Niko katika harakati zangu kapita mdada kafanana sana na aliyekua mpenzi wangu, Caroline.
Carol alinipenda kupita maelezo hadi nikajua na nikawa namchukulia poa kwa kumfanyia vituko visivyokwisha na wakati mwingine nisipoomba radhi mie(na nilikua siomuombi radhi) basi huniomba radhi yeye ili yaishe
Kuna siku yalimfika shingoni. Nilikua nimesahau simu yangu nyumbani kwake na akawa ameikagua hasaa, amepitia katika inbox zangu za text msg na pia wasap. Alikipata alicholitafuta, meseji za appointments, jumbe za kusexchatishana na pongezi za kutosha kutoka kwa wanawake wengine kuhusiana na miyadi tuliyotoka kuitimiza kuvunja amri fulani nadhani ni namba 6.
Japo alikua mwanamke mzuri, mpole mkimya na mstaarabu sana, lakini siku hiyo aliongea akaongea na kuongea kama mtu aliyepagawa akinikumbusha mambo mengi mazuri aliyonifanyia na mwisho wake akanambia "Sesten unapovuka hicho kizingiti hapo cha mlango wa nyumba hii naomba nisikuone tena maishani mwangu na futa kabisa namba zangu usinitafute maishani mwako". Aliposema hivyo akawa amefungua mlango nitoke namimi taratiiibu nikawa natoka nje sikuweza kujitetea kwa lolote maana vitu vilikua wazi kabisaa
Nilipofika mlangoni ile nataka kuinua mguu nitoke nje akaniita tena na kuniambia,"Sesten, kweli unaondoka! You can not even say sorry! You can't fight for this love! Really!" Yaliendelea mambo machache lakini huwezi amini baada ya muda kidogo ikawa mimi ndio naombwa radhi na maisha yakaendelea
Siku ya siku nipozangu safarini napigiwa simu na jamaa zangu kua sweetheart wangu Caroline anaolewa na send off ni kama wiki ijao hivi! Ilikua zamu yangu kuchanganyikiwa,niliumia hasa kikomo cha kuumia. Nikijiuliza imekuaje na kwanini. Juhudi zangu za kuzuia asiolewe ziligonga mwamba na sasa ni mke wamtu ila maumivu niliyoyapata siwezi kusahau maisha yangu yote! Ama kweli thamani ya kitu utaijua kitakapokuponyoka. Natumaini Carol(mama Suzan kwa sasa) waendelea uzuri huko ulipo na yaliyonikuta ni KARMA, what goes around comes around
Ila hii kauli YOU CAN'T FIGHT FOR THIS LOVE NITAIKUMBUKA SANA