Yuko wapi mkaka/mdada aliekuwa anakupenda sana kipindi hicho ukamkataa and viceversa

The Garang

JF-Expert Member
Jan 16, 2018
2,333
4,152
Habarini ndugu zangu, hongereni na poleni kwa majukumu yetu ya kila siku.

Bila kupoteza muda, katika maisha kuna kipindi tunajikuta tunapendwa na wenzetu wa jinsia tofauti, hivyo wanatumia approaches mbalimbali kuweza kutupata. Lakini, yote ya yote tunaishia kuwachomolea mbali kwa sababu ambazo zinaweza kuwa ni kuwa kwenye mahusiano kwa wakati huo, kutokuwa tayari kuwa kwenye mahusiano, KUTOKUKUBALIWA tu jinsi ulivyo etc.

Je, yule mtu aliyekuwa anakusumbua kwa wakati huo anakupenda na anahitaji uwe mpenzi wake yukowapi/ alienda wapi, je bado anafanya attempts hadi sasa au ndo kila lenye marefu na mapana halikosi ncha.

Kwa upande wangu,
Wa kwanza,
Miezi kadhaa nilitokea kupendwa na mdada ambaye tulikuwa tukisoma chuo kimoja, mie nlimchukulia kama rafiki lakini ye kwangu aliniona ni zaidi ya rafiki, kwakuwa sikutaka kumuumiza ilibidi nimuambie nina mke na mtoto hivyo acheki ustaarabu sehemu nyingine.

Mwishowe, kutokana na kumkataa kinamna hiyo akafuta namba yangu since then hakuna chocho yeyote ya chuoni ambayo nlikuja kumuona, since mwezi wa tano hadi namaliza muhula wa pili sikuwahi ing`aza sura yake popote wakati ilikuwa ni mara nyingi tunakutana cafeteria na madarasani.

Wa pili,
Huyu alikuwa ni muuza chispi mtaani kwetu, alikuwa akija kuomba chenji dukani kwetu, namba yangu nliichukua kimasihara tu tukawa tukiwasiliana siku hadi siku, mwishowe akaanza leta nyeusi ,tukashindwana anakanipiga chini mazima, tangu mwaka jana mwezi wa kumi na moja sijawahi kumuona na pale kijiweni kwake hayupo na sms zangu huwa hazifiki.

Wa tatu,
Huyu alikuwa anaitwa Mary, mdada mpole black beauty wa Mbeya, tulikutana advance minikiwa darasa moja mbele yake. Tulifamiana kupitia UKWATA nikiwa mdau mzuri wa maombi na tukaja soma wote tena Central Zone Chuo, alikuja kuanza kuleta habari za kwenda kutambulishana kwetu na kugandana gandana kama kupe. Akaja nipiga chini 2019 February majira ya saa 6 na madakika usiku. Hadi leo sijui yukowapi na sijawahi kumuona tena.

JE, uko tayari kumpa chance kama akija na kutaka aendelee alipoishia????

NB:
Hizo ni baadhi tu nami kuna ambao niliwataka na kufanya kila mbinu ila sijawahi kuwa nao.
Nimetumia lugha isio rasmi kwa wale walimu wa viswahili mtaniwia radhi.

TUPIGE KAZI, TUTAFUTE PESA!!!!!!
 
Daah umenifanya nicheke mleta uzi, asee kuna mdada alikuwa shemeji yangu(nilikuwa nadate na dada yake). Mara akaanza kuniletea habari sio nikawa namtolea nje na kumpa ushauri kadhaa kuhusu maisha yake ya mbeleni na atie bidii katika masomo(kipindi hicho alikuwa form six).

Kwa muda wa miaka kama mitano hatukuwahi kuwasiliana hivi juzi kanitafuta ananiambia kashinda umiss mkoa X. Ananitambia mpaka basi amasema mimi sikuona uzuri wake ila jamii imeuona nilibaki kucheka sana.
 
Daah umenifanya nicheke mleta uzi, asee kuna mdada alikuwa shemeji yangu(nilikuwa nadate na dada yake). Mara akaanza kunletea habari sio nikawa namtolea nje na kumpa ushauri kadhaa kuhusu maisha yake ya mbeleni na atie bidii katika masomo(kipindi hicho alikuwa form six). Kwa muda wa miaka kama mitano hatukuwahi kuwasiliana hivi juzi kanitafuta ananiambia kashinda umiss mkoa X. Ananitambia mpaka basi amasema mimi sikuona uzuri wake ila jamii imeuona nilibaki kucheka sana.
Tafuna miss huyo mkuu uweke rekodi 😄
 
Tafuna miss huyo mkuu uweke rekodi 😄
Hamna mkuu, namheshimu sana dada yake thou tushaachana ila tumebaki kama binadamu tuliotoka mbali(kipindi wote hatuna kitu). Hata nikiwa na mtu huwa namchana mapema kuwa kuna mtu muhimu katika maisha yangu anatakiwa kuelewa sio aje kuona namsaidia vihela kadhaa au tunapigiana simu alete mbwembwe.
 
Daah umenifanya nicheke mleta uzi, asee kuna mdada alikuwa shemeji yangu(nilikuwa nadate na dada yake). Mara akaanza kunletea habari sio nikawa namtolea nje na kumpa ushauri kadhaa kuhusu maisha yake ya mbeleni na atie bidii katika masomo(kipindi hicho alikuwa form six). Kwa muda wa miaka kama mitano hatukuwahi kuwasiliana hivi juzi kanitafuta ananiambia kashinda umiss mkoa X. Ananitambia mpaka basi amasema mimi sikuona uzuri wake ila jamii imeuona nilibaki kucheka sana.
Vipi mkuu umemuacha salaama
 
Hamna mkuu, namheshimu sana dada yake thou tushaachana ila tumebaki kama binadamu tuliotoka mbali(kipindi wote hatuna kitu). Hata nikiwa na mtu huwa namchana mapema kuwa kuna mtu muhimu katika maisha yangu anatakiwa kuelewa sio aje kuona namsaidia vihela kadhaa au tunapigiana simu alete mbwembwe.
Yeaah ni kweli kaka
 
Naweza sema ni mwanaume aliyenipenda kuliko wanaume wote niliowahi tongozwa ama kuwa nao kimahusiano, ila moyo wangu kwake ukawa mzito hakushtua hisia zangu na kwa maadili na wema wake kwangu nikaona iko siku nitamuumiza na kuweka kumbukumbu mbaya kwake, nikamkataa, kuna wakati ilikuwa karibu kabisa anioe.

Mwaka huu Feb nikachomoa mazima, alisikitika mno, Baada ya muda mama Samia akamlambisha uteuzi, kila la heri kwake.
 
Naweza sema ni mwanaume aliyenipenda kuliko wanaume wote niliowahi tongozwa ama kuwa nao kimahusiano, ila moyo wangu kwake ukawa mzito hakushtua hisia zangu na kwa maadili na wema wake kwangu nikaona iko siku nitamuumiza na kuweka kumbukumbu mbaya kwake, nikamkataa,,, Kuna wakati ilikuwa karibu kabisa anioe,

mwaka huu Feb nikachomoa mazima, alisikitika mno,,........ Baada ya muda mama Samia akamlambisha uteuzi, kila la heri kwake
Hahahahhaha hilo nifungu la kukosa dadaangu
 
Mimi nina tu visa twingi miaka imepita ila kuna mmoja tu najua alitoroka kwao akaenda olewa mimi sikuepo huko nyumbani niko zangu masomoni, aliolewa huko Katavi kwa kina MAYOMBI.

Huyu alinipiga kitu kizito kichwani ndiyo nikiwa nakaribia kumaliza paper langu la mwisho chuoni, daah sitasahau nikiri tu yakua nlkua nampenda sana basi tu haikua ridhiki.. Angelisubirigi hata nimalizage mtihani tu make si kwa maumivu yale afu mnyama UE yupo mbele umebaki muda wa lala salama.
 
Naweza sema ni mwanaume aliyenipenda kuliko wanaume wote niliowahi tongozwa ama kuwa nao kimahusiano, ila moyo wangu kwake ukawa mzito hakushtua hisia zangu na kwa maadili na wema wake kwangu nikaona iko siku nitamuumiza na kuweka kumbukumbu mbaya kwake, nikamkataa,,, Kuna wakati ilikuwa karibu kabisa anioe,

mwaka huu Feb nikachomoa mazima, alisikitika mno,,........ Baada ya muda mama Samia akamlambisha uteuzi, kila la heri kwake
Aiseee hii ndo mkataa pema pabaya pamuitaa au hadi huko Bado ni kwema
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom