You are not my type

You are not my type

I don't think kama i'm good enough for you. Huwa najiweka kwenye angle ambayo mtu anayekataliwa ajione hana kasoro na mimi ndio simstahili. Hata mimi im not good for everyone so why should i bellitle someone coz of their own feelings towards me. Kwanza its a blessing kupendwa
Yeah mimi pia huwa napenda kusema hivi sema mwingine ukimwambia hivyo ndio anakugandaaa
 
Kuna dada mmoja alitongozwa na kaka mmoja wakiwa chuo akamjibu 'over my dead body' mwanaume alikomaa mpaka kikaeleweka sasahivi ni wanandoa wana watoto wawili.

Wakati mwingine mtu anajitamkia tu akiona bado anawashika pembe wengi.
hatari sana
 
Naam siye ukimpenda mrembo kwa akili na moyo wako wote huwa hatukatishwi tamaa na kauli kama hizo over my dead body, you’re not my type etc. Unaendelea kuzoza tu mpaka kieleweke na maneno kama hayo kwa baadhi ni motisha tosha kabisa ya kumfukuzia mrembo kwa juhudi zote.

Kuna dada mmoja alitongozwa na kaka mmoja wakiwa chuo akamjibu 'over my dead body' mwanaume alikomaa mpaka kikaeleweka sasahivi ni wanandoa wana watoto wawili.

Wakati mwingine mtu anajitamkia tu akiona bado anawashika pembe wengi.
 
Kama mtu hamuendani ni hamuendani tu hata ipite miaka mia
Si mara zote mtu anayesema hamuendani anamaanisha. Wengi hutoa kauli hiyo out of immaturity, arrogance na kibri.
Mfano unamwambia mtu sio taipu yako kisa hana taco, hapo unakuwa ni msukumo wa immaturity.
 
Si mara zote mtu anayesema hamuendani anamaanisha. Wengi hutoa kauli hiyo out of immaturity, arrogance na kibri.
Mfano unamwambia mtu sio taipu yako kisa hana taco, hapo unakuwa ni msukumo wa immaturity.
Inawezekana ni kweli usemacho, lakini kwa wakati huo si inakuwa iko hivyo?
 
Wanaume na wanawake, let's say umetongoza au unampenda mtu yeye akakujibu 'You are not my type' au ukasikia anamwambia mtu kuwa you are not his/her type utalipokea vipi?

Mimi ninavyojua mtu akisema wewe sio type yake anamaanisha wewe si aina ya mtu ambaye angependa kuwa naye, haimaanishi amekudharau, amekushusha na kukuona una hadhi ya chini kuliko yeye kama wengi tunavyofikiria.

Kwenye mapenzi kila mtu kipo anachopenda iwe ni katika mwonekano au personality kiujumla. Wapo wanaume wanapenda chubby girls, wengine wanapenda English figure, wapo watu wanapenda mtu mchangamfu, anayeweza kufanya acheke muda wote lakini wengine wanapenda makauzu, kuona jino lake mwaka mpya hadi mwaka mpya. Kwa hiyo akikutana na wewe upo kinyume cha hapo ni kwamba wewe si type yake.

Japo si busara kumchana mtu live kuwa 'wewe si type yangu' lakini haina haja ya kukasirika, kuumia na kujenga chuki ukisikia kitu kama hicho. Maana wengine wakiambiwa hivyo wanaanza kuchambua demu mwenyewe miguu yote ya kushoto, sura kama anaramba ndimu anawezaje kutamka maneno kama hayo? Relax, kunywa maji then tafuta wa kufanana na wewe, yupo mahali anakusubiri.

Pengine kilichomfanya Diana asikupende ndio hichohicho kitakachomfanya Mwajuma asilale kwaajili yako.

Thanks
Swala sio kwamba hilo neno linatukwaza, shida inakuja pale tu mnavyolitamka "nadhani mnajua".
 
unajua nini unapukua unatongoza ni kawaida kuwa vulnerable maana wewe unakua muhitaji na ambaye unamtongoza unamuona kama prize vile she is there for you to win her , sometime unakuwa na your own imagination jinsi gani perfect she is , na dhana nyingi tu za uongo zinakuwa zimekujaa kichwani , unamuona yeye ni mkamilifu sana , sasa kitendo cha yeye kusema you are not my type ni kitendo cha kuumiza hisia, maana unamjudge mtu maisha yake ndio manaa wengi wanaogopa kutongoza sio kwamba hawajui kutongoza ni swala la kupokea majibu , hiyo inakua kama hukumu inaumiza hisia za mtu haswa ukiwa kweli unamtaka na umepania kuwa naye , unaambiwa bora shambulio la kupigwa utaumia maumivu yataisha utakasirika utasahau lakini shambulio la maneno lina dumu miaka unaweza kukuta mjukuu wako akaja kubeba kisasi cha maneno uliyowai kutamka na ukasahau kumbe mwenzio bado miaka yote hayo maneno yanamchoma, lakini jambo moja ambalo mwanaume inabidi kuwa nalo ni kuweza kuvumilia upumbavu ambao wanawake wanajibu na kupuuzia , lakini sio wote wanaoweza huo
 
Kwa mtazamo wangu, hayo maneno siyo mabaya kutumia lkn jinsi yanavyokua presented mtu anajiskia vibaya, mfano unamjibu mtu "you're not my type" huku umebinua kidomo unampandisha na kumshusha, hapo ni dharau, na imezoeleka ukijibiwa hivo means hufikii hadhi yake

hivo kama hmtaki mtu tumia maneno mengine ya busara huwezi jua huenda akakufaa baadaye wakati utakaposhusha vigezo
 
Shida ni pale unapoambiwa sio type yangu huku likiambatanishwa na Msonyo,Kunyali, na kunithaminisha kutoka Kichwani hadi miguuni....

Tofauti na hapo hiyo ni sentensi ya kawaida sana na inaelekweka vyema.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom