nambokola
JF-Expert Member
- Jul 1, 2012
- 295
- 47
mapato ya tanganyika ni kiasi gani?
hamna mapato ya tanganyika ama kama unazungumzia tanzania sawa ama tanzania bara mhhh!!!!!
mapato ya tanganyika ni kiasi gani?
Ulishawahi kusikia Wabunge wa Tanganyika wakienda michenzani?Hapo ndipo ninapokushangaa. kama yote hayo ni kweli KWANINI HAMVUNJI MUUNGANO? pasi na shaka kuna mengi ya faida mnapata kutokana na kuwa Znz.
Mbona kwenye EAC mpo makini sana katika mas'ala ya Ardhwi, Ajira na mengine. sasa kwanini msiyaangalie hayo pia kwa Znz ili mvunje kwa amani mbaki kama majirani?
Acha kunung'unika CHUKUA MAAMUZI MAGUMU kwani huna udugu wa kuzaliwa na Znz. Kila mtu abebe msalaba wake kwanini wewe umbebee Znz? Je mpo wasa kweli nyie? au ndo yale yale kunung'unika ndio jadi yenu.
Kweli Zanzibar ni ndogo kieneo ila kiuchumi sidhani kama ilikuwa hivyo ila baada ya huu Muungano ndio mmetutilia ufukara na kutufanya tuwe watu duni sana ,mnataka tuwe tunategemea kila kitu kutoka huko Tanganyika na ndio kama inavyoonekana katika hoja zenu ,nyie nchi ndogo sijui uchumi wenu mdogo ,hebu ulizia na katafute historia ya Zanzibar ,Zanzibar wakati kabla ya Muungano ilikuwa vipi na ilitoa msaada kumsaidia nani ? Yakhe huu Muungano ukifa leo basi nakuhakikishieni machogo ,hautapita muda mrefu tutawasaidia tena tutawasaidia kwa ari na mori na moyo wa jeuri ,huko Tanganyika hamna kitu mmekalia kuti kavu. lazima mtapigana mapanga tu !
Kwa hali yoyote mchango wa ZNZ katika muungano ni jina.period. Kama huo ndio mchango hewala.hamna mapato ya tanganyika ama kama unazungumzia tanzania sawa ama tanzania bara mhhh!!!!!
Ulishawahi kusikia Wabunge wa Tanganyika wakienda michenzani?
Ulishawahi kusikia Wabunge wa Tanganyika wakienda michenzani?
Nadhani hujui unachokiongea na kama umeelimika basi wewe ni mvivu wakufikiri. Tunaoijua unguja basi tunasema katika mambo ya msingi Mzee karume aliyofanya basi nikukubali muungano na Tanganyika, alijua anachokifanya hata kama muungano huu ulikuwa na maslahi ya Marekani lakini naye aliona una maslahi makubwa kwa hatima ya znz wakati huo; walaah! nikuambie tu mara baada ya mapinduzi ya znz kitu kikubwa kingefuata ni migogoro na hata kuchinjana kati ya wapemba na unguja na ingekuwa kama somalia tu. Nadhani maisha yangekuwa yanarudiwa basi tungerejea nyuma baada ya mapinduzi halafu muungano na Bara ungefanyika miaka ya 80 leo hii naamini tungempiga mawe mtu yeyote anayebeza muungano. Pia tuelewe kuwa Dunia inazidi kubadilika hali ya hewa, hivi ikitokea natural calamities kama inavyotokea kwenye nchi za wenzetu hasa VISIWA, tutafanya nini, visiwa vyetu ni vidogo sana ikitokea thoruba ya siku tatu tu inatosha kuosha kila kilichopo kisiwani. SO TUSIFIKIRIE WAZUNGU WANAPOSEMA TANZANIA IMEJALIWA NA KUPENDELEWA NA MUNGU UKAFIKIRI NI WAJINGA, TENA HAWAMAANISHI VISIWANI ILA NI BARA KWANI LICHA YA NATURAL RESOURCES ILIZONAZO TU BALI PIA GEOGRAPGICALY IT IS SECURED. Nahitimisha kwakusema hivi-: kiukweli kati ya Tanganyika na Zanzibar anayemuhitaji na atakayemuhitaji mwenzake hata isingekuwa muungano ni Zanzibar na kama maisha yanajaribiwa basi hebu tujaribu kuvunja muungano.
Kwa hali yoyote mchango wa ZNZ katika muungano ni jina.period. Kama huo ndio mchango hewala.
Muungano si kelele na kidomo domo, muungano ni gharama. Mumeambiwa mchangie sawa mnaruka ruka hovyo.
Wakati huo huo mpo bize kupanga nafasi na vyeo msivyojua anagharamia nani.
ZNZ imechangia nini katika tume ya Warioba? Bunge la katiba na hata wabunge waliopo Dodoma!
Nchi kubwa kama tanganyika kulazimisha muungano na nchi ndogo kama zanzibr ni kutafutiana lawama za bure,nawashangaa wadanganyika mbona kwenye eac wanambwinya?
Ni hivi mchango wa znz ni jina na maneno, hakuna zaidi. Mwenyekiti wa kamati ya BLW kaonyesha wazi kuwa hata 1/10 ya gharama humuwezi. Siyo mimiKama mchango wa znz ni jina je watanganyika ni nini wakula na kujificha huyo anazungumzia gharama za serikali tatu na CCM hawataki serikali tatu lakini kiukweli hasa kama mutaiwacha znz kwenye makucha yenu na mazingaombwe yenu ya muungano na ubadilishaji wa jina basi sisi tunauwezo wa kumudumu halafu shida ya muungano sisi hatuna hebu angalau jaribuni na nyinyi kufanya angalau kama alivyojaribu kufanya mzanzibari mmoja kwamba munafanya kwa vitendo na sio let znz go kuongea na kulalamika waambieni wabunge wenu wawafanyie kazi maana wao hodari kubadilisha katiba na kuikandamiza znz.
Unauliza kwamba znz imechangia nini kwenye tume ya Warioba jee Tanganyika pia imechangia nini kwenye tume ya warioba MUNACHUKUA MSAADA KWA JINA LA TANZANIA HAMUJUI KWAMBA JINA LA TANZANIA NI LA WOTE musitake haki sawa na Tanzania wakati nyinyi tanganyika.wala musijione Tanzania ni nyinyi na uzembe wenu huo mutabakia kua watanganyika hata kama jina hamlitaki mijizi mikubwa nyinyi.
Nchi kubwa kama tanganyika kulazimisha muungano na nchi ndogo kama zanzibr ni kutafutiana lawama za bure,nawashangaa wadanganyika mbona kwenye eac wanambwinya?
Si kweli, hakuna mzanzibar anayethubutu kudai nchi yake.
Wote wanaongea chumbani na uvunguni mwa vitanda, tena wanabweka wakiwa na wamefunga taulo mbela ya ahali zao. Wakitoka nje kimyaa! nitakueleza
1. Tuliwaambia kura ya maoni kuhusu mustakabali wa znz, mkagoma na kujiminya minya
2. Tukaawambia acheni msishiriki tume ya Warioba, mkudai wajumbe sawa hata kama hamjui wanalipwa na nani
3. Tukawaambia nyote mkatae serikali 1.2.3 kilichofuata ni muungano wa mkataba.
Mkagoma kuchomoa mnataka kujificha na kusetiri dhiki zenu kwa mgongo wa mkataba
4. Tukawaambia msichague wajumbe wa bunge la katiba, akili zenu zikwatuma mdai wajumbe zaidi
5. Juzi Wajumbe wa BLW walikuwa Dodoma wanakula msasa na posho, hawakugoma kuja.
Hakuna mzanzibar mwenye nyodo ya kukataa muungano. Tumeshathibitisha na tunasema wazi hakuna!
Ninyi mkae kimya tu mpate mafaio ya sasa na uzeeni. Mnapata mafao kuanzia mnasoma bura hadi kazi na uzeeni. Hakuna anayedai nchi, ni wapiga kelele tu wamejaa
Yana nikhusu sana kumbuka Kitovu changu nilipozaliwa kilizikwa kule Kyanga, Mwera.
Itakuuma sana lakin ukweli laazima tutasema. Na waZnz wamestuka huo unyonyaji wanaofanyiwa na majirani zao.
Pole sana
Kama watoto wanasoma hujui wanasomeshwa na nani, kama unawasha umeme hujui unalipiwa na nani, kama unapata mshahara hujui chanzo chake na kama unaalikwa Dodoma na kupewa pesa nusizojua zinatoka wapi wewe ni KUPE.
Tena neno kupe ni zuri maana linastaha, lilitakiwa neno haswa linaloshabihiana na hali hiyo.
Ndio uliberali au ni uhafidhina?
Kibaya waliokwenda Dodoma ni kutoka pande zote za Liberali na uhafidhina.
Kule kwetu Pongwe na Mjasani ukiomba omba wanakuita mpiga mizinga, ukipokea tuu bila kuhoji wanauliza mwenzetu vipi?
Tayari nimeshaitolea ufafanuzi kauli yangu kwenye post hii: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-kuchangia-sawa-na-bara%92-4.html#post7809996Je umewahi kupitia bajeti yoyote ya Tanganyika au Tanzania ukaona inajitosheleza? Bila kutegemea misaada na mikopo kutoka nje?
Skuli muhimu sana ahali yangu hususan unapotaka kuzungumzia mas'ala ya kiuchumi.
Pole sana.
Hakuna mamlaka kama unaomba msaada wa kuendesha serikali. Mwenye mamlaka ni yule mwenye kitu mezani siyo maneno.Iam sorry brother maneno tele lakin hufahamiki., Wewe ni kada na kibaraka wa CCM lakini ata elimu ya kupambanua na kujielezea huna., Tanganyika mumeghumiwa mana sasa naona mupo bizz munatengeneza katiba yenu kwa siri siri., 66% ya wazanzibari waliunga mkono muungano wa Mkataba.
Wewe kama unahamau na kutaka kujuwa kuhusu BLW la zanzibar subiri kwenye hilo bunge la Katiba uone usiandikie mate, Nilijuwa utashtuka ili CDM kudai Tanganyika yenu bado unaendelea na utumwa. Mamlaka ya Zanzibar ni lazima no way out, mumeumia sana
Kama mchango wa znz ni jina je watanganyika ni nini wakula na kujificha huyo anazungumzia gharama za serikali tatu na CCM hawataki serikali tatu lakini kiukweli hasa kama mutaiwacha znz kwenye makucha yenu na mazingaombwe yenu ya muungano na ubadilishaji wa jina basi sisi tunauwezo wa kumudumu halafu shida ya muungano sisi hatuna hebu angalau jaribuni na nyinyi kufanya angalau kama alivyojaribu kufanya mzanzibari mmoja kwamba munafanya kwa vitendo na sio let znz go kuongea na kulalamika waambieni wabunge wenu wawafanyie kazi maana wao hodari kubadilisha katiba na kuikandamiza znz.
Unauliza kwamba znz imechangia nini kwenye tume ya Warioba jee Tanganyika pia imechangia nini kwenye tume ya warioba MUNACHUKUA MSAADA KWA JINA LA TANZANIA HAMUJUI KWAMBA JINA LA TANZANIA NI LA WOTE musitake haki sawa na Tanzania wakati nyinyi tanganyika.wala musijione Tanzania ni nyinyi na uzembe wenu huo mutabakia kua watanganyika hata kama jina hamlitaki mijizi mikubwa nyinyi.