You can't fight for this love!!!?

You can't fight for this love!!!?

Sesten Zakazaka

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2017
Posts
10,795
Reaction score
19,825
Niko katika harakati zangu kapita mdada kafanana sana na aliyekua mpenzi wangu, Caroline.
Carol alinipenda kupita maelezo hadi nikajua na nikawa namchukulia poa kwa kumfanyia vituko visivyokwisha na wakati mwingine nisipoomba radhi mie(na nilikua siomuombi radhi) basi huniomba radhi yeye ili yaishe

Kuna siku yalimfika shingoni. Nilikua nimesahau simu yangu nyumbani kwake na akawa ameikagua hasaa, amepitia katika inbox zangu za text msg na pia wasap. Alikipata alicholitafuta, meseji za appointments, jumbe za kusexchatishana na pongezi za kutosha kutoka kwa wanawake wengine kuhusiana na miyadi tuliyotoka kuitimiza kuvunja amri fulani nadhani ni namba 6.

Japo alikua mwanamke mzuri, mpole mkimya na mstaarabu sana, lakini siku hiyo aliongea akaongea na kuongea kama mtu aliyepagawa akinikumbusha mambo mengi mazuri aliyonifanyia na mwisho wake akanambia "Sesten unapovuka hicho kizingiti hapo cha mlango wa nyumba hii naomba nisikuone tena maishani mwangu na futa kabisa namba zangu usinitafute maishani mwako". Aliposema hivyo akawa amefungua mlango nitoke namimi taratiiibu nikawa natoka nje sikuweza kujitetea kwa lolote maana vitu vilikua wazi kabisaa

Nilipofika mlangoni ile nataka kuinua mguu nitoke nje akaniita tena na kuniambia,"Sesten, kweli unaondoka! You can not even say sorry! You can't fight for this love! Really!" Yaliendelea mambo machache lakini huwezi amini baada ya muda kidogo ikawa mimi ndio naombwa radhi na maisha yakaendelea

Siku ya siku nipozangu safarini napigiwa simu na jamaa zangu kua sweetheart wangu Caroline anaolewa na send off ni kama wiki ijao hivi! Ilikua zamu yangu kuchanganyikiwa,niliumia hasa kikomo cha kuumia. Nikijiuliza imekuaje na kwanini. Juhudi zangu za kuzuia asiolewe ziligonga mwamba na sasa ni mke wamtu ila maumivu niliyoyapata siwezi kusahau maisha yangu yote! Ama kweli thamani ya kitu utaijua kitakapokuponyoka. Natumaini Carol(mama Suzan kwa sasa) waendelea uzuri huko ulipo na yaliyonikuta ni KARMA, what goes around comes around

Ila hii kauli YOU CAN'T FIGHT FOR THIS LOVE NITAIKUMBUKA SANA
 
Yaani tena mwanamke akikupenda na akakupa moyo wake wote anakuwa yupo tayari kwa kila kitu lkn sio kukukosa wewe.

Atakubali kuwa mjinga, kudharauliwa na pengine hata kuukosa uthamani wake kwako.

Atavumilia sababu moyo wake ndo unaozungumza zaidi ya kile anachokiona kwa macho.

Lakini sasa moyo ukishasema basi there will be no point of return...huwaga hatugeuki nyuma.

Pole kwa yote ukimpata mwingine jifunze kumpenda na kumuheshimu.
 
Na hiyo ndio nguvu ya KARMA

Mwanamke akikupenda, anakua amekubali kufanya chochote kwa ajili ya mwanaume wake, ataruka viunz vyote kuhakikisha mwanaume wake anakua naye lakini moyo ukishasema basi hakuna kitu kitaweza mfanya akabadili maamuzi

Na mtu hatambui thamani ya kitu au mtu had pale kitakapomtoka,

Yan kaolewa huku ukijiona anakupenda sipati picha maumivu yake
 
Ulitaka advantage ya upendo wake.

Ila on the other hand unaweza ukamfanyia mtu ubaya au vituko, na wala yasikurudie, you just go on and live a happy and fulfilling life. That's the sad fact. Hii mambo ya karma ni watu kujifariji tu.

Ila sikutetei ulichofanya, binti wa watu alijiongeza akakulia timing amekupiga knockout. And now you'll forever have a scar kwa alichokufanyia. Serves you right!
 
Duuh! Ila nawapenda sana wanawake wa hivyo jamaani sababu wanasema siku zote uvumilivu uwe na kipimo.

Yaani alivumilia weee mwisho akaona cha kufia nini. Na huenda hata angekuja kuwa ndoani angepata tabu sana.

Hongera kwake.
 
Na hiyo ndio nguvu ya KARMA

Mwanamke akikupenda, anakua amekubali kufanya chochote kwa ajili ya mwanaume wake, ataruka viunz vyote kuhakikisha mwanaume wake anakua naye lakini moyo ukishasema basi hakuna kitu kitaweza mfanya akabadili maamuzi

Na mtu hatambui thamani ya kitu au mtu had pale kitakapomtoka,

Yan kaolewa huku ukijiona anakupenda sipati picha maumivu yake
We acha tu Madame. maumivu yaliisha baada ya muda mreefu sana lakini kovu bado lipo nitaishi nalo maisha yangu yote
Nilichezea shilingi chooni ilipotumbukia nikabaki jilaumu mwenyewe kwa uzembe
 
Back
Top Bottom