Bernard Membe: Kuna umuhimu wa kufanya vetting kwa viongozi wetu kuhusu uraia na afya zao

tang'ana

JF-Expert Member
Apr 3, 2015
11,793
14,808
Mwanasiasa Bernard Membe anasema kuna umuhimu kwa viongozi wote kufanyiwa uchunguzi wa kina ili kujua historia na taarifa zao kwa kuwa baadhi yao si Watanzania.

Huu ni mfululizo wa habari zinazotokana na mahojiano maalumu ya Membe na Gazeti la JAMHURI yaliyofanyika nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam, hivi karibuni.

Toleo lililopita waziri huyo wa zamani wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa alieleza namna Rais John Magufuli alivyomfitini hadi akakosa Ukatibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola.

Membe anasema faida mojawapo aliyoipata baada ya kufukuzwa CCM mwaka jana ni kuwajua watu ambao si raia wa Tanzania, lakini wameshika nafasi kubwa za kisiasa.

“Ukiwa nje ya CCM unajua, ila ukiwa ndani huwezi kujua. Kule upinzani unaambiwa kabisa kuwa huyu amezaliwa mahala fulani, na si Mtanzania na ukiangalia anachokifanya na tabia zake mbona zinalingana na za mtu wa nchi jirani,” anasema na kuongeza.

Hao watu wamo ndani ya serikali na CCM pia wamo, na niko tayari kuthibitisha hilo. Unajua tuna mfumo hapa kwamba hebu fanyeni vetting kwa huyu na kwa huyu na mafunzo tuliyoyapata ni lazima ukitoka nje kuna vitu unaviona kwamba vetting lazima ikamilike, wakati ule Serikali ya Awamu ya Nne, serikali ilikuwa makini mno katika vetting.

“Ninachozungumza hapa ni mwenendo wa baadhi ya viongozi na si mwenendo wa vyombo vya ulinzi na usalama, kwa sababu tukiwa kule upinzani hakuna siri.

“Unaambiwa kiongozi huyu anabaka ofisini. Naomba nieleweke kwamba ninazungumzia baadhi ya viongozi na si vyombo vya ulinzi na usalama, lakini hadi mtu anashitaki fulani amenifanya hivi au vile ili nipate kitu fulani, na kuna vitu vinajulikana vya wazi kabisa.”

Membe ambaye amekuwa mbunge wa Jimbo la Mtama kuanzia mwaka 2000 hadi mwaka 2015, anasema siasa ni ‘uchawi’ na ukiwa CCM unakuwa kama umerogwa.

“Siasa ni uchawi. Kwanza, CCM ndio mwili wako hata kama umevunjika au michibuko mingi, ni kama ilivyo roho na mwili wako. CCM ambayo nimeitumikia tangu mwaka 1977 rasmi, unazungumzia karibu miaka 41,” anasema na kuongeza:

Unapokuwa ndani ya CCM, wewe unakuwa CCM na CCM inakuwa wewe – na CCM ni uchawi, kwa sababu hauoni ubaya wake hadi utoke mle katika angle ndiyo unakiangalia ili ukione kilivyo muhimu, ukione kikiwa na tatizo na ili ukiingia tena uingilie upande gani.

“Kwa hiyo ninapozungumzia siasa ni uchawi ni kwamba ukiwa katika chama muda mrefu umeshajiroga na unaona kiko sawasawa kabisa, na kama ninavyosema kimenilea, kimenitunza na nilikuwa ninakwenda vizuri sana, sikuondoka katika chama kwa kupenda. Nilifukuzwa, nilisikitika sana.

Kwa sababu kama nilivyosema, hakuna chama kitakatifu, kwa kuwa kila chama kina dosari zake, lakini siasa ni uchawi, unapokuwa mle ndani unaishi vizuri na hakuna wa ‘kukuroga’, na tuliishi vizuri sana.”

Anasema amejifunza mambo mawili kutoka CCM; la kwanza ni kwamba ni lazima chama hicho kiwe na uongozi wa Kitanzania na kiongozwe na Watanzania wenyewe; na pili, ni vema kikaongozwa na wana CCM wenye historia nacho.

“Kwa mfano, ukisikia fulani ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM ni lazima msikilizaji aambiwe historia yake katika CCM, na si ahame chama fulani na apewe madaraka. Hilo ni jambo ambalo wananchi lazima tuliingilie. Lazima tupate watu wenye historia katika chama hicho, wanaokielewa chama hicho, ni hatari kuchukua watu ambao hawakijui chama. Huo ndiyo uzoefu wangu mfupi katika upande wa chama.”

Kwa upande wa serikali, anasema alipokaa nje akaanza kugundua kumbe ni vizuri viongozi wakafanyiwa uchunguzi wa kina uliokamilika na kuwajua wanapotoka na afya zao.

Ukikaa nje hili jambo unaliona kama mwezi unapouona ukiwa angani. Tusipoangalia unaweza ukajikuta una kiongozi hana damu ya u-Tanzania, na ninakwambia hivi, lazima sifa hiyo iwepo na isije kusemwa mimi ni mbaguzi, hapana, lazima iwepo, kwa sababu suala la uongozi ni la Watanzania, ndiyo maana tunasema ni uzalendo. Unajiuliza, tabia hii ni ya Watanzania kweli? Tangu lini mwandishi wa habari anatoweka?

“Sisi tulikuwa tunasoma katika vitabu nchi zilizopigana wenyewe kwa wenyewe ndiyo unaambiwa kuna waandishi wametoweka, watu hawawezi kuzungumza kule. Watanzania wanatumwa kwenda kutatua matatizo na si wao kuja kutatua matatizo yetu.

“Jamani kimetokea nini kwa watu hawa waliopotea? Tumekwenda Zimbabwe baada ya Morgan Tsvangirai kupigwa karibu jicho litoke, tumekwenda kumuuliza Rais Robert Mugabe kimetokea nini dunia nzima inakulalamikia jinsi unavyowafanya wapinzani wako.
Mzee Mugabe akasema ‘Morgan alikuwa anatoka zake shambani akaja kulikuwa na maandamano, basi askari wangu mmoja akachukua rungu akampiga jichoni na akapandishwa cheo kuwa sajenti alikuwa koplo’.

“Sikia, ule si u-Tanzania. Ukiona jambo kama hilo limekuja unaanza kujiuliza huu u-Tanzania kweli? Ndilo somo la kwanza kubwa nililojifunza. Lakini la pili ni vetting ya viongozi.

“Tusipofanya vetting ya viongozi kiafya tunaweza kuwa na watu wa magonjwa ya akili. Sikufichi, katika kipindi hiki nilipoona kiongozi aliyepewa dhamana yuko ofisini kwake anawasha muziki anacheza peke yake na kujirekodi, halafu mnamuangalia mtajua kuna tatizo. Ukiona kiongozi amefikia hatua hiyo, ujue kuna tatizo na hatujafanya vetting vizuri,” anasema Membe.
Kwanini alijiunga ACT-Wazalendo?

Membe anasema dalili zilipojionyesha kwamba kuna kikao cha Kamati ya Maadili ya CCM, wakaitwa makada watatu; yeye na makatibu wakuu wa zamani, Abdulrahman Kinana, na Yusuph Makamba.

“Ikaamriwa hivyo kwamba sisi watatu tuitwe katika ile kamati. Mimi, Kinana na Mzee Makamba. Ulikuwa mkutano wa NEC wa Desemba 2019, kwamba sisi lazima tuitwe kwa sababu ya matatizo ya nidhamu, nikashukuru.

“Lakini kwa wakati huo tulidukuliwa, mimi nilikuwa ninaongea na mtu wangu mmoja wa nyumbani kumweleza kwamba kuna mpasuko ndani ya CCM. Kwa hiyo Kamati ya Maadili ikaitwa ilikuwa Machi, mwaka jana, nikaenda mimi peke yangu, Mzee Makamba alikataa na Kinana alikataa na nikawaambia rasmi kabla sijaenda kwamba ninakuja.

Kule nikamkuta Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili, Philip Mangula, Dk. Bashiru Ally (wakati huo akiwa Katibu Mkuu wa CCM), Makongoro Nyerere akiwa ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, mjumbe kutoka Zanzibar, ofisa mmoja kutoka katika chama na ofisa mwingine wa taasisi nyeti aliyepo katika chama – kulikuwa na maofisa kama watano hivi waliokuwa wananisubiri kunihoji.”

Anasema aliwaeleza bayana kwamba kuna kesi imefunguliwa Mahakama Kuu na hawawezi kujadili, kwa kuwa kuna mambo mengine yako mahakamani.

“Ni common sense tu. Pale tukajadili mambo yasiyokuwapo mahakamani, na wanasheria wangu walishaniambia kwamba haya yasijadiliwe, yanaweza kujadiliwa mengine, kwa sababu tutaingilia uhuru wa mahakama. Tukakubaliana na jambo tulilozungumzia siku hiyo pale ni udukuzi.

Suala la udukuzi lilipofika, Mangula akasema tulisoma hapa katika magazeti kwamba katika kudukuliwa uliongea kwamba chama kina mpasuko. Nikamwambia mwenyekiti subiri, suala la kudukuliwa limo ndani ya Katiba, kwa hiyo twende taratibu.

“Usisome kwanza mimi nilichodukuliwa, twende katika udukuzi, kwa sababu udukuzi ni kosa la jinai. Kwa kuwa mmelileta hili, kwanza tuanze na nani alinidukua? Nina kesi ya jinai dhidi yake na Katiba inasema Mtanzania yeyote anayo haki ya faragha na hatakiwi kuingiliwa katika hiyo faragha na kufanya hivyo ni kosa. Iliwachukua nusu saa pale na kila mmoja anaulizwa anakataa, nikiwauliza hao maofisa wanakataa, kwa sababu kuna kosa pale limefanywa.

“Kwa muda wa nusu saa tukawa tunamtafuta mtu aliyenidukua – hayupo, taasisi nyingine zikataa, Chama kikakataa, Serikali ikakataa, lakini nikawaambia sikilizeni, aliyenidukua ninamjua, mashine ya kudukulia ninapajua ilipotoka, mashine iko wapi ninapafahamu na watu waliohusika na udukuzi huu ninawafahamu, kwa hiyo hapa tunafichana tu kiutu uzima.

Kwa muda wa nusu saa tukawa tunamtafuta mtu aliyenidukua – hayupo, taasisi nyingine zikataa, Chama kikakataa, Serikali ikakataa, lakini nikawaambia sikilizeni, aliyenidukua ninamjua, mashine ya kudukulia ninapajua ilipotoka, mashine iko wapi ninapafahamu na watu waliohusika na udukuzi huu ninawafahamu, kwa hiyo hapa tunafichana tu kiutu uzima.

“Nikamwambia mwenyekiti (Mangula) sasa twende katika context, hili nitalishughulikia mwenyewe na hao wakaanza kunihoji katika kudukuliwa,” anasema.

Membe aliulizwa kama anaunga mkono taarifa iliyoandikwa na Kinana na Mzee Makamba iliyopelekwa katika chama.

Anasema akawaambia kuwa maudhui yanafanana na yake aliyoyapeleka Mahakama Kuu na aliyekuwa akijiita mwanaharakati huru Cyprian Musiba ni…, anawavunjia heshima wastaafu na kuwatukana, anazua uongo wa jinai dhidi ya hao wazee na kwa kuwa wameandika yeye akaamua kupeleka mahakamani na wao wamepeleka katika chama.

“Nikasema siwezi kukataa, nimeisoma hiyo document ya kina Kinana, walichokiandika ninakijua, ninakiunga mkono na hakuna mwenye ubavu wa kukikataa, Bashiru akajibu hapana, kwanini hawakumwandikia yeye, kwanini wamepeleka kwa wazee, nikamwambia kesi inakuhusu wewe kwanini wakuletee wewe?”

Membe anasema hajawahi kuvutana na Bashiru hata siku moja na alikuwa hamjui, lakini ghafla tu akalipuka kwa kusema anapitapita mikoani kufanya kampeni.

Baada ya kikao hicho akawaaga kwamba amepata habari kutoka kwa vyanzo vya Bashiru kwamba yeye na Kinana wanafukuzwa CCM na Mzee Makamba anasamehewa.

Of course that was original plan, lakini kamati yote ya maadili ikakataa kwamba hilo haliwezekani na haiwezi kutokea. Nikasubiri matokeo ya kamati na nikajua yatakuwa na favor kwangu, lakini CC (Kamati Kuu ya CCM) ikaitishwa ghafla (chini ya Mwenyekiti Magufuli) ikatangaza mimi nimefukuzwa na hiyo ni kinyume kabisa cha utaratibu wa chama na vikao vya chama, nikasema alaah! Kumbe yote haya yanayofanywa lengo lilikuwa nifukuzwe,” anasema.

Membe anasema yeye ni mwanasiasa na akaona akikaa kimya Magufuli, Bashiru na Humphrey Polepole (wakati huo alikuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM) wataona anawaogopa ndipo akajiunga upinzani katika Chama cha ACT-Wazalendo.

“Nilijiunga upinzani nipate platform ya kusema kilichomo moyoni mwangu na nilifanikiwa sana, na uliona sikufanya kampeni, nilipata platform tano tu,” anasema.
Safari ya kurudi CCM

Anasema baada ya kutangaza anajiondoa ACT-Wazalendo, watu mbalimbali na makundi mbalimbali wakampigia simu na wakatuma ujumbe wa kumtaka arejee CCM.

Pia anasema viongozi wastaafu wawili wakubwa (majina yanahifadhiwa) wakapeleka ujumbe nyumbani kwake, wajumbe wawili wa CC ya CCM (majina yanahifadhiwa) wakampigia simu kumuomba arudi, viongozi wa dini zote mbili (majina yanahifadhiwa); Wakatoliki na Waislamu (Bara na Visiwani), wakamuomba arudi na baadhi ya wanachama wa CCM wa mikoa ya Lindi na Mtwara wakamueleza kwa maandishi kwamba uamuzi wake ni uamuzi wao na akiamua kurudi nao watarudi katika chama hicho.

“Ujumbe wa watu wote hao wakasema nikiamua kukaa kimya nao watakaa kimya, kwa hiyo niliwaweka katika njia panda kubwa mno, wote hao niliwaeleza ningelipenda sana kurudi CCM kwa sababu ndiko nilikozaliwa.

Mimi niljiunga TANU mwaka 1975, baada ya miaka miwili ndipo nikajiunga CCM nikiwa na miaka 23 tu, kwa hiyo hata kama CCM ni mbaya au si mbaya, mimi ni mwana CCM wa kuzaliwa.

“Kwa hiyo wala nisingehitaji sana nguvu kubwa ya wakubwa kuniomba nirudi CCM, isipokuwa nilikuwa na tatizo la uongozi wa chama, kwa maana ya Mwenyekiti, Katibu Mkuu na Katibu wa Itikadi na Uenezi ambao waliungana na Musiba kunihujumu mimi kwa ushahidi na wala sina tatizo lolote.

“Kilichoniondoa CCM si chama. Hakuna chama kitakatifu, wewe huwezi kuhama chama hiki kwa sababu si kitakatifu, unatafuta chama kitakatifu, lakini kuna viongozi wabaya wanaoweza kukuzima usifanye jambo lolote lile, na usisikike kwa jambo lolote lile,” anasema.

Anakumbuka mjumbe wa CC aliyempigia simu na kumwambia anamuomba amtume aende kwa Magufuli akalimalize suala hilo, lakini akakataa kwa kumjibu kuwa wakiondoka yeye atarudi.

Akacheka, nikacheka kisha tukakaa kimya. Hiyo ni Januari, mwaka huu nilipoacha na mabadiliko yakaja Machi, mwaka huu kwa mapenzi ya Mungu. Yakatokea mabadiliko ya uongozi wa nchi, ghafla na viongozi wote wakuu wa chama hawapo kwa maana kwa nafasi zao.

“Nikaanza kupokea maombi tena na delegations mbalimbali, rudi, rudi, rudi CCM lakini nikasema hivi ninarudije, kwa sababu mimi nilifungiwa mlango, labda niseme niko njiani nifungulieni mlango. Sasa hivi tunapoishi ukiwa mahala saa 5 usiku unapiga simu nyumbani nifungulieni mlango, waandae geti uingie, ni common sense, kwa sababu mlango ulifungwa.”

Membe anasema: “…Kiongozi mmoja wa Zanzibar aliniita niende kumzika Maalim Seif Sharif Hamad, nikamwambia sitaweza. Aliniomba pia niende nikazike Chato, nikamwambia sitaweza, nikamwambia hapana, nafsi yangu inakataa, sioni aibu, lakini sitaki kuwa mnafiki. Ni jambo la kawaida tu, hata kwangu asingefika, hata kama ningekufa mimi kila mtu angeshangaa kwamba huyu anakwenda kumzika Membe?

Kama huziki, kama unamchukia huyu eti umemchukia fulani miaka sita halafu unakwenda kumzika, unamdanganya nani? Hao ndio ambao pamoja na wengine wote waliniumiza sana, mjumbe wa CC yule mara baada ya kuona mwangwi ule, alinipigia simu akaniambia ninaomba utekeleze ahadi yako.

“Nilikushawishi ufanye moja, mbili, tatu ukaniambia tusubiri watoke, lakini mimi nikacheka tu Mungu akaingilia kati, sasa ninaomba unipe tarehe ya kurudi. Nikamwambia lakini siwezi kukupa tarehe, kwa sababu mlango umefungwa, akasema ni kweli lakini mbona huu mlango ukiusukuma tu unafunguka? Nikamwambia nikifanya hivyo wataniambia mimi ni mwizi,” anasema.

Membe anasema ametoa kauli ya kuyapa matumaini makundi hayo yaliyomuomba kwamba atarudi CCM kwa sababu alikokwenda hakukumpendeza.

Anasema makundi yote hayo yaliyomuomba akayaeleza kuwa amepeleka kesi Mahakama Kuu inayohusu mrundikano wa mambo ya hatari aliyosingiziwa kuyafanya katika taifa hili, ni vizuri uamuzi aufanye baada ya hukumu.

Wote hao waliafiki kwa sababu unarudije muuaji wewe katika chama, mhujumu mkubwa wa uongozi utaeleza nini? Lazima uende ukiwa umesafishwa, jamani mimi ni mweupe kama mchele na waliokuwa wanasababisha yote haya hawana nguvu ama hawapo.

“Kwa hiyo nikaomba kesi hii vyovyote itakavyoamriwa itoke kwanza hukumu ya Mahakama na kama nitaonekana nimekosa, basi niombe radhi, sitapata shida kuomba radhi. Kama Mahakama itanisafisha sitaona aibu kurudi nyumbani na kusema jamani niliondoka nilirundikiwa mzigo huu, Mahakama imepitia hakuna kitu hapa, mimi nilijua hakuna kitu lakini nilitaka kuiambia dunia kwamba hakuna kitu ili nisiwe na dosari yoyote katika chama, tukakubaliana hivyo, hayawi hayawi sasa yamekuwa.”

Nini kinafuata? Membe anasema ataitaarifu rasmi CCM juu ya hukumu ya kesi yake iliyotolewa na Mahakama Kuu dhidi ya Musiba na atasubiri mwongozo na atafanya hivyo mapema iwezekanavyo na kikubwa alichokifanya kwanza ni kusafisha jina lake.
Kizazi cha uongozi

Katika hatua nyingine, anasema kizazi cha sasa ndani ya CCM ni cha uongozi na haiwezekani kikarukwa na wakachukuliwa watu wa kizazi chake au watu wa nje.

“Hiki ni kizazi chenu na kila kizazi kina kada ya uongozi, nikifanikiwa kurudi ndani ya CCM lazima twende kwa kizazi hata tulipokuwa sisi kwa mfano miaka 30, 35, 40, 45 au 50 hicho ndicho kizazi cha uongozi, msikiruke hiki.

“Niliuliza swali katika Kamati ya Maadili kwanini mnawaacha vijana waliokwenda kukipambania chama wanarudi mnawaacha pembeni na mnawachukua vijana wengine kutoka nje? Hamuoni kwamba mnaleta sokomoko? Nikamuuliza Bashiru, akanijibu ukiangalia hawa vijana huyu ni kundi la Membe, huyu kundi la Kikwete, huyu kundi la Kinana, huyu la Makamba, Wassira, sasa wote hawa wana makundi ndiyo maana tunaamua kwenda nje kuchagua wengine waingie huku.

Kwa hiyo hao mnaowachukua huko kuja humu hao hawana makundi? Mtatiro hana kundi, na ukimleta huku hatakuwa katika kundi lako, ni ujinga gani huu tunaufanya kwa sababu CCM kama vyama vyovyote vile duniani ni ushindani wa ndani kwanza.

“Sasa unapojenga ushindani katika nafasi mbalimbali za uchaguzi ndani ya chama si ndiyo unatengeneza makundi, lazima watu wamshabikie huyu na huyu, kuna ubaya gani? Viongozi wote mnarudi mnakuwa kitu kimoja. Ukisikia kuna makundi maana yake kuna demokrasia na baada ya hapo mnarudi kuwa kitu kimoja, kwa hiyo yeye alitaka vijana wawe kama uyoga vile hakuna anayempenda fulani na fulani,” anabainisha

Membe anahoji, kwanini kuna woga wa ushindani ndani ya CCM? Anasema wakishasema demokrasia ndani ya chama maana yake kuna ushindani na ushindani wowote ule maana yake kuna makundi.

Anasema CCM ina wahafidhina na watu vuguvugu na anahoji, je, hao hawatakiwi?

“Kwani sisi ni Wachina kwamba tunazaliwa siku moja katika incubator, kwamba siku moja tunapewa maziwa na tunafanana akili, haliwezekani hilo. Yaani moja kati ya vitu tutakavyovifanya tukirudi CCM ni kuhakikisha vijana waliokifia chama chao cha CCM na kukipambania tusiwakatishe tamaa.

“Tuwape fursa za uongozi kwa sababu fursa ya nchi hii imo mikononi mwao, na haya mambo yataua zaidi vijana kama unaleta damu mpya ndani ya chama ambao hawana historia yoyote na chama,” anasema.

Anawataja waliokuwa viongozi wakuu wawili wa CCM, na mmoja ambaye bado yumo kwenye madaraka kwamba hawakuwahi kuwa wana CCM.

Anasema kunapokuwa na kundi la viongozi ambao si wana CCM usitarajie likawa linawafundisha na kuwaandaa vijana ndani ya chama hicho.

“Na tusipofanya hivyo CCM itakuwa katika hatari na mazingira mabaya mno, tulikuwa na vyama zaidi ya 50 vya ukombozi Afrika, 48 vyote vimeondoka vimebaki sita tu vya Namibia, Angola, Tanzania, Afrika Kusini, Zimbabwe na Msumbiji,” anasema Membe.

Kwa mengine mengi, yakiwamo ya uhusiano wake na Edward Lowassa, Rostam Aziz, suala la mgombea binafsi, Katiba mpya na utawala wa Jakaya Kikwete usikose toleo lijalo.

Chanzo: Gazeti la jamhuri la November 9,2021.
 
denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
15,054
55,063
Hapo Membe anakiri kuwa CCM ni sawa na kuwa jalalani, hawajui kitu, kama chama tawala kinachounda serikali chenye kupokea kila aina ya taarifa za nje na ndani kuhusu nchi yetu na mipaka yake lakini bado kuna taarifa za watu chamani kwao huwa hawazijui!

Membe anakiri ukiwa CCM hakuna kitu unajua mpaka utoke nje uende upinzani, sasa hao mabalozi tulionao nje, na vyombo vya usalama hapa ndani vina kazi gani? au ndio kubambikia wapinzani (Chadema) kesi tu?

- Usalama wa watanzania uko wapi kama hali yenyewe ndio hii?

Membe japo amejitahidi kutovihusisha vyombo vya ulinzi na usalama kwenye lalamiko lake naona anajidanganya tu, zaidi, anaonesha jinsi "vetting" kwenye chama chao ilivyo mbovu au haifanyiki kabisa, na pia, anazidi kumkaanga rafiki yake wa Msoga bila kujua kwa kumwambia kwamba lile chaguo alilowapa watanzania halikuwa sahihi, maana yake alikurupuka.

Habari ya kuzikana au kutozikana naona anaenda mbali mno, anamsema Magufuli kama vile alikuwa ndani ya nafsi yake na akaiona mpaka siku ya kufa kwake Magufuli asingefika msibani, kama haya ndio mawazo ya Membe vipi wale wazee wengine naamini nao watakuwa na mawazo kama haya ndio maana walionesha kupata nafuu ya nafsi kwa tweets zao baada ya msiba wa Magufuli.

Kumbe Kikwete alivyoenda msibani kwa Magufuli na akatoa ile speech ya kukataa kwamba alikuwa na tatizo na Magufuli itakuwa aliwakwaza baadhi ya watu wake wa karibu ila wakanyamaza, hizi hasira zote za Membe ni kwasababu alikosa nafasi ya Katibu Mkuu wa Jumuia ya madola, huyu mzee alikuwa na malengo gani na hicho cheo? uzalendo? nop, rekodi zake zinakataa, au ni zile pesa za hiyo nafasi??

Membe hii hasira aliyonayo moyoni bora atubu mapema, kumuwekea mtu kinyongo ambaye alishafariki na hajui kama marehemu alipata muda wa kumkumbuka muumba wake kabla hajakata roho naona anajipotezea muda, vyeo vya hii dunia vyote vinapita, na hakuna asiye na kosa, hata Membe wapo aliowakosea, asamehe na asahau.
 
Toxic Concotion

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
4,815
15,627
Wazungu wana msemo wao "learn to quit while you are still ahead". Huyu mzee anahisi kushinda dhidi ya Musiba ndio amekuwa immuned kutokana na makali ya waliopo madarakani sasa. Watamchenjia kibao yeye mwenyewe aonekane ni msomali na wamfilisi kila alichonacho.
Kwa umri wake angeufyata achunge bata asubiri mauti tu.
 
Mpinzire

JF-Expert Member
Jan 18, 2013
6,066
10,745
Awamu ya nne ingekua makini katika Vetting Magufuli na Dk. Mpango wasingefika walipofika...

Afterall Tanzania ni kama marekani tu ni ardhi ya wahamiaji.
Natamani nijue nani aliiharibu CCM kati ya Jakaya na Magufuli, tukipinganisha CCM ya Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Jakaya na Magufuli tukasema tuziweke kwenye mpangilio CCM hipi ilikuwa imara na hipi ilikuwa mbovu kupindukia!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
29,781
34,350
“Nilijiunga upinzani nipate platform ya kusema kilichomo moyoni mwangu na nilifanikiwa sana, na uliona sikufanya kampeni, nilipata platform tano tu,” anasema.
Safari ya kurudi CCM
mzee si useme ukweli tu, ulivyotoka dubai pale airport na msaidizi wako unafikiri sisi hatukujua kilichotokea ? hadi ikakufanya ukashindwa kufanya kampeni hata moja.
 
babu M

JF-Expert Member
Mar 4, 2010
5,225
3,160
DAR ES SALAAM

NA DENNIS LUAMBANO

Mwanasiasa Bernard Membe anasema kuna umuhimu kwa viongozi wote kufanyiwa uchunguzi wa kina ili kujua historia na taarifa zao kwa kuwa baadhi yao si Watanzania.

Huu ni mfululizo wa habari zinazotokana na mahojiano maalumu ya Membe na Gazeti la JAMHURI yaliyofanyika nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam, hivi karibuni.

Toleo lililopita waziri huyo wa zamani wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa alieleza namna Rais John Magufuli alivyomfitini hadi akakosa Ukatibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola.

Membe anasema faida mojawapo aliyoipata baada ya kufukuzwa CCM mwaka jana ni kuwajua watu ambao si raia wa Tanzania, lakini wameshika nafasi kubwa za kisiasa.

“Ukiwa nje ya CCM unajua, ila ukiwa ndani huwezi kujua. Kule upinzani unaambiwa kabisa kuwa huyu amezaliwa mahala fulani, na si Mtanzania na ukiangalia anachokifanya na tabia zake mbona zinalingana na za mtu wa nchi jirani,” anasema na kuongeza:

“Hao watu wamo ndani ya serikali na CCM pia wamo, na niko tayari kuthibitisha hilo. Unajua tuna mfumo hapa kwamba hebu fanyeni vetting kwa huyu na kwa huyu na mafunzo tuliyoyapata ni lazima ukitoka nje kuna vitu unaviona kwamba vetting lazima ikamilike, wakati ule Serikali ya Awamu ya Nne, serikali ilikuwa makini mno katika vetting.

“Ninachozungumza hapa ni mwenendo wa baadhi ya viongozi na si mwenendo wa vyombo vya ulinzi na usalama, kwa sababu tukiwa kule upinzani hakuna siri.

“Unaambiwa kiongozi huyu anabaka ofisini. Naomba nieleweke kwamba ninazungumzia baadhi ya viongozi na si vyombo vya ulinzi na usalama, lakini hadi mtu anashitaki fulani amenifanya hivi au vile ili nipate kitu fulani, na kuna vitu vinajulikana vya wazi kabisa.”

Membe ambaye amekuwa mbunge wa Jimbo la Mtama kuanzia mwaka 2000 hadi mwaka 2015, anasema siasa ni ‘uchawi’ na ukiwa CCM unakuwa kama umerogwa.

“Siasa ni uchawi. Kwanza, CCM ndio mwili wako hata kama umevunjika au michibuko mingi, ni kama ilivyo roho na mwili wako. CCM ambayo nimeitumikia tangu mwaka 1977 rasmi, unazungumzia karibu miaka 41,” anasema na kuongeza:

“Unapokuwa ndani ya CCM, wewe unakuwa CCM na CCM inakuwa wewe – na CCM ni uchawi, kwa sababu hauoni ubaya wake hadi utoke mle katika angle ndiyo unakiangalia ili ukione kilivyo muhimu, ukione kikiwa na tatizo na ili ukiingia tena uingilie upande gani.

“Kwa hiyo ninapozungumzia siasa ni uchawi ni kwamba ukiwa katika chama muda mrefu umeshajiroga na unaona kiko sawasawa kabisa, na kama ninavyosema kimenilea, kimenitunza na nilikuwa ninakwenda vizuri sana, sikuondoka katika chama kwa kupenda. Nilifukuzwa, nilisikitika sana.

“Kwa sababu kama nilivyosema, hakuna chama kitakatifu, kwa kuwa kila chama kina dosari zake, lakini siasa ni uchawi, unapokuwa mle ndani unaishi vizuri na hakuna wa ‘kukuroga’, na tuliishi vizuri sana.”

Anasema amejifunza mambo mawili kutoka CCM; la kwanza ni kwamba ni lazima chama hicho kiwe na uongozi wa Kitanzania na kiongozwe na Watanzania wenyewe; na pili, ni vema kikaongozwa na wana CCM wenye historia nacho.

“Kwa mfano, ukisikia fulani ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM ni lazima msikilizaji aambiwe historia yake katika CCM, na si ahame chama fulani na apewe madaraka. Hilo ni jambo ambalo wananchi lazima tuliingilie. Lazima tupate watu wenye historia katika chama hicho, wanaokielewa chama hicho, ni hatari kuchukua watu ambao hawakijui chama. Huo ndiyo uzoefu wangu mfupi katika upande wa chama.”

Kwa upande wa serikali, anasema alipokaa nje akaanza kugundua kumbe ni vizuri viongozi wakafanyiwa uchunguzi wa kina uliokamilika na kuwajua wanapotoka na afya zao.

“Ukikaa nje hili jambo unaliona kama mwezi unapouona ukiwa angani. Tusipoangalia unaweza ukajikuta una kiongozi hana damu ya u-Tanzania, na ninakwambia hivi, lazima sifa hiyo iwepo na isije kusemwa mimi ni mbaguzi, hapana, lazima iwepo, kwa sababu suala la uongozi ni la Watanzania, ndiyo maana tunasema ni uzalendo. Unajiuliza, tabia hii ni ya Watanzania kweli? Tangu lini mwandishi wa habari anatoweka?

“Sisi tulikuwa tunasoma katika vitabu nchi zilizopigana wenyewe kwa wenyewe ndiyo unaambiwa kuna waandishi wametoweka, watu hawawezi kuzungumza kule. Watanzania wanatumwa kwenda kutatua matatizo na si wao kuja kutatua matatizo yetu.

“Jamani kimetokea nini kwa watu hawa waliopotea? Tumekwenda Zimbabwe baada ya Morgan Tsvangirai kupigwa karibu jicho litoke, tumekwenda kumuuliza Rais Robert Mugabe kimetokea nini dunia nzima inakulalamikia jinsi unavyowafanya wapinzani wako.

“Mzee Mugabe akasema ‘Morgan alikuwa anatoka zake shambani akaja kulikuwa na maandamano, basi askari wangu mmoja akachukua rungu akampiga jichoni na akapandishwa cheo kuwa sajenti alikuwa koplo’.

“Sikia, ule si u-Tanzania. Ukiona jambo kama hilo limekuja unaanza kujiuliza huu u-Tanzania kweli? Ndilo somo la kwanza kubwa nililojifunza. Lakini la pili ni vetting ya viongozi.

“Tusipofanya vetting ya viongozi kiafya tunaweza kuwa na watu wa magonjwa ya akili. Sikufichi, katika kipindi hiki nilipoona kiongozi aliyepewa dhamana yuko ofisini kwake anawasha muziki anacheza peke yake na kujirekodi, halafu mnamuangalia mtajua kuna tatizo. Ukiona kiongozi amefikia hatua hiyo, ujue kuna tatizo na hatujafanya vetting vizuri,” anasema Membe.

Kwanini alijiunga ACT-Wazalendo?

Membe anasema dalili zilipojionyesha kwamba kuna kikao cha Kamati ya Maadili ya CCM, wakaitwa makada watatu; yeye na makatibu wakuu wa zamani, Abdulrahman Kinana, na Yusuph Makamba.

“Ikaamriwa hivyo kwamba sisi watatu tuitwe katika ile kamati. Mimi, Kinana na Mzee Makamba. Ulikuwa mkutano wa NEC wa Desemba 2019, kwamba sisi lazima tuitwe kwa sababu ya matatizo ya nidhamu, nikashukuru.

“Lakini kwa wakati huo tulidukuliwa, mimi nilikuwa ninaongea na mtu wangu mmoja wa nyumbani kumweleza kwamba kuna mpasuko ndani ya CCM. Kwa hiyo Kamati ya Maadili ikaitwa ilikuwa Machi, mwaka jana, nikaenda mimi peke yangu, Mzee Makamba alikataa na Kinana alikataa na nikawaambia rasmi kabla sijaenda kwamba ninakuja.

“Kule nikamkuta Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili, Philip Mangula, Dk. Bashiru Ally (wakati huo akiwa Katibu Mkuu wa CCM), Makongoro Nyerere akiwa ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, mjumbe kutoka Zanzibar, ofisa mmoja kutoka katika chama na ofisa mwingine wa taasisi nyeti aliyepo katika chama – kulikuwa na maofisa kama watano hivi waliokuwa wananisubiri kunihoji.”

Anasema aliwaeleza bayana kwamba kuna kesi imefunguliwa Mahakama Kuu na hawawezi kujadili, kwa kuwa kuna mambo mengine yako mahakamani.

“Ni common sense tu. Pale tukajadili mambo yasiyokuwapo mahakamani, na wanasheria wangu walishaniambia kwamba haya yasijadiliwe, yanaweza kujadiliwa mengine, kwa sababu tutaingilia uhuru wa mahakama. Tukakubaliana na jambo tulilozungumzia siku hiyo pale ni udukuzi.

“Suala la udukuzi lilipofika, Mangula akasema tulisoma hapa katika magazeti kwamba katika kudukuliwa uliongea kwamba chama kina mpasuko. Nikamwambia mwenyekiti subiri, suala la kudukuliwa limo ndani ya Katiba, kwa hiyo twende taratibu.

“Usisome kwanza mimi nilichodukuliwa, twende katika udukuzi, kwa sababu udukuzi ni kosa la jinai. Kwa kuwa mmelileta hili, kwanza tuanze na nani alinidukua? Nina kesi ya jinai dhidi yake na Katiba inasema Mtanzania yeyote anayo haki ya faragha na hatakiwi kuingiliwa katika hiyo faragha na kufanya hivyo ni kosa. Iliwachukua nusu saa pale na kila mmoja anaulizwa anakataa, nikiwauliza hao maofisa wanakataa, kwa sababu kuna kosa pale limefanywa.

“Kwa muda wa nusu saa tukawa tunamtafuta mtu aliyenidukua – hayupo, taasisi nyingine zikataa, Chama kikakataa, Serikali ikakataa, lakini nikawaambia sikilizeni, aliyenidukua ninamjua, mashine ya kudukulia ninapajua ilipotoka, mashine iko wapi ninapafahamu na watu waliohusika na udukuzi huu ninawafahamu, kwa hiyo hapa tunafichana tu kiutu uzima.

“Nikamwambia mwenyekiti (Mangula) sasa twende katika context, hili nitalishughulikia mwenyewe na hao wakaanza kunihoji katika kudukuliwa,” anasema.

Membe aliulizwa kama anaunga mkono taarifa iliyoandikwa na Kinana na Mzee Makamba iliyopelekwa katika chama.

Anasema akawaambia kuwa maudhui yanafanana na yake aliyoyapeleka Mahakama Kuu na aliyekuwa akijiita mwanaharakati huru Cyprian Musiba ni…, anawavunjia heshima wastaafu na kuwatukana, anazua uongo wa jinai dhidi ya hao wazee na kwa kuwa wameandika yeye akaamua kupeleka mahakamani na wao wamepeleka katika chama.

“Nikasema siwezi kukataa, nimeisoma hiyo document ya kina Kinana, walichokiandika ninakijua, ninakiunga mkono na hakuna mwenye ubavu wa kukikataa, Bashiru akajibu hapana, kwanini hawakumwandikia yeye, kwanini wamepeleka kwa wazee, nikamwambia kesi inakuhusu wewe kwanini wakuletee wewe?”

Membe anasema hajawahi kuvutana na Bashiru hata siku moja na alikuwa hamjui, lakini ghafla tu akalipuka kwa kusema anapitapita mikoani kufanya kampeni.

Baada ya kikao hicho akawaaga kwamba amepata habari kutoka kwa vyanzo vya Bashiru kwamba yeye na Kinana wanafukuzwa CCM na Mzee Makamba anasamehewa.

“Of course that was original plan, lakini kamati yote ya maadili ikakataa kwamba hilo haliwezekani na haiwezi kutokea. Nikasubiri matokeo ya kamati na nikajua yatakuwa na favor kwangu, lakini CC (Kamati Kuu ya CCM) ikaitishwa ghafla (chini ya Mwenyekiti Magufuli) ikatangaza mimi nimefukuzwa na hiyo ni kinyume kabisa cha utaratibu wa chama na vikao vya chama, nikasema alaah! Kumbe yote haya yanayofanywa lengo lilikuwa nifukuzwe,” anasema.

Membe anasema yeye ni mwanasiasa na akaona akikaa kimya Magufuli, Bashiru na Humphrey Polepole (wakati huo alikuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM) wataona anawaogopa ndipo akajiunga upinzani katika Chama cha ACT-Wazalendo.

“Nilijiunga upinzani nipate platform ya kusema kilichomo moyoni mwangu na nilifanikiwa sana, na uliona sikufanya kampeni, nilipata platform tano tu,” anasema.

Safari ya kurudi CCM

Anasema baada ya kutangaza anajiondoa ACT-Wazalendo, watu mbalimbali na makundi mbalimbali wakampigia simu na wakatuma ujumbe wa kumtaka arejee CCM.

Pia anasema viongozi wastaafu wawili wakubwa (majina yanahifadhiwa) wakapeleka ujumbe nyumbani kwake, wajumbe wawili wa CC ya CCM (majina yanahifadhiwa) wakampigia simu kumuomba arudi, viongozi wa dini zote mbili (majina yanahifadhiwa); Wakatoliki na Waislamu (Bara na Visiwani), wakamuomba arudi na baadhi ya wanachama wa CCM wa mikoa ya Lindi na Mtwara wakamueleza kwa maandishi kwamba uamuzi wake ni uamuzi wao na akiamua kurudi nao watarudi katika chama hicho.

“Ujumbe wa watu wote hao wakasema nikiamua kukaa kimya nao watakaa kimya, kwa hiyo niliwaweka katika njia panda kubwa mno, wote hao niliwaeleza ningelipenda sana kurudi CCM kwa sababu ndiko nilikozaliwa.

“Mimi niljiunga TANU mwaka 1975, baada ya miaka miwili ndipo nikajiunga CCM nikiwa na miaka 23 tu, kwa hiyo hata kama CCM ni mbaya au si mbaya, mimi ni mwana CCM wa kuzaliwa.

“Kwa hiyo wala nisingehitaji sana nguvu kubwa ya wakubwa kuniomba nirudi CCM, isipokuwa nilikuwa na tatizo la uongozi wa chama, kwa maana ya Mwenyekiti, Katibu Mkuu na Katibu wa Itikadi na Uenezi ambao waliungana na Musiba kunihujumu mimi kwa ushahidi na wala sina tatizo lolote.

“Kilichoniondoa CCM si chama. Hakuna chama kitakatifu, wewe huwezi kuhama chama hiki kwa sababu si kitakatifu, unatafuta chama kitakatifu, lakini kuna viongozi wabaya wanaoweza kukuzima usifanye jambo lolote lile, na usisikike kwa jambo lolote lile,” anasema.

Anakumbuka mjumbe wa CC aliyempigia simu na kumwambia anamuomba amtume aende kwa Magufuli akalimalize suala hilo, lakini akakataa kwa kumjibu kuwa wakiondoka yeye atarudi.

“Akacheka, nikacheka kisha tukakaa kimya. Hiyo ni Januari, mwaka huu nilipoacha na mabadiliko yakaja Machi, mwaka huu kwa mapenzi ya Mungu. Yakatokea mabadiliko ya uongozi wa nchi, ghafla na viongozi wote wakuu wa chama hawapo kwa maana kwa nafasi zao.

“Nikaanza kupokea maombi tena na delegations mbalimbali, rudi, rudi, rudi CCM lakini nikasema hivi ninarudije, kwa sababu mimi nilifungiwa mlango, labda niseme niko njiani nifungulieni mlango. Sasa hivi tunapoishi ukiwa mahala saa 5 usiku unapiga simu nyumbani nifungulieni mlango, waandae geti uingie, ni common sense, kwa sababu mlango ulifungwa.”

Membe anasema: “…Kiongozi mmoja wa Zanzibar aliniita niende kumzika Maalim Seif Sharif Hamad, nikamwambia sitaweza. Aliniomba pia niende nikazike Chato, nikamwambia sitaweza, nikamwambia hapana, nafsi yangu inakataa, sioni aibu, lakini sitaki kuwa mnafiki. Ni jambo la kawaida tu, hata kwangu asingefika, hata kama ningekufa mimi kila mtu angeshangaa kwamba huyu anakwenda kumzika Membe?

“Kama huziki, kama unamchukia huyu eti umemchukia fulani miaka sita halafu unakwenda kumzika, unamdanganya nani? Hao ndio ambao pamoja na wengine wote waliniumiza sana, mjumbe wa CC yule mara baada ya kuona mwangwi ule, alinipigia simu akaniambia ninaomba utekeleze ahadi yako.

“Nilikushawishi ufanye moja, mbili, tatu ukaniambia tusubiri watoke, lakini mimi nikacheka tu Mungu akaingilia kati, sasa ninaomba unipe tarehe ya kurudi. Nikamwambia lakini siwezi kukupa tarehe, kwa sababu mlango umefungwa, akasema ni kweli lakini mbona huu mlango ukiusukuma tu unafunguka? Nikamwambia nikifanya hivyo wataniambia mimi ni mwizi,” anasema.

Membe anasema ametoa kauli ya kuyapa matumaini makundi hayo yaliyomuomba kwamba atarudi CCM kwa sababu alikokwenda hakukumpendeza.

Anasema makundi yote hayo yaliyomuomba akayaeleza kuwa amepeleka kesi Mahakama Kuu inayohusu mrundikano wa mambo ya hatari aliyosingiziwa kuyafanya katika taifa hili, ni vizuri uamuzi aufanye baada ya hukumu.

“Wote hao waliafiki kwa sababu unarudije muuaji wewe katika chama, mhujumu mkubwa wa uongozi utaeleza nini? Lazima uende ukiwa umesafishwa, jamani mimi ni mweupe kama mchele na waliokuwa wanasababisha yote haya hawana nguvu ama hawapo.

“Kwa hiyo nikaomba kesi hii vyovyote itakavyoamriwa itoke kwanza hukumu ya Mahakama na kama nitaonekana nimekosa, basi niombe radhi, sitapata shida kuomba radhi. Kama Mahakama itanisafisha sitaona aibu kurudi nyumbani na kusema jamani niliondoka nilirundikiwa mzigo huu, Mahakama imepitia hakuna kitu hapa, mimi nilijua hakuna kitu lakini nilitaka kuiambia dunia kwamba hakuna kitu ili nisiwe na dosari yoyote katika chama, tukakubaliana hivyo, hayawi hayawi sasa yamekuwa.”

Nini kinafuata? Membe anasema ataitaarifu rasmi CCM juu ya hukumu ya kesi yake iliyotolewa na Mahakama Kuu dhidi ya Musiba na atasubiri mwongozo na atafanya hivyo mapema iwezekanavyo na kikubwa alichokifanya kwanza ni kusafisha jina lake.

Kizazi cha uongozi

Katika hatua nyingine, anasema kizazi cha sasa ndani ya CCM ni cha uongozi na haiwezekani kikarukwa na wakachukuliwa watu wa kizazi chake au watu wa nje.

“Hiki ni kizazi chenu na kila kizazi kina kada ya uongozi, nikifanikiwa kurudi ndani ya CCM lazima twende kwa kizazi hata tulipokuwa sisi kwa mfano miaka 30, 35, 40, 45 au 50 hicho ndicho kizazi cha uongozi, msikiruke hiki.

“Niliuliza swali katika Kamati ya Maadili kwanini mnawaacha vijana waliokwenda kukipambania chama wanarudi mnawaacha pembeni na mnawachukua vijana wengine kutoka nje? Hamuoni kwamba mnaleta sokomoko? Nikamuuliza Bashiru, akanijibu ukiangalia hawa vijana huyu ni kundi la Membe, huyu kundi la Kikwete, huyu kundi la Kinana, huyu la Makamba, Wassira, sasa wote hawa wana makundi ndiyo maana tunaamua kwenda nje kuchagua wengine waingie huku.

“Kwa hiyo hao mnaowachukua huko kuja humu hao hawana makundi? Mtatiro hana kundi, na ukimleta huku hatakuwa katika kundi lako, ni ujinga gani huu tunaufanya kwa sababu CCM kama vyama vyovyote vile duniani ni ushindani wa ndani kwanza.

“Sasa unapojenga ushindani katika nafasi mbalimbali za uchaguzi ndani ya chama si ndiyo unatengeneza makundi, lazima watu wamshabikie huyu na huyu, kuna ubaya gani? Viongozi wote mnarudi mnakuwa kitu kimoja. Ukisikia kuna makundi maana yake kuna demokrasia na baada ya hapo mnarudi kuwa kitu kimoja, kwa hiyo yeye alitaka vijana wawe kama uyoga vile hakuna anayempenda fulani na fulani,” anabainisha.

Membe anahoji, kwanini kuna woga wa ushindani ndani ya CCM? Anasema wakishasema demokrasia ndani ya chama maana yake kuna ushindani na ushindani wowote ule maana yake kuna makundi.

Anasema CCM ina wahafidhina na watu vuguvugu na anahoji, je, hao hawatakiwi?

“Kwani sisi ni Wachina kwamba tunazaliwa siku moja katika incubator, kwamba siku moja tunapewa maziwa na tunafanana akili, haliwezekani hilo. Yaani moja kati ya vitu tutakavyovifanya tukirudi CCM ni kuhakikisha vijana waliokifia chama chao cha CCM na kukipambania tusiwakatishe tamaa.

“Tuwape fursa za uongozi kwa sababu fursa ya nchi hii imo mikononi mwao, na haya mambo yataua zaidi vijana kama unaleta damu mpya ndani ya chama ambao hawana historia yoyote na chama,” anasema.

Anawataja waliokuwa viongozi wakuu wawili wa CCM, na mmoja ambaye bado yumo kwenye madaraka kwamba hawakuwahi kuwa wana CCM.

Anasema kunapokuwa na kundi la viongozi ambao si wana CCM usitarajie likawa linawafundisha na kuwaandaa vijana ndani ya chama hicho.

“Na tusipofanya hivyo CCM itakuwa katika hatari na mazingira mabaya mno, tulikuwa na vyama zaidi ya 50 vya ukombozi Afrika, 48 vyote vimeondoka vimebaki sita tu vya Namibia, Angola, Tanzania, Afrika Kusini, Zimbabwe na Msumbiji,” anasema Membe.

Kwa mengine mengi, yakiwamo ya uhusiano wake na Edward Lowassa, Rostam Aziz, suala la mgombea binafsi, Katiba mpya na utawala wa Jakaya Kikwete usikose toleo lijalo.

Source: https://www.jamhurimedia.co.tz/membe-aibua-mapya/
 
babu M

JF-Expert Member
Mar 4, 2010
5,225
3,160
KWA WALE WASIOPENDA KUSOMA HABARI REFU:

Toleo lililopita waziri huyo wa zamani wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa alieleza namna Rais John Magufuli alivyomfitini hadi akakosa Ukatibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola.

Membe anasema faida mojawapo aliyoipata baada ya kufukuzwa CCM mwaka jana ni kuwajua watu ambao si raia wa Tanzania, lakini wameshika nafasi kubwa za kisiasa.

“Unaambiwa kiongozi huyu anabaka ofisini. Naomba nieleweke kwamba ninazungumzia baadhi ya viongozi na si vyombo vya ulinzi na usalama, lakini hadi mtu anashitaki fulani amenifanya hivi au vile ili nipate kitu fulani, na kuna vitu vinajulikana vya wazi kabisa.

Membe anasema: “…Kiongozi mmoja wa Zanzibar aliniita niende kumzika Maalim Seif Sharif Hamad, nikamwambia sitaweza. Aliniomba pia niende nikazike Chato, nikamwambia sitaweza, nikamwambia hapana, nafsi yangu inakataa, sioni aibu, lakini sitaki kuwa mnafiki. Ni jambo la kawaida tu, hata kwangu asingefika, hata kama ningekufa mimi kila mtu angeshangaa kwamba huyu anakwenda kumzika Membe?

Nine kinafuata? Membe anasema ataitaarifu rasmi CCM juu ya hukumu ya kesi yake iliyotolewa na Mahakama Kuu dhidi ya Musiba na atasubiri mwongozo na atafanya hivyo mapema iwezekanavyo na kikubwa alichokifanya kwanza ni kusafisha jina lake.

SOURCE: Gazeti la jamuhuri
 
Similar Discussions

29 Reactions
Reply
Top Bottom