David ngayanimo
Member
- Nov 8, 2018
- 35
- 33
NGUVU YA VYOMBO VYA HABARI NA ANGUKO LA NGONI TRIBE BAADA YA KUMJIBU LADY JAYDEE:
Nyuma ya miondoko ya ladha ya asili na mashairi yaliyoteka hisia za Watanzania wengi kuanzia mwishoni mwa miaka ya '90, kuna ukweli mzito wasioujua wengi Wadau wengi wa Muziki kuhusu safari, mafanikio na changamoto za kundi la NGONI TRIBE.
Msanii wa kundi hilo maarufu, anayefahamika kama kwa jina la Komba, amefunguka historia kamili ya kundi hilo lililoundwa na miamba watatu—Kombaulaya (Komba), Kalimbwende, na Comedown
ambao kwa sasa wanaishi pamoja kama ndugu mtaa wa Ukonga, Dar es Salaam.
Safari yao rasmi kimuziki ilianza mnamo 1999 walipoachia wimbo wao wa kwanza uliofahamika kwa jina "Manungayembe". Katika studio za MJ Records chini ya mtayarishaji Master Jay, walirekodi na kuachia mfululizo wa nyimbo kadhaa zilizotamba sana kwa wakati ule nyimbo kama vile :
Manungayembe, Bongo Life Noma, Mama wa Kambo, Kainama, Tukichange, Tumerudi Tena, na Kipya Kinyemi. Hata hivyo,
Komba anaeleza kuwa maamuzi yao ya kuimba nyimbo zao kwa kutumia lafudhi na lugha ya kabila la Kingoni ndiyo sababu kuu iliyowafanya wasifike mbali zaidi kimuziki.
Mnamo mwaka 2002 na 2003, walirudi tena Ngoni Tribe kwa kishindo na kuachia nyimbo zingine kali kadhaa kama vile :
Katibu Kata, Mjomba Si Mjomba, Ne Mbwito Kuolewa, Tuneng'e Mule, Magenda Heka, na Naona Baridi. Mbali na Master J, walifanya kazi na P. Funk Majani (Bongo Records) ambapo walirekodi nyimbo kama takribani (4) ikiwemo na "Chindule Liganga", pamoja na mtayarishaji Marco Chali pale Mj Records ambaye walirekodi naye nyimbo kama vile
"Siwezi Kuvumilia Ngumi & Panga Liko Mkononi"
Katika Tuzo za Muziki za Kili (Kili Music Awards zilizofanyika Mwaka 2003), Ngoni Tribe waliwekwa kwenye kundi moja ( nominees) na wasanii takriban saba—akiwemo msanii nguli wa nyimbo za asili kutoka mkoani kagera Saida Karoli ambaye kwa kipindi hicho pia aliyekuwa anang'ara sana na nyimbo za vionjo vya ki asili na matumizi ya lugha ya Kihaya Na kufanikiwa kuibuka kidedea kwa kutwaa Tuzo Hiyo , Wimbo Bora Wenye Vionjo vya Asili.
Lakini kimbunga kilianza mwaka 2003 baada ya msanii Lady Jaydee kuachia albamu yake ya pili iliyofahamika kwa jina la 'Binti' chini ya usimamizi wa Smooth Vibes. Smooth Vibes ilikuwa ni lebo Maalum ya kusimamia kazi za wasanii iliyoanzishwa na kuongozwa na Marehemu Ruge Mutahaba akiwa kama Mkurugenzi. Ruge kupitia lebo hiyo ya Smooth Vibes ndiye aliyekuwa msimamizi mkuu wa safari ya mafanikio ya mwanzo ya Judith wambura a.k.a Lady Jaydee, kuanzia albamu yake ya Mwanzo kabisa 'Machozi' (2001) na Album ya pili 'Binti' (2003).
Katika list ya nyimbo zilizokuwemo kwenye albamu hiyo ya Binti, Jaydee alitoa wimbo wa mmoja uliofahamika kwa jina "Wanaume Kama Mabinti" Akiwa na Hamisi mwinjuma " Mwana Fa.
Ngoni Tribe waliamua kumjibu moja kwa moja msanii huyo Lady jay dee kwa kutoa wimbo wa jibu ama unaweza kuita ni (Diss Track) uliofahamika kwa jina la "Wamama Kama Vijana".
Kitendo hicho kilizusha mtafaruku mkubwa. Kwa kuwa Lady Jaydee alikuwa chini ya lebo ya Smooth Vibes chini ya Ruge Mutahaba ambaye pia alikuwa Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Vipindi Clouds Fm Media Group, kituo cha Clouds FM kilichukua msimamo mkali Dhidi ya kundi hilo la Ngoni tribe na Ma-DJ wote kwenye kituo hicho cha Radio wakasitisha mchakato wa kucheza nyimbo za kundi hilo la Ngoni Tribe.
Komba anasimulia:
"Media hiyo ya Clouds fm radio ilitumia nguvu kubwa sana kutudhoofisha kundi hilo Kimuziki kutokana na ile nyimbo au Diss track." Vikwazo hivyo vilikuwa vikubwa kiasi cha kuwalazimu kupumzika Kimuuziki na kuanza kufanya shughuli zingine nje ya kiwanda cha Muziki kwa miaka takribani miwili. Redio zingine zote zilikuwa zikipiga kazi zao kasoro Clouds FM Radio pekee na ukizingatia Clouds fm radio kwa kipindi hicho ndio kituo kikubwa cha Radio kilichokuwa na nguvu na ushawishi mkubwa kwenye jamii, hadi DJ mmoja wa Kiss FM jijini Mwanza alipowatonya ukweli uliokuwa nyuma ya changamoto zote hizo ama beef yetu na Clouds fm Radio
"akisema walikosea sana kumjibu Lady Jaydee.
Ili kuokoa jahazi, kundi la Ngoni tribe walilazimika kuandika barua rasmi kwaajilin ya kuomba msamaha kwa Ruge Mutahaba.
Komba anahitimisha kwa kukiri kuwa kipindi kile isingekuwa rahisi kusainiwa au kukubaliwa na Ruge Mutahaba kwenye lebo yake ya Smooth Vibes kutokana na mzozo huo mzito ulioharibu uhusiano wao na uongozi huo.
Leo hii, Ngoni Tribe imebaki kwenye kumbukumbu za Wapenzi wengi wa Muziki wa Bongo Flava kama kundi lililoleta mapinduzi kwenye kiwanda cha Muziki wenye vionjo vya asili, huku historia yao ikiwa fundisho kubwa kuhusu athari za mizozo ya kisanaa na nguvu za vyombo vya habari Nchini Tanzania.
Ukwaju wa kitambo
0767 542 202