Zangira ni nani na katumwa na nani kuwashughulikia akina Lema huko ughaibuni?

Just MIND GAMES aiming at deverting attent from other matters.....
 
Unamuuliza kwani yeye ndiye mwenye jukumu la kumlinda Tundu Lisu?

Unaniuliza kwani yeye ndiye mwenye jukumu la kufanya upelelezi na uchunguzi?

Mkuu embu jaribu kutumia Akili yako vizuri.

Unauliza maswali Kama mtoto bhana

Ukisoma vizuri kutokea juu utaelewa kwanini nimemuuliza hilo swali....
 
Tanzania inachota akili Rwanda? Hakuna watu makini nchini? siamini.
 


Nasisitiza tumia akili vizuri unapojadili mambo haya.

Lisu ni mwanachama lakini pia nimuajiriwa wa CHADEMA.

CHADEMA au CCM au chama chochote hakina wajibu wa kulinda usalama wa wanachama wake,
Jukumu hilo linabebwa na Serikali kupitia vyombo vyake vya Dola Kama Polisi.

Polisi ambao ni chombo cha serikali moja ya majukumu yake ni kulinda usalama wa Raia na Mali zao. Polisi wanalipwa mishahara Kwa kazi hiyo, na serikali inachukua Kodi Kwa Raia Kwa ajili ya kuweza kuwalinda na kuwapa Huduma zinginezo.

Lisu ni Raia wa Tanzania Kama ulivyo wewe na Mimi.
Serikali ilishindwa kumlinda akapigwa RISASI licha ya kuripoti mara kadhaa kuhusu vitisho vya kudhuriwa,
Nikiwatetea Polisi na serikali, ni ngumu Kwa serikali au polisi kulinda mtu mmoja mmoja huenda ndio maana Uhalifu unaweza kumtokea yeyote.

Sawa, Uhalifu umeshatokea, Lisu kapigwa RISASI,
Mwenye jukumu la kufanya uchunguzi na upelelezi ni serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama.

Kumbuka ni jukumu na wajibu wa serikali, sio mpaka mtu aende kuomba, uchunguzi ufanyike na waliofanya wakamatwe sheria ifuate Mkondo wake.

Sasa wewe unaleta mambo ya CHADEMA sijui viongozi, sijui blah! Blah! Hujui hata wajibu wa serikali na hii inamaanisha hujui hata wajibu wako
 
Ukisoma vizuri kutokea juu utaelewa kwanini nimemuuliza hilo swali....


Mpaka naamua kukunukuu ujue nimeshapitia Maoni yako tangu huko juu.

Natofautiana na wewe Kwenye kipengele cha kuwalaumu kina Lisu kutoshtaki Kwa Uhalifu waliofanyiwa.

Lakini hapo hapo nashangaa kuona huoni upande wa serikali Kwa kushindwa kutenda wajibu wake.
 
Hatua zilishachukuliwa.... by karma... kwa mhusika mkuu kutangulizwa akhera.
 

Hiyo Serikali unayotaka ifanye hivyo ndio imeshindwa sasa kufanya hivyo , tukae sasa tukunje mikono na kuibembeleza ifanye?..

Wenyewe huwa tunaita CCM mkoloni mweusi, sasa unataka mkoloni mweusi tena akulinde...Fuatilia harakati za Tanu dhidi ya ukoloni au harakati za ANC dhidi ya Kaburu... hivi vyama vilikuwa structured kiasi cha kupambana na mkoloni kila angle...
 


Hivyo unajaribu kuwashawishi CHADEMA, au Lisu, ndugu za Lisu, wafuasi WA Lisu au Wale wote waluotendewa ukatili wachukue sheria mkononi?

Au je unajaribu kuchochea uhaini au mapinduzi Kwa serikali?
 
Just MIND GAMES aiming at deverting attent from other matters.....
It was the same comment when some assassins were reported to tail Lissu's vehicle...

What happened thereafter ?

Only fools can ignore the assassins' footsteps..
 
Umekuja kutetea kwa nguvu sana. Magufuli alipoamrisha Lissu apigwe risasi alikuwa na madhara gani? Idiot!

sijatetea chief, na siwezi kusema huyo unayemtaja ndiye aliyempiga risasi TL...

Ninalo waza na kuhitaji lifanyike ni uchunguzi huru na majibu yawekwe mezani, tunayemtegemea kuyafanya hayo yuko kimya, sisi upande wetu tunafanyaje ili haki ipatikane?... tuendelee kuwa wanyonge?
 
Hivyo unajaribu kuwashawishi CHADEMA, au Lisu, ndugu za Lisu, wafuasi WA Lisu au Wale wote waluotendewa ukatili wachukue sheria mkononi?

Au je unajaribu kuchochea uhaini au mapinduzi Kwa serikali?

Ina maana duniani hapa hakuna njia za kufuata kimataifa haki ikapatikana na wahusika wakaenda kwenye mikono ya sheria?..

Hayo unayosema yanaweza kuwa option pia kama njia zote zimeshindwa, ni nani alishawahi hata kuandamana kwenda ubalozi wowote au popote kudai justice for TL?... mbona tunaonaga maandamano kudai vitu vingine na sio hili?
 
Hatua zilishachukuliwa.... by karma... kwa mhusika mkuu kutangulizwa akhera.

Ni kweli Karma ipo lakini hata Mungu kuna wakati anatuambia haki zetu kwa jasho na damu.... Hittler haikusubuliwa karma watu walichukua hatua, Sadaam nk.. kusubiri karma kwa mambo yaliyo kwenye uwezo wako ni dalili za uoga na unafiki....
 
Chadema si walitaka uchunguzi kutoka nje ya Tanzânia serikali ilikataaa kwasababu wanajua madhambi walioyafanya juu ya Lissu.

Sent from my SM-N9150 using JamiiForums mobile app
 


Maandamano yapo unayoyataka wakati Yale ya kuvaa Tu tisheti zenye taswira ya Lisu na maneno Pray for Lisu yalikatazwa, na waliokaidi walikamatwa Kama walivyoripoti CHADEMA wenyewe, je hayo hukuyasikia?

Maandamano gani zaidi ilhali Wale waliokuwa na Mapenzi na huyo Lisu wakati wakiweka maombi kumuombea nyakati zile walizuiawa, je hayo nayo hukuyasikia?

Nchi hii ni nchi huru, haiwezi kuingiliwa na mataifa mengine, hivyo kusema twende kimataifa itakuwa ni uongo na Jambo lisilowezekana.

Ndio maana mataifa Kama Uchina, Korea ya Kaskazini, na Nchi zenye mifumo migumu ya Kisiasa Kwa kipengele cha demokrasia mpaka Leo sheria za kimataifa zinashindwa kuwadhibiti.

Unapoona watu wanapiga kelele pale serikali inapojisahau au kutelekeza wajibu wake ujue hizo ndizo hatua zenyewe, hasa za mwanzo mwanzo.

Wewe jukumu lako sio kuungana na serikali inaposhindwa wajibu wake na kuwasonda vidole Raia wenzako bali unaowajibu wa kuikemea na kuikumbusha Kama wanavyofanya wengine.

Kitendo cha wewe kuona upungufu wa kina Lisu na CHADEMA Yao badala ya kuona upungufu wa serikali kiuwajibikaji kinajibu maswali uliyoyauliza hapo juu.
 
Lema amekiambia madeni ya Benki Arudi aje alipe
 
Mm zamani Nilikua najua ni bla bla lakini Lisu alivyopigwa masasi yote yale mchana kweupe naamini Haya mambo sio ya kuchukulia poa...usisahau hawa jamaa wana familia kama wewe...Hata wewe usingependa maisha yako yahatarishwe..Tuwe na hekima maisha yetu duniani ni ya muda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…