Si kweli, hiyo thread yako imekosa data. Kwanza hakuna kitu kama article of association badala yake kuna article of union.
Na article hiyo imekuwa ikiongezewa vipengele kadhaa mara kwa mara. Kwa mfano, Aticle ya kwanza kbs ya mwaka 1964 iliainisha mambo 11 tu kama UNION MATTERs. Lakini kwa sasa mambo hayo yameongezwa na kufikia 33.
Cha msingi unachopaswa kujua ni kuwa Article of union halisi ya mwaka 1964 ni siri sana na haijawahi kuonekana hadharani.
Na hii inatokana na mambo makubwa mawili. Kwanza haijaainisha kimsingi masuala ya muungano, pili ambalo ni kubwa zaidi iliweka ukomo wa muunganno ni mwaka 1974.
Kwa mujibu wa makubaliano ya Mwalimu na Karume, ni kuwa muungano uwe wa miaka kumi na baada ya miaka hiyo kumi kama kila upande utaridhia basi waongeze mingine kumi.
Hivyohivyo waendelee kurenew kulingana na makubaliano ya vioogozi wetu na maridhiano ya wananchi wa pande znte.
Lakini ilipofika mwaka 1972 mzee Karume alionekana kuchoshwa na muungano hali iliyomfanya aonekane kuwa ikifika mwaka 74 hatakubali kurenew mkataba.
So inadaiwa zikapikwa njama za kumuua. Ndio maana hadi leo kifo chake ni utata mtupu.