Yona atoswe baharini ili merikebu isizame

Kwanza utubu dhambi ya kupotosha Neno la Mungu katika umma huu wa Jf. Usipotubu hukumu ijuu yako.

Wale wasafiri wengine chomboni na Yona waliomba kwa miungu yao na haikufua dafu kutuliza dhoruba iliyoitishwa na Mungu Mkuu nawa Kweli wa mbinguni. Mungu wa Ibrahim, Yakobo na Isihaka.

Jina la Yona lilipatikana kwa kupiga ramli
. Yona aliwatamkia wazi mimi ni myahudi ninaye Muamini Mungu wa kweli wa mbinguni ambaye na ukimbia uso wake.

Yona hatimaye alifika ni Ninawi/Leo Spain na alifikisha ujumbe wa Mungu na watu wake walipona. Wale waliodhani wamepona kwa kumtosa Yona baharini walipotea maana waliendelea na hasara kuu isiyo wezekana kurecover ya kuabudu miungu yao licha ya hasara za kutosa mizigo bahari.

Tanzania hatutaki kurudi huko Tarshishi, huko kwenye ufisadi uliotamalaki na kuongozwa na timu ya wavaa mipete ya bahati, za waganga, za wapiga ramli na waganga wa abudu mapepo eti wanazunguka nchi zima kulogea mambo ya tulie. Tuko na Yona kama ilivyo kupendeza kumuita eti ukifikiria ni kumdhihaki na kumkejeli tunaelekea Ninawi yetu tutaponea huko Miili na Roho zetu..
Mm naona hamjamuelewa kabisa, kama hujaelewa ni bora ukatulia kuliko kujibu usichokielewa..
Mwandishi anazungumzia dhahama ikiyowakumba wasafiri huku ikisababishwa na Yona..
Ni ANALYSIS nzuri sana, tena sana ila iko out of context kwa tafsiri rasmi kwa yeyote anaesoma biblia with simple understanding on story ya YONA.

Yona ni mjumbe (Nabii) na alikuwa na ujumbe, kosa lake alikimbia assignment ya kupeleka ujumbe Tarshishi

Yona alipotupwa baharini na bahari kutulia alienda Nchi ya Ninawi na kupeleka ujumbe, ujumbe wake ukasikizwa na watu wakatubu na kuyaacha mabaya na nchi yao haikuangamia na ghadhabu ya Mungu.

Kama kuna somewhere Merikebu mambo hayako shwari,si kosa la Captain au wafanyabiashara ku-overload merikebu, but rather ni Yona kukimbia assignment. hicho tu.
 
Anaandika; Robert Heriel.

Moja ya Visa maarufu kwenye Magombo ya kale ya Kiyahudi ni pamoja na Kisa cha Nabii mdogo aitwaye Yona. Kwa Waislam hujulikana kama Nabii Yunus.

Kwa faida ya wasiomjua Yona. Yona ni Nabii mdogo aliyeishi Kaskazini mwa nchi ya Israel. Baba yake aliitwa Amitai. Yona ambaye ndiye Yunus aliagizwa kwenda Mji Mkubwa wa Ninawi akapige kelele na kuwaonya juu ya maovu yao. Lakini Yona alikaidi, Hakuenda Ninawi bali alifunga Safari ya kwenda Tarshishi kujiepusha na Uso wa Mungu. Usafiri pekee aliokuwa akiutegemea ulikuwa ni Usafiri wa Majini kwa kutumia Merikebu. Hapo ndipo Kiini cha mada yetu kilipo.

Yona alipanda Merikebu na safari ya Tarshishi ilianza. Wakiwa njiani mara upepo mkali na Mawimbi yakaanza kuisuka suka merikebu. Wakati huo Yona alitafuta chimbo akajificha huko na kulala kabisa fofofo. Hahaahaha!! Yona Bhana anachekesha kweli.

Wenzake wanahangaika kupambana na dhoruba ya baharini. Yona anakoroma. Ilifikia hatua wakaamua kupunguza Mizigo kusudi Merikebu/Meli isizame lakini haikufua Dafu. Kumbuka Merikebu hii ilipandwa na watu mbalimbali wakiwemo Wafanyabiashara waliobeba mizigo yao ya biashara kwenda kuiuza mji wa Tarshishi.

Embu fikiria wewe ndiye Mfanyabiashara upo ndani ya Merikebu unaambiwa utupe mizigo yako ili meli isizame. Looh! Hakika inaumiza sana. Pia walikuwepo Abiria wengine huenda ni Waalimu, Matabibu, Waandishi wa Habari na wengineo. Wote sasa kila mmoja anaambiwa atupe mzigo wake baharini. Hahaha! Yaani kama ni Mwalimu ataambiwa atupe Mtaala, Muongozo, na Vitabu. Kama ni Mwanasheria au hakimu ataambiwa atupe mavitabu ya sheria, na Katiba. Waandishi nao wataambiwa tupeni Makamera yenu na magazeti yenu majini huko ili meli isizame.

Na kama ni Wachungaji na mashehe waliambiwa tupeni Biblia na Quran ili meli itulie. Looh! Yona yeye kalala.

Watu wakamkumbuka Yona. Ati mbona Yona kalala huko chimbo wakati sisi tupo katika hali ngumu hivi. Jamani Yona aamshwe. Yona akaamshwa.

Hahaha! Yona kuamshwa ati anapikicha macho na kupiga Miayo. Looh! Yona kweli umevurugwa.
Yaani unapiga miayo wenzako wapo hai hai roho mkononi. Khaah!!.

Kumbuka wasafiri hawa hawajuani. Mara paap! Wakampiga Maswali muhimu; Moja, Kazi yako ni kazi gani? mbili, Umetoka wapi? Tatu, Nchi yako ni nchi Ipi
?. Mwisho, Kabila lako ni lipi?. Yona akabung'aa akajua hapa dili limesanukiwa. Akawajibu.

Sasa wakamtambua. Wakamuogopa. Wakamuuliza kwa hadhari na kwa hofu. ''TUKUTENDE NINI BAHARI ITULIE?''
Akawajibu, ''NIKAMATENI, MNITUPE BAHARINI, NAYO BAHARI ITATULIA. akamalizia huku akipiga pikicha macho akiyatazama mawimbi, akasema; Kwa ajili yangu najua ndio maana tufani hii imewapata. Looh!

Napiga picha nami nimo ndani ya Merikebu. Huenda mimi ni Mfanyabiashara na tayari mizigo yangu imetupwa baharini. Alafu punde Anakuja mtu anasema kuwa hasara niliyoipata ni kwa sababu yake. Embu na wewe nisaidie kupiga picha hapo alafu utaelewa Wale wasafiri muda ule walikuwa wanamtazamaje Yona.

Kitu pekee kinachokuja kwenye akili yangu ni kuwa, tayari Yona anajua yeye ni chanzo cha ile Tufani. Pia Wasafiri wenzake nao wameshamjua Yona ndio chanzo cha wao kupatwa na Mabaya yale. Chanzo cha wao kutupa mizigo yao. Biashara zao. Nguo zao. Zawadi zao. Na kila aina ya mizigo. Lakini nilichokigundua ni kuwa Yona hana Ujasiri wa Kujitupa mwenyewe Baharini. Anaomba Msaada wa Kutupwa na Wasafiri wenzake.

Hii inaniambia yakuwa Watu kama wakina Yona kamwe usisubiri ajitupe mwenyewe Baharini kwani hawawezi kufanya hivyo. Watu kama kina Yona ni kuwatosa tuu Baharini.

Basi Wakamtupa Yona Baharini na muda ule ule Bahari ikatulie. Kumbe wangejua muda mrefu kuwa chanzo cha maswahibu na Mabaya yote ni Yona wasingetupa Mizigo yao. Wasingetupa Nguo zao. Biashara zao. Kamera zao wasingezitupa. Vitabu vyao na mizigo mingine. Wangemtupa tuu huyo Yona.

Najifunza katika kisa hiki kuwa Endapo Yona akitoswa Baharini basi bahari inatulia. Ukiona umemtupa Mtu lakini bado majanga yanaendelea ujue umemtupa asiye sahihi.

Huu ni wakati wa Kumtupa Yona baharini. Yona anagharimu wafanyabiashara kutupa biashara zao baharini. Yona anagharimu watu kutupa mitaji yao baharini. Yona akitupwa Baharini Biashara haitatupwa baharini. Watu hawatatupa mitaji majini.

Huwezi Safiri na Yona kwenye merikebu alafu biashara yako ikakaa poa. Ukimuonea huruma Yona basi kubali na usilalamike Uonapo biashara yako ikitupwa baharini.

Huu ni wakati wa Kumtosa Yona Baharini Vinginevyo Wakulima waliomo Kwenye Merikebu watazidi kutupa mazao yao na mbegu zao baharini. Mkulima huwezi safiri pamoja na Yona kwenye Merikebu alafu mazao yako yakabaki salama. Lazima yatupwe baharini. lazima mbegu zitupe baharini. looh! Yona bhana.

Wakati ni sasa wa Kumtupa Yona Baharini ili Ndoa yako ibaki salama. Ili wewe Binti uolewe na kijana uoe lazima Yona atoswe baharini. Vinginevyo Mahari na Zawadi ulizobeba kwenda ukweni zitupwe baharini. Mtaji na faida ya biashara yako ulioubeba kurudi nyumbani utupwe baharini. Je Mkeo atakuelewa ukifika? Ati umwambie Faida na mshahara wote niliutupa baharini kwa sababu ya Yona. Mkeo au mumeo atakuelewa. Tupa Yona Baharini acha kuvunja ndoa kisa Yona.

Yona yeye haoni tufani kwani kalala huko chimboni. Wewe upo juu ya Merikebu unamtolea Maji yanayoingia kwenye Merikebu. Unapandisha na kuliweka vizuri Tanga ili likabiliane vizuri na upepo. Yeye Yona kambonji. Haha! Nacheka kama mazuri.

Kijana unahangaika kutafuta kazi ya kuajiriwa au kujiajiri huko ndiko kutoa maji kwenye Merikebu. Unajua hayo maji unayoyatoa yasingeingia kama sio Yona. Yona ndiye kaleta tufani iliyoingiza maji ndani ya Merikebu ona sasa inazama. Yeye kalala kazi kupiga miayo na kukoroma tuu. Tena anakoroma kama simba. Yeye kutoa Maji hataki wakati yeye ndiye chanzo cha tufani. Looh! Embu mtoseni Yona Baharini msimkawize atazidi kuleta madhara.

Unajua Yona ni kweli alitumwa na Mungu lakini alichokosea ni Kupanda Merikebu yenu wakati yeye haelekei ninyi mnakoelekea. Yeye aliagizwa kwenda Ninawi alafu akapanda Merikebu yenu iendayo Tarshishi. Kwani ndiko alikotumwa.

Sasa Matokeo yake ndio hayo Sasa. Utaona watu wanakufa bila sababu kisa ni Yona. Wanavamiwa na Kutekwa kisa ni Yona. Yona Hicho sicho ulichoagizwa na Mungu. Na kwa vile unakimbia Uso wa Mungu basi Lazima utoswe Baharini.

Hata katika Taifa wapo wakina Yona wengi. Sifa za Yona zinajulikana. Ukiona mtu anatoswa baharini kwenye taifa na bahari haitulii ujue huyo hakuwa Yona. Yona bado yupo Merikebuni. Ukiona mtu kauawa au kafungwa au katekwa lakini Bahari haitulii ujue huyo hakuwa Yona. Yona bado yupo kwenye Merikebu. Yona amelala anakoroma kama simba. Tena ukimuamsha atapiga miayo sura yake akiwa ameikunja na macho yakiwa mekundu.

Yona ukimuuliza yeye ni nani. Atakujibu na lazima utaogopa kwa kuwa wasifu wake si haba. Lakini Usimuogope mtose Baharini uone kama Bahari haitatulia.

Wakati ni Sasa. Yona atoswe Baharini Merikebu ipate kutulia. Wasafiri roho zao zipumzike. Looh!

Kumbuka kamwe Usidhani kuwa Yona atajitosa mwenyewe Baharini. Yona hatofanya hivyo asilani. Mkamateni, mumtupe Baharini, Nayo bahari itatulia.

Taikon Nimemaliza mwenye maswali aweza kuuliza. Ila Majibu yangu yanaweza kumtatiza.

Robert Heriel
Taikon Wa Fasihi.
Napenda ulivyoufikisha ujumbe wako. Umeeleweka vizuri, sina shaka utakuwa na ualimu ndani yako.
Ni kweli maYona hadi sasa yapo tunasafiri nayo. Tofauti na Yona wa kale, hayakoromi wakati wa dhoruba. Hata ukiyahoji, hayasemi ukweli. Ni maongo kuliko shetani na hayako tayari kutupwa baharini. Tunachangamoto kweli!
 
Asante Baba mchungaji kwa somo lako zuri nimeelewa somo. 2020 nitajitahidi kumtosa yona baharini hata kama ataibuka tena 2025 nitamtosa tena sitochoka.
 
Maswali umeyakaribisha:

1. Umesema Yona hawezi kujitupa baharini, ni lazima atoswe na abiria wenzake. Je, huyu Yona hana vifaa vya kuzuia asitoswe, maanake naye ni mwoga. Yona hana vifaru, hana submachinegun? Ni abiria yupi asiyejipenda amsogelee Yona na kumtosa majini.

2. Yona yule hakuwa na wapambe wa kunogesha usingizi na njozi zake? Wapo wapambe wanaopendekeza ili merikebu hii isizame ni lazima watu wanene watoswe ili uzito upungue. Unalo lipi la kupinga hoja hiyo.

3. Wapo wapambe wanaopiga propaganda za kumkingia kifua Yona, wanasema madhambi ya baadhi ya abiria kama hao wafanya biashara na walanguzi ndicho chanzo kikuu cha dhoruba hii inayoikabili merikebu. Yona wao, anayepiga usingizi anapambana na hawa waliozoea unyang'anyi na njia za mkato za kujipatia mali. Wapambe wanapiga mayowe, hawa ndio inafaa watoswe meli ipate kutulia. Hawa nao unawaambia nini?

4. Huyu Yona unayetaka atoswe majini yeye mwenyewe anajihesabu kuwa mteule wa mungu. Ametumwa na mungu aje kurekebisha yote anayoona yeye ni uchafu. Yona wako na Yona wetu ni 'watume wadogo' wawili tofauti na huenda hata vitabu vitakatifu biblia na korani walimo hadithiwa navyo ni machapisho mbalimbali.
Unasemaje kuhusu hili.

Maswali ni mengi kuhusu Yona wako huyu, lakini kwa sasa shughulika na hayo machache kwanza.

Praise and worship @ work
 
Anaandika; Robert Heriel.

Moja ya Visa maarufu kwenye Magombo ya kale ya Kiyahudi ni pamoja na Kisa cha Nabii mdogo aitwaye Yona. Kwa Waislam hujulikana kama Nabii Yunus.

Kwa faida ya wasiomjua Yona. Yona ni Nabii mdogo aliyeishi Kaskazini mwa nchi ya Israel. Baba yake aliitwa Amitai. Yona ambaye ndiye Yunus aliagizwa kwenda Mji Mkubwa wa Ninawi akapige kelele na kuwaonya juu ya maovu yao. Lakini Yona alikaidi, Hakuenda Ninawi bali alifunga Safari ya kwenda Tarshishi kujiepusha na Uso wa Mungu. Usafiri pekee aliokuwa akiutegemea ulikuwa ni Usafiri wa Majini kwa kutumia Merikebu. Hapo ndipo Kiini cha mada yetu kilipo.

Yona alipanda Merikebu na safari ya Tarshishi ilianza. Wakiwa njiani mara upepo mkali na Mawimbi yakaanza kuisuka suka merikebu. Wakati huo Yona alitafuta chimbo akajificha huko na kulala kabisa fofofo. Hahaahaha!! Yona Bhana anachekesha kweli.

Wenzake wanahangaika kupambana na dhoruba ya baharini. Yona anakoroma. Ilifikia hatua wakaamua kupunguza Mizigo kusudi Merikebu/Meli isizame lakini haikufua Dafu. Kumbuka Merikebu hii ilipandwa na watu mbalimbali wakiwemo Wafanyabiashara waliobeba mizigo yao ya biashara kwenda kuiuza mji wa Tarshishi.

Embu fikiria wewe ndiye Mfanyabiashara upo ndani ya Merikebu unaambiwa utupe mizigo yako ili meli isizame. Looh! Hakika inaumiza sana. Pia walikuwepo Abiria wengine huenda ni Waalimu, Matabibu, Waandishi wa Habari na wengineo. Wote sasa kila mmoja anaambiwa atupe mzigo wake baharini. Hahaha! Yaani kama ni Mwalimu ataambiwa atupe Mtaala, Muongozo, na Vitabu. Kama ni Mwanasheria au hakimu ataambiwa atupe mavitabu ya sheria, na Katiba. Waandishi nao wataambiwa tupeni Makamera yenu na magazeti yenu majini huko ili meli isizame.

Na kama ni Wachungaji na mashehe waliambiwa tupeni Biblia na Quran ili meli itulie. Looh! Yona yeye kalala.

Watu wakamkumbuka Yona. Ati mbona Yona kalala huko chimbo wakati sisi tupo katika hali ngumu hivi. Jamani Yona aamshwe. Yona akaamshwa.

Hahaha! Yona kuamshwa ati anapikicha macho na kupiga Miayo. Looh! Yona kweli umevurugwa.
Yaani unapiga miayo wenzako wapo hai hai roho mkononi. Khaah!!.

Kumbuka wasafiri hawa hawajuani. Mara paap! Wakampiga Maswali muhimu; Moja, Kazi yako ni kazi gani? mbili, Umetoka wapi? Tatu, Nchi yako ni nchi Ipi
?. Mwisho, Kabila lako ni lipi?. Yona akabung'aa akajua hapa dili limesanukiwa. Akawajibu.

Sasa wakamtambua. Wakamuogopa. Wakamuuliza kwa hadhari na kwa hofu. ''TUKUTENDE NINI BAHARI ITULIE?''
Akawajibu, ''NIKAMATENI, MNITUPE BAHARINI, NAYO BAHARI ITATULIA. akamalizia huku akipiga pikicha macho akiyatazama mawimbi, akasema; Kwa ajili yangu najua ndio maana tufani hii imewapata. Looh!

Napiga picha nami nimo ndani ya Merikebu. Huenda mimi ni Mfanyabiashara na tayari mizigo yangu imetupwa baharini. Alafu punde Anakuja mtu anasema kuwa hasara niliyoipata ni kwa sababu yake. Embu na wewe nisaidie kupiga picha hapo alafu utaelewa Wale wasafiri muda ule walikuwa wanamtazamaje Yona.

Kitu pekee kinachokuja kwenye akili yangu ni kuwa, tayari Yona anajua yeye ni chanzo cha ile Tufani. Pia Wasafiri wenzake nao wameshamjua Yona ndio chanzo cha wao kupatwa na Mabaya yale. Chanzo cha wao kutupa mizigo yao. Biashara zao. Nguo zao. Zawadi zao. Na kila aina ya mizigo. Lakini nilichokigundua ni kuwa Yona hana Ujasiri wa Kujitupa mwenyewe Baharini. Anaomba Msaada wa Kutupwa na Wasafiri wenzake.

Hii inaniambia yakuwa Watu kama wakina Yona kamwe usisubiri ajitupe mwenyewe Baharini kwani hawawezi kufanya hivyo. Watu kama kina Yona ni kuwatosa tuu Baharini.

Basi Wakamtupa Yona Baharini na muda ule ule Bahari ikatulie. Kumbe wangejua muda mrefu kuwa chanzo cha maswahibu na Mabaya yote ni Yona wasingetupa Mizigo yao. Wasingetupa Nguo zao. Biashara zao. Kamera zao wasingezitupa. Vitabu vyao na mizigo mingine. Wangemtupa tuu huyo Yona.

Najifunza katika kisa hiki kuwa Endapo Yona akitoswa Baharini basi bahari inatulia. Ukiona umemtupa Mtu lakini bado majanga yanaendelea ujue umemtupa asiye sahihi.

Huu ni wakati wa Kumtupa Yona baharini. Yona anagharimu wafanyabiashara kutupa biashara zao baharini. Yona anagharimu watu kutupa mitaji yao baharini. Yona akitupwa Baharini Biashara haitatupwa baharini. Watu hawatatupa mitaji majini.

Huwezi Safiri na Yona kwenye merikebu alafu biashara yako ikakaa poa. Ukimuonea huruma Yona basi kubali na usilalamike Uonapo biashara yako ikitupwa baharini.

Huu ni wakati wa Kumtosa Yona Baharini Vinginevyo Wakulima waliomo Kwenye Merikebu watazidi kutupa mazao yao na mbegu zao baharini. Mkulima huwezi safiri pamoja na Yona kwenye Merikebu alafu mazao yako yakabaki salama. Lazima yatupwe baharini. lazima mbegu zitupe baharini. looh! Yona bhana.

Wakati ni sasa wa Kumtupa Yona Baharini ili Ndoa yako ibaki salama. Ili wewe Binti uolewe na kijana uoe lazima Yona atoswe baharini. Vinginevyo Mahari na Zawadi ulizobeba kwenda ukweni zitupwe baharini. Mtaji na faida ya biashara yako ulioubeba kurudi nyumbani utupwe baharini. Je Mkeo atakuelewa ukifika? Ati umwambie Faida na mshahara wote niliutupa baharini kwa sababu ya Yona. Mkeo au mumeo atakuelewa. Tupa Yona Baharini acha kuvunja ndoa kisa Yona.

Yona yeye haoni tufani kwani kalala huko chimboni. Wewe upo juu ya Merikebu unamtolea Maji yanayoingia kwenye Merikebu. Unapandisha na kuliweka vizuri Tanga ili likabiliane vizuri na upepo. Yeye Yona kambonji. Haha! Nacheka kama mazuri.

Kijana unahangaika kutafuta kazi ya kuajiriwa au kujiajiri huko ndiko kutoa maji kwenye Merikebu. Unajua hayo maji unayoyatoa yasingeingia kama sio Yona. Yona ndiye kaleta tufani iliyoingiza maji ndani ya Merikebu ona sasa inazama. Yeye kalala kazi kupiga miayo na kukoroma tuu. Tena anakoroma kama simba. Yeye kutoa Maji hataki wakati yeye ndiye chanzo cha tufani. Looh! Embu mtoseni Yona Baharini msimkawize atazidi kuleta madhara.

Unajua Yona ni kweli alitumwa na Mungu lakini alichokosea ni Kupanda Merikebu yenu wakati yeye haelekei ninyi mnakoelekea. Yeye aliagizwa kwenda Ninawi alafu akapanda Merikebu yenu iendayo Tarshishi. Kwani ndiko alikotumwa.

Sasa Matokeo yake ndio hayo Sasa. Utaona watu wanakufa bila sababu kisa ni Yona. Wanavamiwa na Kutekwa kisa ni Yona. Yona Hicho sicho ulichoagizwa na Mungu. Na kwa vile unakimbia Uso wa Mungu basi Lazima utoswe Baharini.

Hata katika Taifa wapo wakina Yona wengi. Sifa za Yona zinajulikana. Ukiona mtu anatoswa baharini kwenye taifa na bahari haitulii ujue huyo hakuwa Yona. Yona bado yupo Merikebuni. Ukiona mtu kauawa au kafungwa au katekwa lakini Bahari haitulii ujue huyo hakuwa Yona. Yona bado yupo kwenye Merikebu. Yona amelala anakoroma kama simba. Tena ukimuamsha atapiga miayo sura yake akiwa ameikunja na macho yakiwa mekundu.

Yona ukimuuliza yeye ni nani. Atakujibu na lazima utaogopa kwa kuwa wasifu wake si haba. Lakini Usimuogope mtose Baharini uone kama Bahari haitatulia.

Wakati ni Sasa. Yona atoswe Baharini Merikebu ipate kutulia. Wasafiri roho zao zipumzike. Looh!

Kumbuka kamwe Usidhani kuwa Yona atajitosa mwenyewe Baharini. Yona hatofanya hivyo asilani. Mkamateni, mumtupe Baharini, Nayo bahari itatulia.

Taikon Nimemaliza mwenye maswali aweza kuuliza. Ila Majibu yangu yanaweza kumtatiza.

Robert Heriel
Taikon Wa Fasihi.

Umeongea kweli, japo kuna utata.
Yona wa kwenye biblia alikuwa abiria, ila Yona unayemzungumzia ndo kashikilia usukani wa meli yenyewe (Baharia) sasa mkimgusa anaigongesha meli kwenye mwamba tufe wote.
 
Kwanza utubu dhambi ya kupotosha Neno la Mungu katika umma huu wa Jf. Usipotubu hukumu ijuu yako.

Wale wasafiri wengine chomboni na Yona waliomba kwa miungu yao na haikufua dafu kutuliza dhoruba iliyoitishwa na Mungu Mkuu nawa Kweli wa mbinguni. Mungu wa Ibrahim, Yakobo na Isihaka.

Jina la Yona lilipatikana kwa kupiga ramli
. Yona aliwatamkia wazi mimi ni myahudi ninaye Muamini Mungu wa kweli wa mbinguni ambaye na ukimbia uso wake.

Yona hatimaye alifika ni Ninawi/Leo Spain na alifikisha ujumbe wa Mungu na watu wake walipona. Wale waliodhani wamepona kwa kumtosa Yona baharini walipotea maana waliendelea na hasara kuu isiyo wezekana kurecover ya kuabudu miungu yao licha ya hasara za kutosa mizigo bahari.

Tanzania hatutaki kurudi huko Tarshishi, huko kwenye ufisadi uliotamalaki na kuongozwa na timu ya wavaa mipete ya bahati, za waganga, za wapiga ramli na waganga wa abudu mapepo eti wanazunguka nchi zima kulogea mambo ya tulie. Tuko na Yona kama ilivyo kupendeza kumuita eti ukifikiria ni kumdhihaki na kumkejeli tunaelekea Ninawi yetu tutaponea huko Miili na Roho zetu..
Mtoa mada na mtoa comment wote wanaweza wakawa sahihi kwa kulenga jambo lilelile moja, japo kuwa kuna mmoja anamuona Yona kama mtetezi na mkombozi.

Lakini hapa inaonekana kuwa jina la Yona lilipatikana kwa njia ya kupiga ramli jambo ambalo ni chukizo kwa Mungu,lakini hapohapo pamoja na Yona kutupwa bahari bado Mungu alitumia njia nyingine ya kumuwezesha Yona kufikisha ujumbe wake Ninawi.

Baada ya Mungu kumuokoa Yona asizame baharini kwa kumtuma samaki ammeze na kumtapikia kwenye ufukwe wa Ninawi na kufanikiwa kufikisha ujumbe aliotumwa na Mungu kwa wahusika ambao walitubu na kumugeukia Mungu.

Kitendo ambacho hakikumpendeza Yona kwa kuwa lengo lake alitaka watu wa Ninawi waangamie.

Kwa Yona wetu huyu jina lake litakuwa lilipatikana kwa njia ileile ya kupiga ramli na kwa ajili ya kuiokoa rangi ya kijani ambayo ilikuwa inaelekea kufutika na si kwa ajili ya kupeleka ujumbe wa Mungu kuwaponya watu wa Ninawi.

Kwani hata yeye mwenyewe hajui kama ujumbe aliopewa kupeleka Ninawi kama alipewa na Mungu, bali anachokijua yeye ni kwamba yeye alibipu akasukumiziwa.

Akasukumiziwa na nani, na wale wa rangi ya kijani ambao ua garagaza ilikuwa lazima rangi yao ya kijani iliokuwa inaelekea kufutika iokolewe.
 
Kitu pekee kizuri kwa Yona ni kwamba Yona alikuwa binadamu mwenye akili ndo maana akajua kuwa yeye ndo chanzo cha tatizo,huyu wetu si tu si binadamu bali pia hata akili hana na hivyo hawezi ona kama kuna tatizo na hivyo kujipima kama anaweza kuwa sehemu au chanzo cha tatizo au laa.Kwa kuwa hana akili,wala hakuna sababu ya kumhoji,bali kumkamata na kumtupilia mbali
 
Mm naona hamjamuelewa kabisa, kama hujaelewa ni bora ukatulia kuliko kujibu usichokielewa..
Mwandishi anazungumzia dhahama ikiyowakumba wasafiri huku ikisababishwa na Yona..

Mwandishi hakujua wale wote waliokuwa kwenye chombo na Yona walikuwa wa abudu shwetwani ndio maana walipiga ramli kujua chanzo cha tatizo ni nini? Na kuhakishia angekuwa na hayo maaono asingekuja na huu mfano maana hata yeye kawa exposed kuwa ni wafungu gani. Nimemsaidia kujua upande wa pili wa shilingi.
 
Mtoa mada na mtoa comment wote wanaweza wakawa sahihi kwa kulenga jambo lilelile moja, japo kuwa kuna mmoja anamuona Yona kama mtetezi na mkombozi.

Lakini hapa inaonekana kuwa jina la Yona lilipatikana kwa njia ya kupiga ramli jambo ambalo ni chukizo kwa Mungu,lakini hapohapo pamoja na Yona kutupwa bahari bado Mungu alitumia njia nyingine ya kumuwezesha Yona kufikisha ujumbe wake Ninawi.

Baada ya Mungu kumuokoa Yona asizame baharini kwa kumtuma samaki ammeze na kumtapikia kwenye ufukwe wa Ninawi na kufanikiwa kufikisha ujumbe aliotumwa na Mungu kwa wahusika ambao walitubu na kumugeukia Mungu.

Kitendo ambacho hakikumpendeza Yona kwa kuwa lengo lake alitaka watu wa Ninawi waangamie.

Kwa Yona wetu huyu jina lake litakuwa lilipatikana kwa njia ileile ya kupiga ramli na kwa ajili ya kuiokoa rangi ya kijani ambayo ilikuwa inaelekea kufutika na si kwa ajili ya kupeleka ujumbe wa Mungu kuwaponya watu wa Ninawi.

Kwani hata yeye mwenyewe hajui kama ujumbe aliopewa kupeleka Ninawi kama alipewa na Mungu, bali anachokijua yeye ni kwamba yeye alibipu akasukumiziwa.

Akasukumiziwa na nani, na wale wa rangi ya kijani ambao ua garagaza ilikuwa lazima rangi yao ya kijani iliokuwa inaelekea kufutika iokolewe.

The end justify the, ... Ninawi ambayo ndiyo Uspain ya leo tunayoishudia ilipona, na ndicho tunachokiona Tanzania itapona ukiwemo wewe na mimi, hilo tu.
 
Kwanza utubu dhambi ya kupotosha Neno la Mungu katika umma huu wa Jf. Usipotubu hukumu ijuu yako.

Wale wasafiri wengine chomboni na Yona waliomba kwa miungu yao na haikufua dafu kutuliza dhoruba iliyoitishwa na Mungu Mkuu nawa Kweli wa mbinguni. Mungu wa Ibrahim, Yakobo na Isihaka.

Jina la Yona lilipatikana kwa kupiga ramli
. Yona aliwatamkia wazi mimi ni myahudi ninaye Muamini Mungu wa kweli wa mbinguni ambaye na ukimbia uso wake.

Yona hatimaye alifika ni Ninawi/Leo Spain na alifikisha ujumbe wa Mungu na watu wake walipona. Wale waliodhani wamepona kwa kumtosa Yona baharini walipotea maana waliendelea na hasara kuu isiyo wezekana kurecover ya kuabudu miungu yao licha ya hasara za kutosa mizigo bahari.

Tanzania hatutaki kurudi huko Tarshishi, huko kwenye ufisadi uliotamalaki na kuongozwa na timu ya wavaa mipete ya bahati, za waganga, za wapiga ramli na waganga wa abudu mapepo eti wanazunguka nchi zima kulogea mambo ya tulie. Tuko na Yona kama ilivyo kupendeza kumuita eti ukifikiria ni kumdhihaki na kumkejeli tunaelekea Ninawi yetu tutaponea huko Miili na Roho zetu..
Mwandishi hakujua wale wote waliokuwa kwenye chombo na Yona walikuwa wa abudu shwetwani ndio maana walipiga ramli kujua chanzo cha tatizo ni nini? Na kuhakishia angekuwa na hayo maaono asingekuja na huu mfano maana hata yeye kawa exposed kuwa ni wafungu gani. Nimemsaidia kujua upande wa pili wa shilingi.
The end justify the, ... Ninawi ambayo ndiyo Uspain ya leo tunayoishudia ilipona, na ndicho tunachokiona Tanzania itapona ukiwemo wewe na mimi, hilo tu.
Ni kama kuna mantiki unayo.. Lakin sasa ni kama vile umeshindwa kuunganisha idea ya mleta uzi, post namba 42 na post namba 53 hlf ukaona picha ya fasihi ilivyojengwa na kinachozungumziwa kwa ujumla..

Uko sahihi unavyowaza kwa upande wako ila fasihi iliyotumika imeeleweka kwa wengi zaidi
 
Back
Top Bottom