Mtoa mada na mtoa comment wote wanaweza wakawa sahihi kwa kulenga jambo lilelile moja, japo kuwa kuna mmoja anamuona Yona kama mtetezi na mkombozi.
Lakini hapa inaonekana kuwa jina la Yona lilipatikana kwa njia ya kupiga ramli jambo ambalo ni chukizo kwa Mungu,lakini hapohapo pamoja na Yona kutupwa bahari bado Mungu alitumia njia nyingine ya kumuwezesha Yona kufikisha ujumbe wake Ninawi.
Baada ya Mungu kumuokoa Yona asizame baharini kwa kumtuma samaki ammeze na kumtapikia kwenye ufukwe wa Ninawi na kufanikiwa kufikisha ujumbe aliotumwa na Mungu kwa wahusika ambao walitubu na kumugeukia Mungu.
Kitendo ambacho hakikumpendeza Yona kwa kuwa lengo lake alitaka watu wa Ninawi waangamie.
Kwa Yona wetu huyu jina lake litakuwa lilipatikana kwa njia ileile ya kupiga ramli na kwa ajili ya kuiokoa rangi ya kijani ambayo ilikuwa inaelekea kufutika na si kwa ajili ya kupeleka ujumbe wa Mungu kuwaponya watu wa Ninawi.
Kwani hata yeye mwenyewe hajui kama ujumbe aliopewa kupeleka Ninawi kama alipewa na Mungu, bali anachokijua yeye ni kwamba yeye alibipu akasukumiziwa.
Akasukumiziwa na nani, na wale wa rangi ya kijani ambao ua garagaza ilikuwa lazima rangi yao ya kijani iliokuwa inaelekea kufutika iokolewe.