Yuko wapi wa kuvaa viatu vya Ruge?

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
182,822
2,000
Huwezi kuona thamani ya kitu mpaka siku ukikose!

Wako wapi wasanii wale waliopiga kelele kuwa wanashindwa kung'ara kwakuwa marehemu Ruge alikuwa anawanyonya? Wengi nawaona wakiwa na hali mbaya kuliko hata kipindi cha kunyonywa na marehemu.

Leo sitajadili uwezo na vipawa vya Ruge kwenye tasnia nzima ya mziki wa kisasa lakini kuna siku historia itampa heshima anayostahili...Ninachotaka kusema hapa ni kwamba kama hujui basi katika kundi ambalo halina shukrani wala fadhila basi ni hili kundi la wasanii wa kibongo, wote wa mziki na maigizo kwa mukatadha wa mada hii

Hulka sugu ya hawa watu ni ile dhana ya kupenda kitonga kwenye kila kitu.. Utamtoa jalalani uswekeni akiwa ni kapuku asiye na mbele wala nyuma utatumia gharama kubwa kumbrand na kumng'arisha... Akishang'aa na kuonekana mtu kati ya watu, thamani yako inakomea hapo

Atasahau kila kitu
Atasahau namna ulivyomfadhili
Sehemu ya kulala
Mavazi na mapambo
Chakula na vinywa
Usafiri
Gharama za studio
Matumizi ya kila siku nknk
Ole wako...nasema ole wako akishakuwa maarufu uje umkumbushe ulikomtoa ama ujaribu kumshauri kitu.. Utajuta kumfahamu

Sakata la Harmonise na lundo la tuhuma kwa Diamond limenikumbusha mengi lakini pia limefunua na kufumua mengi...Hakuna ubishi Harmonize ni msanii mzuri mwenye kipaji cha utunzi na uimbaji na ni mpambanaji asiyekata tamaa..kushindwa kuliona hili ni wivu mbaya kabisa.. Lakini kinachomsumbua ni vitu viwili vitatu
Hulka
Elimu/ uzoefu
Wapambe/makundi
Hulka ya kulalamika na kutaka kuona kaonewa sana, hili linatokana na kukosa uzoefu wa maisha unaotaka na elimu haba toka kuhitimu mpaka ajira

Wapambe na makundi.. Hawa ndio wanaweza kuwa kaburi lake kisanaa.
Ni kati ya hawa bila kumpamba pamba kwa maneno mazuri na matamu wanaona kula yao iko hatarini.Hawa ndio chawa wenye kutunga kila aina ya uzushi
Kuna makundi ya washindwa.. Hawa ni haters wa Diamond , wamo wasanii na wasio wasanii, hawa wanamtumia Harmo kutolea hasira zao kwa Mond..Yaani wanaona kushindwa kwao kumesababishwa na Mond

Hawa si kwamba wanampenda na kumjali sana Harmo la hasha wako naye hapo kutaka kupata kula yao lakini pia kutaka kumdidima Mond.. Ni kundi lenye wivu na roho mbaya sana na ni kati yao hao watakaokuja kumgeuka Harmo atakapofanya vizuri zaidi.. Ni kundi hili ndio lilikuwa mstari wa mbele kumsema marehemu Ruge leo limemgeukia Mond

Udhaifu wa mikataba upo popote pale duniani.. Labda pengine Harmo halifahamu hili..kupigwa kwenye mikataba ni jambo la kawaida sana, kama nchi na wasomi wake wote inabamizwa itakuwa yeye? Akumbuke hata lebo yake ya Konde boy kama ikisimama vema na kukua itakuja kukumbana na changamoto hizihizi anazozishikia bango kwa Mond

Ishu ya kusema kuwa alituhumiwa kutaka kumzidi boss wake hayo ni mambo ya kawaida sana mbona? Awaulize walio kwenye ajira hasa sekta binafsi ataambiwa.. Nguo nzuri kumzidi boss zinaweza kukuondoa kazini...
Je ya JK na Lowassa anayajua? Shetani mwenyewe alipoleta ujuaji na kutaka nafasi sawa na Mungu alipatiwa haki yake! Mond kafanya ni bjnadamu, Harmo naye atakuja kufanya.. Boss huwa anabaki kuwa boss kataa kubali!

Katuonesha mfanano wake na Musiba...Kumbe kule kujikomba kote kwa mwendazake ni kwa vile alisaidiwa madai yake! Akasahau kila kitu akajitia upofu mkubwa na kumbwagia kila aina ya sifa hata kama mamilioni walikuwa wanaumia..huu ni ubinafsi na choyo kikubwa

Ameshatapika ya kutosha sana, pengine ana nafuu sasa.. Lakini huu ndio muda wa kujitafakari zaidi.. Aliyemshambulia sana hajamjibu kabisa.. Hili linaumiza pia. Dunia tunayoishi ni ya survival of the fittest .. Ile ya upendo na huruma aliondoka nayo Kristo...Ishu ya kupata connection serikalini kupitia JP inamjengea maadui bila kujijua na wengine kati yao ni hao alionao sasa

Viatu vya Ruge bado vinatafuta mrithi
 

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
2,718
2,000
Ruge alikuwa ni muhuni tu akijificha nyuma ya kivuli cha connections zake serilalini, elimu yake, uzoefu wake, n.k

Ruge alikuwa hataki ushindani, alikuwa anataka awepo peke yake ili anyenyekewe.

Ukikosana na ruge alikuwa anafanya hilo bifu atalihusisha mpaka kwenye kukuua kimuziki.

Nandy alikuwa na kipaji kama wasanii wengi tu lakini kwakuwa alikuwa anampa ruge penzi, Ruge alimfanya awe star.

Tigo wanatoa hata milioni 150 kudhamini fiesta, wasanii wanapewa eld 40!! 😂😂

Ruge alikuwa mbwa mwitu ambae alivaa kinyago cha kondoo.
 

Labani og

JF-Expert Member
Sep 15, 2020
2,584
2,000
ni kweli haya mambo ya kibinadamu yanatisha sana lazima tujiulize maswali haya

je tuache kusaidia wenzetu kwa kuhofia kuwa watakuwa silaha kubwa kwetu

au tuendelee kutumia msemo wa tenda wema nenda zako..............

anyway
BROO MSHANA ....unajua kuleta maada fikirishi

 

Mimi sikulamba sukari

JF-Expert Member
Dec 11, 2019
1,958
2,000
Ruge alikuwa Mbunifu Sana alijua kucheza na nyakati
Ile THT aliyoianzisha pamekuwa mahala paupigaji Kila anayeenda kujifunza wanataka Atoe hela wakati kipindi yupo hai mwenye THT yake hakua na tamaa za kijinga

Ruge alipenda kuwakutanisha wasanii sehemu moja na wakafanya kile ambacho alikiamini na ndiyo maana Mondi anajitahidi Sana kukopi baadhi ya vitu kutoka kwa Ruge kuanzia kwenye Radio Hadi kwenye Tv

Kwakifupi Ruge aliichangamsha Sanaa kuanzia kwenye maigizo mpaka kwenye muziki pengo lake nikama the greaty kanumba halitakaa lizibike ingawa Kuna watu wanajitahidi kuvaa viatu Vyake
 

Mimi sikulamba sukari

JF-Expert Member
Dec 11, 2019
1,958
2,000
Ruge alikuwa ni muhuni tu akijificha nyuma ya kivuli cha connections zake serilalini, elimu yake, uzoefu wake, n.k

Ruge alikuwa hataki ushindani, alikuwa anataka awepo peke yake ili anyenyekewe.

Ukikosana na ruge alikuwa anafanya hilo bifu atalihusisha mpaka kwenye kukuua kimuziki.

Nandy alikuwa na kipaji kama wasanii wengi tu lakini kwakuwa alikuwa anampa ruge penzi, Ruge alimfanya awe star.

Tigo wanatoa hata milioni 150 kudhamini fiesta, wasanii wanapewa eld 40!!

Ruge alikuwa mbwa mwitu ambae alivaa kinyago cha kondoo.
Lakini mkuu pamoja na yoote ila yeye ndiye alikua sources ya hayo yote hivyo sidhani kama ingekua powa sana kama asingekua mnufaikaji mkubwa
 

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
2,718
2,000
Lakini mkuu pamoja na yoote ila yeye ndiye alikua sources ya hayo yote hivyo sidhani kama ingekua powa sana kama asingekua mnufaikaji mkubwa
Kunufaika kwa kuwapa promo wasanii hadi awagonge?? Hapana aisee, Nahisi kina Ruby walimbania ndio maana akawapiga chini.

Ogopa sana aina hii ya watu mkuu.

Haiingii akilini wadhamini wamechanga mamia ya mamilioni kudhamini fiesta halafu msanii anapewa eld 40, rubbish kabisa
 

Mimi sikulamba sukari

JF-Expert Member
Dec 11, 2019
1,958
2,000
Kunufaika kwa kuwapa promo wasanii hadi awagonge?? Hapana aisee, Nahisi kina Ruby walimbania ndio maana akawapiga chini.

Ogopa sana aina hii ya watu mkuu.

Haiingii akilini wadhamini wamechanga mamia ya mamilioni kudhamini fiesta halafu msanii anapewa eld 40, rubbish kabisa
Lakini Ruby bila Ruge asingejulikana
Ruge mwenyewe aliwahi kusema
Nyimbo zote zilizohiti yeye kushirikiana na Barnaba na Amini ndiyo walimtungia Nyimbo ambazo zikawa hits song

Sasa alitaka wasirudishe mazao waliyoyapanda kupitia yeye, akaona ananyonywa rabish girl
 

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
2,718
2,000
Lakini Ruby bila Ruge asingejulikana
Ruge mwenyewe aliwahi kusema
Nyimbo zote zilizohiti yeye kushirikiana na Barnaba na Amini ndiyo walimtungia Nyimbo ambazo zikawa hits song

Sasa alitaka wasirudishe mazao waliyoyapanda kupitia yeye, akaona ananyonywa rabish girl
Kwa hio huko kurudisha mazao ndio kumlipa rubby elf 80 kwenye fiesta azunguke tz nzima, huu ni upuuzi. kuna muda ndio tunahitaji kurudisha fadhila kwa waliotusaidia lakini kuna wakati unaona kabisa unadharauliwa kama nguruwe.

Nampa big up sana rubby kwa kukataa huu ujinga.

Ni kama kumchukua chokoraa huko mtaani umlishe chakula alafu umwambie akulimie shamba heka nzima umpe buku
 

collycool

JF-Expert Member
Nov 24, 2011
200
250
Umezunguka zunguka kujifanya unamsifia Ruge lakini nia yako ulitaka kuzungumzia Harmonize na Diamond ungeenda tu direct. Mbona Diamond alishalalamika sana kuhusu Ruge na watu wakamshambulia Ruge, leo akisema Harmonize mnaleta mabandiko yenu...

Kitu kingine Harmonize hajakataa kusaidiwa anacholalamika yeye ni kuendelea kuandamwa wakati alifanya kila kitu kulingana na matakwa ya mwajiri na mikataba ilivyotaka
 

ngulukizi

JF-Expert Member
Oct 10, 2018
358
1,000
Kwa hio huko kurudisha mazao ndio kumlipa rubby elf 80 kwenye fiesta azunguke tz nzima, huu ni upuuzi. kuna muda ndio tunahitaji kurudisha fadhila kwa waliotusaidia lakini kuna wakati unaona kabisa unadharauliwa kama nguruwe.

Nampa big up sana rubby kwa kukataa huu ujinga.

Ni kama kumchukua chokoraa huko mtaani umlishe chakula alafu umwambie akulimie shamba heka nzima umpe buku
Ni msanii gani fiesta alikuwa analipwa elfu 40 au 80 ndugu huyo Ruby hela aliyokuwa anapaita alikuwa anahonga wanaume tu na kulewa tunamtuhumu mtu KWA vitu ambavyo hakuvifanya kisa hawezi kujitetea nani asiyojua wasanii wa bongo maisha yao hivi unafahmu hao hao unaowatetea ndio wanamkumbukka Ruge kipindi hiki Cha likizo ambacho ndio yalikuwa mavuno yao
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom