Dampo la taka laporomoka, 30 wafariki

Dampo la taka laporomoka, 30 wafariki

Miss Halima

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
302
Reaction score
646
Takribani watu 30 wamefariki dunia na wengine 22 kujeruhiwa baada ya mlima wa taka kuporomoka na kuangukia nyumba zilizokuwa karibu katika mji mkuu wa Guinea, Conakry, kufuatia mvua kubwa kunyesha.

Tukio hilo limetokea majira ya saa nane usiku katika eneo la Dar es Salaam jijini Conakry. Serikali ya Guinea imesema dampo hilo liliporomoka ghafla baada ya mvua kubwa, huku ikihofiwa kuwa watu kadhaa wamekwama chini ya vifusi.

Serikali imetuma idadi kubwa ya vikosi vya usalama, ikiwemo jeshi, kushiriki katika shughuli za uokoaji.

Akizungumza na vyombo vya habari vya ndani, mwanamke mmoja amesema watoto wake watano wamefariki katika tukio hilo.

Mamlaka zinaendelea na shughuli za uokoaji, huku zikihofia kuwa watu zaidi huenda wamefunikwa na vifusi na hivyo idadi ya vifo ikaongezeka.

Waziri Mkuu wa Guinea, Amadou Ouari Ba, ametembelea eneo la tukio na kutathmini hali ilivyo.

Awali, kiongozi wa eneo hilo, Lansine Sila, aliliambia shirika la habari la AFP kuwa kulikuwa na hofu ya idadi kubwa ya waathiriwa. Amesema hadi wakati huo miili 18 ilikuwa imepatikana na kupelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti.

dampo.png
 
Wanajengaje mlima wa taka taka na wao sasa ..mpaka unarefuka kiasi cha kuporomoka tena...Je kuwa wanayachoma?!!!!
R.I.P Wapendwa...
 
Hizo takataka hazikuwa zinawakera kwa harufu kali au ni mlima wa takataka zipi
 
Imagine huwa tunakabidhiwa miundombinu ikiwa safi kabisa tunashindwa kuisimamia yaani mtu mweusi kuna mahala hakukamilika katika uumbaji
Malezi, mambo mengi ya msingi tunapuuza, hata wale tunaotegemea kujifunza kwao nao wanafanya yasiyofaa
 
Malezi, mambo mengi ya msingi tunapuuza, hata wale tunaotegemea kujifunza kwao nao wanafanya yasiyofaa
Hebu angalia hali ilivyo sehemu tunazoita majiji kila kona kumejaa mabanda garage uchwara fremu za maduka kila kona yaani ni wasukuma huwa wana msemo wao
Bhachanganye bhajimelwe
 
Back
Top Bottom