Yuko Wapi Mzimu Wa Ziwa Tanganyika

Yuko Wapi Mzimu Wa Ziwa Tanganyika

kaisar19

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2021
Posts
228
Reaction score
391
Je! aliibiwa?: wakubwa shkamoni wadogo abari zenu mabinti mambo zenu.
FB_IMG_1743071609657.jpg

Nakusogezea kisa hiki cha kusisimua kuhusu Mzimu wa Ziwa Tanganyika. Moja ya sababu ya maji kujaa na kuharibu mali za watu ni ukumbusho kutoka kwa Mzimu huu kwasababu wahusika waliacha kuutambika mzimu wa Ziwa Tanganyika.

Mzimu wa ziwa Tanganyika unaitwa 'Mwanzalulu' kwa kimanyema, kwa kiha unaitwa 'Mganzaruguru' na kwa kibembe huitwa 'mkangialukulu'. Huu ndio mzimu pekee ambao makabila yanayopatikana ziwa Tanganyika yanaweza kutambikia kupitia mfalme huyu wa maji ya Ziwa Tanganyika, Lualaba, Lukuti, na Luiche.

Mvua nyingi zilizoendelea mfululizo zimepelekea kujaa kwa maji ya Ziwa Tanganyika katika maeneo ya Ardhi ya Ujiji na viunga vyake vya mwambao. Ng'ambo ya Kongo Uvira pia mafuriko ya maji ya mvua yamevunja majumba na baadhi ya Wazee wa mji wamedai viongozi wa kimila wamesahau asili na kutotambikia Mwanzalulu.

Makabila mengi ya mwambao yameacha kwa kiasi kikubwa kutambikia mizimu ya wahenga na vijana wengi hawajui hata majina ya Mizimu na sifa zilizohusishwa nayo.

Kiasili Mzimu wa Mwanzalulu wa Ziwani hutokea Unyakarambani. Wanyakaramba, pia huitwa Wakwalumona, hili ni koo la Kimanyema lugha yao ni kibwari cha Kinyakaramba.

Unaweza usielewe vizuri, nakupa mfano wa watu wanaotoka koo ya Kinyakaramba ili twende sambamba: Mfano wao ni Sheikh Amri Abeid Karuta, Sheikh Khalfan Kiumbe, Sheikh Yahya Hussein (mnajimu) na Sheikh Kitama wa Ujiji.

Sasa huyu Mzimu wa Mwanzalulu kiasili hutokea Unyakaramba, ambapo kuna safu ya Milima inaitwa Milima ya Mwanzalulu, Misozi, Kalomba, Kabubili, Kibwe, Kabogo na Nkungwe.

Mwanzalulu yupo katika kundi la Mizimu ya Mazingira. Hii huwa ndiyo mizimu mikubwa zaidi. Mizimu hii hujivisha tashihisi "personification" ya mazingira yake mf. Milima, Mito, Aruta, Ziwa, Misitu n.k mf. Mwanzalulu, Lungwe, Kabogo, Rutale n.k. Mizimu hii ndiyo kwa jamii za wenzetu huiita Miungu (Jambo ambalo ni makosa kiimani).

Mizimu ya mazingira "nature spirits", hii kama ilivyo kwa tamaduni za kipagani za ulaya na asia ni hali za kimazingira zikivishwa roho au tashihisi yenye uhai na umaada wa kujitegemea wenye nguvu fulani. Kundi hili ni kubwa na huingia Visigo, Mwanzalulu, Kabogo, Nkungwe, Mtambala, Ashibo, Nkongolo Mwamba, Rutale, Kwibe n.k

Katika utamaduni wa kuamini uwepo wa viumbe hivyo pia upo utamaduni wa kale wa kuamini uwepo wa Mzimu korofi unaoishi kwenye lindi la Ziwa Tanganyika.

Mzimu huo zamani ukisadikiwa kuonekana usiku ukisoza na mtumbwi hasa kwa kutokea Kaskazini maeneo ya Karamba (Unyakaramba) ukitambaza Ziwa kuja kusini.

Mzimu huo wa jinsi ya kiume, uliokuwa na sifa ya kujipigia ngoma ya mbiu wenyewe kabla ya kuanza kutarai Ziwani. Wamanyema huuita MWANZALULU, Waha huuita MGANZARUGURU na Wabembe huuita MKANGIALUKULU.

Mwanzalulu ni baba wa familia kubwa ya mke na watoto wengi mno. Chakula chake hupendelea Samaki na dagaa sanasana maana yeye kiasili ni mvuvi.

Katika ulingano wa kimaumbile Kwenye milango ya kiruhani ya Ujinini Mwanzalulu hufanana zaidi na Subiani.

Kwa sasa kutokana na mabadiliko ya kimazingira huwa hauonekani tena, ila katika vilinge vya kimanyema kuna watumishi wengi wa Mzimu wa Mwanzalulu.
....................
Sasa tunaingia katika ujio wa wazungu kunako ufahamu wao juu ya Mzimu huyu wa Ziwa Tanganyika'

Mzimu wa ziwani ulitajwa kwa mara ya kwanza na wazungu mwaka wa 1893, wakati Joseph Augustus Moloney aliporipoti kwamba mmishonari wa 'Mpala' alidai kuwa aliona 'Nyoka mkubwa sana Ziwani' mara mbili mara moja ziwani na mara moja ufuoni.

Mnamo mwaka wa 1907, wakati wa majadiliano ya 'Rothschild, mwanasayansi wa mambo ya asili 'Bwana Walter Rothschild' aliripoti kwamba afisa Mwingereza wa polisi alimwona mnyama mfano wa Nyoka mwenye pembe au mwenye manyoya kusini mwa Ziwa Tanganyika.

Kulingana na ripoti za Ujerumani kutoka Juni 1928, "Mwanzalulu" wakati mwingine alionekana akipita kama meli kwenye Ziwa Tanganyika, vijiji vingi vya mwambao wa Ziwa Tanganyika walikuwa wakiona Meli nyakati za usiku ikipita Ziwani ilihali kiuhalisia haikuwa meli bali alikuwa ni Mwanzalulu'

Ripoti hiyo ilidai kuwa nyimbo zisizotambulika zilikuwa zikisikika kwenye ufuo wa ziwa Tanganyika, na "kucha mbili kama za ndege mkubwa, kucha hizo ni kubwa zaidi kuliko tembo mzee.

Kwa mujibu wa mwandishi wa habari Lawrence Green, ambaye alidai kuwa uvumi wa uwepo wa Mzimu katika Ziwa Tanganyika ulikuwa wa kawaida, wakati wa ukoloni serikali ya Ujerumani ya Tanganyika ilitoa zawadi kwa kukamatwa kwa "Nyoka huyo mkubwa' aliyeonekana katika ziwa hilo, ambaye aliwahi kumeza mtumbwi uliokuwa na wasafiri ishirini.

Mwanzalulu aliripotiwa kutoka sehemu ya Burundi ya Ziwa Tanganyika mwanzoni mwa 1914 na kuelekea kusini mwa ziwa. Daktari Mjerumani M. V. Thierfelder, ambaye alikuwa akifanya kazi Tanganyika alishuhudia hali hiyo wakati wa janga la ugonjwa wa usingizi, alikuwa ameenda kuwinda karibu na ziwa akiwa yeye na mwalimu wake 'Ilsgensmeier, na mvulana mmoja wa kiafrika, walishuhudia hilo walipokuwa wakitembea karibu na fukwe ya ziwa iliyozungukwa na miamba.

Ghafla, nikaona, kitu ambacho sikuwahi kuona. Alikuwa ni kiumbe aliyefanana na nyoka wa kutisha. Hata hivyo, hakuogelea kama nyoka katika harakati za mlalo, lakini pete zake nilizihesabu zilikuwa sita, zilipanda wima juu ya maji. Mnyama huyo alifika kwenye ghuba kwa mwendo wa kasi, na akaenda moja kwa moja hadi karibu na ufuo wa mawe, ambapo tulikuwa tumelala. ' M. V. Thierfelder'.

Mnyama huyo alikuwa na urefu karibu mita hamsini na alikuwa na mafundo kadhaa katika mwili wake, kila fundo lilikuwa na urefu wa mita nne na nusu na kipenyo cha mita tatu. Kipenyo cha mnyama mzima kilikuwa sawa kutoka kwa kichwa chake hadi theluthi yake ya mwisho kuelekea mkia. ' M. V. Thierfelder'.

Mnyama huyo hakuwa na miguu, hata hivyo, kulikuwa na miundo myembamba kila upande. Rangi ya mnyama ilikuwa kahawia angavu; haikuwa na magamba, bali ilikuwa imefunikwa na ngozi nene. Kichwa kilikuwa kigumu kukitambua kwa sababu kilionekana kwa muda mfupi tu juu ya maji, lakini hakikuwa kipana zaidi ya mwili. Haikuwa kama kichwa cha nyoka, kwa mfano. Mdomo, ulionekana mwembamba na mrefu.

Mwalimu Ilsgensmeier pia alimwona mnyama huyo, na uchunguzi wake ulikubaliana kikamilifu na ule wa Thierfelder. Wafanyakazi wa Kiafrika, ambao hawakuwa wenyeji wa eneo hilo, hawakumtambua mnyama huyo, lakini walidai kuwa watu wa eneo hilo walimtaja kuwa ni mzimu wa Mwanzalulu' huwa anatokea mara moja kila baada ya miaka mitano. Thierfelder alichapisha alitoa makala ya mzimu huyu mwaka wa 1948.

Itaendelea......
 
Nimebaki kushangaa mpaka sasa watu wanaamini habari za mizimu. Swali la kujiuliza mbona siku hizi hatokei kila baada ya hiyo miaka 5? Mmejuaje kujaa kwa maji ni madhara ya kutomtambua miaka ya sasa? Alitoa ujumbe yeye mwenyewe binafsi kwa wazee kwa njia gani itakayoifanya dunia iamini?Je amefariki huko aliko au mzimu hauna sifa ya kufa?!
Still need to learn something here
 
Je! aliibiwa?: wakubwa shkamoni wadogo abari zenu mabinti mambo zenu.View attachment 3284746

Hizo habari za mizimu ni ujinga mtupu.

Mvua zimezidi, mito inaongeza maji kuingia ziwani, ziwa linajaa, watu wanasema mzimu umejaza maji?

Ujinga mtupu, na watu wanastukia huu ni ujinga ndiyo maana wanaacha kutambika kwa hiyo mizimu ya uongo.
 
Thibitisha mizimu haipo
 
Thibitisha mizimu haipo
Huelewi falsafa ya uthibitisho.

Anayesema kitu kipo ndiye mwenye mzigo wa kuthibitisha kitu kipo.

Kisichopo hakithibitishiki kwamba hakipo, kwa sababu hakipo na kuthibitisha kitu inabidi kiwepo.

Ukiibiwa na mwizi nyumbani kwako unaweza kuthibitisha umeibiwa, kwa ushahidi wa video, kwa kupata fingerprints za mwizi, kwa kuonesha alipovunja.

Kama hujaibiwa, hakuna mwizi, utathibitishaje hujaibiwa? Utatoa fingerprints za mwizi ambaye hayupo? Utatoa video ya kuonesha mwizi ambaye hayupo?

Anayesema kitu kipo ndiye mwenye mzigo wa kuthibitisha kipo.

Ndiyo maana polisi wakija kwako na kusema kuna madawa ya kulevya, na wewe ukasema hakuna, wao ndio wana mzigo wa kuyatafuta hayo madawa ya kulevya mpaka wayapate. Wewe huna wajibu wa kuthibitisha huna madawa ya kulevya.

Thibitisha hiyo mizimu ipo.
 
Kama umedhaniwa umemficha binti wa watu chumbani kwako, kuwathibitishia watu kwamba huyu binti hayupo chumbani kwako kwa kufungua mlango na kuwaonyesha chumba. Kwa kutumia mfano huo thibitisha mizimu haipo
 
Hata ukifungua mlango wanaosema binti yupo wanaweza kusema umemficha sehemu ambayo hawaijui, kwa hiyo hapo hujafanya kitu cha kumaliza mzozo.

Kitu cha kumaliza mzozo ni wanaosema mzimu upo kuthibitisha upo.

Ziwa halijafungwa, mfano wako wa kufungua mlango hauhusiki hapa, thibitisha mzimu upo.
 
Umeibiwa,😂
 
Dunia imebadilika sasa. Mwanzalulu amekuwa obsolete.
 
Hata ukifungua mlango wanaosema binti yupo wanaweza kusema umemficha sehemu ambayo hawaijui, kwa hiyo hapo hujafanya kitu cha kumaliza mzozo.

Kitu cha kumaliza mzozo ni wanaosema mzimu upo kuthibitisha upo.

Ziwa halijafungwa, mfano wako wa kufungua mlango hauhusiki hapa, thibitisha mzimu upo.
Mimi naamini ipo. Nawaona kwa Imani wewe ambae unasema hawapo unatakiwa pia uje na sababu zako ili tujue pengine Imani yetu sio sahihi.
 
Back
Top Bottom