Yussuf Manji, Omba Toba

Yussuf Manji, Omba Toba

Yussuf Manji, ni matumaini yangu kuwa ujumbe huu utakufikia popote ulipo.

Binafsi kama Muislam mwenzako nnachukuwa fursa hii kukukumbusha kuwa hakuna kitu bora kama kukiri na kukubali makosa yako na kuomba toba.

Toba nnayokushauri kuiomba hapa, si kwa serikali wala kwa watawala. Toba nnayokukumbusha mimi kuiomba ni kwa Mola wako Muumba mbingu na ardhi.

Manji uliwakosea sana Waislam kipindi cha nyuma kiasi, kwa kutumia fedha zako kununulia viwanja vya wakf vya Waislam, na kuwa mkaidi kila uliposemeshwa kuhusu hilo.

Viwanja hivyo ambavyo historia inaonyesha kuwa vilikuwa vijengwe chuo kikuu cha kwanza Tanganyika (hilo halikufanyika lakini hilo ni simulizi jingine kabisa ambalo Alama Mohamed Said anaweza kulisimulia vizuri zaidi).

Ulifatwa na Waislam wakikuomba kuwa mkataba ulioingia na BAKWATA ni wa kidhalimu na haufai lakini kwa ukaidi wako hukuwasikiliza na uliwatoa njiani na kuendelea na mkataba wako.

Sakata la viwanja hivyo lilipelekea Waislam kufungwa, kupigwa na kujeruhiwa mpaka walipoona kuwa hawakuwezi kwa ajili ya kutumia fedha zako na nguvu ya baadhi ya waliokuwa BAKWATA, Waislam wakafikia maamuzi makali ya kuwa sasa wanakushtaki kwa Mwenyeezi Mungu.

Miaka imepita ukidhani kuwa shtaka hilo halina meno kwako, lakini leo tunashuhudia ukigeukwa kila upande.

Aibu ya kushikwa na kuwekwa ndani pekee si ndogo kwa mtu wa "caliber" yako. Licha ya kupimwa na kukutwa kuwa u mlevi wa madawa, tumeona sakata la Oysterbay likikutia hasara kubwa sana, tumeona wafanyakazi wako wakifungiwa kuingia kwenye ofisi zao, tunasikia akaunti zako zinafungiwa kila kukicha.

Kama hiyo haitoshi, tunasikia umepatwa na matatizo ya moyo. Mwenyezi Mungu anasema katika Qur'an tukufu:

Qur'an 2:10. Nyoyoni mwao mna maradhi, na Mwenyezi Mungu amewazidishia maradhi. Basi watakuwa na adhabu chungu kwa sababu ya kusema kwao uwongo. Maelezo

Kwa yote hayo bado tu hujashtuka ni kwanini yakukute yote hayo? Nakusihi, zingine zote ni sababu lakini ukweli unabaki kuwa ukweli, Waislam wameitikiwa dua zao dhidi yako.

Yussuf Manji tunakutaka usiwe katika wale ambao:

Qur'an 2:7. Mwenyezi Mungu amepiga muhuri juu ya nyoyo zao na juu ya masikio yao, na juu ya macho yao pana kifuniko. Basi watapata adhabu kubwa. Maelezo

Kwa kuwa Mwenyezi Mungu ni wingi wa kusamehe na hachoki kusamehe, tunakutaka uombe toba kwa mola wako, umtake radhi, uwatake radhi na Waislam na uwarudishie viwanja vyao na mali zao, tena usithubutu kuvirudisha kwa wale wale waliokuuzia, itakuwa haina maana kabisa. Virudishe kwenye taasisi za Kiislam zenye kumuogopa Mwenyezi Mungu au tumia viwanja hivyo hivyo kuanzisha Manji Islamic Trust Fund na uiendeshe mwenyewe kwa manufaa ya Waislam.

Fata nasaha hizo uone mambo yatavyokunyookea.

Jikumbushe:

Maimamu kumsomea Manji Ahla-badri

Mjue Sheikh Ponda Issa Ponda na Kundecha

Waislamu wataka jengo lao toka Quality Group | Bongo5.com

MKATAMBUGA: WAISLAMU WAMELOGWA NA NANI?

Manji hakuna wakukuokoa katika haya na hayatokwisha ukifanya dharau isipokuwa wewe mwenyewe, anza kwa kumrudia Allah na kumuomba toba.

Na Mwenyeezi Mungu ndiye ajuwae zaidi.
Kuna yaya huko Saudia kakatwa kichwa hadharani mbele ya POLISI wa Saudi kwa kosa la kumdondosha mtoto kwa bahati mbaya kwenye ngazi ni RAIA wa Ghana hebu fuatilia na hiyo.
 
wenyewe waliokuwa wamiliki

20140430_151443.jpg
 
Kuna yaya huko Saudia kakatwa kichwa hadharani mbele ya POLISI wa Saudi kwa kosa la kumdondosha mtoto kwa bahati mbaya kwenye ngazi ni RAIA wa Ghana hebu fuatilia na hiyo.

Anahusiana na Manji?
 
Oyster bay inahusiana na vita ya madawa ya kulevya?

Miji mingi duniani imeendelezwa na sekta binafsi..na kimsingi Manji alikuwa na mkataba na jiji alipokuja huyu Anayetaka matajiri waishi kama mashetani na gia yake eti maskini watakosa mahali la kuogelea ndo yakawa yaliyokuwa. Wakati ufukwe bado ungebaki free kwa kila mtu ila facilities nyingine ndo zingekuwa za kulipia.

Bakini na takataka yenu mnayoiita koko beach sijui ambayo ni kichaka cha wakabaji na wavuta bangi.
 
Yussuf Manji ni Muislam na aliwakosea Waislam na ni wajibu wetu kukumbushana.

Toba ni kwa yeyote.
Mimi hapa nakubaliana na wewe 99%, ila hiyo 1% iliyobaki nakupinga.
Nakupinga kwa sababu huyu Sheikh Issa Ponda issa katika harakati zake za kuwatetea Waislam ikiwemo kupigania ule uwanja pale Chamg'ombe ameshawahi kusumbuliwa, kupigwa risasi, kuwekwa ndani, kuitwa gaidi na madhara mengineyo mengi tu na waliokua wakimfanyia hayo sio wengine bali Dola na utawala uliokuwepo awamu ya nne ambayo uliitetea sana.

Siajawahi kukuona ukipinga hili kwa kua tu ulikua na mahaba yako binafsi na utawala uliopita. Lei hii unakuja kukiri kua Manji aliwaonea waislam (utawala ulipita) lakini hukuwahi kuonyesha kukerwa na hili kipindi kile tuko utawala uliopita dada yangu. Anyway, kama sasa unakubali hilo basi Mwenyezi Mungu ni Mkubwa
 
Pia tuwashauri na viongozi wa BAKWATA walioshiriki kufanya biashara na Manji kuomba toba.
BAKWATA ni an organ within CCM,
Manji nae ni Mwanachama wa CCM,
So hii ni Biashara ya ndani kwa ndani,
Wote hawa (BAKWATA, CCM & Manji) hakuna anaeona kuna shida,
Ndio maana utawala uliopita chini ya Serikali ya CCM ulimtuhumu Issa Ponda kuleta uchochezi pale alipopinga huu unyang'anyi uliobatizwa jina la uuzwaji
 
Yussuf Manji, ni matumaini yangu kuwa ujumbe huu utakufikia popote ulipo.

Binafsi kama Muislam mwenzako nnachukuwa fursa hii kukukumbusha kuwa hakuna kitu bora kama kukiri na kukubali makosa yako na kuomba toba.

Toba nnayokushauri kuiomba hapa, si kwa serikali wala kwa watawala. Toba nnayokukumbusha mimi kuiomba ni kwa Mola wako Muumba mbingu na ardhi.

Manji uliwakosea sana Waislam kipindi cha nyuma kiasi, kwa kutumia fedha zako kununulia viwanja vya wakf vya Waislam, na kuwa mkaidi kila uliposemeshwa kuhusu hilo.

Viwanja hivyo ambavyo historia inaonyesha kuwa vilikuwa vijengwe chuo kikuu cha kwanza Tanganyika (hilo halikufanyika lakini hilo ni simulizi jingine kabisa ambalo Alama Mohamed Said anaweza kulisimulia vizuri zaidi).

Ulifatwa na Waislam wakikuomba kuwa mkataba ulioingia na BAKWATA ni wa kidhalimu na haufai lakini kwa ukaidi wako hukuwasikiliza na uliwatoa njiani na kuendelea na mkataba wako.

Sakata la viwanja hivyo lilipelekea Waislam kufungwa, kupigwa na kujeruhiwa mpaka walipoona kuwa hawakuwezi kwa ajili ya kutumia fedha zako na nguvu ya baadhi ya waliokuwa BAKWATA, Waislam wakafikia maamuzi makali ya kuwa sasa wanakushtaki kwa Mwenyeezi Mungu.

Miaka imepita ukidhani kuwa shtaka hilo halina meno kwako, lakini leo tunashuhudia ukigeukwa kila upande.

Aibu ya kushikwa na kuwekwa ndani pekee si ndogo kwa mtu wa "caliber" yako. Licha ya kupimwa na kukutwa kuwa u mlevi wa madawa, tumeona sakata la Oysterbay likikutia hasara kubwa sana, tumeona wafanyakazi wako wakifungiwa kuingia kwenye ofisi zao, tunasikia akaunti zako zinafungiwa kila kukicha.

Kama hiyo haitoshi, tunasikia umepatwa na matatizo ya moyo. Mwenyezi Mungu anasema katika Qur'an tukufu:

Qur'an 2:10. Nyoyoni mwao mna maradhi, na Mwenyezi Mungu amewazidishia maradhi. Basi watakuwa na adhabu chungu kwa sababu ya kusema kwao uwongo. Maelezo

Kwa yote hayo bado tu hujashtuka ni kwanini yakukute yote hayo? Nakusihi, zingine zote ni sababu lakini ukweli unabaki kuwa ukweli, Waislam wameitikiwa dua zao dhidi yako.

Yussuf Manji tunakutaka usiwe katika wale ambao:

Qur'an 2:7. Mwenyezi Mungu amepiga muhuri juu ya nyoyo zao na juu ya masikio yao, na juu ya macho yao pana kifuniko. Basi watapata adhabu kubwa. Maelezo

Kwa kuwa Mwenyezi Mungu ni wingi wa kusamehe na hachoki kusamehe, tunakutaka uombe toba kwa mola wako, umtake radhi, uwatake radhi na Waislam na uwarudishie viwanja vyao na mali zao, tena usithubutu kuvirudisha kwa wale wale waliokuuzia, itakuwa haina maana kabisa. Virudishe kwenye taasisi za Kiislam zenye kumuogopa Mwenyezi Mungu au tumia viwanja hivyo hivyo kuanzisha Manji Islamic Trust Fund na uiendeshe mwenyewe kwa manufaa ya Waislam.

Fata nasaha hizo uone mambo yatavyokunyookea.

Jikumbushe:

Maimamu kumsomea Manji Ahla-badri

Mjue Sheikh Ponda Issa Ponda na Kundecha

Waislamu wataka jengo lao toka Quality Group | Bongo5.com

MKATAMBUGA: WAISLAMU WAMELOGWA NA NANI?

Manji hakuna wakukuokoa katika haya na hayatokwisha ukifanya dharau isipokuwa wewe mwenyewe, anza kwa kumrudia Allah na kumuomba toba.

Na Mwenyeezi Mungu ndiye ajuwae zaidi.
Migogoro yenu ya kidini msituletee hapa,malizaneni wenyewe
 
Kumbe huyu tajiri anahusika kwa kiasi kikubwa na mkasa huu.Kweli itakuwa adhabu yake hapa duniani ndio kwanza ina anza.Toba kwake ndio kimbilio sahihi na atimize masharti ya hiyo toba yake.
 
Amezungumza kwa uwazi masuala yanayowahusu Waislamu na haki zao, na amemshauri Muislam mwenzake alie kwenye matatizo namna ya kufanya sasa sijui wewe unawashwa na nini. Kama ni unafiki basi wewe ndie mnafiki mkubwa kwakuwa husemi ukweli juu ya maradhi yaliyo moyoni mwako, kefule!
Togora mwenehu
 
Ushauri mzuri sana....Toba ndio njia pekee....watu wengi wanaidhulumu Tanzania kwa vigezo vya kufanya biashara...aombe toba pia kwa yote aliyofanya kuwakandamiza wanyonge wa Tanzania
 
Manji hakuna wakukuokoa katika haya na hayatokwisha ukifanya dharau isipokuwa wewe mwenyewe, anza kwa kumrudia Allah na kumuomba toba.

Ishara zipi zinazoonekana kwa macho ya binadamu zinaonesha mhusika ameomba toba kwa Allah, na Allah ametoa msamaha? Hiyo toba inafanyikaje?

Na Mwenyeezi Mungu ndiye ajuwae zaidi.

Kama Allah ndio anajua zaidi kwa nini usimwachie jambo hili Allah?
 
Mawazo mazuri saana FF ila now it is a little too late. Weshamsomea ile kitu mbaya na sasa imeshaanza kutenda kazi. Nafuu ungekuwa upupu tungesema huo ni muwasho tu. Albadir ikishaanza kutenda kazi hakuna dua nyengine tena ya kumwokoa hapo.
Aksante kwa kutufahamisha kuwa kumbe Manji si Makonda kammaliza bali maovu yake alowafanyia hiana waislam. Poleni jamani ila, imani yetu inatufunza kuwa, hatuna hitaji la kupokea najisi. Iliibwa na viongozi ambao wengine weshatangulia mbele za haki. Mwache alilichumia janga lake, asitushirikishe kwani aliowanyima hiyo haki weshazoea kutokukumbuka. Na awe funzo kwa wale wapenda dhuluma. Aksante
 
InshaAllah kama akiupata ujumbe huu basi afanye toubatan nasuuha asa kheri Allah ni msamehevu wa maovu yote kwa yule anaetubia
 
Back
Top Bottom