Tungejua ana changamoto ya akili tusingekubali kumbeba

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,116
Kampuni ya Zan Fast Ferries inayofanya biashara ya kusafirisha Abiria kwa njia ya bahari Tanzania bara na Visiwani, imesema ingefahamu mapema kwamba Kijana aliyejirusha katikati ya bahari juzi ni Mgonjwa wa akili isingekubali kumbeba kwani huwa wanalizingatia hilo.

“Sisi hatukumjua yule toka mwanzo kama alikua ana tatizo hilo, tungekua na taarifa tusingemchukua kabisa, wakati Watu kama hawa wanasafirishwa kwenye vyombo tungeomba wale wanaofatana nao watoe taarifa mapema kabla hawajauziwa ticket ili hatua zinazofaa zichukuliwe” ——— Ali Salum, Msemaji wa Zan Fast Ferries.

"Tunaweza kusikiliza ushauri wa Daktari pia, hata Wajawazito tuna taratibu zao za kupanda kwenye boti, kuna kipindi maalum ambapo huwa tunawakubalia nadhani kama sijakosea akiwa na miezi sita au saba hatuwezi kukubali kwa sababu tunahofia lolote linaloweza kutokea ingawa tuna sehemu ya kina Dada ambao wanahusika na huduma za Wajawazito lakini abiria mwenye tumbo la karibia kujifungua huwa hatukubali ili kuepusha matatizo kama hayo" ——Salum

Pia soma:
- Video: Kijana atoa uhai wake kwa kujirusha baharini
 
Ona sasa, hivi ni kwanini Watanzania mnapenda kuzusha mambo?

Mwenzio alikuwa kwenye mazungumzo ya kushtukizwa, umefanya kutilia mkazo. Tuweni tunapuuzia mambo madogo madogo bhana
 
Back
Top Bottom