Yusuph Makamba: Hayati Mwinyi ni hazina ya Mwenyezi Mungu kwa nchi yetu

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
15,103
22,547
Salaam, shalom!!!

Akizungumza Kwa uchungu mkubwa na majonzi alipokuwa akimuelezea HAYATI Mwinyi, amesema kuwa Mzee Mwinyi alikuwa mtu mwenye kheri, mpole na mstaarabu na muwajibikaji.

Amedai kuwa ulitokea mgogoro kati ya wakulima na wafugaji akiwa mkuu wa mkoa na katika tukio Hilo, alifariki mtu Mmoja, alipoitwa IKULU, Mzee Mwinyi alimtaka ajiuzulu Ili kuonyesha uwajibikaji.

Mzee Makamba akamwomba msamaha Rais Mwinyi na kumwambia amsamehe Kwa kuwa ana familia inayomtegemea, akanukuu maandiko yasemayo, baba hatahukumiwa Kwa dhambi alizofanya mtoto,baada ya kusema hayo, Mzee Mwinyi alitabasamu na kumwambia nimekusamehe,usirudie tena.

Amesema HAYATI Mwinyi amemfaa sana Kwa kumteua Ukuu wa wilaya, Kisha baada ya miezi SITA akamteua ukuu wa Mkoa, na baadaye Mh KIKWETE akaendelea kumwamini.

Akibubujikwa na machozi Kwa Huzuni kubwa, amesema kuwa Ili Nchi iwe salama, inahitaji kuwa mikononi mwa mtu aina ya Mzee Mwinyi, na mtu hiyo wa aina ya Mzee Mwinyi, ni Mh Samia Suluhu Hassan.

Mzee Makamba ameendelea kusema Mzee Mwinyi apumzike Kwa Amani na huko aendako awasalimu waliotangulia HAYATI Mzee Nyerere, HAYATI Mzee Mkapa na HAYATI Magufuli.

Source: Tanzania Broadcasting Corporation ( T. B. C).

Maombolezo yaendelee😪🙏
 
Salaam, shalom!!!

Akizungumza Kwa uchungu mkubwa na majonzi alipokuwa akimuelezea HAYATI Mwinyi, amesema kuwa Mzee Mwinyi alikuwa mtu mwenye kheri, mpole na mstaarabu na muwajibikaji.

E akaendelea kumwamini.

Akibubujikwa na machozi Kwa Huzuni kubwa, amesema kuwa Ili Nchi iwe salama, inahitaji kuwa mikononi mwa mtu aina ya Mzee Mwinyi, na mtu hiyo wa aina ya Mzee Mwinyi, ni Mh Samia Suluhu Hassan.

Mzee Makamba ameendelea kusema Mzee Mwinyi apumzike Kwa Amani na huko aendako awasalimu waliotangulia HAYATI Mzee Nyerere, HAYATI Mzee Mkapa na HAYATI Magufuli.

Source: Tanzania Broadcasting Corporation ( T. B. C).

Maombolezo yaendelee
MWINYI NI HAZINA YA MWENYEZI MUNGU binafsi ya MWINYI MWENYEWE na sio hazina kwa NCHI.
MUNGU alikwishailaani nchi hii kutokana na Matendo ya Kishetani yafanywayo na CCM Viongozi ni Wabinafsi wabaguzi wezi wamejilimbikizia Mali na Vyeo Wakatili
 
Sidhani kama uko Sahihi. Hapa umeandika kwa Mihemko. Ukitaka kuwa Kiongozi kuwa Mbunifu wa Ulichonacho na kuwafanya Wengine wajifunze kwako hapo tayari unakuwa Kiongozi. Kama Umeshindwa kuwaongoza Watoto wako Wamche Mungu, Umeshindwa kuwaongoza Watoto wako Wasipende vya Bure, Umeshindwa kuwatengenezea Watoto wako kesho yao njema na yenye Baraka kwa Mungu, Kutwa unaishi kwa kuangalia nani kafanikiwa zaidi ya Mwingine badala ya kujipima umefanya lipi lililokuletea Mafanikio, Kutwa kuwanenea Wengine Mabaya na kuomba laana kwa Wengine unasahau kama kuna kitu kinaitwa “Karma” kwamba unachowaombea Wengine ndicho kitakuwa sehemu ya Maisha yako, Kutwa Kuwatungia Uongo Wengine ili mradi kufurahisha nafsi yako na kukera Wengine, Kuishi kwa Kuvizia Wengine wakosee ili uwaseme badala ya kuwashauri Wasiharibu kwa Maslahi yako ya kisiasa au Kiumbea.
Nb: Mtu anayemkejeli Marehemu ni Hasara kwake Mwenyewe, Kwa Familia yake, Kwa Ukoo wake , Kwa Mtaa wake na Kwa Taifa. Usije ukadhani Machizi wote mitaani wamelogwa wengine ni Marudio ya Maombi mabaya ya Wazazi wao dhidi ya Wengine.
==¥¥ Mungu Ailaze Mahala pema Peponi Roho ya Mzee Ruksa. Amen.
Ila na Mafisadi nao Waache Wizi na hii iwe moja ya Kimuenzi Mzee wa Ruksa Maana Shekh yule alikuwa hana Ka Ufisadi rohoni mwake.

PIa: Aendelee Kukumbukwa Hayati Dr JPM
 
Back
Top Bottom