A ni a girl about town. Alianza sexual relationships akiwa na umri wa miaka 16, akiwa na miaka 17 alipata mimba, kwakuwa wazazi wake wanathamni elimu alipelekwa Aghakan Hospital mimba ilitolewa.
A amefika chuo na kuona wanaume wamemchezea sana, ameamua kuwa mlokole.
Umehangaika sana kuingiza mtongozo kwa A amekukubalia lakini kwa masharti kuwa hakuna sex mpaka ndoa. Kwakua unampenda A umekubaliana na hali.
Unaenda na A kwenye office party, mnakutana na rafiki aliyesoma na A Upanga primary. Jumatatu ofisini rafiki anakupa story za A alivyokua anagombaniwa enzi hizo. Moyo wako unakosa amani unaamua kumwacha A. Bila kosa.
Unaamua kutafuta ambae hana history. Umpata B, ambae ni bikra. Umemuoa B mmeanza maisha. Umesafiri marafiki wa B wamemfahamisha B kwa mkaka mwenye boutiques. Anaanza kumpa B magauni ya laki, B anataka kuwa wa mjini.
Anaanza kukitoa kwa mkaka na kupewa nguo za bure. Haishii hapo anampata na mwingine wa kujirusha, B hajawahi kwenda club maishani mwake. Kuona raha amezipenda. Hatimae wewe ni mwanaume wa nne kwa B na yuko kwenye ndoa na aliolewa bikra
Kati ya hawa ni nani mke mwema?