Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

20190828_071823.jpg
Nahodha wa Yanga Papy Tshishimbi amesema kikosi chao kimeanza kuchanganya baada ya wachezaji kuzoeana

Yanga iliwasili usiku wa kuamkia juzi kutoka Botswana ambako ilitinga raundi ya kwanza ya michuano ya ligi ya mabingwa baada ya kuichapa Township Rollers bao 1-0

Tshishimbi amesema mechi za kirafiki walizocheza pamoja na michezo miwili dhidi ya Township Rollers, imesaidia kuwaunganisha

Mcongomani huyo amesema wana matumaini makubwa ya kufanya vizuri kwenye ligi huku wakipiga hesabu ya kutinga hatua ya makundi michuano ya ligi ya mabingwa "Mwanzo tulikuwa hatuchezi vizuri kwa sababu wachezaji wengi wapya, hatujazoeana," amesema "Lakini michezo tuliyocheza imetusaidia, tutafanya vizuri zaidi kadiri tunavyoendelea kucheza pamoja"

Aidha kuelekea mchezo dhidi ya Ruvu Shooting, Tshishimbi amesema watapambana kupata matokeo ili kuwapa furaha mashabiki pamoja na kutimiza malengo ya timu msimu huu
 
Mwinyi Zahera Yanga ikifungwa tu akihojiwa anaongea kifaransa eti Doblivee Doblivee sijui ndio nini sasa?
 
Niliwahi kuwaambia mapema Zahera sio kocha yule ni muhamasishaji tu,Alijificha kwenye matatizo ya Yanga na huu ni mwanzo tu.
 
Mikia yabidi mtushukuru kwani tumewapa ahueni ndani ya nafsi mana mlikuwa mnaelekea kupagawa.

Pia niwaambie ile ni ligi kuu jamani na bado kuna mechi kibao na ndio sababu hata Barca mechi ya kwanza ya ufunguzi wa la Liga alipoteza pia na wala haikuwa jambo la ajabu.

"DAIMA MBELE NYUMA MWIKO"
 
Sasa Simba itafungwa na kagera tu team kama Yanga ,Azam ,Mtibwa ,kmc ni vipigo tu ilo no daught ni muda tu ata wewe unajua,acheni masikhara hakuna viporo tena, Wambura yuko vizuri kiporo ni kimoja vikizidi vitatu mtalaumiana tu na msimu unaokuja team ni 2 tu kimataifa ,mliopita hakuna mwenye nguvu ya kutetea nafasi NNE za kimataifa.
 
Yani nna mahaba ya Makubwa sana na Yanga na nahitaji kupata group lolote la YANGA ntafarijika sanaaaaaaaaaaaaaaaaaa, naomba mwenye kujua anisaidie niweze kupata hilo group
 
Sasa Simba itafungwa na kagera tu team kama Yanga ,Azam ,Mtibwa ,kmc ni vipigo tu ilo no daught ni muda tu ata wewe unajua,acheni masikhara hakuna viporo tena, Wambura yuko vizuri kiporo ni kimoja vikizidi vitatu mtalaumiana tu na msimu unaokuja team ni 2 tu kimataifa ,mliopita hakuna mwenye nguvu ya kutetea nafasi NNE za kimataifa.
Hata sijakuelewa Mkuu. Unamaanisha nini kwani?
 
20190830_053625.jpg

Wachezaji watatu waliokosa mchezo wa hatua ya awali ligi ya mabingwa, Farouk Shikalo, Mustapha Suleyman na David Molinga wanaweza kuivaa ZESCO United

Imefahamika Shirikisho la soka Barani Afrika (CAF) tayari limetoa vibali kuwaruhusu wachezaji hao kushiriki ligi ya mabingwa

Nyota wote jana walicheza kwa dakika zote 90 mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ruvu Shooting, Yanga ikipoteza kwa kufungwa bao 1-0

Hii ni habari njema kwa kocha Mwinyi Zahera ambaye ana wiki mbili za kukiandaa kikosi chake kabla ya mchezo wa kwanza utakaopigwa jijini Dar es salaam kati ya Septemba 12-15

Yangadaima27
 
Back
Top Bottom