina ya Tgk na Znz ni kubwa mno kiasi kwamba siku zote kutakuwa na malalamiko baina yetu.
..Znz ikitumia vizuri rasilimali zake, pamoja na kuwa na mahusiano mazuri ya kiuchumi na majirani zake, inaweza kabisa kusimama yenyewe nje ya muungano.
Na sisi tunasema tunawatakia heri wakapae na uchumi wao.
Tusichokitaka ni kelele za uongo. Mwenyekiti kasema katika serikali 3 hawawezi kuchangia hata asilimia 10. Maana yake ni kuwa zigo hilo alibebe Mtanganyika, haina shida kwasababu tumebeba miaka 50. Shida ni pale wenzetu wanapokaa katika mikutano ya mabara ya taasisi zao kama BAKUZA, UAMSHO, BAZAZI n.k. wakipanga nafasi za uwaziri na vyeo, ajira na fursa sawa. Hakuna hata siku moja utwasikia wakitoa hesababu. Sasa kama huwezi kuchangia unapata wapi ushujaa wa kutaka vyeo na ajira.
Mfano, eti rais wa muungano awe kwa zamu. Kwamba, rais anayetoka walikochangia 0 awe na kauli kwa mali za watu.
Mawaziri na ajira sawa kwasababu ni nchi mbili, tukiweka hesabu za malipo yao wenzetu wanakimbia wanasema sisi wadogo, sisi wachache n.k. Sawa kama ni wachache hoja ya nchi mbili sawa inatoka wapi?
Akili za wznz ni katika vyeo na ajira baasi, hakuna kingine cha ziada. Ndio matunda ya kubebwa kila siku mtu anadhani ana haki ya kukaa mgongoni. Miaka 50 inatosha tumechoka
Tuacheni tupumue