Msanii Soggy Doggy

Feb 6, 2024
40
51
HABARI ZA WAKATI HUU WAFUATILIAJI WA JAMVI HILI LA UKWAJU WA KITAMBO.
...................................

✍🏻kama ilivyo destru yetu wadau na wafuatiliaji wa jamvi la Ukwaju wa Kitambo, huwa tuna desturi yakufanya mahujiano na wasanii wakongwe katika Game hii ya bongo fleva..

✍🏻wiki hii katika pita pita zetu tuli bahatika kukutana na soggy doggy anter au unaweza kumuita chief rumanyika.

Tulipiga nae story nyingi kuanzia maisha yake ndani na nje ya sanaa. Lakin tulijikita zaidi katika maisha yake ya sanaa Tangu akiwa anaaza game ya bongo fleva baada ya kuhitimu Elimu yake ya msingi..

Mahojiano hayo ni kama ifuatavyo..

UKWAJU WA KITAMBO.

" Karibuni sanaaaaaa Anselm Tryphone Ngaiza a.k.a chiefu rumanyika ama soggy doggy anter katika jamvi hili LA Ukwaju wa Kitambo . ... Naimani tutakuwa pamoja kwa kipindi chote cha mahojiano haya.

Karibu sanaaaaa @Sogggy Doggy

@soggy doggy

"Asante"

UKWAJU WA KITAMBO ..

Brother soggy nilikuwa na maswali kadhaa napenda kukuuliza brother..

@soggy doggy .. Uliza

UKWAJU WA KITAMBO ..

. vip Ile ngoma yako inayoitwa Story nilisikia kwamba beat uligonga we mwenywe je ni kweli au

@Soggy doggy ..

Kweli

UKWAJU WA KITAMBO...

Kwa nini katika wimbo wako wa rais wa bongo, Afande Sele hakupewa nafasi yoyote ya uongozi?

Wakati Afande alikuwa na ngoma kali.

@Soggy doggy ....

Nilifanya makusudi tu, ni muhimu wakati mwingine


UKWAJU WA KITAMBO..

je unakumbuka kipindi unatangaza RFA mwaka 2000.
Pamoja na DOUBLE G unaweza ukanitajia crew nzima ya watangazaji mlikokuwa hapo RFA kwa kipindi kile tukianza na
Deo kiduduye
Na Gabriel Yotam!!!!
Lakini pia Nilisikia Mara kadhaa kuwa ile track Yako ya story kwamba ile ajali ukupata Moro.ila ulifanya hivyo kuitaja Morogoro kwa maana msimu wa fiesta ulindodokea huko hivi ni kweli.

@soggy doggy

... Niliitaja Morogoro sababu ya kutaka mashabiki wa Morogoro maana kipindi hicho sikutaka watu wa Moro waichukie sababu ya kutoelewana na Sele

Lakini kuhusu radio presenters tuliofanya nao kazi Radio free Africa enzi hizo ni


Mimi
Fredwaa
Kid bway
Lazaro Matalange
Zuberi Msabaha
Jacob Usungu Young Millioner
Wiltrudis Mtembei
Juma Ahmed Baragaza

UKWAJU WA KITAMBO....

Je, nini kilikushawishi kuingia katika tasnia ya mziki?

Je, uliweka malengo gani na kwa muda gani katika kazi ya usanii?

@soggy doggy ...

Ilitokea tu, sikuwahi kupanga kuwa mwanamuziki na kwa sababu ilikuwa ndio kwanza muziki unaanza sikuwa najua kuhusu malengo, nilikuwa najifurahisha tu

UKWAJU WA KITAMBO...

kwenye ngoma ya kulwa na dotto kuna sauti mbili zinasikika kwenye kiitikio yaani Daz mwalimu na Juma Nature ambapo hizi sauti kwa wakati ule zilikuwa zinaendana sana na hata mie ilinichukua muda sana kujua mule kuna juma Nature.

Je
Hapakuwa na namna ya kutokuweka kwa huo wimbo msanii mmoja wapo!
Kwa mfanano wa sauti!

@soggy dogy ..

Hawafanani sauti na techniques, wimbo ilikuwa nifanye na Daz Baba tu ila kuna sauti za Juma zilihitajika

Ukwaju Wa Kitambo: UKWAJU WA KITAMBO..

Mara kadhaa nimesikia wasanii wengi wa zamani walipata changamoto kubwa sanaa hadi kuja kupata chance yakukutana na majani katika studio za bongo record, wasanii wengi walitolewa nje na wengi walikata tamaa juu ya hilo ..

Vipi kwa upande wako je? Na wewe pia ulipata changamoto kama waliozipata wasanii wezako kipindi kile cha mwanzo kabisa unaaza game ( underground)

@soggy doggy..

Haikuwa ngumu kuingia Bongo Record maana mimi na Majani tulikuwa kama familia, rejea hata msiba wa mama yake mimi ndio nilikuwa Mwenyekiti

UKWAJU WA KITAMBO..

Wasanii wa zamani nikisikiliza interview zao nyingi wanasema ilikuwa gumu sana kwao kuingia kwa majani bongo record kwa Mara ya kwanza. Wakiwa ma under ground kwa kifupi wakiwa wanaaza game.

UKWAJU WA KITAMBO..

Mara kadhaa nilisikia kuwa wasanii wa nyumbani hawapewi malipo wanayostahili wakiwa katika majukwaa ya fiesta . ila wasanii ambao walikuwa wanapewa fedha ndefu ni wasanii kutoka nje ?

Nikitaza kwa miaka ile ya nyuma hata nyinyi wasanii wazawa mlikuwa na vibe kubwa katika stage hamkuhitaji hata wasanii kutoka nje kuwapa vibe mashabiki zenu..

Unalizungumziaj hili

@soggy doggy
...

Nisingependa kujibu hili maana sio Fiesta tu, shows 99% za kibongo malipo hayaeleweki.

Ukwaju Wa Kitambo: UKWAJU WA KITAMBO...

Ni msanii gani unamkubali katika sanaa ya mziki? Ukibe excluded

Pia

Ninaomba kuwafahamu angalau watano?

@soggy doggy

Jay Moe
Feruuz
Sugu
Profesa Jay
Nikki Mbishi
P the MC
Jos Mtambo
Stamina
Diamond
Kiba
Dully Sykes... wengi

@soggy Dogg

Wako wengi sana

UKWAJU WA KITAMBO
..

Kwa nini Soggy Doggy?

Ila pia Katika show mbalimbali ulizobahatika kufanya hapa nchin na nje ya nchi Msanii gani alikuumiza kichwa ukitafakari namna yakumu wine katika stage ..

pale ataposhuka katika stage ili wewe ukienda jukwaani ukafanye makubwa zaid yake
..

@soggy doggy..

Wapo wengi..

UKWAJU WA KITAMBO..

Sawa.
Ninaweza pata angalau kwa ufupi?

@soggy doggy...

Nay wa Mitego
Juma Nature
Rostam
WASANII WA SINGELI

@soggy doggy..

Soggy ni neno la kiingereza (Kitu kilicholoa kwa maji chapachapa)

Nilikuwa napenda kukaa kwenye maji muda wote utotoni so mama akasema walikuwa wakiniita Soggy.

Doggy tulikuwa tunaitana shule so niliunganisha na ANTER (Anselm Ngaiza Tryphone Evarist Rumanyika)

UKWAJU WA KITAMBO..

Kati ya wewe na Mr Blue ni nani alianza mziki akiwwakiniita mdogo zaidi katika zama zenu?

@soggy doggy..

Of course mimi

UKWAJU WA KITAMBO..

Je, una album ngapi?
Na ipi kwako ilikuwa bora kuliko nyingine?

@soggy doggy...

...Niite Chifu Rumanyika ya mwaka 2004

UKWAJU WA KITAMBO

Vip kitu gani kilipelekea muwe na beef na afande sele enzi hizo..

@soggy doggy...

Hatuna bifu hata jana usiku tulikuwa pamoja, game inatakiwa ichangamke.

UKWAJU WA KITAMBO...

Bac poa soggy next time tukiwa na shidah. Tutakuchek..

Ukwaju wa kitambo
#tunakurudishakaleee
FB_IMG_1709974628819.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom