Shadeeya
JF-Expert Member
- Mar 12, 2014
- 48,323
- 115,323
Yanga iliwasili usiku wa kuamkia juzi kutoka Botswana ambako ilitinga raundi ya kwanza ya michuano ya ligi ya mabingwa baada ya kuichapa Township Rollers bao 1-0
Tshishimbi amesema mechi za kirafiki walizocheza pamoja na michezo miwili dhidi ya Township Rollers, imesaidia kuwaunganisha
Mcongomani huyo amesema wana matumaini makubwa ya kufanya vizuri kwenye ligi huku wakipiga hesabu ya kutinga hatua ya makundi michuano ya ligi ya mabingwa "Mwanzo tulikuwa hatuchezi vizuri kwa sababu wachezaji wengi wapya, hatujazoeana," amesema "Lakini michezo tuliyocheza imetusaidia, tutafanya vizuri zaidi kadiri tunavyoendelea kucheza pamoja"
Aidha kuelekea mchezo dhidi ya Ruvu Shooting, Tshishimbi amesema watapambana kupata matokeo ili kuwapa furaha mashabiki pamoja na kutimiza malengo ya timu msimu huu