Yupo wapi Makongoro Nyerere kada wa CCM?

Yupo wapi Makongoro Nyerere kada wa CCM?

mwembemdogo

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2016
Posts
2,282
Reaction score
1,253
Nimeshtushwa Na ukimya wa Kada maarufu wa CCM aliyeipigania CCM Kwa nguvu zake zote mpaka akadiriki kukufuru Kwa kuwabeza Na kuwatukana matusi wanasiasi wenzake akiwemo Mzee Steven Wassira aliyeshindwa ubunge Na Binti Bulaya kama haitoshi akamtukana Kamanda Mzee Lowassa.

Tunaomba ajitokeze huko mafichoni azungumzie hata haya MAJIPU yanayotumbuliwa au kachukia ule mchujo wa kumpata mgombea wa CCM ulioendeshwa Kule Dodoma?
 
Nimeshtushwa Na ukimya wa Kada maarufu wa CCM aliyeipigania CCM Kwa nguvu zake zote mpaka akadiriki kukufuru Kwa kuwabeza Na kuwatukana matusi wanasiasi wenzake akiwemo Mzee Steven Wassira aliyeshindwa ubunge Na Binti Ulaya kama haitoshi akamtukana Kamanda Mzee Lowassa.Tunaomba ajitokeze huko mafichoni azungumzie hata haya MAJIPU yanayotumbuliwa au kachukia ule mchujo wa kumpata mgombea wa CCM ulioendeshwa Kule Dodoma?
Makongoro anadai kadhulumiwa na Kikwete kwenye kupitisha majina. Anasema wagombea watano waliochaguliwa ni 1. Augustine Mahiga 2. Augustine Ramadhani 3. Makongoro Nyerere 4. Mizengo Pinda na 5. Asha Rose Migiro. Lakini Kikwete akaja na listi yake ya mfukoni na kuwaacha solemba. cc. Andrew Nyerere
 
Hii ID nadhani ni fake au inaingiliwa,sina hakika kama Andrew,the jet fighter pilot kuandika hivi dhidi ya nduguye,lazima kuna jambo....ila naskia Serikalia hii haiwataki Nyerere 's kwa kuogopa kkufunikwa na kukosolewa hadharani ndo maana woote wamepigwa kimya na ni ka mkakati...japo sina hakika ila Kwa kuwa Mokongoro nae hupitagga humu atatuambia kama ni kweli au ni blah blah
 
Siku nyingine kama huna uhakika wa jambo ni vyema tu ukauchuna kuliko kukurupuka kwani utazidi kudharaulika. Kwa kukusaidia tu ni kwamba THINK TANKS wa Rais wako sasa ni wale wazee mahiri waliokuwa wasaidizi wa karibu wa Mwalimu Nyerere ( siwezi kuwataja majina kwa umuhimu na unyeti wao ) na wakisaidiana na Kiongozi wako mmoja mstaafu na baadhi ya watu aliokuwa nao. Hakuna mtu ambaye Rais wako haipiti siku lazima amjulie hali au hata aombe kuonana nae kama Mama Maria Nyerere na Rais wako anamuheshimu huyu Mama kama ambavyo anamuheshimu Mama yake na hata ushauri pia huomba kutoka kwake kisha unafanyiwa kazi na Wataalam. Kuna mengine ngoja niyamezee tu mate kwani yamekaa KIITIFAKI zaidi na jamaa karudi jana tu kutoka huku kwetu Kigali. Huyo Makongoro kuna kazi MAALUM na yeye atapewa na ukimya wake ni wa KIMKAKATI zaidi kutoka " eagle wing house ". Naomba niishie hapa niwahi zangu sasa kumshangilia Mwarabu leo taifa!
 
Huyu alitumika kama chid benz kutukana wakubwa kuliko yeye kiumri. Chid kaanza kupata malipo naye asubiri wakati wake unless akatubu
 
Al
Nimeshtushwa Na ukimya wa Kada maarufu wa CCM aliyeipigania CCM Kwa nguvu zake zote mpaka akadiriki kukufuru Kwa kuwabeza Na kuwatukana matusi wanasiasi wenzake akiwemo Mzee Steven Wassira aliyeshindwa ubunge Na Binti Bulaya kama haitoshi akamtukana Kamanda Mzee Lowassa.

Tunaomba ajitokeze huko mafichoni azungumzie hata haya MAJIPU yanayotumbuliwa au kachukia ule mchujo wa kumpata mgombea wa CCM ulioendeshwa Kule Dodoma?
Alifikiri siasa ni porojo za kitotokitoto, kasigezwa pembeni!
 
Back
Top Bottom