Yona na Mramba: Mashtaka na yatokanayo

Yona na Mramba: Mashtaka na yatokanayo

Inaonyesha mna kiherehere hii mechi inachezwa hapa ni kampeni za uchaguzi tu,ila CCM wakumbuke msemo wa kiswahili usemao samaki mmoja akioza wameoza wote ,ule ushairi walio nao siku hizi jamii ya CCM eti wakifanya kwa maslahi yao na sio Chama ,ingawa hii inaonekana ni tafu inayotokana na misaada na kwa vile Nchi imekalia vibaya wafadhili wamesukuma ili kuwaweka sawa wananchi ,lakini kama uchumi wa dunia unavyoanguka hata wakijaza mamilioni katika mabenki bado hali inaendelea kuwa mbaya na ndio hivyo hivyo kwa CCM kadiri wanavyojaribu kuziba na kuweka viraka ndivyo hivyo hivyo na wao wanavyozidi kuporomoka nachelea mwisho wa uvumilivu wao ni ubabe.
 
Kwa maoni yangu JK amefanikiwa kufanya kile ambacho wengi hatukutarajia and for that ninampa hongera.

LAKINI kamwe sitampongeza JK kwa kutekeleza wajibu wake. Na ningependa waTanzania wenzangu tuamke kwenye huu usingizi mzito tuliomo ambapo kiongozi akitekeleza wajibu wake tunamsifia as if ametufanyia fadhila, kana kwamba utekelezaji wa wajibu ni zawadi kwetu. Let's learn to expect nothing but the best kutoka kwa viongozi wetu. Tujifunze kuwawajibisha na ku-demand more kutoka kwao. Tukiweza ku-raise standard za uongozi na expectation kutoka kwa viongozi wetu, then mambo kama yaliyotokea leo hatutayashangilia wala kuyastaajabia bali tutayaona kama habari za kawaida, kwa maana tutakuwa tayari tunatarajia serikali iwachukulie hatua viongozi wahalifu kama akina Mramba, Yona, Karamagi, Lowassa. Chenge, Mkapa, Rostam Aziz na wengineo.

Kwa hiyo kwa wale wana JF ambao bado mpo usingizini, PLEASE, PLEASE, PLEASE amkeni na tuwaamshe wenzetu. Kama wewe mwana JF umepumbaa kiakili namna hii kiasi cha kuanza kumsifia JK na kum-absolve kutoka kwenye uzembe na uongozi wake uliokosa dira, je yule mkulima wa kule Cholesamvula atakuwa katika hali gani?? Let's keep the pressure ili hawa jamaa wasipate tena mwanya wa kutuibia. Tukumbuke kwamba maasi yote dhidi ya waTanzania huanza katika second term.......hence 2010!!
 
Mkuu mbona naona kama Mramba ana Ndala hapo?

Watu wengine kwa kucopy na kupaste wapo juu, yaani anachukua post ya mwenzake kama aliandika MALAPA yeye atasema kandambili sijui ni kukurupuka au kutaka kuongeza idadi ya post dah inachekesha sana
 
I have seen things that most people never get to see, and experience events from a perspective that most people do not realize exists. Naturally, I feel a need to tell people about it. The other reason that I am blogging, the main one as things stand, is because I occasionally feel incredibly exasperated at the ignorance that is allowed to exist in the world, and by the actions of several groups who seems to be going to concerted effort to maintain this ignorance
 
Watu kusema kuwa JK asipewe pongezi kwa kufanya hili sababu ni moja ya majukumu yake wanakosea sana::

JK lazima apewe pongezi na sababu kubwa ya pongezi ni :: Ameset Precedent

From now on kuwafikisha matajiri mahakamani sio issue tena sababu kina Jeetu wamefika.
Kuwafikisha mawaziri, wabunge sio issue sababu ya kina Mramba na Yona.

So lazima tumpe JK pongezi kwa kuliangalia suala hilo la precedent kwa undani.
 
Mramba, Yona waenda rumande kwa ufisadi
*Wakosa dhamana ya Sh7.8bn, waenda rumande na kandambili

MAWAZIRI wawili waliowahi kuongoza wizara mbalimbali ikiwamo nyeti ya fedha katika serikali ya awamu tatu, Basil Mramba na Daniel Yona wamefikishwa kortini kwa matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya Sh11.7 bilioni.

Kufikishwa kizimbani kwa mawaziri hao kunaashiria mwanzo wa utekelezaji wa ahadi ambazo zimekuwa zikitolewa na serikali na watendaji wake kuwa itashughulikia vigogo wote wanaotuhumiwa na ufisadi baada ya wananchi wengi kutoridhishwa na ukubwa wa majina ya watu walioshtakiwa katika kashfa ya wizi wa fedha kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA).

Ni wiki iliyopita tu wakati Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk. Edward Hoseah alipotangaza kuwa muda mfupi ujao vigogo wanaohusika kwenye kashfa mbalimbali za ufisadi watafikishwa mbele ya mkono wa sheria.

Na hali ilikuwa hivyo jana wakati habari zilipozagaa asubuhi kuwa Mramba na Yonah wangepandishwa kizimbani na hivyo kufanya watu waliopata fununu hizo kujazana mahakama ya Kisutu.

Wawili hao walikuwa wameshafika mahakamanio hapo majira ya saa 2:45 asubuhi, wakiwa kwenye gari aina ya Toyota Land Cruiser VX, lenye rangi ya kijani na mistari ya rangi nyekundu na nyeupe ubavuni lenye namba za usajili T319 ATD.

Lakini namba za gari zilizokuwa katika kisahani cha namba (Plate number) zilikuwa tofauti na zilizokuwa katika vioo vya gari hilo ambazo ni T 562 AJK.

Lakini hawakushuka kwenye gari hilo lililokuwa na vioo vya giza, hadi walipotakiwa kwenda kizimbani.

Mramba na Yona walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana mbele ya Hakimu Hezron Mwankenja saa 5.40 na wakasomewa mashtaka na baadaye kupelekwa rumande kutokana na kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

Vigogo hao walifikishwa mahakamani baada ya uvumi wa tukio hilo kudumu kwa takribani majuma mawili.

Wakati wakiingia mahakamani jana Mramba, ambaye ni mtuhumiwa wa kwanza katika kesi hiyo namba 1200 ya mwaka huu, alisikika akiwahoji waandishi iwapo wamefurahi kufikishwa kwao mahakanai hapo, huku akidai kuwa watapiga picha nyingi sana kwa kuwa huo ni mwanzo tu.

Watuhumiwa hao walipandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka matano ya pamoja, baadaye Mramba akasomewa manane zaidi peke yake, na kufanya akabiliwe na jumla ya makosa 13.

Mwendesha mashtaka ambaye ni wakili wa serikali, Stanslaus Boniface aliyataja makosa yanayowakabili wote kwa pamoja kuwa ni matumizi mabaya ya ofisi kwa kuiruhusu kampuni ya M/S Alex Stewart (Assayers ya Uingereza kuingia mkataba wa kudhibiti madini ya dhahabu kinyume cha sheria.

Boniface alifafanua kuwa kati ya Agosti 2002 na Juni 14, 2004 watuhumiwa wakiwa katika nafasi za uwaziri wa fedha na uwaziri wa Nishanti na Madini waliruhusu kampuni hiyo na mshirika wake, M/S Alex Stewart (Assayers) Government Business Corporation kusaini mkataba wa kudhibiti madini ya dhahabu kinyume cha sheria ya Manunuzi ya Umma na ya Madini.

Katika kosa la pili, Boniface alidai kuwa Mei 28, 2005 watuhumiwa hao walitumia vibaya madaraka yao kuingia mkataba wa nyongeza wa miaka miwili kwa kampuni hiyo kuanzia Juni 14, 2005 hadi 23 Juni 2007 kinyume cha sheria ya Manunuzi ya Umma na ya Madini.

Katika kosa la tatu Boniface alidai kuwa kati ya Machi 28 ,2005 na Mei 28,2005 watuhumiwa wakiwa watumishi wa umma walitumia vibaya madaraka yao kwa kumwalika Dk Enrique Segura wa kampuni hiyo kurasimisha mkataba huo wa nyongeza ya muda kabla ya mazungumzo na timu ya serikali kushughulikia suala hilo.

Boniface aliendelea kuieleza mahakama kuwa katika kosa la nne kati ya Machi 2005 na Mei 28, 2005 watuhumiwa waliachia suala la udhibiti wa madini lifanywe kienyeji bila kumshirikisha mwanasheria wa serikali kama ilivyopendekezwa na timu ya mazungumzo ya serikali, jambo lililosababisha ongezeko la muda wa mkataba huo wa miaka miwili.

Na katika kosa la tano ambalo lilimhusu mshitakiwa wa kwanza, Mramba, Boniface alidai kuwa Oktoba 10 Mramba alitumia vibaya mamlaka yake kwa kudharau ushauri wa Mamlaka ya Mapato (TRA) wa kutotoa msahama wa kodi kwa kampuni ya M/S Alex Stewart (Assayers) Government Busines Corpotion.

Katika kosa la sita ambalo pia linamhusu Mramba peke yake Boniface alidai kuwa kati ya Desemba 18 na 19, 2003 Mramba akiwa Waziri wa Fedha alitumia vibaya mamlaka yake kwa kutoa Tangazo la Serikali (GN) la mwaka 2003 lilitoa msamaha wa kodi kwa kampuni hiyo katika shughuli zake za usambazaji wa bidhaa na utoaji huduma kinyume cha mapekezo yaliyotolewa na TRA.

Boniface alidai kuwa kuanzia kosa la saba hadi la 11 ambayo karibu yote yanafanana ambapo Mramba akiwa waziri wa fedha anadaiwa kutoa msahama wa kodi ya mapato kwa kampuni hiyo ikiwa ni pamoja na kutumia madaraka yake kutoa GN namba 424 /2003 na 497/2004 kati ya Desemba 19, 2003 na Oktoba 15, 2004 kinyume cha mapendekezo ya TRA.

Katika kosa la 12 ambalo linawahusu watuhumiwa wote wawili, Boniface aliendelea kudai kuwa watuhumiwa hao wakiwa mawaziri kwa makusudi na kwa kutokuwa makini waliruhusu makataba ambao uliipa upendeleo kampuni hiyo na kuisababishia serikali hasara ya Sh 11,752,350,148.00.

Na katika kosa la 13 ambalo pia linamhusu Mramba peke yake Boniface alidai kuwa Mramba akiwa waziri wa fedha kati ya 2003 na 2007, alishindwa kuchukua tahadhari katika, kutoa matangazo ya serikali namba GN 23/2003, 424/2003, 497/2004, 498/2004 , 377/2005 na 378/2005 yaliyolenga kusaidi kampuni hiyo kutolipa kodi na hivyo kuisababishia serikali hasara ya Sh11.7 bilioni.

Watuhumiwa wote walikana makosa hayo na mawakili wao kuomba dhamana huku upande wa mashtaka ukisema kuwa hauna pingamizi.

Pamoja na maombi hayo ya dhamana, mmoja wa mawakili wa utetezi Tadayo alimuomba Hakimu Mwankenja atoe masharti nafuu kwa wateja wao akidai kuwa suala hilo limekuwa likipelelezwa kwa zaidi ya miaka mitatu na walitoa ushirikiano ikiwa ni pamoja na kufika mahakamani hapo bila kukamatwa.

“Hivyo hakuna hofu kuwa wanaweza kukimbia,” alisisitiza Tadayo na kumuomba hakimu azingatie sehemu ya pili ya sheria ya dhamana ya watuhumiwa kutoa nusu ya fedha wanazodaiwa kuiba au hati ya mali yenye tahamani sawa na nusu ya fedha hiyo.

Hata hivyo, akitoa masharti ya dhamana Hakimu Mwankenja alitupilia mbali ombi la mawakili hao la kuwataka washtakiwa kuwasilisha hati ya mali na badala yake watoe pesa taslimu Sh3.9 bilioni kila mmoja.

Pia aliwataka wawasilishe hati zao za kusafiria na kutokutoka nje ya Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na kuwa wadhamini wawili waliothibitishwa na mahakama.

Mwankenja aliahirisha kesi hiyo hadi Desemba 2 itakapotajwa tena na kuwataka washtakiwa wapelekwe mahabusu hadi hapo watakapotimiza masharti hayo.

Mara baada ya kesi hiyo kuahirishwa mamia ya watu waliofurika mahakamani hapo kiasi cha kujaa ndani na nje ya ukumbi wa mahakama waliwafuata mlango wa nyuma wa mahakama hiyo lilikokuwa gari walilokwenda nalo mahakamani hapo na kuwasubiria.

Wakati washtakiwa hao wakiingia ndani ya gari hilo na kuondoka mahakamani kupelekwa mahabusu, wananchi waliwazomea kwa kuimba wimbo wa “wezi, wezi hao huku wengine wakitaka hata kuwamwagia mchanga ndani ya gari hilo.

Wakati hayo yakiendele baadhi ya ndugu wa watuhumiwa hao walikuwa wakilia kimyakimya na kujifuta machozi huku wakiwa wameshikilia viatu vya washtakiwa hao mikononi na kuwaangalia wakiondoka na kanda mbili ambazo waliwanunulia mahakamani hapo.

Mapema saa 2: 45 waandishi wa Mwananchi walipofika mahakamani hapo waliwakuta watuhumiwa wakiwa wamekwishafika mahakamani hapo huku wakiwa ndani ya gari aina ya Toyota Landcruiser VX, lenye rangi ya kijani na mistari nyekundu na nyeupe ubavuni lenye namba za usajili T319 ATD.

Lakini namba za gari zilizokuwa katika kisahani cha namba (Plate number) zilikuwa tofauti na zilizokuwa katika vioo vya gari hilo ambazo ni T 562 AJK.

Watuhumiwa hao waliendelea kukaa ndani ya gari hilo na walipoteremka moja kwa moja walipandishwa kizimbani.

Kitendo cha watuhumiwa hao na kuendelea kubaki ndani ya gari hata baada ya kufika mahakamani hapo kiliwashangaza wengi na kufanya wajiulize maswali kuwa iweje wao wasishuke ndani ya gari na kuingizwa katika chumba maalumu cha mahabusu wakati wakisubiri kupandishwa kizimbani kama ilivyo kawaida kwa watuhumiwa wengine.

Mramba alikuwa amevalia kaunda suti yenye rangi ya kijivu na viatu vyeusi, mshirika wake, Yona akiwa amevalia kaunda suti yenye rangi ya khaki na viatu kahawia.
 
Katika mashitaka yote 13, hakuna sehemu inayotaja shitaka la ufisadi au rushwa.

Yote yamelenga zaidi abuse of power na maadili ya utumishi....Unless mnishauri vinginevyo, sioni kikubwa katika hayo. Hii inaweza ikawa ni sinema nyingine. Yes, wakubwa hawa kufika mahakamani ni news, lakini we need to see more than that, kwa sababu wananchi wa kawaida, we bear more than that.
 
As usual, watanzania tumeshaanza kusifia mafanikio hewa, yaleyale ya kumsifia baba/mama kwa kumnunulia mwanae nepi. Interesting...

Mayu leka kwone kwanza, tunaitaji kumpongeza Jk kwa hatua aliyofikia kama anatuchezea sinema basi NZUA MKULU, majibu yake yatamyumbisha hata yeye
 
Watu kusema kuwa JK asipewe pongezi kwa kufanya hili sababu ni moja ya majukumu yake wanakosea sana::

JK lazima apewe pongezi na sababu kubwa ya pongezi ni :: Ameset Precedent

From now on kuwafikisha matajiri mahakamani sio issue tena sababu kina Jeetu wamefika.
Kuwafikisha mawaziri, wabunge sio issue sababu ya kina Mramba na Yona.

So lazima tumpe JK pongezi kwa kuliangalia suala hilo la precedent kwa undani.

Watu huwa wanasahau mapema sana!! JK lazima abebe sifa

Kama mtakumbuka kazi ya kwanza ya JK ilikuwa ni kuhakikisha usalama wa ndani na hasa jijini Dar es Salaam, hayo yote mmesahau! wizi na ujambazi kweli upo lakini si kwa kiwango uliokuwepo wakati wa awamu ya tatu, mitutu kila kuikicha Dar huyu kauwawa banki hii imeibiwa n.k

Waulize kina Alex Masawe(AM) wako wapi? Zombe Je.

Hata kama mnasema ni picha inachezwa, tu mi hata kama Mramba atatoka kesho kukaa kwenye lile bench la Kisutu is no JOKE!!!!!!!!! GUYS wote picha mmeona amekaa kwenye bench!!!!

The is on Track, matatizo ni mengi na hawaezi maliza yote cku moja
 
JK msanii tu, hana lolote. Yeye mwenyewe anahusika kwenye ma issue sasa unategemea atafanya kweli aumbuliwe?
 
JK msanii tu, hana lolote. Yeye mwenyewe anahusika kwenye ma issue sasa unategemea atafanya kweli aumbuliwe?[/QUOTE]

Sijui huyu Jk afanye nini ndo muache kumfikiria the way mnavyomfikiria doh
 
Ajiuzulu tu na kurudisha hela za watu alizokwiba, na hata hapo rekodi yake iko pale pale tu.
 
Awe serious kusimamia haki na kupambana na ufisadi, kuna mengi tu ameyafanya ambayo yanafanya watu wawe na wasiwasi. Unakumbuka jinsi ujanjaujanja ulivyofanyika kwenye kesi ya Ditto? Unakumbuka kauli yake ya kwanza kuhusu Richmond alipokutana na waandishi wa habari? unakumbuka alivyosema mwacheni Mkapa apumzike? Unakubaliana naye kwa hayo?
 
Ni malapa yale nayaona kwenye miguu ya Mramba? jibuni pse! kama ni malapa it could mean alot!
 
Ajiuzulu tu na kurudisha hela za watu alizokwiba, na hata hapo rekodi yake iko pale pale tu.

Hahaha Pundit let me ask u a simple question,,, kama leo Jk atasema najiuzulu wadhifa wangu wa uraisi wewe ungempendekeza nani akalie kiti cha uraisi??

Halafu mbona tunaambiwa kuwa muungwana yeye hakuiba kabisa katika kipindi chake leo we unatuambia kwua ameiba hebu tueleze mheshimiwa
 
Date::11/25/2008
Mawaziri wa zamani, Mramba, Yona waenda rumande kwa ufisadi

mrambayohah.jpg

Mawaziri wa zamani, Daniel Yonah, anayejifuta jasho na Basil Mramba, wakiwa kortini jijini Dare es Salaam Jumanne kujibu mashtaka mbalimbali ya ufisadi. Walipelekwa rumande ya Keko baada ya kushindwa masharti ya dhamana.

*Wakosa dhamana ya Sh7.8bn, waenda rumande na kandambili

James Magai na Paulina Richard
Mwananchi

MAWAZIRI wawili waliowahi kuongoza wizara mbalimbali ikiwamo nyeti ya fedha katika serikali ya awamu tatu, Basil Mramba na Daniel Yona wamefikishwa kortini kwa matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya Sh11.7 bilioni.

Kufikishwa kizimbani kwa mawaziri hao kunaashiria mwanzo wa utekelezaji wa ahadi ambazo zimekuwa zikitolewa na serikali na watendaji wake kuwa itashughulikia vigogo wote wanaotuhumiwa na ufisadi baada ya wananchi wengi kutoridhishwa na ukubwa wa majina ya watu walioshtakiwa katika kashfa ya wizi wa fedha kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA).

Ni wiki iliyopita tu wakati Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk. Edward Hoseah alipotangaza kuwa muda mfupi ujao vigogo wanaohusika kwenye kashfa mbalimbali za ufisadi watafikishwa mbele ya mkono wa sheria.

Na hali ilikuwa hivyo jana wakati habari zilipozagaa asubuhi kuwa Mramba na Yonah wangepandishwa kizimbani na hivyo kufanya watu waliopata fununu hizo kujazana mahakama ya Kisutu.

Wawili hao walikuwa wameshafika mahakamanio hapo majira ya saa 2:45 asubuhi, wakiwa kwenye gari aina ya Toyota Land Cruiser VX, lenye rangi ya kijani na mistari ya rangi nyekundu na nyeupe ubavuni lenye namba za usajili T319 ATD.

Lakini namba za gari zilizokuwa katika kisahani cha namba (Plate number) zilikuwa tofauti na zilizokuwa katika vioo vya gari hilo ambazo ni T 562 AJK.

Lakini hawakushuka kwenye gari hilo lililokuwa na vioo vya giza, hadi walipotakiwa kwenda kizimbani.

Mramba na Yona walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana mbele ya Hakimu Hezron Mwankenja saa 5.40 na wakasomewa mashtaka na baadaye kupelekwa rumande kutokana na kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

Vigogo hao walifikishwa mahakamani baada ya uvumi wa tukio hilo kudumu kwa takribani majuma mawili.

Wakati wakiingia mahakamani jana Mramba, ambaye ni mtuhumiwa wa kwanza katika kesi hiyo namba 1200 ya mwaka huu, alisikika akiwahoji waandishi iwapo wamefurahi kufikishwa kwao mahakanai hapo, huku akidai kuwa watapiga picha nyingi sana kwa kuwa huo ni mwanzo tu.

Watuhumiwa hao walipandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka matano ya pamoja, baadaye Mramba akasomewa manane zaidi peke yake, na kufanya akabiliwe na jumla ya makosa 13.

Mwendesha mashtaka ambaye ni wakili wa serikali, Stanslaus Boniface aliyataja makosa yanayowakabili wote kwa pamoja kuwa ni matumizi mabaya ya ofisi kwa kuiruhusu kampuni ya M/S Alex Stewart (Assayers ya Uingereza kuingia mkataba wa kudhibiti madini ya dhahabu kinyume cha sheria.

Boniface alifafanua kuwa kati ya Agosti 2002 na Juni 14, 2004 watuhumiwa wakiwa katika nafasi za uwaziri wa fedha na uwaziri wa Nishanti na Madini waliruhusu kampuni hiyo na mshirika wake, M/S Alex Stewart (Assayers) Government Business Corporation kusaini mkataba wa kudhibiti madini ya dhahabu kinyume cha sheria ya Manunuzi ya Umma na ya Madini.

Katika kosa la pili, Boniface alidai kuwa Mei 28, 2005 watuhumiwa hao walitumia vibaya madaraka yao kuingia mkataba wa nyongeza wa miaka miwili kwa kampuni hiyo kuanzia Juni 14, 2005 hadi 23 Juni 2007 kinyume cha sheria ya Manunuzi ya Umma na ya Madini.

Katika kosa la tatu Boniface alidai kuwa kati ya Machi 28 ,2005 na Mei 28,2005 watuhumiwa wakiwa watumishi wa umma walitumia vibaya madaraka yao kwa kumwalika Dk Enrique Segura wa kampuni hiyo kurasimisha mkataba huo wa nyongeza ya muda kabla ya mazungumzo na timu ya serikali kushughulikia suala hilo.

Boniface aliendelea kuieleza mahakama kuwa katika kosa la nne kati ya Machi 2005 na Mei 28, 2005 watuhumiwa waliachia suala la udhibiti wa madini lifanywe kienyeji bila kumshirikisha mwanasheria wa serikali kama ilivyopendekezwa na timu ya mazungumzo ya serikali, jambo lililosababisha ongezeko la muda wa mkataba huo wa miaka miwili.

Na katika kosa la tano ambalo lilimhusu mshitakiwa wa kwanza, Mramba, Boniface alidai kuwa Oktoba 10 Mramba alitumia vibaya mamlaka yake kwa kudharau ushauri wa Mamlaka ya Mapato (TRA) wa kutotoa msahama wa kodi kwa kampuni ya M/S Alex Stewart (Assayers) Government Busines Corpotion.

Katika kosa la sita ambalo pia linamhusu Mramba peke yake Boniface alidai kuwa kati ya Desemba 18 na 19, 2003 Mramba akiwa Waziri wa Fedha alitumia vibaya mamlaka yake kwa kutoa Tangazo la Serikali (GN) la mwaka 2003 lilitoa msamaha wa kodi kwa kampuni hiyo katika shughuli zake za usambazaji wa bidhaa na utoaji huduma kinyume cha mapekezo yaliyotolewa na TRA.

Boniface alidai kuwa kuanzia kosa la saba hadi la 11 ambayo karibu yote yanafanana ambapo Mramba akiwa waziri wa fedha anadaiwa kutoa msahama wa kodi ya mapato kwa kampuni hiyo ikiwa ni pamoja na kutumia madaraka yake kutoa GN namba 424 /2003 na 497/2004 kati ya Desemba 19, 2003 na Oktoba 15, 2004 kinyume cha mapendekezo ya TRA.

Katika kosa la 12 ambalo linawahusu watuhumiwa wote wawili, Boniface aliendelea kudai kuwa watuhumiwa hao wakiwa mawaziri kwa makusudi na kwa kutokuwa makini waliruhusu makataba ambao uliipa upendeleo kampuni hiyo na kuisababishia serikali hasara ya Sh 11,752,350,148.00.

Na katika kosa la 13 ambalo pia linamhusu Mramba peke yake Boniface alidai kuwa Mramba akiwa waziri wa fedha kati ya 2003 na 2007, alishindwa kuchukua tahadhari katika, kutoa matangazo ya serikali namba GN 23/2003, 424/2003, 497/2004, 498/2004 , 377/2005 na 378/2005 yaliyolenga kusaidi kampuni hiyo kutolipa kodi na hivyo kuisababishia serikali hasara ya Sh11.7 bilioni.

Watuhumiwa wote walikana makosa hayo na mawakili wao kuomba dhamana huku upande wa mashtaka ukisema kuwa hauna pingamizi.

Pamoja na maombi hayo ya dhamana, mmoja wa mawakili wa utetezi Tadayo alimuomba Hakimu Mwankenja atoe masharti nafuu kwa wateja wao akidai kuwa suala hilo limekuwa likipelelezwa kwa zaidi ya miaka mitatu na walitoa ushirikiano ikiwa ni pamoja na kufika mahakamani hapo bila kukamatwa.

"Hivyo hakuna hofu kuwa wanaweza kukimbia," alisisitiza Tadayo na kumuomba hakimu azingatie sehemu ya pili ya sheria ya dhamana ya watuhumiwa kutoa nusu ya fedha wanazodaiwa kuiba au hati ya mali yenye tahamani sawa na nusu ya fedha hiyo.

Hata hivyo, akitoa masharti ya dhamana Hakimu Mwankenja alitupilia mbali ombi la mawakili hao la kuwataka washtakiwa kuwasilisha hati ya mali na badala yake watoe pesa taslimu Sh3.9 bilioni kila mmoja.

Pia aliwataka wawasilishe hati zao za kusafiria na kutokutoka nje ya Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na kuwa wadhamini wawili waliothibitishwa na mahakama.

Mwankenja aliahirisha kesi hiyo hadi Desemba 2 itakapotajwa tena na kuwataka washtakiwa wapelekwe mahabusu hadi hapo watakapotimiza masharti hayo.

Mara baada ya kesi hiyo kuahirishwa mamia ya watu waliofurika mahakamani hapo kiasi cha kujaa ndani na nje ya ukumbi wa mahakama waliwafuata mlango wa nyuma wa mahakama hiyo lilikokuwa gari walilokwenda nalo mahakamani hapo na kuwasubiria.

Wakati washtakiwa hao wakiingia ndani ya gari hilo na kuondoka mahakamani kupelekwa mahabusu, wananchi waliwazomea kwa kuimba wimbo wa "wezi, wezi hao huku wengine wakitaka hata kuwamwagia mchanga ndani ya gari hilo.

Wakati hayo yakiendele baadhi ya ndugu wa watuhumiwa hao walikuwa wakilia kimyakimya na kujifuta machozi huku wakiwa wameshikilia viatu vya washtakiwa hao mikononi na kuwaangalia wakiondoka na kanda mbili ambazo waliwanunulia mahakamani hapo.

Mapema saa 2: 45 waandishi wa Mwananchi walipofika mahakamani hapo waliwakuta watuhumiwa wakiwa wamekwishafika mahakamani hapo huku wakiwa ndani ya gari aina ya Toyota Landcruiser VX, lenye rangi ya kijani na mistari nyekundu na nyeupe ubavuni lenye namba za usajili T319 ATD.

Lakini namba za gari zilizokuwa katika kisahani cha namba (Plate number) zilikuwa tofauti na zilizokuwa katika vioo vya gari hilo ambazo ni T 562 AJK.

Watuhumiwa hao waliendelea kukaa ndani ya gari hilo na walipoteremka moja kwa moja walipandishwa kizimbani.

Kitendo cha watuhumiwa hao na kuendelea kubaki ndani ya gari hata baada ya kufika mahakamani hapo kiliwashangaza wengi na kufanya wajiulize maswali kuwa iweje wao wasishuke ndani ya gari na kuingizwa katika chumba maalumu cha mahabusu wakati wakisubiri kupandishwa kizimbani kama ilivyo kawaida kwa watuhumiwa wengine.

Mramba alikuwa amevalia kaunda suti yenye rangi ya kijivu na viatu vyeusi, mshirika wake, Yona akiwa amevalia kaunda suti yenye rangi ya khaki na viatu kahawia.
 
Awe serious kusimamia haki na kupambana na ufisadi, kuna mengi tu ameyafanya ambayo yanafanya watu wawe na wasiwasi. Unakumbuka jinsi ujanjaujanja ulivyofanyika kwenye kesi ya Ditto?
Kaka ujanja gani ulichezwa hapa na wakati sheria zipo wazi?? Ilionekana hakuua kwa kusudia na dhamana ipo wazi kwa mtu ambaye ameua bila kukusudia

Unakumbuka kauli yake ya kwanza kuhusu Richmond alipokutana na waandishi wa habari?

Kwani kauli yake ya kusema viongozi wachague moja biashara au siasa na katika mapendekezo ya kamati teule ya Bunge wakaja kusema hayo hayo haikukutosha kuona kuwa Jk ameamua kuvalia njuga mambo haya??

unakumbuka alivyosema mwacheni Mkapa apumzike? Unakubaliana naye kwa hayo?

Ofcoz Mkapa amefanya mambo mengi tu katika uongozi wake inabidi aachwe apumzie na kumbuka ana kinga ya kutoshitakiwa... hehehehe
 
Watu huwa wanasahau mapema sana!! JK lazima abebe sifa

Kama mtakumbuka kazi ya kwanza ya JK ilikuwa ni kuhakikisha usalama wa ndani na hasa jijini Dar es Salaam, hayo yote mmesahau! wizi na ujambazi kweli upo lakini si kwa kiwango uliokuwepo wakati wa awamu ya tatu, mitutu kila kuikicha Dar huyu kauwawa banki hii imeibiwa n.k

Waulize kina Alex Masawe(AM) wako wapi? Zombe Je.

Hata kama mnasema ni picha inachezwa, tu mi hata kama Mramba atatoka kesho kukaa kwenye lile bench la Kisutu is no JOKE!!!!!!!!! GUYS wote picha mmeona amekaa kwenye bench!!!!

The is on Track, matatizo ni mengi na hawaezi maliza yote cku moja

Hakuna umuhimu wa kumpa hongera yeyote Rais Kikwete mpaka pale Majambazi wote kutoka Chama Cha Mafisadi na Majambazi (CCM) yatakapofungwa jela na mali zao kutaifishwa. Huwezi kuniambia eti utaridhika tu pale kumuona Mramba amekalia benchi la Mahakama ya Kisutu halafu inakuja siku anaachiwa bila ya hatia yeyote. Hawa Majambazi wa CCM wameiibia sana nchi, ingekuwa vizuri kama Tanzania kungekuwa na sheria kama ya China ambapo hawa wahujumu Uchumi na wala rushwa wangepigwa risasi mpaka kufa pale uwanja wa Taifa (execution style)

Kikwete bado sana tunahitaji utendaji zaidi wa Kazi kutoka kwako. Ulichaguliwa na mamilioni ya watanzania wakitegemea utawala wako utafuata kanuni na sheria za nchi.
 
Back
Top Bottom