Dunia hii kuna watu wazuri sana ila sio wengi

Black poison The Factor

JF-Expert Member
May 31, 2020
852
1,256
Wakuu I hope mko shwari kabisa.

Kuna jambo liliwahi kunitokea kipindi mdogo, na sijawahi kulisahau mpaka Leo.

Siku ya kwanza kabisa mimi kupelekwa shule, nilifanyiwa kitendo cha ajabu sana na dada yangu mtoto wa mama mkubwa.

Nakumbuka ilipofika saa nne muda wa mapumziko, katika kutembeatembea pale shuleni nikamuona dada na wanafunzi wengine pale, kwa furaha kabisa nikawa naenda pale nikamsalimie.

Wakati naenda yeye hakuniona ila kuna mtoto wa bamkubwa wake alimwambia umemuona mdogo wako ameanza shule?

Ndo akaniona sasa, aisee alisonya halafu akamwambia yule dada yake kwamba, Mimi kwetu nimezaliwa peke yangu wala sina mdogo wa hivyo, yule mwenzake akamwambia si mtoto wa mama mdogo wako? akasema haimuhusu.

Aisee nilipata aibu ya kufa mtu nguvu zikaisha, akili ikawa haifanyi tena kazi nikawa nimeduwaa tu pale. Huku najuta nilifata nini pale kidogo nilie kabisa, alafu ukizingatia m bado mtoto kabisa alafu wao
ni wakubwa.

Sasa pale kulikua na mdada mwanafunzi mwenzao darasa la saba, alivyoniangalia akanisalimia ., alafu akamwambia dada yani una mdogo mzuri hivi unamkataa??

Yule dada akamwambia una laana ww mm siwezi kumkataa mdogo wangu. akasema tena angekua wakwetu huyu mngenitambua.

Sasa kuna mmama alikua anauza vitumbua pale na dada angu alikua amenunua kama vinne hivi akaambiwa mpe mdogo wako basi akasema kama hajaja na hela imekula kwake.

Yule dada nisiemjua akatoa mia mbili akanipa ninunue ila nikakataa, nikamwambia nmeshiba, itakua alijua kua siko sawa akavinunua yeye alafu akanisindikiza akaenda kunipa kule mbele huku akinipa pole kwa yaliyotokea,
Nikachukua nikarudi darasani. Vilikua vinauzwa 50/50 ni muda kidogo.

Yule dada akawa rafiki yangu kila siku ananitafta tunasalimiana, hata mitihani yangu alikua anaangaliaga, kifupi alikua mtu poa sana kwangu.

Isivyo bahati alinasa mimba aisee akaacha shule na sijawahi kumuona tena mpaka Leo, sjui hata aliendega wapi ni zaidi ya miaka 24 sasa, ila natamanigi sana nmuone nimpe zawadi yeyote ile maana alinisitiri sana.

Huyu dada angu sasa hivi amekuwa muhimiza upendo kweli alafu hajui kwamb sjasahaug alichonifanyia, ila mama mkubwa wangu yuko poa sana mme wake pia Sasa sjui mtoto wao ile roho aliitoa wapi, maana ulafi pale ndo makao makuu yake.

Kama nawewe una uliwahi pigwa tukio karibu
 
Sometimes inakuaga ni utoto tu.

Mimi nna bro wangu alikua ananikataa sana, hataki tuongozane full kunikosoakosoa, full kupigana (ni kupigwa maana alikua ananidunda kweli).

Ila saivi tuko poa, ndo ananiokoa sana sana kwenye majanga.
Zamani wakubwa walikua hawatuelewi maana madogo sometimes ni wanoko.
 
Hatar mkuu alafu akija hom anatak kunipiga mizinga, kuna kipindi aliniambia nimwachie smart yangu kidogo nmtukane
Hii nayo ni shida nyengine,kwanini utumtukane?

Unaposema ”Dunia hii kuna watu wazuri sana ila sio wengi” jitahidi na wewe uwe mmoja wa hao wachache ili wengine waige dunia iwe nzuri kwetu sote sasa wewe unamsifia mtu kitu ambacho huwezi kukifanya?kumbe siku ile uliponunuliwa vitumbua hakuna ulichojifunza pale eti?!
 
Hii nayo ni shida nyengine!!!

Unaposema ”Dunia hii kuna watu wazuri sana ila sio wengi” jitahidi na wewe uwe mmoja wao ili wengine nao waige dunia iwe nzuri kwetu sote sasa wewe unamsifia mtu kitu ambacho huwezi kukifanya,kumbe siku ile uliponunuliwa vitumbua hakuna ulichojifunza pale!!!
Nilijifunza kua wa kukuthamn sio lazm awe ndugu, so tuish kwa wema
 
Sometimes inakuaga ni utoto tu.

Mimi nna bro wangu alikua ananikataa sana, hataki tuongozane full kunikosoakosoa, full kupigana (ni kupigwa maana alikua ananidunda kweli).

Ila saivi tuko poa, ndo ananiokoa sana sana kwenye majanga.
Zamani wakubwa walikua hawatuelewi maana madogo sometimes ni wanoko.
Sasa m pale nilikua naenda tu kumpa hai reaction yake ikawa tofaout mkuu
 
Sometimes inakuaga ni utoto tu.

Mimi nna bro wangu alikua ananikataa sana, hataki tuongozane full kunikosoakosoa, full kupigana (ni kupigwa maana alikua ananidunda kweli).

Ila saivi tuko poa, ndo ananiokoa sana sana kwenye majanga.
Zamani wakubwa walikua hawatuelewi maana madogo sometimes ni wanoko.
Itakuwa mli kuwa Mna gombea u katibu wa banyeta😆🤣
 
Wakuu I hope mko shwari kabisa.

Kuna jambo liliwahi kunitokea kipindi mdogo, na sijawahi kulisahau mpaka Leo.

Siku ya kwanza kabisa mimi kupelekwa shule, nilifanyiwa kitendo cha ajabu sana na dada yangu mtoto wa mama mkubwa.

Nakumbuka ilipofika saa nne muda wa mapumziko, katika kutembeatembea pale shuleni nikamuona dada na wanafunzi wengine pale, kwa furaha kabisa nikawa naenda pale nikamsalimie.

Wakati naenda yeye hakuniona ila kuna mtoto wa bamkubwa wake alimwambia umemuona mdogo wako ameanza shule?

Ndo akaniona sasa, aisee alisonya alafu akamwambia yule dada yake kwamba, Mimi kwetu nimezaliwa peke yangu wala sina mdogo wa hivyo, yule mwenzake akamwambia si mtoto wa mama mdogo wako? akasema haimuhusu.

Aisee nilipata aibu ya kufa mtu nguvu zikaisha, akili ikawa haifanyi tena kazi nikawa nimeduwaa tu pale. Huku najuta nilifata nini pale kidogo nilie kabisa, alafu ukizingatia m bado mtoto kabisa alafu wao
ni wakubwa.

Sasa pale kulikua na mdada mwanafunzi mwenzao darasa la saba, alivyoniangalia akanisalimia ., alafu akamwambia dada yani una mdogo mzuri hivi unamkataa??

Yule dada akamwambia una laana ww mm siwezi kumkataa mdogo wangu. akasema tena angekua wakwetu huyu mngenitambua.

Sasa kuna mmama alikua anauza vitumbua pale na dada angu alikua amenunua kama vinne hivi akaambiwa mpe mdogo wako basi akasema kama hajaja na hela imekula kwake.

Yule dada nisiemjua akatoa mia mbili akanipa ninunue ila nikakataa, nikamwambia nmeshiba, itakua alijua kua siko sawa akavinunua yeye alafu akanisindikiza akaenda kunipa kule mbele huku akinipa pole kwa yaliyotokea,
Nikachukua nikarudi darasani. Vilikua vinauzwa 50/50 ni muda kidogo.

Yule dada akawa rafiki yangu kila siku ananitafta tunasalimiana, hata mitihani yangu alikua anaangaliaga, kifupi alikua mtu poa sana kwangu.

Isivyo bahati alinasa mimba aisee akaacha shule na sijawahi kumuona tena mpaka Leo, sjui hata aliendega wapi ni zaidi ya miaka 24 sasa, ila natamanigi sana nmuone nimpe zawadi yeyote ile maana alinisitiri sana.

Huyu dada angu saiv amekua muhimiza upendo kweli alafu hajui kwamb sjasahaug alichonifanyia, ila mama mkubwa wangu yuko poa sana mme wake pia Sasa sjui mtoto wao ile roho aliitoa wapi, maana ulafi pale ndo makao makuu yake.

Kama nawewe una uliwahi pigwa tukio karibu
Yes,
Kuna Watu na Viatu humu Duniani 🐒

R.I.P Laigwanani comrade ENL
 
Tangu nianze Jf kuna watu nimejua wana moyo mzuri Kabisa ila kuna mtu anamoyo mzuri sana kwangu National Anthem ulitoa gharama za kuuguza bibi yangu aliyenilea tangu nikiwa 2 years old mama alivyoniacha kwake,japokuwa mama alikuja kunichukua nikiwa 11years old lakin grandmaa she is my everything......Mwenyezi Mungu akubariki sana popote ulipo bro🙏🏽
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom