Kwanza kabisa napenda niwashukuru watu wote ambao mmeamua kuchukua muda wenu kusoma uzi huu, wale mliochangia, wale mliochukua hatua zaidi kunipigia kutaka ufafanuzi, nimepata PM na simu toka nje ya nchi pia, kama India, UK, na Ujermani, watu wana kiu ya kuona wanatimiza malengo yao kwa muda mfupi, kuna wale waliondoa woga, wakachukua hatua kuja ofisini tukaonana uso kwa uso, walioudhuria darasa la Ijumaa, wakajionea kwa macho kile kinaachonekana kama ni ndoto, wapo waliochukua maamuzi magumu na kuanza safari ya kuona malengo yao yakitimia, nyumba na gari ni sehemu tu ya vile ambavyo mtu anapata, kuna malipo kadhaa ya kila mwisho wa mwezi, kulingana na kazi mliyofanya.
Kipekee niwashukuru wote mliotoa changamoto, ama critics, kuponda, kutokuamini, kufananisha na jinamizi flani kumenifanya niende maili moja zaidi, mmenipa changamoto ya kuona kuna haja mjadala huu ukapanuliwa zaidi, hii si kwa ndoto ndogo kama za gari na nyumba bali za kubadili mitazamo ya wengi kuhusu maisha na maono, tunahitaji mitazamo chanya, ninyi mmenifanya nianze kupekua maktaba yangu na kuanza kutafuta cha kuandika, lengo likiwa ni jinsi gani kama taifa watu wanaweza wakageuza mitazamo (MINDSET MAINTANANCE) na kuambukizana mitazamo chanya ama POSIBILITY MINDSET. Hii yaweza kuwa na FORUM yake hapa JF, ikiwa mod wataona inafaa. Kabla ya kuendelea na mjadala huu, tuangalie NDOTO/MAONO ni nini?
Katika kutafuta tafsiri ya NDOTO/MAONO tutaongozwa na maandiko matakatifu, Biblia, hii ndio dira kuu ama ramani kuu itakayotuongaza kupata tafsiri sahihi (bila shaka vitabu vingine vitakatifu vitakuwa na tafsiri, sina utalaamu navyo, waliona utaalamu navyo watatujuza), pamoja na Biblia tutaangalia pia watalaamu na waandishi mbalimbali wanasema nini juu ya ndoto/maono.
Ieleweke kuwa ndoto ama maono si ndoto zile tuotazo usingizini, haya si maono, je MAONO/NDOTO/NJOZI ni nini? Je Ina sifa gani? Biblia katika Habakuki 2:2-3 inasema "Bwana akajibu, akasema, iandike njozi hii ukaifanye iwe wazi sana katika vibao, ili aisomaye apate kuisoma kama maji. Maana njozi hii ni bado kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili kuufikila mwisho wake wala haitasema uongo, ijapokawia ingojee, kwa kuwa haina budi kuja, haitakawia."
Ukiangalia kwa makini neon hili utagundua vitu vingi sana, kwanza hii ilitokana na Habakuki kumlilia Mungu juu ya CHANGAMOTO zilizokuwa zilizokuwa zinalikabili taifa, akamlilia Bwana na Bwana akamjibu. Hivyo sifa mpjawapo ya maono au ndoto au njozi ni kutoa JAWABU kwa changamoto katika taifa au kanisa. Hii haiwezi kuwa kumiliki gari au nyumba, hizi si changamoto za taifa au kanisa, bali vyaweza fananishwa na kalamu, karatasi na meza na kiti, haya ni malupulupu tu.
Mungu anasema IANDIKE, si hivyo tu, anasema IWE WAZI sana, NZOJI ama MAONO yanakuwa makubwa sana na tena yanategemea zaidi ya mtu mmoja kutimia, tena yanarithishwa, hivyo kuiandika ni muhimu sana, ili utakayemshirikisha ama atakayerithi njozi hii aweze kuitambua kiurahisi kama mtu anyway maji. Mfano ni Mfalme Daudi, alikuwa na ndoto za kujenga hekalu la Bwana, moyoni mwake alidhamiria jambo hili, lakini ni mwanae Suleimani ndiye alijenga hekalu, hivyo maono ya Daudi yalitimizwa na mwanae Suleimani. (1 Wafalme 8:17-18)
"Njozi hii ni kwa WAKATI ulioamriwa" Njozi/maono/ndoto zina muda maalamu, hii ni sifa nyingine ya ndoto, gari au nyumba haviwezi kuwa ndoto, kwani waweza kuzipata hata kwa bahati nasibu tu, hata kama ni gari ya thamani kubwa kiasi gani, bado haiwezi kuwa ndoto kwani haina kitu inaweza kubadili katika taifa.
Njozi/ndoto/maono inahitaji sio muda tu, bali uvumilivu pia, IJAPOKAWIA INGOJE, kwa kuwa haina budi kuja, haitakawia. hii nayo ni sifa nyingine iliyo ya muhimu sana, SUBIRA, kwa kuwa ndoto au maono uja katika kipimo kikubwa sana, yawezekana ukaianza ndoto yako lakini usione ikifikia nusu ya mafanikio, kwa kuwa ulianza na mwisho mwanzo, hautakuwa na shaka kutimia kwake, kwani uliiandika kwenye vibao, wazi sana.
Maono/ndoto/njozi (vision) ni muhimu sana katika maisha ya binadamu, biashara, huduma, kanisa, nchi kwa sababu nchi, jamii, taifa, kanisa, shirika ama mtu pasipo maono hupoteza mwelekeo, maandiko yanasema, "pasipo maono watu huacha kujizuia, ama taifa uangamia"
Mtaalamu wa mambo ya uongozi, John Maxwell anaitafsiri NDOTO/MAONO hivi, "a dream is an INSPIRING PICTURE of the FUTURE, that energizes your mind, will, and emotions, empowering you to do everything you can to achieve it." A dream worth pursuing is a picture and blueprint of a person's purpose and potential.
Sharon Hull anasema, "A dream is the seed of possibility planted in the soul of a human being, which calls him to persue a unique path to the realization of his purpose." Sitotoa tafsiri katika haya, nikichelea kuharibu maana au kupunguza utamu wake.
Mtu asiye na ndoto ni sawa na masikini, lakini ni wa kuonea huruma na kumkomboa, kwani anafananishwa na meli kuubwa sana iliyotengenezwa kufanya kazi bahari, maji malefu, lakini yeye yu katika kuangaika na vidimbwi, si maneno yangu, bali ya Mwandishi Keneth Hildebrand, anasema, "The poorest men of all is not the one without a nickel to his name. he is the fellow without a dream, he is like a great ship made for the mighty ocean but trying to navigate in millpond." Hii si habari njema, mtu huyu anahitaji msaada, kumwonyesha bahari, anapopaswa kuwa.
Hildebard anaongeza, "one of the life's greatest tragedies is a person with a 10 by 12 capacity and a 2 by 4 soul." Haya ni majanga, una eneo kubwa sana, lakini unaona moyoni mwako eneo dogo sana, unaota ndoto ndogo sana, ujiamini, hauamini kuwa Mungu anaweza kukupa mambo makubwa sana. Maandiko yanasema "atukuzwe yeye awezaye kutenda mambo makubwa mno, Kuliko tuyaombayo au tuyawazayo"
Jambo la kuzingatia ni kuwa NDOTO/MAONO/NJOZI nit eke sana, hasa zinapokuwa mpya sana kwako, tena pale wale uwapendao na kuwaheshimu wasipokuelewa ama kukubariana na ndoto zako, mbaya zaidi unapokuwa huna historia yoyote ya kufanukisha jambo lolote maishani mwako. Hapa waweza kukuta ndoto iliyokuwa kubwa ya kuacha jina chini ya jua inayeyuka kama siagi katika kikaango motoni.
Kusudi la Mungu ni kumfanya kila aliye na maono kulifanya jina lake kumbukumbu ya milele, "JINA LAKO NITALIFANYA KUWA KUMBUKUMBU KATIKA VIZAZI VYOTE…" Zaburi 45:17, hili ndilo kusudi la Mungu katika maisha yetu, kuacha kumbukumbu, alama chini ya jua ama kwa kimombo LEGACY, kumiliki gari, kumiliki nyumba hata iwe na thamni kubwa kiasi gani haviwezi kuwa LEGACY, hatuna budi kufanya zaidi, tuzidi kutafakari, TAFAKURI ndio udongo mzuri kufanya ndoto kuwa kweli.
Mwandishi Max Lucado anatukumbusha kwamba hatukuumbwa kwa bahati mbaya, bali tuliumbwa kwa kusudi, tunalo jukumu, "You aren't an accident. You weren't mass produced. You aren't an assembly line product. YOU ARE DELIBERATELY PLANNED, SPECIFICALLY GIFTED, AND LOVINGLY POSITIONED on earth by the Master Craftsman."
Uwe na siku njema.