Latino na harakati za kuzamia ughaibuni mpaka kutoswa baharini

IBRA wa PILI

JF-Expert Member
Oct 12, 2017
572
1,000
Anasimulia mwaka 1998 wakati nipo shule ya msingi ndio naingia darasa la saba mama na baba walitengana, ivyo baba akamwambia mama kama unaenda we nenda ila watoto waache mama akaondoka na kutuacha na baba mim na ndugu yangu apo rasmi shule nikaacha.

Na darasa la saba niliishia kunusa tu sikusoma chochote. Kutokana na harakati za maisha ya hapa na pale nikajichanganya uko bagamoyo kwenye harakati za uvuvi nikawa na vua samaki wadogodog mradi kupata riziki za hapa na pale .

Lakini nilikutana na jamaa zangu flani ambao nao walikua wakivua isipokua wao walikua wanaenda mbali maji marefu uko karibu na Zanzibar walinishawishi nijiunge nao ili tuwe tunakwenda uko kweli nikajiunga nao na rasmi nikaanza kuvua nao uko. Ilikua ni kawaida kukutana na mawimbi makubwa muda mwingne tulilala uko uko visiwani palikua na visiwa kama pungume ,chime ,kware na vingne ambavyo tulikua tunaweka makazi kwa shughli zetu izi za kuvua samaki.

Lakini katika shughuli izi za kuvua samaki akili yangu ilikua ainitumi kabisa japo pesa ilikuepo ya kawaida ila akili yangu ilikua kuelekea mbele ughaibuni lakini ni katika njia za panya zile za kuzamia kwenye meli sio njia halali. Mpaka kuwaza ivyo tayari palikua na jamaa zetu wengne ambao walikua wamezamia uko na kwa kipindi icho ilikua kama ukifanikiwa kutoboa kwa njia izo ukafika uko ughaibuni basi umetoboa kweli. Ilikua swala la kupata visa ili uweze kwenda uko ni kizungumkuti maswali mengi utaulizwa na vitu kibao kwaiyo njia nyepesi ililikua ni kuzamia kwenye meli pasipo kuangaika na maswala ya viza.

Basi siku iyo nikiwa na washkaji zangu lile wazo la kuzamia likanijia kichwani nilikua najamaa zangu wote vichwa maji na akili zetu zilikua sawa kabisa niliwapa ili wazo la kuzamia na wakalipokea na kitu cha kawaida kipindi icho watu kuzamia meli alafu wao walikua wakubwa kwangu na pia tulijua kuogelea tuliwaza ata kama tuta tosawa aitakua ugumu kwetu majini ni kama tu umemetosa mamba kwenye maji mawazo haya.

Basi tukajipanga vizuri Siku iyo na washkaji zangu tulielekea maeneo ya feli kucheki magoma (Meli) tukazikuta pale zimepaki na zipo na bendera za mataifa mbali mbali zikipepea kuonesha zitapita kwenye izo nchi. Lakini pia tukachunguza kuweza kujua kwamba hii itaondoka lini na muda gani maana sometimes unaweza bugi kwamba mkaingia tu kwenye meli pasipo kujua na ukajikuta unakaa apo mwez mzima meli aijaondoka kweli tukapata ambayo inaondoka siku chache mbele ilikua meli ya mizigo ya wagiriki, kabla ya kuondoka tukahakikisha tunapata mikate na maji ya kwenye makopo na vyakula vingine ambavyo sio vyepesi kukushika na aja kubwa pia tulibeba pombe kali kwajili ya baridi ikitokea zile ukinywa zinaleta joto mwilini pia bangi pamoja kiberiti cha gesi ivi vilikizi.

Na siku ya kuzamia tuliingia kwemye meli kupitia tundu la nanga lile ambalo wanapitisha minyororo mikubwa ya kushikia meli.
Tulikua ni watu kama wa nne au wa tano sikumbuki vizuri sana yess tukaingia ndani ya ile meli na kutafuta sehemu iliyo karibu na damp ya chakula pale ambapo wanatupa uchafu kama mabaki ya chakula na vitu vingne ili iwe kazi nyepesi tukiishiwa chakula Basi tutakwenda hapo kutafuta chakula ikumbukwe pia muda wa kuingia ndani ya meli tuliingia usiku sana mida kama ya saa Tisa ivi ndio tulizama ndani ya meli.

Ilichukua siku tatu mpaka meli kupiga honi ya kuhashiria sasa inataka kuondoka hapa kila mtu alishtuka na tukawa kimya akuna ambae alimsemesha mwenzake pia hofu ikatuingia kwamba hakilino mwetu ndio muda mfupi ujao tutaicha ardhi ya Tanzania ki ukweli unakua na taharuki kwakua pia unako enda akuna ndugu wala ujui utakutana na nani ila maji ushayavulia nguo sharti uyaoge akuna budi.

Baada ya muda tukasikisa mtetemo wa meli ndio ina achia nanga sasa na kuondoka eneo lile taratibu ndio inakwenda ilituchkua kama muda wa nusu saha akuna aliemsemesha mwenzake wote tulikua kimya kabisa nafikiri kila mtu alikua na mawazo yake uko tuendako binafsi nilipiga dua kwa kumuomba mungu na mizimu yetu pia inisimamie uko tuendako na wenzangu.

Basi safari ilisonga na izi meli za mizigo azikua na kasi sana mwanzoni mpaka uko mbeleni kwenye maji marefu ndio kasi inazidi tukiwa mule ndani tulikua tuna kadiria tu muda kwamba saiz usiku saiz mchana ngoma inazdi kusonga na vile vyakula vyetu tukawa tunatumia taratibu kwa kujibana visiishe, ila ndani ya siku tano au sita vyakula vilikwisha.

Sasa basi baada ya kuishiwa chakula na kukaa bila kula aiwezekani na nia ya kukaa eneo tulilo jificha ni kalikaribia damp la kutupa uchafu sasa muda uliwadia kwenda kusaka msos pale dampo na Mimi nilikua wa kwanza Ila umakini tu ndio ulihitajika mno isije ukaonwa ikawa shida na kinapoingia kiza ndio unakua muda sahihi kwani wao muda huo hua wanapumzika kama pombe ndio wanakunywa wa kutumia madawa wanatumia kucheki picha za ngono awana purukushani tulikua kama panya tu pale binadamu wanapotulia wao ndio wanaingia kazini kusaka chochote kitu.

Yap nilienda kusaka msosi kwenye lile dampo pia niliakikisha miguu yangu aichi alama unaweza ukakanyaga kitu ukaacha alama za vidole ndio mmedakwa apo nilkwenda nikafanikiwa kupata pande la samaki kubwa navyosema kubwa ni kubwa hasa sio viji samaki likiwa limeandamana na kichwa walikula kidogo tu wakaliacha pia kulikua na vyakula vya kopo navyo nikachukua na pombe flan ivi ilinywewa nusu ikaachawa basi nikatoka na mzgo mpaka tulipo nikafika salama tukala msoi vizuri na yule samaki alikua mkubwa kwaiyo atukutoka siku ya pili kwenda kusaka tena na alikua kaokwa samaki wale bongo hapa ni watu wa pesa ndio wamekua wakiwala sana mwenzangu Mimi utaishia kuwaona tu au kula walio haribika kama ngulu wa chumvi wale ni samaki walio haribika kwaiyo wamewekwa chumvi nyingi kuondoka ukakasi tu ukiwakuta ngulu wenyewe original awachachi na watu wanawapiga vizuri tu Ila pesa ndio inatulisha vya bei chee wapo ngulu wenyewe safi watamu ndugu zanguni.

Tuendelee katika vile vyakula pia palikua na pombe ambayo niliichukua nje ya kopo palikua na picha ya nyoka yani hapa sumu ya nyoka ndio ilitumika katika utengenzaji wa hii pombe na pia ilikua na kipimo chake kuna namba ziliandikwa pale unywi ovyo ovyo tu pia ilitakiiwa umix na vinywaji vingne kupunguza ukali wa alcohol

Sasa kuna mwenzetu alikua mbishi alisema yeye pombe anazijua vizuri na awezi kusumbuka na pombe kabla ajanywa tulichanganya na maji na kisha yeye kunywa baada ya muda tu kidogo akaanza kutetemeka na baadae akaanza kutoka manundu manundu mwilini bila shaka ile pombe ilianza kufanya kazi tukamnywesha maji kwa wingi lakini baadae alipata nafuu na kuna mmoja wetu alikwenda kule kwenye damp katika kusaka alipata maziwa yaliyo ganda akaja akampa mshkaji akanywa walau akawa na nafuu sasa ila Yale manundu ayakutoka.

Basi kama kawaida siku iyo mwenzetu mmoja akaenda kucheki misos kule kwenye ile damp wakati kaenda kucheki zaga kuna sehemu kama mafuta ivi alikanyaga sasa wakati anarudi akaacha alama za mguu wale jamaa walipokuja kutupa mchana panakaua na mwanga wakakuta zile alama hapa walishtuka na wakaisi kabisa kuna watu ndani wakanza kutusaka.

Walisaka siku ya kwanza awakutushika lakini pale tulipo tulikua tunasikia zile movement zao sisi tukiwa tumejibanza wale jamaa awakukata tamaa waliendelea na hatimae wakatukuta kule tulipo na wote tukashikwa na kutolewa hapa sasa ikawa ni vitendo tu maana lugha ilikua ni lugha gongana akuna maelewanao vitendo ivyo ilikua ni kichapo wale wazungu walikua wana tupiga makofi mateke mladi kichapo tu.

Tukapelekwa eneo flani ivi tukapewa kazi ya kusafisha pale ilikua ni siku nzima akuna chakula wala maji kazi tu full usafi yule jamaa yetu mwenye manundu sele alikua anaitwa wakamuhoji kwa vitendo imekuaje akawa ambia vile vile akawapa ishara ya kunywa akataja na alcohol wale jamaa wakamu elewa walicheka sana walielewa jamaa kaparamia pombe ile ngumu .

Basi jamaa waliendelea kutuweka chini ya ulinzi pale na msosi tulipewa Mara moja tu uku wakitafakari lakini bila shaka waliona wakiendelea kubaki nasi uko mbele ni matatizo wale jamaa tulikua nao ila ni bahat tu sababu uwaga awakawizi mtu akishikwa wanakurusha baharini utajijua mwenyewe.

Mara nyingi walikua wakijadiliana naona ilikua ni mipango ya kutuhua sasa na kweli muda uliwadia ilikua usiku niliwasikia wakitamka Mozambique bila shaka tulikua msumbiji walitupa Bible (biblia) tujiombee kama ni mkristo msilamu iyo aiwahusu wakatupa pamoja na boya kubwa mfano wa boti ili tuweze kusurvive nalo tukiwa majini baada ya kutoswa

Tupate maji na ftari tutarudi
 
IBRA wa PILI

JF-Expert Member
Oct 12, 2017
572
1,000
Naamu kwa jina la jamhuri ya muungano wa jamii forum mzigo unaendelea thanos

Latino mwamba ana endelea na story yake...........

Wale wa giriki walitupa iyo biblia ya kujiombea uko majini baada ya kutoswa pia walitupa pesa wote jumla kama dola 100 ivi kila mtu yake lakin namaanisha ukijumlisha ndio inaweza fikia apo pia na maji ya kunywa kwenye kidumu flani,
kwa haraka niliona jamaa wanaona kabisa atuwez pona iyo biblia ni kama kujiombea tupokelewe uko akhera akuna jipya kwetu tena ivi vingne ni gelesha tu atuta toka navyo huo ndio utakua mwisho wetu sisi ni marehemu watarijiwa tu.
Lakini jamaa ni kama walituonea huruma tu awakuamua kutuua moja kwa moja ila walijua sie kutoka wazima ni ishu kwaiyo kama yupo atakae pona basi izo pesa zimsaidie mbeleni wale jamaa huwaga wanawafunga watu vyuma na kamba ukishikwa alafu wanakutosa baharini ivyo vyuma vinakupeleka chini kabisa na ndio mwisho wako.

Basi wakatoa kile kiboya kipo mfumo wa boti na wakatupakia mule ndani kisha wakakifunga kamba mbele na nyuma alafu wakaanza kukiteremsha taratibu awakuturusha hapa tulifika mpaka kwenye maji wao wakaona hapa sasa pana tosha wakakata zile kamba na sie tukabaki majini na lile life boya wao wakatembea mbele.
Lakini pia sie pale tulipokua atukua mbali sana na fukwe za msumbiji isipokua upepo sasa ndio ikawa shida kwetu na lile boya ndio likawa linapelekwa na upepo linafata uelekeo wa upepo unakoenda atukujua wapi tunakwenda kama kwenye maji mengi kina kirefu au wapi iyo ilikua ni twende twende tukisubiri tu kudra za mwenyezi mungu.
P
Ki ukweli hapa ndio tuliona sasa jamaa ndio wameamua kabisa kutuuua akuna jipya palikua na mawimbi na tukaona kabisa hapa tunakwenda kua msosi wa papa chakula ya papa akuna jingine.

pale tulipo atukuona ata mwisho zaidi ya kuona tu wingu limefika chini kisha bahari tulizungukwa na maji tu kiujumla na pale tulipo tulikua ni eneo la maji meusi au sehemu yenye mkondo kina kirefu apo ata meli uwezi weka nanga yani apo unaweza ukatumbukiza mistimu ya umeme ata 40 ndio ikafika chini au isifike ndio mana panakua na weusi yani pana kiza kwaiyo ni kina hasa.

Basi sehemu kama izo kwa watu wenye utalamu na maji ayo ni maneo ambayo papa ndio nyumbani kwao kwaiyo apo papa kukupitia ni dakika sifuri tu hii ilikua hofu yetu sana na atukujua Yale mawimbi yata tupeleka mpaka wapi.
Kuna muda ilifika tukaona kama taa mbele yetu kwa mbali kidogo lakini tulipokua tuna karibia atuzioni zinapotea kabisa jamaa yetu mmoja akasema hawa ni viumbe wa kwenye maji wanafanya shughuli zao mida iyo wanaitwa (vibwengo) ni kama majini tu ndio huonekana na kupotea na ukikutana nao ni wakorofi korofi wanatishia watu tu.
Kama mnakutana macho kwa macho utakiwi kukimbia cha msingi we mkazie macho alafu Fanya kama una mzungukia kwa nyuma awataki kabisa uwaone mgongoni ila inahitaji roho ngumu kufanya ivyo sio laisi imani ina hitajika sana apo lazima atoke atakimbia.

Basi muda umekwenda upepo mkali bardi usiseme ni Kali hasa miili yetu ikaanza kushikwa na chumvi mwili wote yani unakua ka kitoweo ivi ile chumvi ya bahari ni Kali ndugu basi tukasonga mbele tukipeana mioyo kibishi tu ila mbele zoruba ya mawimbi ilizidi ikawa inatuyumbisha mno mwenzetu mmoja hali yake aikua nzur ilishindwa kuhimili vile vishindo kutkana na zile pepo za kusi ivyo hali ilikua mbaya uyu tulimpoteza alifariki ila kabla ya kufa aliacha ujumbe kama ikitokea tutarudi nyumbani sisi basi tumpe taarifa bi mkubwa wake na tumwambie chumbani kwake kuna visjisent alichimbia chini ya kitanda kwaiyo avichukue kisha mshkaji akatulia akiwa ana tabasamu tu lakini si tulimwambia huwez kufa bado mungu yu nasi jamaa aliongea dunia ina mambo mengi mi ndio nafia hapa kweli badae alitulia mazima kabisa tuli ndio ikawa kaenda mwanetu.
Tulijifunga kamba wote wa nne ili kama ikitokea mmoja akabebwa na wimbi iwe laisi kumsaidia sasa baaada ya mshkaji kufariki tukamtoa kwenye kamba tukampigia dua mwenyezi ampoke kisha tukamshusha kwenye maji ilikua ni majozi na akuna namna tusingeweza kukaa na maiti sababu mahiti ina mambo mengi pia ingetupa uzito jamaa alikwenda namna iyo apo tukabaki wa tatu tu.
Tulizidi kusonga zaidi mbele tukisubir nini kitatokea mbeleni apo sijui ni siku ngapi toka jamaa watutose tulikaa alafu pia ata njaa atukuiskia lakini tulikua tunakunywa maji Yale walaiyo tupa baadae ya liisha Yale maji na toka yule mmoja wetu afariki aikupita siku nyingi tukaja pata msaada kuna muda boti ya watalii ilipita mwenzetu mmoja alikua anajiweza kidogo alichukua nguo na kunyoosha juu kwa mkono kama bendera ivi hii ilisaidia wale watu wakatuona na wakaja mpaka tulipo pale na kutupa msaada wakatutoa kwenye lile boya na kisha kutuingiza kwenye boti yao tukiwa hoi dhoofu atujiwezi aiku chukua muda tukazimia wote tukiwa ndani ya boti tulizimia.
Tulikuja shtuka baadae tukiwa pwani ya msumbiji tukipewa huduma ya kwanza lakini pia walituandalia uji baada ya kuamka wote walitupatia uji tulikunywa tukamaliza akatupa mwingne nao tulimaliza tukaomba mwingne wakatunyima sababu pale tuliona bado atushibi kumbe tumbo bado alijawa kwenye hali yake baadae lilipokuja kukaa sawa ndio tukaona tulishiba kupitiliza.
Sasa basi baada ya kukaa sawa jamaa walituhoji ilikuaje tuka wadanganya kwamba tulipata matatizo sisi ni wavuvi tulikumbwa na matatizo ndio ikapelekea mpaka kua hapa atukuwaambia ukweli kwamba tulikua stolo way.
Basi katika wale wa tatu tuliobaki sele yule wa manundu alirudi Pemba mwingne aliitwa mangushi uyu alielekea richadbay Mimi niliamua kubaki pale pwani ya msumbiji sikuona haja ya kuondoka tena na pale ilikua bichi kuna shughuli za uvuvi zinafanyika basi nikaona nijiongeze pale kwenye mishe ya uvuvi.
pale nikajiunga na washkaji flani wa pale msumbiji ambao walikua wenyeji wa kusin uku mtwara uzuri kiswahili walikiweza vizuri na palikua na wa makonde na makabila mengne ya msbiji ivyo ikawa wepesi kwangu kuelewana nao.
Sasa katika ile pwani ya Mozambique republican ambapo ndio nilijiunga na wale washkaji palikua na kisiwa kinaitwa Angoche island kina samaki wengi sana isipokua kisiwa hiki kilikua na maajabu mengi mengi na hata watu ilikua nadra kwenda uko kilihusishwa sana na imani za kishirikina ila inavyosemekana aya mambo kwenye icho kisiwa yalianza kitambo sana kwaiyo sisi ni ubishi tu kwamba izo ni imani tu na ilikua zamani enzi hizo kwaiyo akuna kipya sie tuende kwa kujiamin kwenda kufanya shughuli zetu za uvuvi ndani ya angoche island kinachosemekana kilikua na maajabu iki kisiwa.....................
Tupumzike tutarejea swaumu kali
Sio kwieli ThemiOne
 
Vera ginger

JF-Expert Member
Dec 25, 2016
1,093
2,000

Daaah yan kutafuta hela sio jambo rahisi
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom