Yu Wapi Askari Mkama Sharp?

Mambo ya Daslam, nimekumbuka wauza minazi pale ubungo mataa pamoja na soko kubwa tu la bidhaa mbalimbali(ilipo stendi ya daladala), kulikuwa na hoteli opposite na Olicom pale Tanesco wale Wapemba walikuwa wanauza Kashata na kalimati balaa.
 
Dah! Sharp... kitambo sana! Sie watoto wa Temeke habari ya Sharp ilikuwa Taifa bhana!! Ilikuwa Sharp akitimba Taifa, haina kuruka ukuta hiyo!!
 
Mara ya mwisho kumuona alikuwa osteray polisi miaka ya 2004/2005 alikuwa na cheo cha major(staff sajent),kwa kijeshi
Miye pia nolimuona ostabey 2002 alikuwa anatutambia yeye ni meja anapata lak 2 hapa mjini hakuna wa kumbabaisha.
 
Sharp alikufa kitambo SANA......adhanidakaga na akanileta kituo cha polisi mtambani badala ya kunipekeka obay.....wakanitoa hela....
Sharp alikuwa kwenye payrol ya wauza ng@da Kino tena aliwalinda SANA...
Nlikuja onana naye tena Yuko hoi anaumwa maana ilisemekana aliukwaaaaa.....akanipiga mzinga nkamkaziaaa

OVA
 
Kwa wale wakazi wa Dar kuanzia miaka ya mwishoni mwa `1980 na mwanzoni mwa miaka ya 1990 pale kituo cha polisi Msimbazi kulikuwa na askari mmoja mkakamavu kwelikweli ambaye alikuwa kiboko cha makonda na madereva jeuri na sugu wa daladala,wakati wote alikuwa akitembea na vitendea kazi vyake muhimu kama vile bastola,pingu na rungu huku buti zake zikishine na uniform zake zikiwa safi na zimepigwa pasi kwa kutumia wanga,hata inzi alikuwa anaogopa kutua kwenye nguo zake,yuko tofauti na askari wa siku hizi ambao wanavitambi,uniform chafu na sifa yake kuu ilikuwa ni UKAKAMAVU NA KUTOCHUKUA KITU KIDOGO,alikuwa ahongeki.

POLE SANA MKUU MKAMA SHARP AMBAYE ALIKUWA AKITEMBEA SANA MITAA KARIAKOO KONGO MASIMBAZI AKIWA NA PINGU KIRUNGU PISTOL NA ALIKUWA FIT KWA NGUMI JUDO KARATE NA MENGINEYO ALISHAFARIKI MIAKA MITATU AU MIWILI ILIYOPITA TENA ALIFARIKI GHAFLA KWA HOMA KALI NA KAMA NAKUMBUKA VIZURI AMEFARIKI AKIWA NA CHEO CHA NYOTA MOJA AU SSGT. NIKO TAYARI KUKOSOLEWA KAMA WASIFU WAKE NIMEUKOSEA ILA NI HAKIKA ALISHATUTANGULIA MBELE ZA HAKI.
 
MAREHEMU MKAMA SHARP
 
Wakuu habari,

Wale watoto wa mjini wa enzi hizo miaka ya tisini hili jina la mkamashamu hakuna asiyekuwa analijua
ni polisi machachari ambaye hajawahi tokea kwa Tanzania.

Mkama Sharp huyu bwana alikuwa anabeba pingu, kirungu, bastola, smg zote yeye tu na zote kazining'iniza.

Mkama sharp huyu huyu alikuwa anaweza kwenda kukamata kundi la vibaka hata ishirini na wote akawafunga mashati na kuwapeleka mpaka polisi.

Mkama Sharp huyu alikuwa akikaa uwanja wa taifa kwenye mechi kubwa kubwa kulikuwa hakuna cha vurugu wala kukuru kakara za siku hizi.

Mkama Sharp huyu huyu alikuwa akisema sitaki vurugu watu walikuwa wanatuli autafikiri wamemwagiwa maji ya moto.

Mkama sharp alipotea ghafla na kuna conspirancy kibao kuhusu Mkama sharp,wengine wanasema yuko jela sasa hivi wengine wanasema amekwishafariki.

Wale wanaomkumbuka huyu jamaa nani anaweza kutuambia yuko wapi huyu jamaa na sifa zake ambazo bado ziko kwenye memory ya kichwa chako waweza ku share na sisi.

Karibuni kwenye mada........
MKAMA SHARP ALISHAFARIKI KARIBU MIAKA MITATU ILIYOPITA NA ALIZIKWA KWAO MKOANI MARA ILA ALIKUWA SHARP KWELI .
 
POLE SANA MKUU MKAMA SHARP AMBAYE ALIKUWA AKITEMBEA SANA MITAA KARIAKOO KONGO MASIMBAZI AKIWA NA PINGU KIRUNGU PISTOL NA ALIKUWA FIT KWA NGUMI JUDO KARATE NA MENGINEYO ALISHAFARIKI MIAKA MITATU AU MIWILI ILIYOPITA TENA ALIFARIKI GHAFLA KWA HOMA KALI NA KAMA NAKUMBUKA VIZURI AMEFARIKI AKIWA NA CHEO CHA NYOTA MOJA AU SSGT. NIKO TAYARI KUKOSOLEWA KAMA WASIFU WAKE NIMEUKOSEA ILA NI HAKIKA ALISHATUTANGULIA MBELE ZA HAKI.
Alifariki alipokuwa anatoka kuchukua nyota alikuwa muda mwingi yupo kituo kidogo cha Kinondoni Mtambani.
 
Wakuu habari,

Wale watoto wa mjini wa enzi hizo miaka ya tisini hili jina la mkamashamu hakuna asiyekuwa analijua
ni polisi machachari ambaye hajawahi tokea kwa Tanzania.

Mkama Sharp huyu bwana alikuwa anabeba pingu, kirungu, bastola, smg zote yeye tu na zote kazining'iniza.

Mkama sharp huyu huyu alikuwa anaweza kwenda kukamata kundi la vibaka hata ishirini na wote akawafunga mashati na kuwapeleka mpaka polisi.

Mkama Sharp huyu alikuwa akikaa uwanja wa taifa kwenye mechi kubwa kubwa kulikuwa hakuna cha vurugu wala kukuru kakara za siku hizi.

Mkama Sharp huyu huyu alikuwa akisema sitaki vurugu watu walikuwa wanatuli autafikiri wamemwagiwa maji ya moto.

Mkama sharp alipotea ghafla na kuna conspirancy kibao kuhusu Mkama sharp,wengine wanasema yuko jela sasa hivi wengine wanasema amekwishafariki.

Wale wanaomkumbuka huyu jamaa nani anaweza kutuambia yuko wapi huyu jamaa na sifa zake ambazo bado ziko kwenye memory ya kichwa chako waweza ku share na sisi.

Karibuni kwenye mada........
Alifariki baada ya kuugua kwa muda mrefu
 
Dah!Mkuu umenikumbusha mbali sanaaaa,wkt nasoma primary pale uhuru siku moja nikasukumwa kwenye daladala nikaanguka kumbe Mkama Sharp alikuwa hapo,aisee abiria wote walishushwa gari nzima tukapakia wanafunzi.Dah siwezi msahau huyu bwana
Kumbe mdogo sana
 
Interesting story police wa leo mtakumbukwa kwa lipi? Hata jeshi la magereza alikuwepo mmoja mfia jeshi huyu alikuwa mkufunzi chuo cha magereza kiwira mwenye story zaidi za huyu jamaa aje atiririke. Alikuwa na maarufu kwa jina la SEITUNDU KAMANDA NGUVU YA NYANI.
 
ASKARI MWINGINE ALIYETUSUMBUA ALIKUWAGA HAPI CENTRAL MAARUFU KAMA KOBA KABANDA....ALIKUWA ANAJIFANYA NGUMI JIWE ASHANINYANGANYA SIM MITAA YA AZAM KWA YAHYA .....HIVI BADO YUPO CENTRAL.

OVA
 
Interesting story police wa leo mtakumbukwa kwa lipi? Hata jeshi la magereza alikuwepo mmoja mfia jeshi huyu alikuwa mkufunzi chuo cha magereza kiwira mwenye story zaidi za huyu jamaa aje atiririke. Alikuwa na maarufu kwa jina la SEITUNDU KAMANDA NGUVU YA NYANI.
Mara nyingi wanaishia kuwacha misifa....askari inategemea unaishi Vp n'a jamii
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom