Lowassa awatosa. wengi wajutia nafsi kwa uamuzi wa pupa

kalulukalunde

JF-Expert Member
May 27, 2016
1,056
1,083
Sasa ni wazi kwamba aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA, Edward Lowassa, amewatosa kiana karibu makada wote alioondoka nao kutoka CCM na kuhamia chama hicho kikuu cha upinzani nchini.
Lowasa aliondoka mwishoni mwa Julai, mwaka wa jana na kujiunga na CHADEMA kwa lengo la kupata fursa ya kugombea urais baada ya jina lake kukatwa wakati wa mchakato wa vikao vya uteuzi ndani ya CCM.

Kutokana na uamuzi wake huo, baadhi ya makada wa CCM waliokuwa wakiunga mkono mbio hizo za urais wa Lowassa waliamua kumfuata huko, wakiwa na matumaini makubwa kuiondoa CCM madarakani, baada ya mgombea huyo kuungwa mkono na vyama vya CUF, NLD na NCCR mageuzi.
Miongoni mwa makada hao wa CCM waliochukua uamuzi wa kumfata Lowassa CHADEMA, ni pamoja na waliokuwa wenyeviti mikoa CCM Arusha, Singida, na ,Shinyanga, Onesmo Ole Nangole,
Mgana Msindai na Hamis Mgeja.

Baadhi ya makada wengine waliomfuata Lowassa walikuwa na majina makubwa, waziri mkuu mstaafu Fredirick Sumaye, Matson Chizii, Lawrence Masha, John Guninita na Tambwe Hizza. Aidha, katika orodha hiyo, yumo mzee Kingunge Ngombale Mwiru ambaye pia aliamua kumfuata Lowassa na kuzunguuka naye kwenye kampeni zake za kuusaka urais, baada ya kuhangaika naye kwenye ndani CCM na kuambulia kapa, akianzia kumnadi katika mkutano wa kutangaza nia jijini Arusha kana kwamba huyo ndiye aliyekuwa mtangaza nia pekee ndani ya chama tawala hicho.

Hata hivyo, tangu kumalizika kwa kwa uchaguzi mkutj wa october 25 mwaka jana, ni majina mawili tu pekee ya Lowassa na Sumaye ndio yameendelea kusikika ndani ya CHADEMA, huku majina pia wakiwa wamepewa vyeo vya kuwa wajumbe wa kamati kuu na baraza kuu. Wengine wote hadi sasa majina yao hayasikiki ndani ya CHADEMA, kiasi ambacho baadhi yao kukiri waziwazi kuwa wametoswa na Lowassa kutokana na kile kinachodaiwa mwanasiaïa huyo ameshindwa kuwapigania ili nao waweze kupata nafasi za uongozi ndani ya chama hicho.

Ukimwachia Ole Nangole, ambaye baada ya kuondoka CCM alikwenda kugombea ubunge katika jimbo la Longido kwa tiketi ya CHADEMA na kushinda mpaka sasa yupo bungeni kwa tiketi ya CHADEMA, karibia wengine hao wote wamebaki hewani kiasi baadhi yao kuanza kufikiri kurudi CCM.
Mmoja wa makada hao wa CCM aliyemfuata Lowassa, amezungumza kwa kutotajwa jina, akisema kwamba yeye na wenzake hao, wanafikiri kurudi tena CCM, huku akijinasibu kuwa CCM ni nyumbani kwao siku yeyote wanaweza kurejea.

"ukweli ni kama tumetoswa. Tulimfuata Lowassa CHADEMA baada ya kushindwa kwenda ikulu ametutosa kabisa hataki hata kutuona ofisini kwakwe mikocheni, hata sim zetu wakati mwingine hataki kuzipokea kila tunapompigia kutaka kuzungumza naye", anasema kada huyo ambaye amewahi kuwa kiongozi wa CCM mkoa. "lakini CCM ni nyumbani, wote tumelelewa huko, muda wowote tunaweza kutangaza kurejea huko. Hakuna cha ajabu katika siasa kuondoka ndani ya chama siasa na kurejea tena. "Kina Guninita waliondoka kwenda kuanzisha CHADEMA, steven wassira waliondoka kwenda NCCR lakini mambo yalivyowashinda walirejea tena nyumbani, wakapokelewa na kuaminiwa na kupewa uongozi.

"wapo kina Makongoro Nyerere. Huyu aliondoka CCM wakati baba yake ni mwasisi wa CCM akiwa bado hai, lakini alirejea nyumbani akawa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mara na sasa ni mbunge wa Afrika Mashariki.
"usisahau kwamba hata balozi Mwapachu tulikuwa naye huku, akiwa amefuatana na Lowassa, lakini amesharejea CCM. Hivyo haitakuwa dhambi sisi kurudi"

Kwa upande wake kada mwingine wa CCM aliyemfuata Lowassa, ambaye naye haoneshi kufurahishwa na kitendo hicho cha kutoswa, bila kutaka jina lake lisitajwe, lakini pia amewahi kuwa kiongozi serikalini na CCM: "kinachotufanya sisi tufikirie kurudi si kwa sababu ya kutoswa ndani ya CHADEMA, bali ni mabadiliko kwenye uongozi huu wa sasa wa Dk. Magufuli." Tunaiona Tanzania mpya chini ya Dk. Magufuli lakini pia tunaiona CCM mpya ikija baada ya Rais Magufuli kukabidhiwa kijiti mwishoni mwa mwezi huu au mapema mwezi ujao.

Chanzo Tazama
 
Gazeti gani? TAZAMA? nenda na ukurasa wapili utakutana na habari na unajimu na matangazo ya waganga wa kienyeji. Watatu na wanne ni makala za ufreemason na zinazobaki ni nukuu za magazeti mengine ya nje za zamani.
 
Gazeti gani? TAZAMA? nenda na ukurasa wapili utakutana na habari na unajimu na matangazo ya waganga wa kienyeji. Watatu na wanne ni makala za ufreemason na zinazobaki ni nukuu za magazeti mengine ya nje za zamani.
Hivi hili gazeti linamilikiwa Na Nani? Huwa silielewi kabisa.!
 
Back
Top Bottom