Zakia Meghji na uuzaji wa Mbuga zetu je atapeta pia ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zakia Meghji na uuzaji wa Mbuga zetu je atapeta pia ?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lunyungu, May 22, 2008.

 1. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #1
  May 22, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Wataznania
  Wote mnakumbuka adha ya Loliondo na watu wa kule , mnakumbuka wanyama kusombwa kwenda Arabuni na Ulaya , mnakumbuka Utalii kukabidhiwa wageni yote haya kwa kiasi kikubwa yalifanywa na Meghji Waziri ambaye aliupata Uwaziri kwa Ubunge wa rais mwenyewe .Hazina mnajua madudu ya kule hata wakawaza kusema tunaweza kutumia a USD pamoja na sisi kuwa huru zaidi ya miaka 40 .

  Sasa mimi nauliza si wakati wa kujua kwa Zakia aliamua kutuhujumu na sasa hakuna anayemgusa anakula kwa utulivu huku Nchi ina angamia ?
   
 2. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #2
  May 22, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Zakhia Meghji amekaririwa jana na Gazeti la Daily News akisema alikuwa na uhusiano mzuri wa kikazi na Billal. Ina maana alivyo tueleza kwamba alidanganywa na Billal alikuwa anaongopa?

  May 21st, 2008, Baada ya Ballal 'kufa.'

  Former Minister for Finance, Mrs Zakhia Meghji told the 'Daily News' that Dr Ballali was ailing for the nearly two years she worked with him and that he needed to travel regularly to the US to visit his doctor. She said that they enjoyed a good working relationship, and prayed for his soul to rest in peace.

  January 14th, 2008, Kabla Billal 'hajafa'

  "I agreed to sign the letter, drafted by the governor himself, because I trusted the governor at that time. It was only later that I realized the payments to Kagoda Agriculture Limited were not related to any government expenditure."

  Huyu Mama aidha fisadi, au mwongo mwongo.
   
 3. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #3
  May 23, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Kuhani,

  Si ndio utamaduni wetu wa marehemu hasemwi huo.

  Hata Idd Amin alipokufa alisifiwa kuwa alikuwa mtu mzuri.
   
 4. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #4
  May 23, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Duuuuh!

  Mbona hapa Billal watu wanammaliza? JF wako out of touch na tradition?
   
 5. BabaH

  BabaH JF-Expert Member

  #5
  May 23, 2008
  Joined: Jan 25, 2008
  Messages: 703
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Zakia chakula ya Rostam Azizi
  Rostam Azizi ndio King Maker wa mafisadi Tanzania

  Rostam ndiye kamuweka kusura madaraki kwa kuiba na kuonga

  Sasa hapa unatarajia ZM akamatwe na kufikiswa wapi?

  Hili linchi letu limeoza
   
 6. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #6
  May 23, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145


  Kuhani haya ni maelezo ya ziada tu na uongo wao wote hawa ila nataka kujua .Are we gonna let her walk free na hasara yote aliyo tutia ? Mbona tunawabana akina Chenge kuanzia mikataba nk lakini huyu na Mbuga zetu tunakaa kimya ? Loliondo ndiyo imeisha sasa wale watu wa kule tuache Mungu awatetee siku ya Kiama?
   
 7. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #7
  May 23, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Tuonyeshe statistics!
   
 8. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #8
  May 23, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Hivi unaijua skandali ya Loliondo au unapiga kelele tu hapa? Unakumbuka ni waziri gani hapa Tz ambaye alipewa hata jina la skandali ikiwa mojawapo ya hiyo Loliondo?
  Hebu usisushe hadhi ya JF..
   
 9. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #9
  May 23, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Rudia kusoma bandiko langu nadhani baada ya hapo utaelewa .
   
 10. M

  Mwakilishi JF-Expert Member

  #10
  May 23, 2008
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 484
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Saa nyingine hizi traditions zetu nyingine ni za kinafiki sana, cha ajabu jamii hata kama inajua uovu wa mtu, akifa basi atamwagiwa misifa kemkem... sasa akina Watson wakiona hivyo wana-conclude... tunaanza kulalama!
   
 11. I

  Ipole JF-Expert Member

  #11
  May 23, 2008
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 296
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Lunyugu uechemka hakuwa Zakhia kwenye kashfa hiyo kumbuka kulikuwa kun mtu anaitwa skandali
   
 12. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #12
  May 23, 2008
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  tumekuwa ni watu tunaobururwa sana kimawazo!!

  wakuu wametutaka tuimbe wimbo wa ufisadi basi bila ya kuvuta pumzi na kujiuliza tumekuwa wa kuhemkwa tu.


  akisemwa Mwatumu fisadi hufikiri unaruka kweli fisadi.

  zakia mwanamme wake rostam kweli na vipambio tuengeze kama vile tunajua sana.

  JF makini lazima tuipiganie irudi na ni ile yenye kuja na data za uhakika halafu ndio tunafanya analysis kwadata sio kukurupula tu
   
 13. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #13
  May 23, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145


  Mtu wa pwani wewe si mtu wa data bali kubeza kama hapo ulipo beza .hapa watu tuna uliza Maliasili wakati wa Meghji kuna mengi yametokea.Tunataka kuweka rekodi straight na ibaki iko siku tutakuja kutafuta data hizi .Mtu wa pwani data zako zimekuwa ni utetezi na vijembe na labda kuhamisha data na kupeleka huko unako husika wacha kutukana watu .Hapa haimbishwi mtu na mambo huwa yanaanza namna hii .Tunataka kujua mambo wakati yanaenda mrama kule Maliasili na Utalii yeye alifanya nini .
   
 14. J

  Jamco_Za JF-Expert Member

  #14
  May 23, 2008
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Hili alina ubishi mariasili kumeoza sana wakati wa zakia, nafikiri hawa mawaziri wakifika wanapewa mafundisho na makatibu wa wizara maana uozo umeanza siku nyingi na unaongezeka kila siku, ila wakati wa zakia nafikiri ulifika kiasi ambacho kilikuwa kinatisha zaidi kulinganisha na vipindi vingine.
   
 15. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #15
  May 23, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Wewe ndie huna data, kama unataka kuweka rekodi, basi Loliondo na Meghji futa hiyo kwanza, Kama hujui kitu usione aibu kuuliza na sio kuandika kitu ambacho hakipo...
   
 16. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #16
  May 23, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,705
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Kwani mambo yameacha kwenda mrama huko Maliasili na Utalii? Haya yanayoendelea Serengeti (ujenzi wa airstrip, mahoteli), Ngorongoro (ujenzi wa mahoteli) na Ziwa Natron (ujenzi wa kiwanda) hatuyaoni? Au ndio tunasubiri mpaka yatakapoharibika ndiyo tuanze kuwashughulikia wahusika!
   
 17. S

  Savimbi Member

  #17
  May 23, 2008
  Joined: Apr 17, 2008
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu
  Hapa sijui kama watu wanalielewa hili som kwani limetokea kipindi kirefu kidogo!

  Ni kweli kipindi kile kampuni ya uwindaji ya Kiarabu ilipopewa kibali cha kuendesha shughuli za uwindaji Loliondo Bi. Zhakia alikuwa waziri wa maliasili na Utalii.

  Kampuni hiyo ilipatiwa kibali cha kuendesha shughuli zake kwa muda mrefu (sikumbuki vizuri, walipewa miaka mingapi) kitendo ambacho kiliwashangaza wadau wautalii, mpaka yakatokea manung'uniko ya chini kwa chini. Lakini sababu Mke wa mzee Ruksa alikuwemo ndani yake, mambo yalikubalika na shughuli ikaendelea.

  Serikali iliamua kustisha mkataba wa kampuni hiyo kabla ya muda walipewa kumalizika, baada ya kugundua kuwa wanaibiwa, wale jamaa walikuwa na uwanja wao wa ndege, kwa hiyo wakichukua wanyama wanaruka moja kwa moja toka Loliondo kwenda kwao nani atajua kuwa kile kilichochukuliwa ndicho walichokubaliwa kuchukua.

  Nakumbuka walipofunga shughuli zao hawakuondoka na kitu chochote, vifaa vyao vyote walivyokuwa akivitumia walivitoa zawadi kwenye kikosi cha jeshi ambacho kiliendesha oparesheni ya kuwasaka wasomalia waliokuwa wakifanya uporaji sehemu za Loliondo na Ngorongoro wakifadhiliwa na matajiri wauza mirungi wa Kenya

  kwa vipindi 2 ambavyo Zakia amekuwa waziri wa maliasili na utalii, kulikukuwa na mambo kibao ya kimauza -uza.
   
 18. Mr Kiroboto

  Mr Kiroboto JF-Expert Member

  #18
  May 23, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 321
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  yakhe!huyu zakhia n yupi au yule mama mkwe wa kisura?
   
 19. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #19
  May 23, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Mwaka 1992 sehemu ya Loliondo(LGSA) ilikodishwa kwa asasi ya uarabuni kwa ajili ya uwindaji na ubebaji wa wanyama kwa kipindi cha miaka 10. Mwaka mmoja baadae (1993) Waziri wa utalii wakati huo Abubakar Mgumia alijiuzuru kutokana na kashfa ya LGSA...

  Sasa huyo Meghji anahusika vipi na hili... Hebu fafanueni
   
 20. Kidzogolae

  Kidzogolae Senior Member

  #20
  May 23, 2008
  Joined: Apr 20, 2008
  Messages: 134
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  unakumbuka huyu mmama alitaka kuuza hata ule msitu wa Tanga wa selikali kwa shs.7billion, wakati walipokuja kufanya tathmini ulikuwa halali uuzwe kwa shs.60bill., kuna daktari mmoja hivi wa mazingira kule morogoro(nikipata jibu nitawaambia)ndo alikuwa repsonsible na misitu akapinga sana. mpaka leo huyo Dr.hapatani na zakia. huyu mmama ni mama mmoja fisadi sana..anatisha. mimi niliumia sana hata kipindi kile alipochaguliwa kuwa W.wa fedha. yaani tz wakati mwingine kama hatuna macho vile. tunaweka uchafu kwenye uongozi, hivi wasomi wameisha kweli mpaka tunaendelea kuhangaika na mafisadi madarakani? hivi wewe unaesoma hii msg, ukipewa madaraka uwe waziri, utashindwa kufanya kazi bora kuliko hawa? sasa kwanini wasipigwe chini wakapewa watu waadilifu, mbona wasomi waadilifu tunao wengi tu hapa tz. inauma sana kwakweli.
   
Loading...