Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 16,317
- 33,814
Kama hana shida mkataba mnaong'ang'ania ni wa nini? Niambie nani aliwahi kusimama hadharani na kusema hataki muungano katika mentors wenuKama mchango wa znz ni jina je watanganyika ni nini wakula na kujificha huyo anazungumzia gharama za serikali tatu na CCM hawataki serikali tatu lakini kiukweli hasa kama mutaiwacha znz kwenye makucha yenu na mazingaombwe yenu ya muungano na ubadilishaji wa jina basi sisi tunauwezo wa kumudumu halafu shida ya muungano sisi hatuna hebu angalau jaribuni na nyinyi kufanya angalau kama alivyojaribu kufanya mzanzibari mmoja kwamba munafanya kwa vitendo na sio let znz go kuongea na kulalamika waambieni wabunge wenu wawafanyie kazi maana wao hodari kubadilisha katiba na kuikandamiza znz.
Unauliza kwamba znz imechangia nini kwenye tume ya Warioba jee Tanganyika pia imechangia nini kwenye tume ya warioba MUNACHUKUA MSAADA KWA JINA LA TANZANIA HAMUJUI KWAMBA JINA LA TANZANIA NI LA WOTE musitake haki sawa na Tanzania wakati nyinyi tanganyika.wala musijione Tanzania ni nyinyi na uzembe wenu huo mutabakia kua watanganyika hata kama jina hamlitaki mijizi mikubwa nyinyi.
Nikutajie kwa uchache
Jusa alisema anataka muungano(rekodi ipo)
Ahmed alisema anataka muungano(rekodi ipo)
Maalim alisema anataka muungano(rekodi ipo)
Nasor Moyo anataka muungano(rekodini)
Mansour Himid anataka muungano(rekodi ipo)
Karume ndiye kabisa anaishi mikocheni
Jumbe anaishi mji mwema
Profesa Sahrif anataka muungano
Nahodha anataka muungano
Raza anataka muungano(rekodi ipo)
Hamad Rashid anataka muunganano(rekodi ipo)
Pili, hakuna aliyewashikilia kilichopo mumejishikilia wenyewe
1. Tuliwashauri mdai kura ya maoni na si katiba mkagoma
2. Tukawaambia msilete wajumbe tume ya Warioba, mkaleta tena Ally Salehe wa BBC akiwemo
3. Tukwaambia mchakato si sahihi kwa kupata katiba mpya, mkaungana CCM na CUF kupitisha mswada kirahisi
4. Tukwaambia katika maoni semeni hamtaki muungano, mkagoma na kusema mnataka mkataba
5. Tukawashauri makamu wa rais arudi nyumbani kwasababu uwepo wake ni uwakilishi wa znz katika muungano
6. Tukashauri muache kazi katika JMT na kurudi nyumbani, mkagoma
7. Tukwaambia anzisheni sarafu yenu kama mlivyopata wimbo wa taifa na bendera, mkagoma
8. Tukawashauri msijishughulishe na shughuli za muungano, juzi BLW likahamia Dodoma
9. Tukawaambia wabunge wenu wasije Dodoma, mkachomoa kila kikao wapo na wanashughulika na maneno kama Uliberali
10. Tukwaambia pelekeni mswada BLW muiondoe znz katika muungano kama mlivyoanzisha vikosi na saluti 21 za mizinga
11. Tukasema kama mumeshindwa wabunge wenu wanaokuja Dodoma japo waombe muongozio kuua mkataba,nothing
Sasa imebaki nafasi moja ambayo hamtaki kuitumia
12. Susieni bunge la katiba, hadi hapo katiba mpya na muungano kwisha, hamataki mnataka wajumbe wengi kwa jinsi mnavyotamani muungano.
Si kweli kama hamtaki mnachofanya ni kutishia ili mupewe mafao zaidi, this time around hakuna.
Kasome rasimu halafu uniambie wapi kuna unafuu, ndio taraibu tunafungua mbeleko.
Tanganyika ikipata serikali rasmi ndio tunawaweka katika zulia tunaendelea na safari.
Tanganyika ni njema atakaye na aje
Migongo inauma, tuacheni tupumue.