Zaidi ya watanzania 100 wafariki Mererani

Hivi kuna fisadi gani yameyafungulia yale maji ya mvua yakaingia kwenye mashimo ya madini?Sijui! huenda kuna wana CCM wamefanya hivyo!sijui!Au utawala wa KIkwete umesababisha hiyo Gharika ya mafuriko kwenye hayo mashimo!Sijui!Sijui!
 
Laiti ungejua maji yaliingia kupitiwa wapi na ni kwanini yaliingia; laiti ungejua kwamba hapo maji yalipopitia palishafanyiwa 'mradi hewa' wa kupaziba kwa pesa za serikali! Laiti ungejua jinsi wenye migodi walivyowazembe pia kwa upande wao; laiti ungejua jinsi ambavyo Tanzanite One nayo ilizembea kwa sababu zao. Laiti yote yangefanyika kwa wakati mwafaka kabla na hata mara baada ya tukio. Pasingekuwa kuwa na vifo vingi hivyo vya vijana wana-apollo, na wala tusingekuwa tunasubiria sasa hivi kufukuliwa kwa maiti zilizoharibika vibaya. Nikipata wasaa siku moja nitaandika niliyoyaona kwa macho yangu. For now, everything remains a wish. And If wishes could have been horses, even beggars would ride!

JJ

John hii serikali imeshaoza tangu zamani. Kumbuka madini ni private sector, na serikali kazi yake ni kuangalia mazingira ya kazi ya wana Appolo

Mimi ni ombi langu wewe binafsi kwa niaba ya JF, Naomba uangalie kama utaweza kupata SAFETY POLICY ZA MGODI, then waulize KAMA KILA MWANA APPOLLO ANAELEKWEZA SAFETY ISSUE PRIOR KUINGIA MGODINI.

THEN, YOU WANNA ASK NI LINI LAST TIME MGODI ULIKUWA INSPECTED NA SERIKALI, AND WHAT WAS MATATIZO, MAFANIKIO AND RECOMMENDETION.

please don't take it as political arena, but public figure. Tanzania need stronger representative.Swala la Migodi na madhara yake ni nyeti sana, watu wengi sana wameshakufa na maneno kutoka serikalini yanasema ni kazi ya mungu.

Lakini kama kuna safety code zimekuwa breached then unaweza kuona kwa nini human error zinaweza kusababisha vifo. Mgodi wa Tanzanite unatengeza pesa sana kwa hizo big corporation, ninachoshangaa ni kwanini hawa wachimbaji hawako full equiped? Yaani Kofia ya chuma yenye tochi, na sio kufunga tochi kwenye kichwa. Then first Aide Kit, yenye dawa za huduma ya kwanza.

Kama utangaalia statistics, unaweza kushangaa kwamba labda hiii migodi imeshaua watanzania wengi kushinda hata ajali za barabani za Tanzania nzima kwa miaka 5.
 
Tatizo ka kushindikana muafaka Zanzibar - Kazi ya Mungu
Jinsi tulivyokwapuliwa BoT - Kazi ya Mungu
Ditopile alivyomtwanga jamaa risasi - Kazi ya Mungu
Tatizo la njaa kwenye nchi ya maji ya kutosha - Kazi ya Mungu
Tatizo la nishati - Kazi ya Mungu

Hivi huyu Mungu anayefanya kazi hasi namna hii kwanini tumuamini? Yaani amekula njama dhidi ya Tanzania na watu wake?

Pesa za msaada zilizotolewa na japan kwa ajili ya kusaidia wananchi na kisha kutumbukia mfukoni kwa AZIZI----kazi ya Mingu!!
 
ninavyojua mimi hakuna mafuriko yanayoweza kutokea ghafa namna hii ni lazima kuna mkono wa fisadi
 
I think poor management, safety and security checks, obsolete technology should come first and foremost, kabla ya kumbebesha lawama Sir God. Mvua isiponyesha tunamtupia lawama god, ikinyesha na kusababisha disaster kama hizi tunamlaumu God, wapi na wapi wandugu?? Sisi wenyewe ndio chanzo cha matatizo.

Mkuu Mwanamalundi nakunga mkono 100%, ninavyoelewa mie mgodi wowote ni lazima uwe na Safety checks ambazo zinazuia ajali na pia zinalinda usalama wa wafanyakazi wakati wote wawapo kazini. na inapotokea ajali basi kuna Emergency preparedness Team ambayo iko full equiped na hutoa msaada kwa wakati muafaka. Tatizo kubwa wa migodi ya mererani ni kwamba hayo yote hayafuatwi na naweza sema kuwa ni fujo tupu hakuna usalama kabisa makazini kwao kwani rushwa inafanya kazi kuliko sheria,nadhani si wizara ya madini wala wizara ya kazi wameshaenda kufanya Safety auditing toka migodi hiyo ianze na kama wamefanya basi itakuwa ni ushahidi wa kutafuta night allowonce.kwa kifupi naweza sema hapo hakuna excuse ya kazi ya mungu kwani muda wa kujitayarisha kwa ajali kama hiyo walikuwa nayo katika miaka ya nyuma na wakati mvua inaanza waliiona na kuidharau kwani system yetu ya usalama hapo mererani hakuna. nashangaa kwenye hiyo TV sikuona hata gari moja la Resque achilia mbali resque member akiwa kazini ila mashangi yalikuwa mengi kedekede,je tutafika?
 
Hata hivyo lililonigusa ni lile la kusema kuwa "tumekuja hapa kutafuta chochote, lakini hatukutegemea haya, sisi tunapanga na Mungu anapanga".. Kwa kadiri nilivyomuelewa ni kuwa yaliyotokea Mererani ni kazi ya Mungu

na aliahidi kuwa baada ya uchunguzi na utafiti wa kina basi machimbo hayo yatafunguliwa mara moja.

Maafa yametokea, Waziri Mkuu ametuma mawaziri watatu haraka sana, na hatimaye rais mwenyewe ameenda, ametopa poel na ameahidi uchunguzi kujua chanzo cha maafa, unless kuna something I am missing, hivi amekosea nini hapo wakuu?

Naomba kuelimishwa kidogo?
 
Maisha yako so cheap Tanzania.

JK Ka orrder siku 3 za rescue, baada ya kukaa kwenye kikao cha CCM apparently alichofikiri kina umuhimu zaidi ya rescue work, kwa siku kadhaa.

Wachimbaji wanadai wapewe hela zaidi (40,000 instead of 10,000 per body), hawa ni watu waliokuwa wanafanya nao kazi!

Hapa ndipo tulipofikia. Nilikuwa naangalia blog ya photojournalist mmoja kampiga picha kijana mmoja mdogo tu, anasema huyo kijana "alishapasua" akawa na hela sana kiasi akawa anakodisha ndege na kuzunguka nayo sana mbugani huko akitanua na ku spend, halafu kamaliza hela karudi tena shimoni in the hopes za kupasua tena. Kazi ya hatari kama hii.Hii ndiyo desperation tuliyo nayo kutokana na elimu ndogo tunayowapa watu wetu, no investment no hopes of taking things to the next level, just subsistence existence, hand to mouth with the paltry millions, shortchanged by the government, shortchanged by the market, caught up in the life, sheer desperation.

One more reason to unseat CCM and Kikwete.

Nakumbuka kuna wakati wakubwa walikuwa wanajadiliana uwezekano wa kujenga hospitali kubwa pale Tumbi kutokana na wingi wa ajali zinazotokea. Na walikuwa serious hawa mabwana. Hakuna aliyesema tufanye nini ili hizo ajali zisitokee bali walienda moja kwa moja kwenye mpango wa kujenga hospitali!Bila shaka dhana ya kuwa ajali zinazotokea pale ni mapenzi ya mungu ilitawala.

Si viongozi tu hata sisi wananchi tunaamini hivi. Mtoto anakufa kutokana na uzembe wa daktari, tunasema kazi ya Mungu kwani hata nikipiga kelele vipi mwanangu atarudi!

Jamii yetu imefika mahali ambapo pakitokea ajali tunakipingilia kupiga sachi na kama majeruhi atatikisika si ajabu tukimsindikiza ahera! Hao maapolo wanaona huu ndiyo wakati wa kuvuna na bila haya wanadai malipo hayo ( nasikia kuna wengi wanaona kuwa hii ni kafara kwa mwenyezi na neema kubwa itafuata). Lakini, tujiuulize, baada ya maafa yote haya kama alivyoainisha Mzee Mwanakijiji hatuna chombo maalum cha kukimbilia kwenye majanga kama haya? Fast response team kwa maneno mengine. Kwa nini tunategemea maapolo kufanya kazi ambayo bila shaka inahitaji utaalamu wa hali ya juu?

Baada ya haya yote kutokea hatuna political will ya kuwaambia hao wanaojiita wachimbaji wadogo kuwa hawataruhusiwa mpaka hapo tutakapohakikisha kuwa kanuni za uchimbaji salama zinatekelezwa. Ikumbukwe kuwa hao wachimbaji wadogo wengine wao ndio hao tunaowaita vigogo. Sheria ziwekwe na zisimamiwe bila kuangalia uzalendo. Na wale wenye migodi iliyohusika katika tukio, ichunguzwe kama ilikuwa salama na kama sio, wachukuliwe hatua kali za kisheria.

I am not holding my breath on this one.
 
Maafa yametokea, Waziri Mkuu ametuma mawaziri watatu haraka sana, na hatimaye rais mwenyewe ameenda, ametopa poel na ameahidi uchunguzi kujua chanzo cha maafa, unless kuna something I am missing, hivi amekosea nini hapo wakuu?

Naomba kuelimishwa kidogo?


Mkuu alichokosea ni kutoa sababu zisizo na kichwa wala miguu . Mzee ES anapoanza kumwingiza Mwenyenzi Mungu katika hili jambo lengo lake ni kuibua hisia za watu kuwa emotional and they will start saying it was meant to be. Hiyo slogan " Kazi ya Mungu " inatumika vibaya siku hizi na watu ambao wanataka kupotray ya kuwa kulikuwa hakuna njia nyingine ya kusolve tatizo na mara nyingi hawa watu ni wavivu wa kufikiri lakini zaidi wanaogopa kujua ukweli ....

Kitu kingine kinachoniuzi mimi binafsi ni trendi ya Rais wetu kufanya uchunguzi kwenye kila jambo hata kama chanzo la tatizo lake linafahamika . Huu ni upotevu wa hela za walipa kodi, Kwa nini ufanye uchunguzi wakati unajua kabisa ile migodi aina storm water drainage systems ?Jee kuna safety standards zozote zinazofuatwa pale? Huu ni ujinga wa hali ya juu and can someone please tell me which govt entity oversees that mgodi ?

Rais ni lazima atambue ya kuwa awezi kuwa mzuri kwa kila mtu na saa nyingine ni lazima uwaambie watu maneno ambayo hawatafurahia ! This is what i would have done if i were the president . I would ask the ministry of minerals to make sure that safety regulations are implemented and followed . Secondly , I would build a nice infrastructure that will enable those miners to perform their duties effectively but more importantly safely throughout the year , in return they ought to pay taxes.

Suala sio kupeleka mawaziri matatu , suala ni jee wamefanya nini ? Na jee serikali imeplay role gani kuhakikisha ya kuwa safety kwenye hii migodi inaboreshwa ? Mind you this is not the first incidence in Mererani, we are talking about innocent lives that been lost simply because the government as well as the owners didn't play their part. ...something needs to de done .
 
Maafa yametokea, Waziri Mkuu ametuma mawaziri watatu haraka sana, na hatimaye rais mwenyewe ameenda, ametopa poel na ameahidi uchunguzi kujua chanzo cha maafa, unless kuna something I am missing, hivi amekosea nini hapo wakuu?

Naomba kuelimishwa kidogo?

That something missing is that this is happenning over and over and there are no measures implemented to prevent the same thing happenning tomorrow.Hakuna vision wala leadership ya ku deal with these disasters, sio kitu kipya kinachotushtua, ni kitu tunachokijua na kinatokea year in year out, kwa nini hatuwezi kuchukua challenges za environment na kuzifanyia kazi?

Wajapani walikuwa wanakufa sana kutokana na matetemeko ya ardhi, wakaamua kulifanyia kazi hilo swala sasa Tokyo yote skyscrapers ni quake resistant, hapo likitokea quake halafu akafa mtu nitaamini ni kazi ya mungu.Sisi tumefanya nini? Tena watu wana hela hawa wakipata leadership na ideas kuboresha usalama wao sifikiri kama watakataa kutoa hela.

This is not only directed to the government, but to the miners and their organizations also.

SEE ALSO
Thirty feared dead in Tanzania mine
20 Jun 02 | Africa
Over 50 dead in Tanzanian mining disaster
14 Apr 98 | Africa
Tanzania suspends gem mining
22 Jun 02 | Africa
More than 100 feared dead in Tanzania mine floods
12 Apr 98 | Africa
 
Maafa yametokea, Waziri Mkuu ametuma mawaziri watatu haraka sana, na hatimaye rais mwenyewe ameenda, ametopa poel na ameahidi uchunguzi kujua chanzo cha maafa, unless kuna something I am missing, hivi amekosea nini hapo wakuu?

Naomba kuelimishwa kidogo?
FMES, tatizo ni kwamba huwa marais na viongozi wanatumia tragedy kama hizi to make a statement yaani kuhakikisha kwa mfano that things get done. Issue ya safety kwa mfano ingeweza kuibuliwa na angeweza kuja na statement ya kuwa katika siku za hivi karibuni watatangaza conditions mpya kwa wamiliki wa mgodi ambayo ni lazima wafuate kuhusiana na usalama kwa wafanyakazi wa migodini. Ni lazima azungumzie responsibility ya wamiliki. Unafikiri vitalu vile havina wenyewe? Vina wamiliki ambao ni watanzania wenzetu wengine wanatanua na ma VX na ma Vogue Dar na Arusha na wanawatumia vijana wetu kuchimba. We have to talk about this, siyo siku zote tunawasema tu akina AFGEM! Na this tragedy is a good reason to start that discussion, siyo kusema eti Mungu!
 
Nadhani sasa wakati umefika kwa wananchi kuuliza serious questions

1. Jee hii migodi mara ya mwisho ilikaguliwa lini kuhakikisha ya kuwa safety standards zinafuatwa?

2. Na kama jibu la hapo juu ni ndiyo , jee ni kitengo gani cha serikali kilifanya hivyo.

3. Kwa kuwa hii sio kesi ya kwanza kutokea , serikali ilichukua hatua gani kuhakikisha ya kuwa maafa kama haya yasingetokea.
 
Haya njoo kwenye vivuko vyetu hapo, tukiwa tunakumbuka ajali ya kivuko kule kilombero, leo mavivuko yetu katika Tanzania yetu ni mabovu kupindukia tena sana, lakini serikali inafanya usanii kwenye hili mpaka watu watakapozama ndio watasema mapenzi ya Mungu.

Na hapo ni hao 60 wamekufa kwa pamoja ndio maana hata kikwete kaenda, lakini kwenye jiji la Dar es Salaam, watu kila siku ya mungu wanakufa kwa ajali za barabarani tena wengi tu, nazo wanasema ni mapenzi ya Mungu.

Haya pamoja na haya yote, serikali hata haina jinsi ya kuwaokoa watu wake wakipatwa na majangaa kama haya, ebu fikilia Mgodi kama ule eti hauna hata First aid Kits za kusaidia wachimbaji wadogo wadogo, pili hata machine za kutolea maji hakuna!! LOOO

Majuzi kivuko cha panagani kimezama nusu, Kivuko hicho kimeahidiwa kuwa kingewekwa kipya mapema sana, hii ni wakati wa kampeni za Muungwana.
Kivuko cha Mv kigamboni kila siku kinapoteza mwelekeo siku kikiuwa tutasema - kazi ya Mungu.
Huyu Mungu Jamani afanye nini na nini aache? Unajua watu tunaitupia lawama serekali kwa kuwa wameshidwa kusimamia yale waliotuahidi au wameshidwa kutekeleza majukumu yao.. CCM kwa kweli wakati wake umefika
 
..kitengo cha Uokoaji na Maafa kiko chini ya Waziri Mkuu.

..Waziri Mkuu Mizengo Pinda alitakiwa kuwa kati ya viongozi wa kwanza wa serikali ktk eneo la ajali.

..haiyumkiniki wananchi zaidi ya 100 wamekwama ktk mgodi, halafu Waziri Mkuu anaendelea kukaa Butiama huku akituma wasaidizi wake.

..katika hili kwa kweli Mizengo Pinda amenichefua. ameshindwa hata na sumaye "zero" ambaye aliondoka ktk kikao cha bunge kwenda kusimamia uokoaji ktk ajali ya treni.

..inaelekea maisha ya Watanzania hayana dhamani kabisa. wachimba madini zaidi ya 100 wanapoteza maisha and all we can say ni "kazi ya MUNGU."

NB:

..JWTZ kwanini hawawezeshwi ktk masuala ya uokoaji? badala ya kupoteza mapesa huko Comoro bora tungefundisha askari wetu shughuli za uokoaji kama hizi.
 
Damn,

Not to be morbidly sarcastic but I cannot help noticing the parallels.

This turned into Katrina, complete with an airhead president with delayed response (Bush/Kikwete) and the troops in other missions (Iraq / Comoro).

No wonder they vibed so much.

Only thing missing

Kikwete dont care about CHADEMA.
 
Nah....bad parallelism....because your concept is predicated on a conspiracy theory...
 
You are using Euclidean Geometry in the territory of Non-Euclidean Geometry, of course you can't see the deal.
 
Nah....bad parallelism....because your concept is predicated on a conspiracy theory...

Hivi wawekezaji hana policy ya kuwasaidia wazawa na hasa yakitokea maafa kama haya ? Je Kikwete anasemaje ama alisemaje hata baada ya kuwaona watu wanatumia vyombo duni ku fetch maiti ?
 
Back
Top Bottom