Yussuf Manji, Omba Toba

Hatimaye leo Nimejifunza kitu toka kwa Faiza
 
kama Manji alijua ile ilikua ni mali ya wakfu na halafu akanunua basi yeye na wauzaji wote ni kundi moja
 
Mkuu Bashite amehusiana nini na hili bandiko? Hebu kaa chini, soma upya tafakari utajua alichoandika Faiza.
 
Kwani kuna dini inakubali dhulma?malipo ya dhulma yapo kwa dini zote

Dini ni njia na kuna wafatao njia za kishetani, kudhulumu, kuiba, kutapeli kwao ni kawaida.

Hili la Manji ni somo kwa wote. Dhulma ni mbaya.
 
Soma vizuri post namba moja.

Lini nilikubali Ponda kuadhibiwa? Lini nilikubali Manji kuuziwa viwanja vya Waislam?

Fikiri kabla hujakurupuka.
Wewe ulikaa kimya, hukukemea Utawala uliokua ukimuadhibu, means ulikubaliana nao na walichokua wakifanya.
Mimi tumepewa namna ya kufanya tuonapo uovu. Kwamba Tuuondoe kwa Mikono yetu, tukishindwa tukemee kwa mdomo, nayo tukishindwa basi tunung'unike moyoni imgawa hii imetajwa kua ni ishara ya udhaifu.
 

Ulitaka nikujulishe wewe?

Si kila kitu cha kukemewa, kuna njia nyingi nyingine za kuambizana.

Kukemeana ni huko mnakotoana mapepo mnaojipachika wenyewe.
 
yaan;waislamu hata mkikaa wenyewe ni watu wa kulalamika mnaonewa!
[HASHTAG]#mnachoosha[/HASHTAG] sasa!
 
Uislam hauna adui, labda uwe na uadui na Waislam.
Mi sina uadui wowote na Waislam, tena nna marafiki wengi waislam kuliko hata Wakristo wenzangu, ila nnachosema ni kwamba nyinyi waislam ndo huwa kila mwaka wa uchaguzi mnawapa CCM ushindi wa kishindo halafu ndo wakwanza kuja kulalamika mnaonewa.

Sina ubaya wa nyie kuchagua CCM ila nakereka na hali yenu ya kulalamika kila siku kwamba mnaonewa angali ndo huwa mnatoa ushindi. Ina maana ni kwanini mnachagua chama halafu mnaweka kando maslahi yenu halafu baadae mnakuja kulia mnaonewa??.?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…