Yu Wapi Askari Mkama Sharp?

Sio Mkamashamu ila ni Mkama Sharp, alikua ni Corporal yaani mwenye V mbili begani. Huyu alishafariki dunia na kuzikwa kwao mkoa wa Mara.

Duh, MMUNGU ailaze roho yake mahali pema peponi. Yaani huyu jamaa alikuwa anawasaidia sana madenti pale Kariakoo. Ukifika pale na Mkama Sharp yupo, basi unauhakika wa kufika nyumbani mapema.
 
Kuna Polisi alikuwa anaitwa Sabasita Kimaro kule Arusha huyu naye alikuwa mbabe balaa.
 
Ni mkama sharp. Kariakoo ilala mpaka Msimbazi mission quarters yote walikuwa wanamjua. Ni kweli alikuwa mdau wa mchiriku lakini ilikua ni mbinu ya kumsaidia kukamata wahalifu!
 
Na Caroli wa stend Mwanza,Enzi hizo kulikuwa na polisi commted kweli,bahati mbaya wengi wao walikufa wakiwa ni maskini wa kutupwa,waliobaki wengi ni mababu wanalinda kwa virungu maduka ya wahindi.
 
Kuna mwingine aliwahi kuvuma miaka hiyo mikoa ya Kaskazini aliitwa 'Saba-Sita' mwenye taarifa atujuze tafadhali

sijui yupo au lah ila kwa shabaha alikua anatisha,majambazi sugu wastaafu taarifa zake wanazo,wengi wao aliwauwa!Enzi ya Mahita na Chico walimtumia sana kuweka heshima Moshi
 
Kuna mwingine aliwahi kuvuma miaka hiyo mikoa ya Kaskazini aliitwa 'Saba-Sita' mwenye taarifa atujuze tafadhali
PATRICK%2BKIMARO%2BSABA%2BSITA%2BNAGAWA%2BCHAI%2BKWA%2BWAETHIOPIA%2B103%2BKTK%2BMAHAKAMA%2BYA%2BHAKIMA%2BMKAZI%2BMORO%2BPIX%2BNO%2B4.JPG


sabasita in red shirt

 
jamaa nakumbuka siku moja nimesimama pale chang'ombe kituo cha basi jamaa kawafunga mashati watu kama 20hivi wasela wa mikoroshini wanaelekea kituoni,wote mstari mmoja mnyoofu naye yuko nyuma mbali kabisaa..
jamaa alikuwa kiboko...
 
Kamanda ALFRED TIBAIGANA....[Mtahalamu wa sheria} Alikuwa na roho nzuri sana ,siku moja kwao mapolisi waliingia kijijini kwake kukamata watengeneza/wauzaji wa pombe za kienjeji [a.k.a NKONYAGI) kwa nguvu ,pia kuwanyang'anya pesa...,siku hiyo alikuwa likizo alikamata mapolisi wate waliokuwa kwenye diffender, kunyanganya bunduki na koffia,,,akiwashutum kwanini wanakamata raia masikini na kuwaacha wezi kibao waliokijijini kwao....tangu siku hiyo pombe za kienyeji akawa halali.2008 nilikwenda ofisin kwake nikawa sinapesa boom lilikuwa limekwisha...akanipa laki moja na kunikatia tiketi ya ndege kwenda kwetu....hata nilisikia mapolisi wengi wakimsifia kwa kusikiliza matatizo yao nje ya kazi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom