gombesugu,JokaKuu,
Nimekusoma,khabar za siku tele ndugu yangu.
Binafsi nisingalipenda kuchambua kwa kina hapa,maana ni kweli usemavyo yakuwa haya majambo yameshajadaliwa mno humu Jf,tena kwa nyakati mbalimbali bila ya kupata usuluhishi/ufumbuzi!?
Hata hivyo nimependa yakuwa kama dasturi yako,unajitahidi mno kutumia lugha ya kiungwana.
Kuhusu huo mfano wako kiduchu ulotoa hapo mwisho wa hiyo bayana yako;ati Zanzibar imejifaragua kuongeza majimbo ya uchaguzi ili "ifanane" na Tanganyika/Bara!? Yaani imenilazim kucheka kiduchu....
Kwani hiyo population ya Zanzibar kwa sehemu mbalimbali visiwani mle ndo ile ile tangia ile 1964!?...haijawahi kuongezeka japo kiduchu!?
Sasa kama kuna mabadiliko/ongezeke la population kwenye maeneo/majimbo mbalimbali visiwani humo,sasa huoni yakuwa hali hiyo ndo ilofanza wao kukidhi haja ya kuongezeka kwa majimbo ya uchaguzi,badala tu ya kudai ati wamefanza/wanafanza hivyo kwa kutaka "kujifananisha" na hiyo Tanganyika!?
Nimefurahika tumezungumza japo kiduchu,nami tajitahidi kufuatilia huu mnakasha kwa utuvu.
Ahsanta.
..niwie radhi kwa uchechefu wangu.
..naomba niweke wazi kwamba sikuwa na nia ya kuwafunjia heshma wa-Znz ktk bandiko langu la mwanzo.
..nakubaliana na wewe kwamba population ya Znz imeongezeka tangu tuingie ktk muungano.
..lakini sidhani kama hiyo ni justification ya kuwa na wanasiasa[wawakilishi na wabunge] wengi kiasi tunachoona sasa hivi.
..pia sidhani kama ongezeko hilo la wawakilishi na wabunge ni kwa ajili ya kukidhi matakwa na mahitaji ya wananchi, bali ni kwa ajili ya kukidhi matakwa ya MUUNGANO.
..kwa mtizamo wangu huu "utitiri" wa wanasiasa[wawakilishi na wabunge] ni mzigo wa gharama kwa wananchi wa Znz. sasa ili muutue mzigo huo inabidi mtoke ktk muungano, na muunde serikali ndogo, inayosimamiwa na baraza la wawakilishi dogo kuliko hili lililoko sasa hivi.
Last edited by a moderator: