donlucchese
JF-Expert Member
- Mar 23, 2011
- 17,076
- 21,552
Habari za jioni wakuu,
Let me get straight to the point... Young Lunya ni msanii ambae ni mkali wa mashairi na flows pia. Huwa namfananisha na bwana mdogo mmoja enzi hizo kule states wa kuitwa Soulja Boy Tell 'em. Pamoja na ukali wake na kumkubali, siafiki kabisa kitendo cha yeye kujiita GoaT (Greatest Of All Time).
Twende taratibu, tukienda kwenye mchezo wa ngumi ukimtaja Mike Tyson au Mohamed Ali kwamba ni ma goat watu hawatopinga. Ukienda kwenye mziki wa pop ukiwataja watu kama wacko jacko au Elvis Presley kwamba NI ma goat watu watakubali. Same applies kama Tiger Woods kwenye golf, Bob Marley kwenye reggae, Oliver mtukudzi, Yossou ndor, Mano Debango kwenye traditional African music, Maradona, Pele, Messi kwenye football etc.
Kwa hapa bongo, kwa mziki wa bongo flavour, it's without a doubt, ukimtaja Prince Dully Sykes huyu ni goat haswa. Ili mtu tumuite goat, tunaangalia nini? Tunaangalia consistency ya not less than two decades kwenye game. Dully tangu Enzi za Hi, lady's free, julieta, bongo flava mpaka sasa kiukweli ameweza ku-maintain consistency ya hali ya juu.
Kwa wanamuziki wa kike, ukimtaja Lady Jaydee 'komando' bila kupingwa ni goat.
Kwenye bongo hip-hop ukimtaja Prof Jizze anafaa kua na hadhi ya u-GOAT. Sasa huyu Lunya ambaye two decades ago probably alikua bado anasoma primary anapata wapi ujasiri wa kujiita GoaT? Ame-menteini kwenye game kwa muda gani?
Halafu na hili la kufanya freestyle session mpaka volume ngapi huko, freestyle gani mpaka unaenda location kabisa kushoot video aisee?
Unaikariri vipi freestyle hadi uweze kwenda kuitolea video? Goat I'll be damned, the kid has alot to learn from the true GOATs of the game!