"You are not my type"

..sipati picha ulivotumia dudu yako kwenye avatar hapo
 
Hahahaha hapana aisee sister sina unyama nina roho moja ya huruma sana ,sema sasa mtu akivuka mipaka yake ,Repercussions zake zinakuwa mbaya sana ,kwa sababu nikishaamua jambo nimeamua huwa siangalii nyuma
..kitabia tunafanana mkuu!...
 
Mbona hata nyie wanaume mpo mnaosema hivo. Aisee nilishaambiwa nililia nilikaa najiangalia najiuliza Mungu kaniumba vipi. Kwakweli huyu mtu alinifanya nijihisi ninamapungufu mengi ambayo yakanikosesha raha kusimama mbele za watu. Ila Mungu yupo. Nadhan Iwe kwa mwanamke Au mwanamme maneno ya aina hii si mazuri yanaumiza yanavuruga. Unaweza jiuliza mara kumi kumi. Muheshim na mthamin kila mtu huwez jua. Hata kama umpendi mpe utukufu Mungu maana kamuumba hivo.
 
Hongera sana, hapo kwenye point umeongea point kubwa sana. Ulipe ubaya ili iweje. Nataka nimkomoe yule dada/kaka! Mie wenye kauli hizi hunishangaza sana. Mkishindana kila mtu achukue 50 zake hakuna sababu ya kuwekeana visasi vya namna yoyote ile.

Mkuu ni wachache sana ambao huamua kumove on bila drama.
Sasa hivi burudani ya drama za breakups zimehamia WhatsApp.
Mara huyu kaweka DP hii na status ya mafumbo mwenzie nae kaweka nini sijui


Mimi nikiachana na mtu wala huwezi jua,ndio kwaaaanza naweka DP's na status za kawaida kabisaaaa.
Huku Ex yeye anahangaika


Kiufupi kufanyiana visa baada ya kuachana ni kutokukomaa kiakili.
Mapenzi sio maisha,na maisha lazima yaendelee.

Eid Mubarak brother

 
Mkuu teh teh umenikumbusha mbali sana,me kuna mmoja alinambia et me na yeye hatuendani hata kidogo na sbb kuu et sisi wanaume wa "kimarangu" tunamaringo sana so ntamsumbua kwenye mahusiano,unfortunately siku iz kazalishwa na jamaa kamtemaa yupo anahaha tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…