Yuko wapi Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango?

Fumadilu Kalimanzila

JF-Expert Member
Dec 10, 2016
1,651
5,122
Ni muda kidogo huyu Makamu wetu wa Rais Dr. Philip Isdor Mpango hajasikika!

Huyu ni Mchumi japo mimi binafsi sina imani na aina ya uchumi anaosimamia ( uchumi wa kijamaa).

Inavyoonekana huyu Makamu wetu wa Rais Dr.Mpango ana mchango mkubwa sana katika kupatikana kwa mchumi mwingine katika nafasi ya Waziri wa fedha Dr.Mwigulu Lameck Nchemba.

Dr.Mwigulu ni mchumi ambaye mimi binafsi sijui na siwezi kusema kwa hakika ni aina gani ya uchumi anaosimamia zaidi ya nadharia za kukariri ( economic models za kukariri )! Naweza kusema kwa kipindi kifupi hiki ambacho amekuwa Waziri wa Fedha amejitanabaisha kama mchumi wa makaratasi,asiye na ubunifu wowote wenye kuleta tija na unafuu katika maisha ya Watanzania zaidi ya kero na ufukara wa kutisha kwa Wananchi!

Hapo ndipo kiu ya kumsikia Dr.Philip Isdory Mpango kama mchumi imechagizwa sana na hili ombwe ambalo liko wazi na hali hitaji kujua rocket science kwamba the boat is sinking!

Dr.Mwigulu amekuja na ubunifu wa ajabu ajabu wa UCHUMI WA TOZO na bado anaendelea na ndoto za ajabu ajabu!

Ameanza na tozo za miamala ya simu na tena sasa anaelekea kwenye digital platform zingine!

Kwa kifupi Dr.Mwigulu amekuja na UCHUMI WA TOZO!
Miezi miwili amepata michango (TOZO) za kiasi cha Bilioni 63 ( Fedha za Wananchi na si kodi zitokanazo na uzalishaji).Yaani hizi fedha ni mitaji, faida baada ya kodi za wananchi zinazohamishwa kutoka point A kwenda point B na Waziri " anazivizia kwenye miamala" na kuzichukua tena!

Kabla sijaenda mbali naomba wafuatao watambue yafuatayo:-

Mosi, CCM- tambueni kuwa aina hii ya "UCHUMI WA TOZO " ambao mmemruhusu Dr.Mwigulu kwenda nao kwa Wananchi ni uthibitisho kuwa kuendesha Nchi kumewashinda!

Wananchi waliwapa kura (Serikali) baada ya kuwashawishi kuwa mnao uwezo wa kuendesha Nchi na rasilimali zao na kuwaletea tija na unafuu katika maisha yao badala yake mmeshindwa na sasa mnaendesha Nchi kwa michango ya Wananchi (Tozo)!

Hatuoni ubunifu wa Waziri wa Fedha ( Mchumi wa PHD) katika kubuni miradi ya uzalishaji kwa kushirikiana na Mawaziri wengine kama wa Kilimo, Madini, Uwekezaji, Maliasili n.k.
Badala yake yeye anawaza TOZO TU!

Tozo ni dhuluma kwa Watanzania kwa kile kidogo walichobakiwa nacho baada ya kuporwa kikubwa chao!

Ebu fikiria Mwalimu anayeangaika mwezi mzima kupata mshahara ghafi ( gross salary) ya milioni moja (1M) akikatwa kodi ((PAYE) akabakiwa mathalani na laki nane ( laki 8), bado akitaka kuwasaidia watoto wake wanaosoma mbali na nyumbani au wategemezi wake wengine kwa kuwatumia fedha kwa njia ya miamala ya simu anakatwa tena TOZO kubwa kwenye miamala hiyo!

Huu ni UNYONYAJI wa kutisha! Katika kipindi ambacho uchumi wa Wanananchi umeporomoka kutokana na COVID- 19 , ungetegemea tupate viongozi wanaokuja na ubunifu hata wa kuwapa Wananchi unafuu (ruzuku) badala yake tumepata Wachumi nguli duniani kwa kubuni TOZO!!

Kwa kweli Wachumi (PhDs) Dr.Mpango na Dr. Mwigulu kwa muda mfupi mlioshika nafasi katika Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan mmepoteza mwelekeo kwa kasi ya mwanga ( the speed of light)!

Na katika hili huku mtaani kwetu Wananchi wameanza kumkumbuka sana Hayati Dr. John Pombe Joseph Magufuli!
Angalau Dr.Magufuli japo hakuwa mchumi kama nyie lakini mwelekeo na ubunifu wake ulionekana!!
Alijizungushia maukuta yake kule Mirerani, aliwabana Wawekezaji wakubwa kama Barrick na kuanzisha masoko ya madini kila mkoa n.k na mipango yake ilienda na kila alipopata nafasi alituambia " PESA ZIPO" ! na hakuwaza kuwawekea Watanzania MATOZO ya ajabu ajabu kama haya ya Dr.Mwigulu.

Rais Samia akimaliza kurekodi Tamthiliya yake ya Utalii afanye tathmini katika sekta tu ya madini kama hajashangazwa na utoroshaji wa madini kwenda nje baada ya kifo cha Dr.John Pombe Joseph Magufuli!

Kwahiyo niseme Dr.Mwigulu na Serikali yenu mnachofanya ni "at the risk ya kura za CCM comes 2025"!
" Watanzania hawa si Wajinga by JPM"!

Pili,Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan, tambua kuwa ulianza vizuri sana na ukasifiwa na wengi sana! Lakini kama miezi 3 nyuma kidogo umepoteza mwelekeo na inavyoonekana kuna watu wanakupoteza kwa makusudi kwa manufaa wanayoyajua wao! Ama unajua ama hujui but it will be too late for you my Mom! My President!

Chukulia hata ili dogo tu la juzi la GWAJIBOY!!!!!!!
Aliyekushauri usimame Tegeta na umpromoti GWAJIBOY mwangalie mara mbili mbiili! Ilikuwa ni total miscalcution of the life time!!!

Sidha kama Rais wangu ulifuatilia hata mawasilisho ya Bunge kuhusu GWAJIBOY !!!

GWAJIBOY mpaka sasa ameshinda na kampeni yako ya chanjo ya COVID- 19 imedoda kwani Chupa/Chanjo milioni moja mwishowe zita- expire maana mwamko wa kuchanja hakuna na waliochanja hawazi laki 4 ( niko tayari kupokea takwimu mpya kama zipo)!

Bunge lilifanya kazi nzuri sana ya kukuheshimisha Mheshimiwa Rais, wewe ukalifanyia ulivyofanya kwa kumpromoti GWAJIBOY!!!!
Mimi bila hofu kabisa nasema, My President your act undermined the Parliment.!!!

Lingine Mheshimiwa Rais kuwa macho sana hawa wasaidizi wako,wengine ni wapenda sifa watumia nafasi zao kujijenga kwa ajili ya Urais hapo baadaye bado sina hakika kama ni kwa ajili ya 2025 au 2030!

They are trying to colour you as an unpopular President ever! ,
" Be eyez" and watch it Madam President!
 
Jaribu kukua kidogo kiakili! Siongelei physical presence, naongelea mental presence!
Jaribu nawe kupunguza hizo akili zisizowaza kabla ya kuandika.

Makamu wa Rais ni kivuli cha Rais sasa unataka ajitokeze aanze kupiga kelele wakati mkuu wake yupo. Makamu wa Rais anaenda sawa na mkubwa wake akilala analala, akisimama anasimama, akikakaa anakaa.

Wakati wa JPM uliwahi kuona Mh. Samia anafanya jambo gani lililoteta tija kwa wananchi?
 
Mkuu hongera kwa mada mzuri. Kwa ujumla sijaona waziri wa fedha ambaye yupo committed na wenye NCHI. Kwa hali tuliyonayo tulitegemea waziri wa fedha ambaye angepambana vyema na bajeti ya Serikali katika kuwapa unafuu wenye NCHI kwa kupunguza matumizi makubwa ya Serikali, kutafuta mbinu mbadala za kukomesha ubadilifu, upotezu na wizi wa fedha na mali za Serikali.

Huyu tuliyenaye baada ya kukaa BoT kwa muda, muda mwingi alikuwepo kwenye Chama.
 
Serikali hii ni aibu tupu. Makamu wa rais wa Nigeria alikuwepo Arusha na kama sikosei ameondoka leo kurejea Nigeria.

''Vice President Yemi Osinbajo, yesterday, left for Arusha, Tanzania, where he was received by his Tanzanian counterpart, Dr. Philip Mpango.

A statement by Senior Special Assistant (SSA) on Media and Publicity, Laolu Akande, said during the short stay Osinbajo would visit the African Court of Justice and Human Rights (ACJHR), an African Union agency sited in the city in addition to other engagements before returning to Abuja on Monday.''

 
Mtu mwenye PhD anapaswa kua mbunifu lkn Hawa wakwetu wamekariri economic modals za nji za ulaya mashariki na kutaka zifanye kazi Tanzania.
Ni ishara Tanzania Kuna PhD nyingi za ku plagiarise. Almaaruf copy and paste
 
Back
Top Bottom