Zangira ni nani na katumwa na nani kuwashughulikia akina Lema huko ughaibuni?

Hatuhitaji hata Elimu ya Cert kujua nani walimpiga risasi Tundu Lissu! Kwa kifupi ni Serikali ya Awamu ya Tano,chini ya Marehemu John Pombe Joseph Magufuli!

Bila shaka kupitia uchunguzi wako wa kitalaam ulioufanya ndio umepelekea kubaini hivyo..

Tuambie sasa, TL na chama CDM wamechukua hatua gani za kisheria local and international ilo haki ipatikane na wahusika wakamatwe au uchunguzi huru ufanyike....wapi wamefungu kesi dhidi ya ushahidi walionao...

Sifurahii TL kupigwa risasi, lakini sitaki kuingia kwenye ushabiki wa kisiasa unaoweza kutoa hukumu zisizo za haki...
 
Sinema hizi, unafikiri unaweza kuua kirahisi mkimbizi wa kisiasa Canada na Belgium?...

Impact ya Lema na TL kwa nchi ni ipi kiasi cha nchi kuharibu image yake?.... kuna wakati zinatafutwa attention tu...

Waripoti hizo taarifa kwa mamlaka za nchi walizopo halafu uone moto wake...ukiona wameishia twitani tu ujue ni zile zile sinema tu..
Sio twitter tu.

Kagame staili hiyo mkuu maana Kagame alifanikiwa sana kuwafuata wapinzani wake walipokimbilia na kuwadhuru.

Ila naungana nawe kuwa ni kazi ngumu sana ila tahadhari ni bora..
Waliotajwa hawajafikia hatua ya kuwa na madhara kiasi cha kuchukuliwa hatua aka PK style.... hao wapinzani wa PK walikuwa na madhara makubwa kwa PK ndio maana aliamua kuwaeliminate... hao wapinzani wa PK ndio walikuwa wanavufund vikundi vya wanamgambo kama Maimai na fdla nk wakiwa ughaibuni..

Lema ana madhara gani kwa Taifa hili mpaka likamuue Canada, TL ana madhara gani kwa Taifa hili mpaka akauliwe Belgium... naomba niwaambie watu kitu tu...TL weupe walishamdharau hivyo hakuna backup wanaweza kumpa dhidi ya harakati zake na Tanzania, Lema hana uwezo wakufanya lolote dhidi ya Tanzania huko aliko kifupi hana madhara ndio maana hizo naita story za twita...
Tatizo unafikiri kuwa madhara ni kufadhili vita tu.

Propaganda na kuanika ubaya/uchafu/ukaburu wa serikali una madhara makubwa sana...tazama namna Rais wetu alivyochukuliwa UN.

Vigogo wa G8 wote walimkimbia,amehaha walau kupiga picha tu ikashindikana! ata makamu tu wa USA mama na black mwenzie akamtosa..it's a shame!
Usione hii ni kawaida unless na wewe ni wa kawaida sana uko upstair
 
Magufuli alishindana na upinzani na mwisho wake sote tunajua. Huyu Mama nae asipokua muangalifu. Atapambana na wapinzani na mwisho wa siku hakuna atakolofanya la maana
 
Kuna taarifa zimenistusha sana,zinarushwa kwa mtindo wa onyo hasa kwenye mtandao wa heshima...Twitter kuwa kuna mtu anaitwa Zangira ambae katumwa kuwashughulikia kimafia akina Lema na wenzake uko ughaibuni walipokimbilia kunusuru kesho yao.

Huyu mtu ni nani hasa na katumwa na nani?

Je 'muuaji' Zangira atafanikiwa au ameshashindwa kabla baada ya taarifa zake kujulikana?

Intelijensia ya magharibi itakubali uchafu ufanyike kwenye ardhi yao?

Je kuna wasiokubaliana na namna mambo yanavyoendeshwa na wameamua kuwa wavujishaji siri?

My take:
Kama yasemwayo ni kweli basi tumefika mahali pabaya sana na mh.Rais inabidi asimame imara sasa kusafisha uchafu huu unaofanywa na wachache na wasiojulikana vizuri bado. Kama ni kweli,Zangira adhibitiwe uko uko ili liwe fundisho kwa akina Zangira wengine.
Kiki tu hizo, nani ana muda wa kupoteza na hizo garasa zikina Tundu Lissu na Lema
 
Sinema hizi, unafikiri unaweza kuua kirahisi mkimbizi wa kisiasa Canada na Belgium?...

Impact ya Lema na TL kwa nchi ni ipi kiasi cha nchi kuharibu image yake?.... kuna wakati zinatafutwa attention tu...

Waripoti hizo taarifa kwa mamlaka za nchi walizopo halafu uone moto wake...ukiona wameishia twitani tu ujue ni zile zile sinema tu..
Sasa Roma alikuwa anaimpact gani hadi wamrekodi wakimbaka na kumvunja miguu?
 
Chadema wafungue kesi wapi?? Mahakama za Tanzania, ni jambo ambalo haiwezekani!

Kimataifa,kuna utaratibu wake,mfano Magufuli hawezi pandishwa the Hague, sababu hajaleta mass destruction kwa watu wake! Angeuwa watu wengi,The Hague wangetoa warranty wakumdaka!

Naomba nikupe mfano,hivi ukisema nitakuonyesha Mimi ni nani,halafu kesho napata matatizo au nakufa,ni nani atakua mtu wa kwanza kua suspected??

Unajua Magufuli aliwahi sema,watu wanaopingana nae hua wanauwawa?? The same day,Lissu akapigwa risasi,tena mchana kweupe pee! 17.09.2017 hadi 17.03.2021! Opaga sana hizi tarehe,it's not just a collusion,ni kuonyesha kwamba Mwenyezi Mungu ana nguvu kuliko mtu yoyote!

Kwa nilivyokusoma hapo kuna mtu umemtaja kama suspect number moja hapi tumaliza kwa kusema bado ni tuhumu mpaka itakapogundulika ni kweli ametenda na hatua zikachukuliwa..

Hivi unaniambia hakuna namna nyingine ya TL kupata haki yake tofauti na ICC? hivi CDM na TL wakaomba jumuiya za kimataifa msaada wa haki yake kwa either kuishinikiza serikali ya Tanzania ifanye uchunguzi huru au vyombo vya nje vije kufanya uchunguzi huru...
Hivi unaniambia CDM kupitia wing yao ya usalama kwa siri wanashindwaje kutafuta msaada wa majasusi waliobobea independe kuja kuchunguza na kukusanya ushahidi then wafungue charge hapa na kokote kule kudai haki yao..

Unaanzaje kumshinikiza mtu unayemtuhumu kukufanyizia ndio afanye uchunguzi wa tukio na kukamata wahusika..?
 
Hizo style zinatumika kwa watu wenye madhara na si vinginevyo, huwezi ukaniambia eti TL na Lema wanamadhara kiasi cha system ya Tanzania kwenda kuwatafuta na kuwaua ughaibuni na kuharibu vibaya image ya nchi..

Kama hizo taarifa ni za kweli wahusika watoe taarifa kwa mamlaka za nchi walizopo halafu uone Tanzania itakavyoshukiwa na hilo jina tajwa sijui ZINGIRA atakamatwa huko Europe mara moja.....vinginevyo zitakuwa porojo za twita kutafuta porojo nyumbani.....System haiwezi kuwa Pumbavu kuwaza kijinga hivyo...
Hawa hawana madhara ila mange ndio alikua na madhara sio🤔🤔🤔🤔
 
Kiki tu hizo, nani ana muda wa kupoteza na hizo garasa zikina Tundu Lissu na Lema
Ata TL aliporipoti kufuatiliwa na wasiojulikana wakiwa kwenye gari ilisemwa ni kiki.

Lisemwalo lipo,huyu muuaji afuatiliwe na serikali za magharibi na ikibidi wamrudishe akiwa kwenye 'casket' ili waliomtupa wakazike uchafu wao
 
Kwa nilivyokusoma hapo kuna mtu umemtaja kama suspect number moja hapi tumaliza kwa kusema bado ni tuhumu mpaka itakapogundulika ni kweli ametenda na hatua zikachukuliwa..

Hivi unaniambia hakuna namna nyingine ya TL kupata haki yake tofauti na ICC? hivi CDM na TL wakaomba jumuiya za kimataifa msaada wa haki yake kwa either kuishinikiza serikali ya Tanzania ifanye uchunguzi huru au vyombo vya nje vije kufanya uchunguzi huru...
Yaani unasubiri mpaka atende ndipo achukuliwe hatua!? Au sijakuelewa?

Mkuu wahusika wa TL wanajulikana na mmoja wao alishapigwa stop kukanyaga US. Time will tell...jinai haifi ata miaka 20 ipite
 
Hivi unadhani Serikali ya Magufuli ingekubali wachunguzi kutoka nje waje waivue nguo serikali yake?? Hukumbuki kama IGP aliwahi sema wao,wanaweza kuchunguza kesi na wala hawahitaji msaada toka nje??

Hivi ni kwa nini Marekani walimpiga marufuku Bwana Makonda kuingia Nchini Marekani??

Nimekwambia shinikizo kutoka nje, huyo JPM angepewa shinikizo angetulia tu, wapi CDM na TL wameomba msaada huo? haki yao ipatikane.
CDM hawana wing yao ya usalama kwa siri ikaita watu wakaja wakafanya yao na kukusanya kila evidence then wakafungua charge mahala...?..

Ya Makonda na USA wanajuana wenyewe, Makonda yuko mtaani kama raia, mfungulieni kesi au mnasubiri jamhuri...?
 
Toka lini Criminal ikafunguliwa na Raia?? Au hili nalo hujui??

huko CDM bila shaka kuna wanasheria wasomi, kwahiyo tutasubiri CDM ishike dola ndio Makonda aburuzwe mahakamani? au tunasubiri huruma za watawala ndio tupate haki? hao wanasheria wetu hawana cha kufanya ili bwana Makonda aburuzwe kortini?
 
Nimekwambia shinikizo kutoka nje, huyo JPM angepewa shinikizo angetulia tu, wapi CDM na TL wameomba msaada huo? haki yao ipatikane.
CDM hawana wing yao ya usalama kwa siri ikaita watu wakaja wakafanya yao na kukusanya kila evidence then wakafungua charge mahala...?..

Ya Makonda na USA wanajuana wenyewe, Makonda yuko mtaani kama raia, mfungulieni kesi au mnasubiri jamhuri...?
Kwa mahakama ipi?

Shinikizo? Labda shinikizo la damu maana kwa nchi yenye utawala bora haihitaji shinikizo bali kauli ingetosha... wengi wametoa kauli ya uchunguzi lakini serikali ilipotezea. It's a matter of time before things come up to light.
 
Hivi unajua kweli mambo au unapinga tu just kupoteza mda?? Serikali wakisema hawataki wachunguzi kutoka nje,na kweli hawawezi kuja!

unajua maana ya shinikizo la kimataifa?..

Kama chama hakina mbinu kwa maana ya kuwa hata na wing ya usalama inayoweza kulink na watu duniani kazi ikafanyika na evidence zikapatikana kinawezaje kutaka kupewa dola sasa....
 
huko CDM bila shaka kuna wanasheria wasomi, kwahiyo tutasubiri CDM ishike dola ndio Makonda aburuzwe mahakamani? au tunasubiri huruma za watawala ndio tupate haki? hao wanasheria wetu hawana cha kufanya ili bwana Makonda aburuzwe kortini?
Korti gani ilivyo huru mkuu?

Au unamaanisha koti la kuvaa?
 
Ulishawahi ona wapi mtu binafisi kaenda fungua kesi ya Jinai dhidi ya mtu au watu?? Serikali ndiyo hufanya hivyo! Ingekua kila mtu anamfungulia kesi mtu yoyote,Mimi ningeanza na wewe!

kwa hiyo tukae tusubiri huruma ya serikali hiyo hiyo tunayoituhumu..?
 
Back
Top Bottom