Zaidi ya watanzania 100 wafariki Mererani

Wakuu Rufiji, Susuviri, na Pundint,

Heshima mbele na nimewasikia, naomba kuuliza tena, hivi kweli sheria ikifuatwa inavyotakiwa huko kwenye migodi ya wazawa kuna hata mmoja utakaobaki wazi? Sasa what that will do kwa ajira za wananchi wanyonge?

Maana wakuu mkumbuke kuwa hii ni bongo, sio majuu, mimi ninaaamini ukiamua kufuata sheria hasa za kila sekta, huenda itabidi ku-close bongo nzima sasa itakuwaje?

I respectfully disagree, sheria ni lazima ifuatwe! Kama huna uwezo usifanye shughuli hizo. Naomba kuuliza: kama mimi leo nikiamua kujiingiza katika taaluma ya udaktari na nikaanza kutibu watu nyumbani na kuwapasua ubongo nikisema 'natafuta kula'itakuaje? Na migodi nayo ina sheria zake na ni kwa ajili ya kulinda afya na uhai ya wafanyakazi wa migodini. Hakuna mjadala! Kama huna uwezo nayo, find another line of business. Mimi nakwambia matajiri wa Merarani wana pesa ya kutosha na siyo wao wanaoingia migodini. Badala ya kuwanunulia mahawara wao magari na nyumba wange-invest kwenye migodi.
 

Jamani tusamehe, kazi ya Mungu hii, nchi yetu duni, teknolojia hatuna. Bush alipokuja Airport tukampigia mizinga. Basi acha ifuke moshi. Mwanangu Bush akafikiri yuko kwenye Civil War ya karne ya 19!

Makachero wa Bush wakaona hii mibaruti nishai, isije ikakosea ikaruka kwingine. Basi unaambiwa ulipofika mzinga wa kumi wakauliza bado mingapi. Wakaambiwa mizingi si ishirini na moja!

Wakasema 'that's allright!' Kikosi cha mizinga kikazidi kuichochea, wakati wanyamwezi wamesema hapo poa, yaishe. Basi mwanangu ikaburuzwa yote 21. Masizi hayo!
 
haya mambo ya kusema ndio kazi ya mungu, ndio yanawapa wakina Nyani Ngabu ubavu wa kusema "ndivyo tulivyo"......watu mia kufia mgodini ktk karne hii si kazi ya mungu, hapo tuna mpakazia!!!
ingekuwa kwa wenzetu mgodi ungefungwa, tume ingianzishwa, sheria mpya za usalama zingetungwa na watu wizarani wangewajibika. kwanza mara ya mwisho inspection juu ya safety ktk mgodi huu ilifanyika lini na matokeo yalikuwaje?? lazima ajali kama hizi migodini zikome, na zitokee tu pale ambapo kweli ni kazi ya mungu, let say tetemeko la ardhi au kitu kama hiyo!!

Watu kuishi kwenye nyumba za udongo na watu kula mizizi ndiyo yananifanya kuamini sisi Ndivyo Tulivyo!!
 
Maiti walioopolewa Mererani sasa wafikia 35

2008-04-04 17:24:54
Na Radio One Habari


Idadi ya maiti waliopolewa kutoka migodi ya tanzanite huko Mererani imefikia 35 baada ya wengine saba kuopolewa jana usiku.

Habari hizo zinasema maiti hao saba wameopolewa kutoka mgodi wa Roita.

Pamoja na kuendelea kuwatafuta maiti wengine kutoka migodi hiyo, kazi inayofanyika sasa ni kuziba eneo lililobomolewa na kujenga mifereji ya kuongoza maji kutoka maeneo ya mafuriko, kazi ambayo inafanywa na vikundi mbalimbali wakishirikiana na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.

Habari zaidi kutoka eneo la tukio zinasema wawakilishi wa Benki ya National Micro Finance wako eneo hilo kukabidhi msaada wa shilingi milioni kumi ili kusaidia kazi hiyo.

Aidha, viongozi mbalimbali wa serikali wakiwemo Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Mheshimiwa Adam Malima, Mkuu wa Mkoa Manyara, Bwana Henry Shekifu Kamanda anayeongozi operesheni hiyo, Naibu Kamishna wa Polisi Venance Tossi.

SOURCE: Radio One
 
Back
Top Bottom