Zantel na Zain wapunguza gharama za internet

Zantel na Zain wapunguza gharama za internet

Guys, mimi nina ka internet cafe ka mchwara mtaani sehemu za nyuma ya Airport (VITUKA) hapa Dar maeneo ambayo siwezi kupata broadbend service za TTCL kwani hakuna nyaya za simu zao, natumia CATS-NET, unlimited services, USD 150 kwa miezi mitatu kwa 64kbps. Wanacharge USD250 kwa miezi mitatu kwa 128kbps. It's 100% unlimited. Tatizo kidogo wakati fulani inasumbua lkn kutegemeana na maeneo ulipo. Nimezunguka sana sijaona ISP mwingine mwenye good rates kama hawa jamaa. Tumia 24 hours 7 days a week kwao sawa tu.

Mkuu,

64kbps inatosha kweli ? Au unacomputer chache. Mwenyewe nina cafe yangu link ni 256kbps computer 6 lakini naona bado. Halafu hawa CATS-NET hawakucharge installation costs kubwa ?

B.P
 
Sasa naamini wengi watakuwa na access ya mtandao zaidi kwa Bongo.

Modem ya Zantel ni Tshs 150,000/= na ya Zain ni Tshs 60,000/=

Zantel:

Monthly
2GB - 10,000/=
8GB - 50,000/=

ZAIN:

Weekly 3GB - Tshs 15,000/=

Monthly 8GB - Tshs 70,000/=

Quarterly 24GB - Tshs 200,000/=

Yearly 96GB - Tshs 750,000/=

Nadhani tunaelekea kuzuri, wengi wataweza kumudu matumizi ya internet

Haya yote ni mazuri, lakini kwa watumiani kama mimi, ninachojali ni uwezo wa mtandao (throughput). Je, kuna utafiti wowote uliofanywa kuthibitisha ni nani mwenye uwezo mkubwa zaidi kimtandao, kuweza kupitisha data (bandwidth rate) kwa kasi zaidi?

So far, Sasatel inaongoza! Ila kuna jambo moja tu wameniudhi! Bundle ya SurFUNlimited haipatikani kwa wanaotumia EVDO modems!
 
Yaani mwaka 2010 intaneti ilikuwa bei juu mara 2 ya sasa au mimi sielewi! GB ni 10,000 wiki?
Kabla ya kusambazwa mkongo gharama za intaneti zilikuwa kubwa,, mwaka 2009 mb 20 ilikuwa ni sh 500 voda, baadae zain(airtel), ulikuwa unapaata mb 400 Kwa 2000 hii ilikuwa nafuu Sana maana zantel mb 500 ilikuwa 10,000 hapo hujazungumzia bei za modem maana simu hazikuwa sana. Lakini kuanzia 2013 mambo yalianza badilika. 1gb Kwa buku ikawa kawaida, bando za usiku unlimited Kwa 200 vodacom
 
Tigo wakapindua meza shilingi 500 mb 50 extreme pack, vodacom walishawahi kuuza MB 1 shiling 250
 
Kabla ya kusambazwa mkongo gharama za intaneti zilikuwa kubwa,, mwaka 2009 mb 20 ilikuwa ni sh 500 voda, baadae zain(airtel), ulikuwa unapaata mb 400 Kwa 2000 hii ilikuwa nafuu Sana maana zantel mb 500 ilikuwa 10,000 hapo hujazungumzia bei za modem maana simu hazikuwa sana. Lakini kuanzia 2013 mambo yalianza badilika. 1gb Kwa buku ikawa kawaida, bando za usiku unlimited Kwa 200 vodacom
Nakumbuka ilikuwa ikifika saa sita usiku tunaingia mtandaoni bure

Ni kudownload miziki waptrick na tubidy dah ilikuwa raha sana
 
Nyie wazee wa 2010,vkwamba 3GB kwa pesa yote hiyo? Au sijalewa mlichoandika
 
Enzi hatujui kama Kuna kitu kitaitwa 3g 4g 5g. Mwendo E tu, kucheza game java n.k 🤣
 
Back
Top Bottom